Showing posts with label Mapenzi na Ushauri. Show all posts
Showing posts with label Mapenzi na Ushauri. Show all posts

Sunday, February 18, 2018

Ukimpenda mtu Mwambie ukweli...

2/18/2018 08:46:00 PM 0
Sema tu Usiogope..

Siku ya kwanza alimkuta akiwa pekee huku akiwa hana furaha. John alijitahidi kumbeleza Sarah na kumfanya atulie. Alifanya hivyo kwa kuwa ukaribu wake na Sarah ulikuwa hauwez kuficha kitu abadini. Kila mmoja  alijua bayana mabadiliko ya mwenzie. Ndio walikuwa marafiki wakushiba, hakuna kilichowatenga mapacha hawa wasiofanana.


Walitembea pamoja. Walikaa pamoja, wakasoma pamoja. Alichokula John lazima Sarah akionje. Ndio mtindo wao wa kuishi. Siku, wiki, miezi  miaka ikaenda, wakakua, wakanawiri na kupendeza. Minong'ono ikaanza, hawa wawili wana kitu sirini...

John alibeba donge zito kooni. Donge la kuwa na hisia kali kwa Sarah. Yamkini aliona kabisa kuwa Sarah alikuwa mtu wake. Ndio alimpenda kimapenzi kwa muda mrefu! Angetoboaje siri ili Sarah ajue? Piga moyo konde, John alipotezea, maswali lukuki yakatiririka katika bongo yake. Nivunje yai? Niseme? Atanionaje? Itakuwaje!.? Akikataa je? Asiponikubalia? Akikasirika?.. Acha tu tuendelee hivi hivi.. Sarah ni rafiki baki kuwa rafiki, akajisemea huku akibeba mfuko wa daftari na kumkuta Sarah nje akimsubiri..

"unawaza nini J wangu? Hujui kuwa wiki ijayo birthday yangu? Usinifanye nikose furaha!"
Sauti ya Sarah haikufua dafu ya kumtoa John katikati ya pori la mawazo. Alimtizama Sarah macho yakongea nakupenda ila moyo ukamsaliti, ubongo  ukazuia usiseme... Akameza funda la mate kwa fujo..

Birthday...
Siku ikafika. John akawa na wakati mgumu ampe zawadi gani. Kila alichofikiri hakuona kama kitakuna moyo wa Sarah. Aliona kila kitu kigumu .. Mwishowe akamua kiume  akapita dukani na kununua ua zuri.. Red rose.. Yes lilikua ua jekundu la ghali  akalihifadhi vema. Alifika nyumbani na kulipulizia perfume yake nzuri. Akalifunga vema na kuelekea kunako pati...

Ndani ya party...
Kila kitu kilifana, tabasumu zilitokeza katika kila uso uliokuwako ndani ya ukumbi. Keki ikaletwa. Wakala vyakula vya kila aina na vinywaji. Muda ukafika Mc akagawa vikadi fulani. John alistuka kupata kadi ikiwa imeandikwa 1. Akiwa anasubiri maelezo mara Mc akang'aka kwa bashasha.
"Namba moja popote ulipo simama na zawadi njoo kwa mtoto aliyezaliwa leo, utampa zawadi na kucheza nae. Atakutambulisha hapa, tafadhali mheshimiwa inuka"

John akasimama kwa uoga, hakuamin, akatembea pole  alifika mbele ya Sarah akapokelewa kwa kumbatio murua lililoambata na busu zito katika paji la uso.. Mwili ukamzizima, moyo ukaagana na mwili kusawiri mapigo yake. Akatoa zawadi akacheza nae ziro distance.. Kitu murua, akatamani aseme, nafsi ikamhukumu kwa maamuzi yake, akausaliti moyo wake.. Akatambulishwa kwa kimombo He is my everything, he is my best friend.. Akarudi kukaa...part ikaisha, siku zikaenda wakashibana kama kumbikumbi..

