Showing posts with label Mapenzi. Show all posts
Showing posts with label Mapenzi. Show all posts

Sunday, February 18, 2018

Ukimpenda mtu Mwambie ukweli...

2/18/2018 08:46:00 PM 0
Sema tu Usiogope..

Siku ya kwanza alimkuta akiwa pekee huku akiwa hana furaha. John alijitahidi kumbeleza Sarah na kumfanya atulie. Alifanya hivyo kwa kuwa ukaribu wake na Sarah ulikuwa hauwez kuficha kitu abadini. Kila mmoja  alijua bayana mabadiliko ya mwenzie. Ndio walikuwa marafiki wakushiba, hakuna kilichowatenga mapacha hawa wasiofanana.


Walitembea pamoja. Walikaa pamoja, wakasoma pamoja. Alichokula John lazima Sarah akionje. Ndio mtindo wao wa kuishi. Siku, wiki, miezi  miaka ikaenda, wakakua, wakanawiri na kupendeza. Minong'ono ikaanza, hawa wawili wana kitu sirini...

John alibeba donge zito kooni. Donge la kuwa na hisia kali kwa Sarah. Yamkini aliona kabisa kuwa Sarah alikuwa mtu wake. Ndio alimpenda kimapenzi kwa muda mrefu! Angetoboaje siri ili Sarah ajue? Piga moyo konde, John alipotezea, maswali lukuki yakatiririka katika bongo yake. Nivunje yai? Niseme? Atanionaje? Itakuwaje!.? Akikataa je? Asiponikubalia? Akikasirika?.. Acha tu tuendelee hivi hivi.. Sarah ni rafiki baki kuwa rafiki, akajisemea huku akibeba mfuko wa daftari na kumkuta Sarah nje akimsubiri..

"unawaza nini J wangu? Hujui kuwa wiki ijayo birthday yangu? Usinifanye nikose furaha!"
Sauti ya Sarah haikufua dafu ya kumtoa John katikati ya pori la mawazo. Alimtizama Sarah macho yakongea nakupenda ila moyo ukamsaliti, ubongo  ukazuia usiseme... Akameza funda la mate kwa fujo..

Birthday...
Siku ikafika. John akawa na wakati mgumu ampe zawadi gani. Kila alichofikiri hakuona kama kitakuna moyo wa Sarah. Aliona kila kitu kigumu .. Mwishowe akamua kiume  akapita dukani na kununua ua zuri.. Red rose.. Yes lilikua ua jekundu la ghali  akalihifadhi vema. Alifika nyumbani na kulipulizia perfume yake nzuri. Akalifunga vema na kuelekea kunako pati...

Ndani ya party...
Kila kitu kilifana, tabasumu zilitokeza katika kila uso uliokuwako ndani ya ukumbi. Keki ikaletwa. Wakala vyakula vya kila aina na vinywaji. Muda ukafika Mc akagawa vikadi fulani. John alistuka kupata kadi ikiwa imeandikwa 1. Akiwa anasubiri maelezo mara Mc akang'aka kwa bashasha.
"Namba moja popote ulipo simama na zawadi njoo kwa mtoto aliyezaliwa leo, utampa zawadi na kucheza nae. Atakutambulisha hapa, tafadhali mheshimiwa inuka"

John akasimama kwa uoga, hakuamin, akatembea pole  alifika mbele ya Sarah akapokelewa kwa kumbatio murua lililoambata na busu zito katika paji la uso.. Mwili ukamzizima, moyo ukaagana na mwili kusawiri mapigo yake. Akatoa zawadi akacheza nae ziro distance.. Kitu murua, akatamani aseme, nafsi ikamhukumu kwa maamuzi yake, akausaliti moyo wake.. Akatambulishwa kwa kimombo He is my everything, he is my best friend.. Akarudi kukaa...part ikaisha, siku zikaenda wakashibana kama kumbikumbi..

Miaka ikaisha na miezi kenda.. Mficha maradhi kifo humuumbua akajisemea John.. Bado walikuwa zaidi ya marafiki. Safari hii wakiwa chuo. Ndio walisoma pamoja hadi chuo. Kila mtu akimuangalia mwenzake anaonekana ana kitu cha zaidi ya urafiki. Nani abomoe ukuta huu wa urafiki uliojengwa kwa zege zito na kwa muda wa miaka mingi? Nani angeanza, si John wala Sarah, wote walimeza gundi, wakatulia tuli kama maji mtungini wakisaliti mahitaji ya moyo na nafsi. John aliusulubu moyo wake zaidi hasa alipomkuta Saraha akiwa na mwanaume mwingine, wivu ulipenya na kuganda ndani ya moyo kama barufu.. Akawa muoga, akihofia kupigwa kete na wajanja wa mjini..

Mwaka wa tatu chuo..
Miaka nayo ikasonga, wakazidi kuwa wakubwa. Kila mmoja akificha. Wakahitimu masomo yao kwa ufaulu wa kishindo. Ilikuwa furaha kwao. Siku ya mahafali ikafika. Safari hii John alidhamiria na kuuapisha moyo wake kuwa lazima aseme. Ndio afunguke kuwa ana mapenzi mubashara na mujarabu juu ya Sarah  rafiki wake kipenzi.. Alijiapiza kutotenda kosa tena.. Yes alijisemea: moyo usisaliti nafsi na nasfi isisaliti ubongo na ubongo uamrishe mdomo umwambie Sarah maneno haya sita, NAKUPENDA SANA SARAH, NAOMBA NIWE WAKO... John alifanya mazoezi namna ya kusema akajiridhisha na kuona ya kuwa kila kitu ni chema, akavaa suti akapendeza akaenda kunako mahafali...

