HISTORIA YA SIKU YA VALENTINE...
Ilianzia wapi na dhana yake ni ipi.?
Leo nakusogezea makala hii inayohusu historia fupi ya sikukuu pendwa kabisa kwa wapendanao duniani Valentine. Ungana nami katika makala hii nzuri na ya kukusimua
Sikuku ya Valentine ama sikukuu ya wapendanao chanzo chake hasa ni utawala wa Dola ya Warumi. Ni siku ya kumbukumbu (memo9ria day) na sehemu nyingine ni (festum) maana yake siku kuu ya daraja la kwanza kwa kumkumbuka Padre Valentine aliyeuawa na utawala wa kirumi.
Padre Valentine aliua sababu ya kutetea waumini waweze kufunga ndoa. Katika miaka hiyo kulikuwa na vita kama ilivyokuwa desturi ya falme nyingine ili ziweze kujipanua hivyo ili lazimu mfalme Caldius azuie watu kuoa kwani aliamini askari walio oa hawakuwa wazuri katika vita na wasingeweza kuwa huru kufanya majukumu ya familia na vita. Hata hivyo licha ya zuio hilo la kuwataka vijana wasifunge ndoa na badala yake wajiunge katika jeshi, Padre Valentine bado aliendlea kufungisha ndoa kwa siri..
Akawa anafungisha ndoa kwa siri kwenye makatakombe (mahandaki chini ya kanisa ambako kuna sehemu za ibada kwa watu wachache), alifanya hivyo kwa vile kufunga ndoa hadharani ilikuwa ni kukiuka amri ya wakuu wa dola ya kirumi..
Miaka kadhaa ilienda huku Padre Valentin akifungisha ndoa kwa siri na Baadhi ya watu walifichua siri hiyo, hivyo Padre Valentin alishikwa na dola ya Warumi na kutiwa gerezani akisubiri hukumu ya kifo kwa kukiuka amri ya kutofungisha ndoa..
Inasemekana akiwa gerezani Padre Valentin alimpenda binti kipofu aliyekuwa mtoto wa msimamizi wa gereza alipokuwa amefungwa. Mara kadhaa binti huyo kipofu alihudhuria gerezani ili kumuona padre Valentin. Kwa muda kadhaa padre Valentine alikuwa akimtumia binti salamu akiwa gerezani na ndio dhana ya sikukuu hii..
Baadae padre Valentine alitakiwa kuikana imani yake na kuacha kufungisha ndoa kama dola ya Kirumi ilivyokuwa ikitaka. Lakini kutokana na msimamo wake hakuikana imani yake hivyo A D 270- Valentin aliuawa.
Wakristo wakaweka siku ya kumkumbuka Padre Valentin kama mfia dini sababu ya kutetea maisha ya wanakanisa kwa wanandoa. Ikaenea katika kanisa nchi za magharibi na hata duniani ambako wanakanisa wanamkumbuka Mt. Padre Valentin.
Sikukuu ya Valentine’s: Siku ya mapenzi??
Papa Gelasius aliitangaza rasmi tarehe 14 ya mwezi wa pili kama sikukuu ya mtakatifu Valentine,yaani Valentines day.Miaka michache baadae sikukuu hiyo ilibeba maudhuhi au uzito wa mapenzi zaidi.Kati ya karne ya tano na karne ya kumi na tano, nchini Uingereza na Ufaransa ,iliaminika kwamba tarehe 14 ya mwezi wa pili ilikua ndio mwanzo wa kipindi cha ndege kupandana,hii ilijenga dhana kwamba siku ya sikukuu ya Valentin lazima iwe siku ya kuonyesha mapenzi (romance).Ndio maana ndege hutumika kama alama ya Valentine.
Baadaye ikapokeleka na watu hata wasio na imani ya kikristo kama ni siku ya kufanya kumbukumbu kwa Mt. Valentin kama mtetezi wa Ndoa.
Maudhui ya siku hiyo kwa wasiowanakanisa imechukua maana nyingine ya kwamba ni siku ya wapendanao hata kwa wasio wanandoa ili mradi wanapendana, kitu ambacho ni kinyume cha malengo ya mfia dini Mt. Padre Valentin aliyetaka vijana wafunge ndoa badala ya kuwa na hawara tu (vimada) kama sheria ya Rumi ilivyokuwa ikitaka.
Hata sasa duniani koti watu huadhimisha sikukuu hii kwa kuonesha mapenzi romance kwa wawapendao kwa kuwapa zawadi ikiwemo kadi, maua na chocolate kma ishara ya upendo. Rangi nyekundu ndio hasa hutumika katika sikukuu hii..
Waweza kuona na kudownload kadi nzuri hapa na kumtumia umpendae..
baadhi ya kadi na maua ya Valentine hapa
Na
WhatsApp 255768800687
No comments:
Post a Comment