Miaka ikaisha na miezi kenda.. Mficha maradhi kifo humuumbua akajisemea John.. Bado walikuwa zaidi ya marafiki. Safari hii wakiwa chuo. Ndio walisoma pamoja hadi chuo. Kila mtu akimuangalia mwenzake anaonekana ana kitu cha zaidi ya urafiki. Nani abomoe ukuta huu wa urafiki uliojengwa kwa zege zito na kwa muda wa miaka mingi? Nani angeanza, si John wala Sarah, wote walimeza gundi, wakatulia tuli kama maji mtungini wakisaliti mahitaji ya moyo na nafsi. John aliusulubu moyo wake zaidi hasa alipomkuta Saraha akiwa na mwanaume mwingine, wivu ulipenya na kuganda ndani ya moyo kama barufu.. Akawa muoga, akihofia kupigwa kete na wajanja wa mjini..

Mwaka wa tatu chuo..
Miaka nayo ikasonga, wakazidi kuwa wakubwa. Kila mmoja akificha. Wakahitimu masomo yao kwa ufaulu wa kishindo. Ilikuwa furaha kwao. Siku ya mahafali ikafika. Safari hii John alidhamiria na kuuapisha moyo wake kuwa lazima aseme. Ndio afunguke kuwa ana mapenzi mubashara na mujarabu juu ya Sarah  rafiki wake kipenzi.. Alijiapiza kutotenda kosa tena.. Yes alijisemea: moyo usisaliti nafsi na nasfi isisaliti ubongo na ubongo uamrishe mdomo umwambie Sarah maneno haya sita, NAKUPENDA SANA SARAH, NAOMBA NIWE WAKO... John alifanya mazoezi namna ya kusema akajiridhisha na kuona ya kuwa kila kitu ni chema, akavaa suti akapendeza akaenda kunako mahafali...

Dakika 15....
Sekunde dakika masaa yakasogea,baada ya mahafali kuisha! Wakapiga picha pamoja  na ndugu jamaa na marafiki. Hakuna aliyeficha hisia zake kibindoni. Kila mtu alionesha mapenzi na mbwembwe kede kede.. Naam ilikuwa kama mashindano...

John na dhamira yake huku akitetemeka akamshika mkono Sarah na kumpeleka sehemu bustani ya maua ya kuvutia. Akamkumbatia. Akamsogeza Sarah karibu wakatazamana kwa macho ya huba... Macho yakaongea.. Moyo ukapaa kwa mapigo, dakika tano sasa zilipita, hakuna aliyesema neno. Ila mioyo ikasema kwa kundunda kama watu waliopanda mlimaa kwa kukimbizwa. Joto la mwili likapanda haraka, macho ya Sarah yakajifumba.. Akabakia John mdomo ukitetemeka... Akaufungua sasa dakika ya 10....akauelekeza sikioni mwa Sarah...
NAKUPENDA SANA SARAH, NAOMBA NIWE WAKO... ndio alisema kwa usahihi bila kukwama. Maneno yake sita...

Maneno haya yalisikiwa na kupenya vema katika ngoma za masikio ya Sarah na kumfanya afumbue macho yake. Akamkumbatia zaidi John, akamwangalia vema. Ukimya ukatanda, John akaanza kujawa na woga. Nafsi ikamsuta moyo ukamhukumu, bora ningesubiri, akateta na ubongo wake...

Kimya, kimya kikatanda, kimya dakika ya15,
 Sarah akamgeukia John kimahaba akasema..
NILIKUSUBIRI USEME, I LOVE YOU JOHN!... Maneno yake sita yakaponya msononeko wa John, yakatibu msokoto wa tumbo uliokuja ghafula ndani ya dakika tano, Cameraman akatokea akapiga picha wakiwa wamekumatiana.. Wakaondoka zao wakikokotana kimahaba mara busu, mara hug, mara John akambeba Sarah mpaka chumbani. Aliweza licha ya Sarah kuwa na uzani mkubwa, wabwagana katika samani, kazi ya mikono ya seremala.. Dakika moja mbele .. Camera na taa vikazimwa.. Giza... *************

Morales....
Urafiki uliodumu kwa miaka mingi ni mgumu kuugeuza kuwa uhusiano wa kimapenzi

Ukimpenda mtu sema mapema, kuna wakati ukishampoteza harudi tena

Kukaa kimya kutakufanya upoteze mtu wa ndoto zako...

Ukimpenda sema tu....