Dakika 15....
Sekunde dakika masaa yakasogea,baada ya mahafali kuisha! Wakapiga picha pamoja  na ndugu jamaa na marafiki. Hakuna aliyeficha hisia zake kibindoni. Kila mtu alionesha mapenzi na mbwembwe kede kede.. Naam ilikuwa kama mashindano...

John na dhamira yake huku akitetemeka akamshika mkono Sarah na kumpeleka sehemu bustani ya maua ya kuvutia. Akamkumbatia. Akamsogeza Sarah karibu wakatazamana kwa macho ya huba... Macho yakaongea.. Moyo ukapaa kwa mapigo, dakika tano sasa zilipita, hakuna aliyesema neno. Ila mioyo ikasema kwa kundunda kama watu waliopanda mlimaa kwa kukimbizwa. Joto la mwili likapanda haraka, macho ya Sarah yakajifumba.. Akabakia John mdomo ukitetemeka... Akaufungua sasa dakika ya 10....akauelekeza sikioni mwa Sarah...
NAKUPENDA SANA SARAH, NAOMBA NIWE WAKO... ndio alisema kwa usahihi bila kukwama. Maneno yake sita...

Maneno haya yalisikiwa na kupenya vema katika ngoma za masikio ya Sarah na kumfanya afumbue macho yake. Akamkumbatia zaidi John, akamwangalia vema. Ukimya ukatanda, John akaanza kujawa na woga. Nafsi ikamsuta moyo ukamhukumu, bora ningesubiri, akateta na ubongo wake...

Kimya, kimya kikatanda, kimya dakika ya15,
 Sarah akamgeukia John kimahaba akasema..
NILIKUSUBIRI USEME, I LOVE YOU JOHN!... Maneno yake sita yakaponya msononeko wa John, yakatibu msokoto wa tumbo uliokuja ghafula ndani ya dakika tano, Cameraman akatokea akapiga picha wakiwa wamekumatiana.. Wakaondoka zao wakikokotana kimahaba mara busu, mara hug, mara John akambeba Sarah mpaka chumbani. Aliweza licha ya Sarah kuwa na uzani mkubwa, wabwagana katika samani, kazi ya mikono ya seremala.. Dakika moja mbele .. Camera na taa vikazimwa.. Giza... *************

Morales....
Urafiki uliodumu kwa miaka mingi ni mgumu kuugeuza kuwa uhusiano wa kimapenzi

Ukimpenda mtu sema mapema, kuna wakati ukishampoteza harudi tena

Kukaa kimya kutakufanya upoteze mtu wa ndoto zako...

Ukimpenda sema tu....

Created by King Franco Samuel

Kindly share
Comment

Tuesday, February 13, 2018

Historia ya Valentine Day. Siku ya wapendanao

2/13/2018 09:53:00 AM 0
HISTORIA YA SIKU YA VALENTINE...
Ilianzia wapi na dhana yake ni ipi.?
Leo nakusogezea makala hii inayohusu historia fupi ya sikukuu pendwa kabisa kwa wapendanao duniani Valentine. Ungana nami katika makala hii nzuri na ya kukusimua

Sikuku ya Valentine ama sikukuu ya wapendanao chanzo chake hasa ni utawala wa  Dola ya Warumi. Ni siku ya kumbukumbu (memo9ria day) na sehemu nyingine ni (festum) maana yake siku kuu ya daraja la kwanza kwa kumkumbuka Padre Valentine aliyeuawa na utawala wa kirumi.

Padre Valentine aliua sababu ya kutetea waumini waweze kufunga ndoa. Katika miaka hiyo kulikuwa na vita kama ilivyokuwa desturi ya falme nyingine ili ziweze kujipanua  hivyo ili lazimu mfalme Caldius azuie watu kuoa kwani aliamini askari walio oa hawakuwa wazuri katika vita na wasingeweza kuwa huru kufanya majukumu ya familia na vita. Hata hivyo licha ya zuio hilo la kuwataka vijana wasifunge ndoa na badala yake wajiunge katika jeshi, Padre Valentine bado aliendlea kufungisha ndoa kwa siri..

Akawa anafungisha ndoa kwa siri kwenye makatakombe (mahandaki chini ya kanisa ambako kuna sehemu za ibada kwa watu wachache), alifanya hivyo kwa vile kufunga ndoa hadharani ilikuwa ni kukiuka amri ya wakuu wa dola ya kirumi..

Miaka kadhaa ilienda huku Padre Valentin akifungisha ndoa kwa siri na Baadhi ya watu walifichua siri hiyo, hivyo Padre Valentin alishikwa na dola ya Warumi na kutiwa gerezani akisubiri hukumu ya kifo kwa kukiuka amri ya kutofungisha  ndoa..
Inasemekana akiwa gerezani Padre Valentin alimpenda binti kipofu aliyekuwa mtoto wa msimamizi wa gereza alipokuwa amefungwa. Mara kadhaa binti huyo kipofu alihudhuria gerezani ili kumuona padre Valentin. Kwa muda kadhaa padre Valentine alikuwa akimtumia binti salamu akiwa gerezani na ndio dhana  ya sikukuu hii..

 Baadae padre Valentine alitakiwa kuikana imani yake na kuacha kufungisha ndoa kama dola ya Kirumi ilivyokuwa ikitaka. Lakini kutokana na msimamo wake hakuikana imani yake hivyo  A D 270- Valentin aliuawa.

Wakristo wakaweka siku ya kumkumbuka Padre Valentin kama mfia dini sababu ya kutetea maisha ya wanakanisa kwa wanandoa. Ikaenea katika kanisa nchi za magharibi na hata duniani ambako wanakanisa wanamkumbuka Mt. Padre Valentin.