Created by King Franco Samuel

Kindly share
Comment

Tuesday, February 13, 2018

Historia ya Valentine Day. Siku ya wapendanao

2/13/2018 09:53:00 AM 0
HISTORIA YA SIKU YA VALENTINE...
Ilianzia wapi na dhana yake ni ipi.?
Leo nakusogezea makala hii inayohusu historia fupi ya sikukuu pendwa kabisa kwa wapendanao duniani Valentine. Ungana nami katika makala hii nzuri na ya kukusimua

Sikuku ya Valentine ama sikukuu ya wapendanao chanzo chake hasa ni utawala wa  Dola ya Warumi. Ni siku ya kumbukumbu (memo9ria day) na sehemu nyingine ni (festum) maana yake siku kuu ya daraja la kwanza kwa kumkumbuka Padre Valentine aliyeuawa na utawala wa kirumi.

Padre Valentine aliua sababu ya kutetea waumini waweze kufunga ndoa. Katika miaka hiyo kulikuwa na vita kama ilivyokuwa desturi ya falme nyingine ili ziweze kujipanua  hivyo ili lazimu mfalme Caldius azuie watu kuoa kwani aliamini askari walio oa hawakuwa wazuri katika vita na wasingeweza kuwa huru kufanya majukumu ya familia na vita. Hata hivyo licha ya zuio hilo la kuwataka vijana wasifunge ndoa na badala yake wajiunge katika jeshi, Padre Valentine bado aliendlea kufungisha ndoa kwa siri..

Akawa anafungisha ndoa kwa siri kwenye makatakombe (mahandaki chini ya kanisa ambako kuna sehemu za ibada kwa watu wachache), alifanya hivyo kwa vile kufunga ndoa hadharani ilikuwa ni kukiuka amri ya wakuu wa dola ya kirumi..

Miaka kadhaa ilienda huku Padre Valentin akifungisha ndoa kwa siri na Baadhi ya watu walifichua siri hiyo, hivyo Padre Valentin alishikwa na dola ya Warumi na kutiwa gerezani akisubiri hukumu ya kifo kwa kukiuka amri ya kutofungisha  ndoa..
Inasemekana akiwa gerezani Padre Valentin alimpenda binti kipofu aliyekuwa mtoto wa msimamizi wa gereza alipokuwa amefungwa. Mara kadhaa binti huyo kipofu alihudhuria gerezani ili kumuona padre Valentin. Kwa muda kadhaa padre Valentine alikuwa akimtumia binti salamu akiwa gerezani na ndio dhana  ya sikukuu hii..

 Baadae padre Valentine alitakiwa kuikana imani yake na kuacha kufungisha ndoa kama dola ya Kirumi ilivyokuwa ikitaka. Lakini kutokana na msimamo wake hakuikana imani yake hivyo  A D 270- Valentin aliuawa.

Wakristo wakaweka siku ya kumkumbuka Padre Valentin kama mfia dini sababu ya kutetea maisha ya wanakanisa kwa wanandoa. Ikaenea katika kanisa nchi za magharibi na hata duniani ambako wanakanisa wanamkumbuka Mt. Padre Valentin.

Sikukuu ya Valentine’s: Siku ya mapenzi??
Papa Gelasius aliitangaza rasmi tarehe 14 ya mwezi wa pili kama sikukuu ya mtakatifu Valentine,yaani Valentines day.Miaka michache baadae sikukuu hiyo ilibeba maudhuhi au uzito wa mapenzi zaidi.Kati ya karne ya tano na karne ya kumi na tano, nchini Uingereza na Ufaransa ,iliaminika kwamba tarehe 14 ya mwezi wa pili ilikua ndio mwanzo wa kipindi cha ndege kupandana,hii ilijenga dhana kwamba siku ya sikukuu ya Valentin  lazima iwe siku ya kuonyesha mapenzi (romance).Ndio maana ndege hutumika kama alama ya Valentine.

Baadaye ikapokeleka na watu hata wasio na imani ya kikristo kama ni siku ya kufanya kumbukumbu kwa Mt. Valentin kama mtetezi wa Ndoa.

Maudhui ya siku hiyo kwa wasiowanakanisa imechukua maana nyingine ya kwamba ni siku ya wapendanao hata kwa wasio wanandoa ili  mradi wanapendana, kitu ambacho ni kinyume cha malengo ya mfia dini Mt. Padre Valentin aliyetaka vijana wafunge ndoa badala ya kuwa na hawara tu (vimada) kama  sheria ya Rumi ilivyokuwa ikitaka.