Sikukuu ya Valentine’s: Siku ya mapenzi??
Papa Gelasius aliitangaza rasmi tarehe 14 ya mwezi wa pili kama sikukuu ya mtakatifu Valentine,yaani Valentines day.Miaka michache baadae sikukuu hiyo ilibeba maudhuhi au uzito wa mapenzi zaidi.Kati ya karne ya tano na karne ya kumi na tano, nchini Uingereza na Ufaransa ,iliaminika kwamba tarehe 14 ya mwezi wa pili ilikua ndio mwanzo wa kipindi cha ndege kupandana,hii ilijenga dhana kwamba siku ya sikukuu ya Valentin  lazima iwe siku ya kuonyesha mapenzi (romance).Ndio maana ndege hutumika kama alama ya Valentine.

Baadaye ikapokeleka na watu hata wasio na imani ya kikristo kama ni siku ya kufanya kumbukumbu kwa Mt. Valentin kama mtetezi wa Ndoa.

Maudhui ya siku hiyo kwa wasiowanakanisa imechukua maana nyingine ya kwamba ni siku ya wapendanao hata kwa wasio wanandoa ili  mradi wanapendana, kitu ambacho ni kinyume cha malengo ya mfia dini Mt. Padre Valentin aliyetaka vijana wafunge ndoa badala ya kuwa na hawara tu (vimada) kama  sheria ya Rumi ilivyokuwa ikitaka.



 Hata sasa duniani koti watu huadhimisha sikukuu hii kwa kuonesha mapenzi romance kwa wawapendao kwa kuwapa zawadi ikiwemo kadi, maua na chocolate kma ishara ya upendo. Rangi nyekundu ndio hasa hutumika katika sikukuu hii..

Waweza kuona na kudownload kadi nzuri hapa na kumtumia umpendae.. 
baadhi ya kadi na maua ya Valentine hapa































Na
WhatsApp 255768800687

Tuesday, November 21, 2017

Ishi kwa Furaha Bila Mpenzi

11/21/2017 02:09:00 AM 0
MAISHA MAPYA  NA YENYE FURAHA BAADA YA KUSALITIWA NA KUVUNJIKA KWA MAHUSIANO….

Leo nitazaungumzia namana gani mtu anaweza kuishi baada ya kuachana  na mpenzi wake au kuvunjika kwa uhusiano. Maisha baada ya mahusiano kuisha yamekuwa magumu sana miongoni mwa watu  ambao tayari walishaonja joto hili kali ya kuumizwa na mapenzi. Kiufupi kwa aliyekuwa ampenda na kudhamiria huumia  sana na huhisi kama hakuna tumaini tena  katika safari ya mapenzi kwa ujumla.



Ulisahawahi pengine kujiapia kuwa siatapenda tena ua hata kufikri kujiua kwaajili ya kusalitiwa ama kuvunjika kwa mahusiano ya mpenzi? Ama ushawahi sikia mtu akisema yeye basi hatopenda tena ama umejisemea mimi mapenzi basi?

Kama jibu ni ndio au ulishwahi kumbana  na maumivu ya kuachwa leo nitakufundisha mbinu kadhhaa ili uwe na furaha tena. Acha kujiapiza hutapenda tena wakati una moyo, acha kulia irejee furaha yako kwa kusoma haya mambo ninayokuandikia hapa. Fanya yafuatayo ili uwe na furaha:

1: Kubaliana na hali halisi: yaani kubali ukweli kuwa mmeshaachana na unatakiwa kuwa huru, kuna watu wameachana ila bado moyoni mwao wameweka mtu ambaye yeye hata hayupo miyoni mwao. Kumbuka ndugu kukabiliana na maji yapande milima ni kazi kubwa sana namaanisha kulazimisha mtu aliyesema muachane ni kazi na ipo siku utakuja kuumia zaidi.

2: Uspendelee kuonana au kuongea na Yule aliyekusaliti: simaanishi msiongee ila kuna wakati mtu anaweza kupata hasira au kujhisi vibaya sana kwa kuendelea kuongea naye. Kuachana na mtu haimaanishi kuwa maadui ila usipende sana kuongelea tena mambo ya mahusianao na mtu ambaye tayari kakusaliti.

3: Pendelea kukaa na marafiki na kujichanganya na watu, hapa ni muhimu pia marafiki wasiwe watu wa kukupa stress au wnaopenda kuzungumzia habari za kauchana na kukucheka, usipende kuwa na marafiki wa aina hii kwani hukatisha tamaa zaidi. Usipende kukaa chumbani pekee kwa kuwa utakuwa ukifikiria sana  na utakuwa na msongo wa mawazo juu ya hilo na kuchukua maamuzi magumu  kama kunywa sumu au hata kukijtia kitanzi. Pia waweza kuwa eleza watu wa muhimu kwako  ili wawe na msaada juu yako kama utashindwa kufanya mambo yako vizuri mfano wazazi au watu auanwaoamini sana.

4: Kubali kusamehe: msamehe na mwache aende ili uwe na fursa nyingine mpya katka  maisha. Roho au moyo usiosamehe huumia zaidi. Ili kuwa na furaha samehe na jisikie huru kabisa. Kwa kutoa msamaha una ruhusu Moyo wako kuwa huru kabisa.

5: Futa kumbukumbu na viashiria vya mtu uliye achana nae, mfano picha au namba za simu nk. Kama kunapicha mlipiga pamoja na zinakufanya ukumbuke mambo Fulani ya nyuma yanayoumiza moyo basi ni vizuri ukazifuta. Wengi huwa hawapendi kuona picha kwakuwa hukumbushia tukio linaloweza kukuumiza zaidi. Waweza kubakiza picha chache zisozo kuumiza, pia jitoe urafiki nae mfano fb kwa kuwa unaweza kuzikuta post zake zikazidi kukuumiza zaidi na zaidi.