 Hata sasa duniani koti watu huadhimisha sikukuu hii kwa kuonesha mapenzi romance kwa wawapendao kwa kuwapa zawadi ikiwemo kadi, maua na chocolate kma ishara ya upendo. Rangi nyekundu ndio hasa hutumika katika sikukuu hii..

Waweza kuona na kudownload kadi nzuri hapa na kumtumia umpendae.. 
baadhi ya kadi na maua ya Valentine hapa































Na
WhatsApp 255768800687

Tuesday, December 5, 2017

Madhara ya Kujichubua

12/05/2017 09:28:00 AM 0

Madhara ya kujichubua

Urembo na kuwa na ngozi yenye mvuto  ni kitu ambacho karibia kila mtu anapenda. Siku hizi imekuwa kawaida kukutana na mtu akiwa kajipendezesha hasa uso. Hii ni kwasababu wengi tunaamini uso ndio kitu cha kwanza kuonwa na watu yaani face is introduction for everyone 


Katika baadhi ya sehemu duniani watu wanaamini kuwa ngozi angavu huashiria uzuri, utajiri na uwezo(kifedha) alionao mtu. Katika baadhi ya sehemu watu wenye ngozi nyeusi huchukuliwa kuwa wapo chini ya kiwango, hii hupelekea watu hawa kutumia ving´arisha ngozi kama krimu, vidonge au nyenzo zingine kubadilisha ngozi zao. Idadi inazidi kukua maradufu ya matumizi ya ving'arisha ngozi, na siku hizi hata wanaume wapo tofauti na zama za kale ambapo mabinti walishika usukuni.

 Tafiti zinaonyesha kwamba wavulana na wasichana hupendelea kutumia bidhaa zinazong´arisha ngozi ili waweze kupata hadhi nzuri katika kundi la familia zao, na jamii. Kwa kweli,hata matangazo yanayoonyeshwa kwenye televisheni mbalimbali huonyesha kitu hiki.

Mambo hayo yote huwa na athari kubwa juu ya mawazo ya vijana wa kiume na wakike ambayo hupelekea kuwafanya wachague chochote wanachomudu kati ya krimu au vidonge.

Je kuna madhara kujichubua...?

  • Jibu ni rahisi tu, ndiyo yapo tena sana kama sio leo basi kesho kwa wewe unayetumia! Nimekuandikia hapa madhara yasome uelewe mtu wangu..u anaeyejichubua anaweza kupata kansa ya ngozi, chunusi, uvimbe katika ngozi, ngozi kuwa nyembamba na kukosa uimara katika uvutikaji yaani stretiching ambapo mtu huyu akipata ajali sio rahisi kushona kwa kuwa ngozi hukatika tu! 
  • Kuongezeka kwa hamu ya kula na uzito, wengi wameongezeka uzito bila kujijua hii inatokana na baadhi ya krimu ama vidonge kuongeza hamu ya kula
  • Kutokwa na mabaka na mavipele makubwa ambayo siyo rahisi kupona na hufanya mtu akose mvuto na raha, wapo wengi wako katika hali hii. U
  • Ugonjwa wa pumu kutoka na krimu ama vidonge kuathiri mapafu na mfumo wa upumuaji. K
  • Kupata watoto wenye kasoro baadhi ya madini na viambata vilivyopo kwenye ving'arisha ngozi huathiri mbegu na mfumo wa uzazi hivyo kuathiri aina ya watoto mtu atako zaou
  • Kupata matatizo ya akili na kuharibika kwa ini, ini huaribika kutokana na kushindwa kukabili sumu ya dawa ambazo mtu katumia. K
  • Kuharibika kwa mishipa ya fahamu pamoja na figo kutokana na kiwango kikubwa cha zebaki(mercury) kilichomo katika krimu, Osteoporosis(kupungua kwa uzito wa mifupa ambapo huongeza hatari ya kuvunjika kwa mifupa)

Kuungua kwa uso na kubaki na ngozi yenye makovu makovu na isiyovutia.. 
Baadhi ya madhara haya huonekaa mara moja na mengine hujitokeza kadri mtu anavyotumia ving´arisha ngozi na kadiri anavyozidi kuzeeka. 
Waweza kupendeza leo ila ukawa unajichimbia kaburi la mateso hapo baadae, kumbuka fainali uzeeni na siku zote kujikubali ulivyo ndio silaha ya kwanza. 
Waweza kushare maarifa haya kuokoa wengine



Rudisha mvuto wa ngozi kwa Njia asilia

12/05/2017 09:08:00 AM 0
Njia za asili za Kuondoa mikunjo ya ngozi
MIKUNJO katika ngozi ni miongoni mwa matatizo yanayowakabili wanawake wengi.