 6:Jifunze madhaifu  yako na  maweza yako na kujikubali ulivyo:  jiulize  una mapungufu gani yaliyopelekea kuachana? Je ulikosea wapi ili iwe rahisi kuanza mahusiano mapya! Kumbuka tunajifunza kupitia makosa na kama hujakosea bado hujajifunza kitu. Pia jikubali kuwa wewe unaweza kwaajili ya mahusiano mapya.

7:  Acha kuwaza mtazamo hasi (negative attitude) kuna watu mpaka leo bado anasikitika na kuaona watu wote ni  wasaliti. Huo ni mtazamo mbaya na hufanya mtu asipende tena. Aliye kusaliti ni mmoja tu, usiichukie dunia nzima, wapo wanaoweza kukupenda mpka ukajihisi ni mfalme, kwanini uwachukie wote wakati aliyekusaliati ni mmoja tu? Ama mtu anajiona yeye basi hana bahati nani kasema huna bahati? Acha mawazo potofu na uishi kwa furaha kabisa ukiamini kuwa ipo siku utapendwa zaidi.

8:Baada ya muda pata mpenzi mpya, usikae ukiumia wakati moyo unao, irejesha fuaraha yako kwa kupata mtu mpya uanendana nae. Hutakiwi kukataa ukipendwa tena, mfano, una miaka 20 tu unakata tamaa ya kupata mpenzi tena, je uataweza kuishi miaka 50 bila kuwa na mahusiano? Jibu ni hapana na haiwezekani, hivo haraka iwezekanavo pata mtu mpya kabisa wa kukufanya usahau na usirudie makosa ya kipindi cha nyuma.

*****************NJIA MBAYA WANAZOTUMIA WATU WAKIaCHANA AU UHUSIANO UKIVUNJIKA***************************************

 Kuna watu wanatumia njia zisizofaa kurejesha furaha pindi mahusiano yanapoisha. Njia hizi huwa hatari na huathiri afya ya muhisika na pengine kuathiri maisha yake yote hadi kupelekea kufa. Tafadhali usitumie hizi njia

1: Kunywa pombe na vilevi, unakuta mtu alikuwa hanywi akiachana tu basi anakunywa sana, hilo ni tatizo kwa kuwa ukinywa uta sahau tu, pombe ikiisha unarudi katika hali ya kawaida. Pia unauchosha mwili kwa pombe kali wakati usio wake.

2: Kufanya ngono, mtu akiachana na mpenzi wake basi anakuwa wa moto kweli, mara yuko na huyu mara huyu kama vile anamkomesha aliyeacahana nae! Jua tu unajikomesha Kumbuka kuna magonjwa siku hizi, na pia unauchosha tu mwili wako.

3: Kukataa kula au kula sana, unatakiwa ule kwa afya na ufanyee  mazoezi, usikate kula japo chakula huwa ni kichungu ila jikaze ule tu na uwe na amani. Usile sana kwani huathiri tumbo na mfumo wa kumeng’enya chakula.

4: Kutolala au kulaa sana, hapa utaathiri mwili wako ila lala kawaida tu. Wengine hutumia muda mwingi kuangalia TV au komputa kwa muda mrefu sana.

5: Kujaa hasira na kubwatukia kila mtu, yaani unakuwa mkali kama mbogo , haifai.

6: Kulia lia na kunung’unika sana. Mtu kila siku yeye ni kulia tu, utalia mpka lini rafiki yangu? Kila kitu kina mwisho na ipo siku utapata furaha.

7: kutangaza kila sehemu: mara fb moyo sukuma damu, mara sijui nini ila jua sio kila mtu lazima ajue kuwa umeachika. Pia kutangaza sifa za mtu uliyeachana  nae haifai kabisa….

Mwisho: kuvunjika kwa nyundo hakumanishi mwisho wa uhunzi, nikimaanisha kuachana hakumaanishai huatapenda tena, bado una wakati mzuri kabisa wa kupenda na kuw ana furaha yako katika maisha haya.

Kwa wale wanao waacha wapenzi wao: tambua kuwa chozi la mtu lina thamani sana na ipo siku yatakukuta nawewe pia. Sio vizuri sana kwani hakuna aliyekamilika. Maumivu ya kuachwa na unaempenda ni makali mno na haufanya mtu asiwe na amani tena.
Kwa mnaopendana ni vizuri kudumisha upendo wenu vizuri ili usiumie baadae.
Love is sweet
Love is enjoyable
Love is fantastic : post by Franco Samuel   2017
usiasahu kulike page yetu

Kwanini Wapenzi Wanaachana?

11/21/2017 02:03:00 AM 0
KUACHANA NA MPENZI WAKO AU MCHUMBA

Kuvunjika kwa uhusiano au kusalitiana baina ya wapendanao kimekuwa kitu cha kawaida sana siku hizi. Angalabu zaid ya asilimia 95% ya vijana wamekumbwa au walishawahi kukumbwa na kisanga hiki. Kiufupi kusaliatiana au kuacha katika uhusiano ni jambo baya sana kwa kuwa hakuna mtu mjinga anaye anzisha mahusiano  na mtu pasi  na malengo.