Tofauti na mikunjo ya uzee, mikunjo hii hutokana na kuchoka kwa ngozi kunakosababishwa na mambo mablimbali ikiwemo matumizi ya vipodozi vyenye kemikali kali ambayo huondoa uhalisia wa ngozi.
Katika kupambana na tatizo hilo, wadau wa urembo wa asili wamegundua njia mbalimbali zinazoweza kutumika kutatua tatizo hili.
Wadau hao wanashauri kumwona mtaalamu wa afya kwa ushauri zaidi wa matumizi ya njia hizo za asili kabla ya kuanza kutumia njia za asili kwani hata kama ni vipodozi asilia, haina maana kama ni salama kwa watu wote.
Kwa mujibu wa wadau hao, unaweza kutumia viungo vinavyopatikana jikoni kwako kupambana na mikunjo katika ngozi. Baadhi ya viungo hivyo ni pamoja na:
Karoti
Tumia juisi ya karoti kwa kupaka katika ngozi yako, hasa katika maeneo yaliyoathirika.
Karoti ina virutubisho muhimu kwa ngozi yako. Pia ina uwezo mkubwa wa kuondoa sumu ndani ya ngozi.
Si hivyo tu, karoti inaweza kuondoa kabisa tatizo la mikunjo ya
ngozi hasa sehemu za pembeni ya macho, shingo na maeneo kama hayo.
Jinsi ya kuandaa na kutumia.
Chukua karoti, saga kwenye mashine kisha kamua ili kupata juisi yake.
Tumia pamba kupaka katika maeneo yaliyoathirika, fanya hivyo mara kwa mara, itakusaidia kupunguza ama kuondoa kabisa tatizo hilo.
Maziwa
Maziwa yana virutubisho vinavyochochea kunawiri kwa ngozi.  Pia yana chembechembe za 'Alfa-Hydroxide Acid' ambazo zina uwezo mkubwa kuondoa seli zilizokufa mwilini.
Yote haya husaidia kwa kiasi kikubwa kuondoa tatizo la mikunjo katika ngozi.
Unachotakiwa kufanya
Kuchukua maziwa kiasi na chovya pamba ndani yake, kisha paka maeneo yaliyoathirika.
Aloe Vera
Jeli ya Alovera ndiyo hasa inayotakiwa katika zoezi hili. Chukua jani lake na kisha likate ili kupata utomvu wake.
Chukua utomvu au jeli hiyo kama wengine wanavyoita na kisha pakaa sehemu iliyoathirika, itapunguza ama kuondoa kabisa tatizo hilo.
Parachichi
 'Mask' ya Parachichi husaidia kuifanya ngozi iwe na mng'ao. Siyo hivyo tu, bali huchangia kwa kiasi kikubwa pia kuifanya ngozi iwe laini na nyororo.
Jinsi ya kutayarisha na kutumia
Chukua parachichi liloiva vizuri, kisha saga hadi lilainike.
Baada ya hapo pakaa sehemu iliyoathirika na acha kwa muda wa dakika 10, kisha osha sehemu hiyo uikaushe.

Papai
Mask ya Papai pia husaidia kuondoa tatizo hili.
Unachotakiwa kufanya...
Chukua kipande cha papai kilichoiva na kuchanganya na kijiko kimoja cha unga wa ngano.
Pakaa sehemu iliyoathirika na kaa nayo kwa muda usiopungua dakika kumi. Mbali na kupaka pia unaweza ukatumia kula kwani lina vitamin E kwa wingi, ambavyo ni muhimu katika ukuaji wa ngozi.
Danzi
Juisi ya tunda hili husaidia katika uzalishaji wa sehemu ya juu ya ngozi 'collagen'. Danzi lina kiwango kikubwa cha vitamini C.  Na kwa kawaida aina hii ya vitamin husaidia kuchochea ukuaji wa ‘collagen’, hivyo kuifanya ngozi yako kunawiri.
Maji
Kunywa maji mengi kwani husaidia kuifanya ngozi yako iwe na unyevu muda wote.
Ikiwa utazingatia zoezi hili mikunjo kati ngozi yako itakuwa ni historia.