Vijana wengi kwa sasa wanaumwa ugonjwa kitaalamu  unaitwa “LOVE CONCUSION” yaani kutokana na kusalitiwa basi wanaogopa sana kuwa na mahusiano ama hawawi na imani tena pindi wawapo na mahusiano kwa mara nyingine.  Hili ni tatizo kubwa sana na linahitaji muda kulijadili…

TATIZO LIKO WAPI? KIPI KINSABABISHA?
Kuna mambo mengi  sana yanayosabababisha uhusiano wa wapendanao kuvunjika. Leo mwalimu wako nitakufunza machache ili udumishe uhusiano wako na kama basi yamekukuta uone namna gani ya kuishi upya ukirekebisha pale ulipo kosea…karibu…

1: AHADI, katika mahusiano  ahadi hutawala sana, mara nitakununulia gari, mara nyumba kimala mara masaki. Mara nitakuoa, au lazima niolewe na wewe! Hatukatai ila angalia kabala ya kutamka utaweza kutekeleza? Pia kuna kipindi ambapo watu hulewa sana mapenzi na kujikuta unatoa ahadi usizoweza hasa wanaume..mwisho wa siku yanakushinda unajikuta unaliaa…NOTE “KAMWE USITOE AHADI UKIWA NA FURAHA SANA” kwa kuwa utaongea hata usivo weza kutekeleza. Toa ahadi ukiwa katika hali ya kawaida mno..

2: Aina ya mahusiano na Umri: katika vitu vinavyo umiza ni pamoja na kuwa na uahusiano na mtu katika umri ambao bado akili haija pevuka. Yaani bado hujabalehe kisawasawa ukajua kutofautisha kati ya kupenda na tamaa na hisia za mwili. Unakuta mtu alimpenda mtu wakiwa wadogo mno maybe miaka 16 wakikua na kufika 23 anaona vizuri zaidi mwisho ana achana na mchumba wake ambaye wametoka  naye mbali, umri sahihi kwa mwanaume kutulia na kuanzia22  so usione kwanini wanaachana kozi umri ni tatizo. Kama hujakua vizuri acha hizo, wazuri wapo na mahendsome wapo, unawahi nini?

3: Kipi kilikuvutia na mlianzishaje Mahusiano: unakuta watu wakati wanaanza walikuwa wanapendana sana simu kila dakika, kutembeleana kila mara, wameshikana mikono kama kumbikumbi, leo usipomshika mkono lazima ajiulize kwanini? Usipopokea simu lazima ajiulize kwann? Usipotembea nae barabarani lazima ajiulize kwanini? So usiigize tabia kuwa wewe ni mwema sana, onesha tabia yako halisi ili mtu akujue mapema, kuigiza tabia mpka lini?, ndio hapo mwisho mtu akigundua anakuacha. Ulipendelea kuhonga sana endelea kuhonga si ulimdekeza kama hutatoa jua wengine watahonga maana ndio ulimdekeza hivo…

4: Umbali na mpenzi wako: hapa ndio penye tatazo kwa macho yakinifu, uko Mwanza jamaa yuko huko Peramiho Songea. Siwakatishi tamaa ila kuna mtu alishwahi sema “ni Waafrika wachache  sana wanaweza Far love” yaani mapenzi yambali. Kwahiyo kama unataka kuoa hakikisha upo karibu na mpenzi waka au kama upo mbali basi mtembelee kila mara laasivyo ujue tu mambo yataharibika. Ukikaa na mtu karibu kwa mda mrefu hata km ni rafiki tu unajikuta kuna upendo flani ambao mwisho wa siku unaleta mapenzi kabisa so akiwa mbali ndio hivyo tena. Muombe Mungu mwema na kuwa na imani nae hakika subra ndiyo ushindi..  

5: Matumizi ya Simu na Mitandao ya kijamii: hapa pameleta kiza zaa kwa watu wengi. Je huwa unaichunguza simu ya mpenzi au mchumba wako? Je unafuatilia post maybe insta, wasap, fb nk? Kma jibu ni ndiyo  basi upo hatarini na kama jibu ni hapana  basi uko salama ila SI SALIMINI! Simu zinadanganya sana watu, yaani unaongea nae saa 2 anakwambia “bebi nimchoka nalala mwaa”! Nenda fb online, wasap online, insta ndio anapest saa 7 usiku, hilo jipu jua tu yupo ANAYE MUWEKA ONLINE ndio maana akakwambia  analala. Usijidanganye, simaanishi ukavuruge uhusiano kwa kuwa online mpaka saa 8 ila kuwa makini, hata mbuyu ulianza kama mchicha…..

6: Tabia za kuiga, wengi sana wanalia baada ya kuachana na wapenzi waliowapenda kwa dhati kisa wameiga na kujikuta katika hali ngumu. Kwanini uige kisa Fulani kasema hiki au kafanya hiki? Kuwa na wapenzi wangi sio kitu na wala sio ustaarabu kabisa, sasa utasikia nakuwaje nae mmoja akiniacha je?  hapo mimi pia sina jibu ila tuache kuiga tabia fulani zitakazo pelekea kuvunjika uhusiano, unakuta mtu alipendwa akiwa na kipara na anavaa nguo za kawaida, baada ya muda mara sijui vimini mara visuruali vya ajabu ajabu, kama mtu hakukuta katika hayo na hapendi basi acha, usiige fasheni itakuachanisha na mtu wa muhimukwako…

7: Kupenda vya Mteremko, hapa wanaume wengi imewaumiza sana kwa kuachwa, kwa kuwa hawaa pesa na unakuta binti alie nae anataka vitu vya bei ila tambua penzi la kweli latoka moyoni si pesa. Kwa kuwa mvulana hana basi atasemwa kila neno mwisho ATAKA TAMAA. Ewe binti, mwanaume bora ni Yule uanyeanza nae AKIWA HANA KITU. Hao wenye  pesa watakutumia tu wakuache kama TAMABARA bovu lisiliafaa hata kwa kudekia. Leo hii unamwacha mchumba anayekupenda kisa mwanaume mwenye pesa utaolewa kama mke wa tatu jidanganye, endelea kujidanganya utajuta sana. Mwanume hangaika utafanikiwa na anayekukacha kisa masikini muombee heri tu aendako…ila akirudi utajua wewe umsamehe au laa!!!!!!!!!!!!!!