Tuesday, November 21, 2017

Ishi kwa Furaha Bila Mpenzi

11/21/2017 02:09:00 AM 0
MAISHA MAPYA  NA YENYE FURAHA BAADA YA KUSALITIWA NA KUVUNJIKA KWA MAHUSIANO….

Leo nitazaungumzia namana gani mtu anaweza kuishi baada ya kuachana  na mpenzi wake au kuvunjika kwa uhusiano. Maisha baada ya mahusiano kuisha yamekuwa magumu sana miongoni mwa watu  ambao tayari walishaonja joto hili kali ya kuumizwa na mapenzi. Kiufupi kwa aliyekuwa ampenda na kudhamiria huumia  sana na huhisi kama hakuna tumaini tena  katika safari ya mapenzi kwa ujumla.



Ulisahawahi pengine kujiapia kuwa siatapenda tena ua hata kufikri kujiua kwaajili ya kusalitiwa ama kuvunjika kwa mahusiano ya mpenzi? Ama ushawahi sikia mtu akisema yeye basi hatopenda tena ama umejisemea mimi mapenzi basi?

Kama jibu ni ndio au ulishwahi kumbana  na maumivu ya kuachwa leo nitakufundisha mbinu kadhhaa ili uwe na furaha tena. Acha kujiapiza hutapenda tena wakati una moyo, acha kulia irejee furaha yako kwa kusoma haya mambo ninayokuandikia hapa. Fanya yafuatayo ili uwe na furaha:

1: Kubaliana na hali halisi: yaani kubali ukweli kuwa mmeshaachana na unatakiwa kuwa huru, kuna watu wameachana ila bado moyoni mwao wameweka mtu ambaye yeye hata hayupo miyoni mwao. Kumbuka ndugu kukabiliana na maji yapande milima ni kazi kubwa sana namaanisha kulazimisha mtu aliyesema muachane ni kazi na ipo siku utakuja kuumia zaidi.

2: Uspendelee kuonana au kuongea na Yule aliyekusaliti: simaanishi msiongee ila kuna wakati mtu anaweza kupata hasira au kujhisi vibaya sana kwa kuendelea kuongea naye. Kuachana na mtu haimaanishi kuwa maadui ila usipende sana kuongelea tena mambo ya mahusianao na mtu ambaye tayari kakusaliti.

3: Pendelea kukaa na marafiki na kujichanganya na watu, hapa ni muhimu pia marafiki wasiwe watu wa kukupa stress au wnaopenda kuzungumzia habari za kauchana na kukucheka, usipende kuwa na marafiki wa aina hii kwani hukatisha tamaa zaidi. Usipende kukaa chumbani pekee kwa kuwa utakuwa ukifikiria sana  na utakuwa na msongo wa mawazo juu ya hilo na kuchukua maamuzi magumu  kama kunywa sumu au hata kukijtia kitanzi. Pia waweza kuwa eleza watu wa muhimu kwako  ili wawe na msaada juu yako kama utashindwa kufanya mambo yako vizuri mfano wazazi au watu auanwaoamini sana.

4: Kubali kusamehe: msamehe na mwache aende ili uwe na fursa nyingine mpya katka  maisha. Roho au moyo usiosamehe huumia zaidi. Ili kuwa na furaha samehe na jisikie huru kabisa. Kwa kutoa msamaha una ruhusu Moyo wako kuwa huru kabisa.

5: Futa kumbukumbu na viashiria vya mtu uliye achana nae, mfano picha au namba za simu nk. Kama kunapicha mlipiga pamoja na zinakufanya ukumbuke mambo Fulani ya nyuma yanayoumiza moyo basi ni vizuri ukazifuta. Wengi huwa hawapendi kuona picha kwakuwa hukumbushia tukio linaloweza kukuumiza zaidi. Waweza kubakiza picha chache zisozo kuumiza, pia jitoe urafiki nae mfano fb kwa kuwa unaweza kuzikuta post zake zikazidi kukuumiza zaidi na zaidi.

 6:Jifunze madhaifu  yako na  maweza yako na kujikubali ulivyo:  jiulize  una mapungufu gani yaliyopelekea kuachana? Je ulikosea wapi ili iwe rahisi kuanza mahusiano mapya! Kumbuka tunajifunza kupitia makosa na kama hujakosea bado hujajifunza kitu. Pia jikubali kuwa wewe unaweza kwaajili ya mahusiano mapya.

7:  Acha kuwaza mtazamo hasi (negative attitude) kuna watu mpaka leo bado anasikitika na kuaona watu wote ni  wasaliti. Huo ni mtazamo mbaya na hufanya mtu asipende tena. Aliye kusaliti ni mmoja tu, usiichukie dunia nzima, wapo wanaoweza kukupenda mpka ukajihisi ni mfalme, kwanini uwachukie wote wakati aliyekusaliati ni mmoja tu? Ama mtu anajiona yeye basi hana bahati nani kasema huna bahati? Acha mawazo potofu na uishi kwa furaha kabisa ukiamini kuwa ipo siku utapendwa zaidi.

8:Baada ya muda pata mpenzi mpya, usikae ukiumia wakati moyo unao, irejesha fuaraha yako kwa kupata mtu mpya uanendana nae. Hutakiwi kukataa ukipendwa tena, mfano, una miaka 20 tu unakata tamaa ya kupata mpenzi tena, je uataweza kuishi miaka 50 bila kuwa na mahusiano? Jibu ni hapana na haiwezekani, hivo haraka iwezekanavo pata mtu mpya kabisa wa kukufanya usahau na usirudie makosa ya kipindi cha nyuma.

*****************NJIA MBAYA WANAZOTUMIA WATU WAKIaCHANA AU UHUSIANO UKIVUNJIKA***************************************

 Kuna watu wanatumia njia zisizofaa kurejesha furaha pindi mahusiano yanapoisha. Njia hizi huwa hatari na huathiri afya ya muhisika na pengine kuathiri maisha yake yote hadi kupelekea kufa. Tafadhali usitumie hizi njia

1: Kunywa pombe na vilevi, unakuta mtu alikuwa hanywi akiachana tu basi anakunywa sana, hilo ni tatizo kwa kuwa ukinywa uta sahau tu, pombe ikiisha unarudi katika hali ya kawaida. Pia unauchosha mwili kwa pombe kali wakati usio wake.

2: Kufanya ngono, mtu akiachana na mpenzi wake basi anakuwa wa moto kweli, mara yuko na huyu mara huyu kama vile anamkomesha aliyeacahana nae! Jua tu unajikomesha Kumbuka kuna magonjwa siku hizi, na pia unauchosha tu mwili wako.

3: Kukataa kula au kula sana, unatakiwa ule kwa afya na ufanyee  mazoezi, usikate kula japo chakula huwa ni kichungu ila jikaze ule tu na uwe na amani. Usile sana kwani huathiri tumbo na mfumo wa kumeng’enya chakula.

4: Kutolala au kulaa sana, hapa utaathiri mwili wako ila lala kawaida tu. Wengine hutumia muda mwingi kuangalia TV au komputa kwa muda mrefu sana.

5: Kujaa hasira na kubwatukia kila mtu, yaani unakuwa mkali kama mbogo , haifai.

6: Kulia lia na kunung’unika sana. Mtu kila siku yeye ni kulia tu, utalia mpka lini rafiki yangu? Kila kitu kina mwisho na ipo siku utapata furaha.

7: kutangaza kila sehemu: mara fb moyo sukuma damu, mara sijui nini ila jua sio kila mtu lazima ajue kuwa umeachika. Pia kutangaza sifa za mtu uliyeachana  nae haifai kabisa….

Mwisho: kuvunjika kwa nyundo hakumanishi mwisho wa uhunzi, nikimaanisha kuachana hakumaanishai huatapenda tena, bado una wakati mzuri kabisa wa kupenda na kuw ana furaha yako katika maisha haya.

Kwa wale wanao waacha wapenzi wao: tambua kuwa chozi la mtu lina thamani sana na ipo siku yatakukuta nawewe pia. Sio vizuri sana kwani hakuna aliyekamilika. Maumivu ya kuachwa na unaempenda ni makali mno na haufanya mtu asiwe na amani tena.
Kwa mnaopendana ni vizuri kudumisha upendo wenu vizuri ili usiumie baadae.
Love is sweet
Love is enjoyable
Love is fantastic : post by Franco Samuel   2017
usiasahu kulike page yetu

Audio