Mwisho, kuvunjika kwa uhusianao ama kuachana ni kitu kibaya sana, tumeshudia watu wakijiua, wakiwa machizi na wakfeli mitahani na kuwa na vusasi moyoni ! Kwanni turudishane nyuma kwa tamaa tu? Ewe binti, ewe kijna hakuna mpenzi  bora ZIDI YA HUYO ULIYE NAYE, hebu vumilia na utaona raha. Kma unapendwa pendeke na kama UMESALITIWA POLE. Dunia siyo mbaya walimwengu ni wabaya. Na ewe binti au kijana unayeharibu mahusiano ya wengine  basi jua kuwa ipo siku tu na wewe utapenda na Yule uliempenda atatwaliwa na wengine. 
Tukumbuke Kumshrikisha Mungu kwakuwa kila chema kimeumbwa na yeye. Pia ni mhimu mno kuwa karibu na mpenzi wako mkawa mnasali pamoja na kumuomba Mungu awasaidie ili baadae muwe baba na mama….

Pole kwa wale wenye maumivu na makovu ya kuvunjika kwa uhusiano, usijali mwingine  yupo kwaajili yako ….

Well said
#want_see_you_change_everyday
Franco Samuel

Monday, November 13, 2017

KISA HIKI KITAKUTOA MACHOZI

11/13/2017 06:57:00 PM 0
James akimfukuzia mkewe mtarajiwa Ester kabla ya ajali. Picha kwa Hisani ya Mtandao

Siku ya harusi ikafika. Kila mmoja akawa makini kufuatilia nini kitatokea. Ndugu hasa wa upande wa familia ya kiume kwa akina James wakawa makini wakiwa wanafuatilia mwana wao James atafanya nini baada ya ushauri wa muda mrefu kuwa mtu aliyempenda hakuwa sahihi kwake.

Mawifi na mashemeji wote hawamkubali kabisa mke mtarajiwa wa James binti Ester isipokuwa mtu mmoja tu nae ni mjomba wake James. Huyu alimtia James moyo kuwa harusi ingefanyika na angemuoa mtu wa ndoto zake Ester.
Masaa yakapita, dakika zikaenda bila Ester kutokea kanisani kwenye harusi kutoka huko saloon alikokuwa akipambwa. James woga ukamuingia,  akawaza sana. Akaomba simu yake toka kwa msimamizi wake na kumpigia mkewe mtarajiwa. Muda wote huo wazazi mawifi na wengine walikuwa wakifurahi kuona Ester hatokei wakijua adhima yao ya kumzuia James asimuoe imetia.

Alimpigia simu ikaita bila kupokelewa. Akilli yake ikaanza kuchanganyikiwa, moyo ukajikunyata kwa machungu,  chozi likamlenga mwanaume.
"kapatwa na nini huyu, mbona tulikubaliana leo lazima tufunge ndoa yetu?  Ina maana kaamua kuniacha na kunitia aibu dakika za mwisho. Mungu nipe wepesi katika hili,  natia aibu mie." alijisemea James baada ya simu kutopokelewa.

Wakati huo muda wa kuanza ibada ulikaribia mno. James alitazama saa yake akaona hakuna muda kabisa. Akapiga simu tena. Safari hii ikapokelewa na bi harusi mtarajiwa Ester na kwa sauti ya huzuni akasema
"James mpenzi wangu Nakupenda sana na moyo wangu uko kwako,  nasikitika sana kukataliwa kwenu. Mwanzoni nilijipa moyo kuwa yataisha,  nikwambie siwezi kuvumila matusi ya mawifi kuwa mimi masikini na sio msomi hivyo siwezi kuwa nawe.

Nimevumilia sana ila nimeshindwa. Siwezi kujiingiza katika ndoa ambayo hakuna hata mmoja aliyeupande wangu. Hakuna hata anayeniona kama mtu. Hata nikiolewa nawe nani atanisaidia?  Nani atapiga nami story!?  Nani atanifariji nikiumwa! James nakupenda sana,  tafadhali chakula na sherehe iliyoandaliwa itakuwa kwaajili ya msiba wangu kwa heri na nakutakia maisha mema hapa duniani.!  Aliongea Ester na kukata simu hima. James alichangayikiwa sana. Alitimua mbio na kuanza safari kwenda kule saloon. Alifika pale akambiwa Ester aliongoza njia kuelekea barabarani kwa sharti la kutaka mtu yeyote asimfuate. James aliacha gari na kuanza  kuongoza barabara, mbele kidogo alimuona mkewe mtarjiwa na kumwita..
"Ester Ester usinikimbie tafadhali.... "
Ester kusikia vile aligeuka huku akikimbia, akajikwaa na kudondoka barabarani na kwa bahati mbaya gari likamgonga akapoteza fahamu pale pale. James akaubeba mwili na kuuweka kando huku akilia sana, watu walikusanyika  Tayari na wazazi nao walifika. Alichukua pete yake mfukoni na kumvika Ester aliyekuwa akivuja damu maeneo ya kichwani
"Ester mke wangu,  nakupenda nakuvika pete hii ishara ya upendo wangu kwako. Iwe ishara ya uaminifu wangu kwako, Katika shida na raha mpaka kifo kitutenge. " alisema na kumvika Ester pete kidoleni kisha akaunyanyua mwili na kupakia kwenye gari kupeleka hospital. Walipokelewa na kupelekwa moja kwa moja ICU, madaktari wakatumia juhudi na uwezo wao kumtibu ili  kuokoa maisha ya binti Ester.  Masaa matatu baadae, daktari alimwita James na kumweleza kitu
"Mwanangu,  tumejitahidi sana kwa uwezo wetu. Tumefanya kila lililo ndani ya uweo wetu ila  Mungu ni mkuu siku zote. James mwanangu Ester hatunaye tena duniani, pole sana katika hili"
James alilia sana. Akaingia ndani kwenye chumba ulipokuwa mwili wa Ester akaubusu uso wake, akabusu na kidole chenye pete. Akauangalia mwili na  kulia sana.
Akatoka nje na kuanza kutabasamu huku watu wengine wakillia na kumshangaa. Mjomba wake akamuuliza nini maana ya kucheka na kutabasamu wakati wa msiba wa  mtu aliyempenda.. James kwa sauti akaongea
"Kipindi chote tumekataliwa nilikuwa nikilia na kuomboleza ili mtukubalie na kuturuhusu tuoane. Mke wangu Ester alikuwa akilia na kuumia pia. Tumekuwa watu wa kuumia mioyo kwa kukataliwa. Sasa nimeshinda. Nimemvika pete mke wangu nashukuru sana Mungu mwema kwa kulifanikisha hilo.
Mke wangu Ester pumzika kwa amani. Nakupenda sana,  pumzika mateso ya dunia ni mengi, Mungu akipenda tutaona. Nyie wanafiki mwalilia nini? Mwamlilia mtu mliyemkataa?  Ana thamani gani gani kwenu?  Nadhani huu ni muda wa kupongezana na kufanya sherehe ya ushindi ya kuhakikisha mimi siiishi na Ester. Ndio mfurahi, dada zangu mnalilia nini, ni wakati wenu kushangilia ushindi"

alimalizia kuongea na kupanda gari kwenda nyumbani. Msiba ukarudi nyumbani ila James muda wote akawa mtu wa kufurahi tu, hakulia tena. Ester akazikwa,  James akafanya sherehe na hakuoa tena..

Funzo
..Usipende sana kuzuia wapendanao
.. Heshimu maamuzi ya mtu kuhusu kuoa ama kuolewa..
.. Usiwe muuaji wa ndoto na malengo ya wengine,  jiulize hadi sasa umeua ndoa ngapi!? Umefanya wangapi wasioane kwa msimamo usio na maana?
... Kijana ukipenda shikilia msimamo wako nawe utakuwa imara kam jabari.
..Mali, usomi,  pesa na utajiri sio mapenzi,  ila vipo kunogesha mapenzi. Usiegemee mali au usomi katika mahusiano..
tumia sekunde kadhaa kuomba hii sala.
"Ee Mungu mwema mwenye Enzi Kuu, unisaidie nipate hitaji la moyo wangu. Nipate kile ulichonipangia,  nifanikiwe katika ndoa yangu na mahusiano yangu na kuwaambisha watesi wangu.
Ni wewe liyeumba mahusiano unisaidie nipate na kuvikabili vikwazo vyote, kwani kila lililo jema na lenye neema latoka kwako Mungu,  Amina"
Love is beautiful
Love is powerful
Love is invincible and wicked
Marriage is blessing from God ..
Share..
#wants_to_see_you_change_everday..

Simulizi fupi: USIMDHARAU USIYEMJUA

11/13/2017 06:45:00 PM 0

Soma simulizi fupi ya kusisimua
 "Usimdharau usiyemjua undani wake"
 

Msichana mmoja alikuwa amempenda kijana mmoja mtanashati na mcha Mungu.. Malengo yao ilikua waje kuoana baada ya muda. Kijana huyu alijitoa sana kwa binti huyu
hadi wenzie wakamuona mjinga, lakini ukweli ni kuwa alimpenda msichana yule
kwa dhati. Alimtafutia kazi alipomaliza chuo, alimshauri kuhusu mipango ya maisha na alikua akimuombea kila  alipopata nafasiya kuomba.
 

Siku moja binti alikua anasherehekea siku yake ya kuzaliwa...hivyo akaalika marafiki zake, na watu wengine muhimu akiwemo mpenzi wake. Wageni wote walifika kwa wakati isipokua yule kijana alichelewa kidogo... Hivyo msichana akatumia muda ule ambao mpenzi wake hajafika kuwaeleza wageni  namna yule kijana alivyokua wa muhimu kwake..

Akamsifia sana, akasema atamvalishapete ya uchumba soon, na akasema siku hiyo ya birthday yake anategemea zawadi kubwa sana kutoka kwa huyo mpenzi wa nafsi yake.

Baadae kijana akaingia na kuketi high table.. Muda wa zawadi ulipofika watu wakamtunza binti zawadi mbalimbali na kijana akawa wa mwisho... Hivyo wageni wote wakawa na hamu ya kutaka kujua zawadi aliyoleta hasa baada ya yule msichana kumsifia sana.

Kijana akaamka na kutoa mfuko.. kila mtu akataka kujua kilichokua ndani ya mfuko..mara kijana akafungua mfuko na kutoa mkate..!!Lahaula... watu wote wakastaajabu..mkate??? Lakini kabla hajasema lolote kuhusu ule mkate, yule msichana akaanza kulia.. akapandwa hasira kwa kuwa mpenzi wake amemuaibisha..!!Akiwa analia kwa kwikwi, akamkwida shati na kumvua tai yake, akamwagia juisi, kisha akauchukua ule mkate na kuutupa.!!

Maskini..yule kijana akaukimbilia ule mkate na kuuokota.. Kisha akarudi hightable na kusema "baby nakushukuru kwa yote..Huenda umenidharau kwa kuwa nimekuletea zawadi hii ndogo kwenye siku yako muhimu kama hii. Lakini kamaungetambua thamani ya zawadi hii,usingefanya haya.."

Kisha akafungua ule mkate na kutoa vituviwili alivyoficha ndani ya mkate.. Kwanza akatoa ufunguo wa gari, ambalo alikuwa amemnunulia mpenzi wake na alitaka amkabidhi siku hiyo ya birthday. Kisha akatoa pete ya uchumba na kusema
"Nilimuomba Mungu anipe mwanamke atakayenipenda katika hali yoyote. Nilipanga leo nikuvalishe pete hii ili kuelekea ndoto yetu ya ndoa....Lakini kwa kuwa uliangalia nje, uliona mkate, badala ya pete hii ya thamani iliyokua ndani.. Naamini mwanamke niliyemuomba kwa Mungu bado sijampata.. Nashukuru kwa yote uliyonifanyia, nimekusamehe, nawe naomba unisamehe kama nimekukwaza.."

Kisha akachukua mkate wake, huyooakaondoka. Msichana akaomba msamaha lakini ilikua too late..

MORAL OF THE STORY..!
Usidharau kitu/mtu kwa kumtizama nje.. Mungu huangalia thamani ya kitu ndani lakini Wanadamu huangalia nje.. Thamani ya kitu/mtu ipo ndani na si rahisi kuonekana..
Usiwe mwepesi wa kuhukumu kwa kutizama umbo la nje.. Wale wanaokudharau leo na kukuona mkate, ipo siku watagundua haukua mkate wa kawaida... kuna vingi vya thamani ndani yako.
Wote wanaokudharau leo ipo siku watakusalimia kwa heshima..!!

Thursday, November 9, 2017

Sifa Hizi Zitafanya Mwanamke Akose Mume

11/09/2017 07:49:00 PM 0
*KUOLEWA NI NDOTO KUU YA KILA MWANAMKE ALIYEKAMILIKA ILA KAMA UNA TABIA HIZI UTAZEEKEA NYUMBANI**


1. Tamaa ya utajiri* fedha na mali nyingi pasipo kutambua kuwa vitu hutafutwa, hapa wengi hupoteza nyota zao kwa kukataa wengi wenye kipato cha kawaida na kujirahisisha kwa wenye nazo ambao kwa bahati mbaya wengi wao sio waoaji bali ni wahuni tu na watu wa anasa na kula bata mjin

.*2. Dharau,* maringo, kiburi na mashauzi yaani we kila mtu akikusogelea na kujaribu kuzungumza na wewe unaanza kumpandisha na kumshusha kisha una msonya. Wengi huishia kukupotezea wakijua either umewadharau au tayari una mtu wako ndio maana nyodo nyingi. Unajiona km wakwanza kupendwa, ukiitwa unadharau, utapishana na mume ukaitika kwa wahuni wakuchakaze bila huruma!

*3. Husali* hakika lazima wahuni watapata nafasi kwako na kukuchezea mpaka uchakae kama mtumba wa uvira. MWENYEZI MUNGU ndo anaetoa BARAKA ukimuomba hakika atakuepushia kuingia midomon mwa dubu na fisi wanaokuwa wakikuvizia na kuja kama MALAIKA. Atakupa ufahamu wa kuwatambua na kuwashtukia mapema.

*4. Kuvaa nguo za ajabu ajabu kama changudoa*. Sijui ni nani aliyewaambia kuwa mkivaa hivyo mnapendeza! Unakuta binti unavaa kama mcheza show za Casino yaani ukipita nguo yaonyesha kila kitu ukiinama ndio balaa kabisa yaani kimin kinafunuka kila kitu nje nje kwa style hiyo nani atakupeleka kwao? Zaidi atakuja kama malaika anafunua anakula anasepa! Wengine hata shepu hana kiuno utadhani kichuguu, miguu spoko ya baiskeli, kifua matikiti maji ila bado unavaa vinguo vya ajabu hata hueleweki!

*5. Kujipaka marangi ya ajabu ajabu usoni kama mwali wa kibembe* au kizaramo kwanza mnatutisha tu. Unakuta binti una rangi rangi kma mzuka wa makaburini! Unatisha utadhani jini makata, mdomoni umenyonya damu, yaani kila kitu ovyo ovyo..

*6. Kupenda kujirahisisha au kujipendekeza pendekeza kwa wanaume,*yani ukiguswa kidogo tu twende. Mwanaume huamini angalabu mwanamke awe msumbufu alikubali fasta akitongozwa, wewe leo umeambiwa unapendwa kesho geto umeingia na nguo umesaula zote ushaliwa! Hapa subiri upako tu kwenye maombi kuolewa!

*7. Kuwa na picha karibia 500 Facebook,* Twitter nk halafu picha zenyewe hazieleweki yani zimepigwa katika mavazi au mapozi ya ajabu ajabu, mara umebinua makalio, mara tumbo, mara mdomo, unakuta binti kaonyesha makalio yenyewe hata hayana shepu, alafu anaandika "Asanteeee Mungu mwema! " Haki vile siku ya hukumu ipo na unaanza hapa hapa kwa kuonyesha ujinga wako! Wapo waliokuzidi wengi tu kwa shepu zao wametulia tuli!

*8. Kila unachofanya basi unakimbilia kupost mfano kwenye Facebook* na kadhalika nyinginezo hata ukienda haja basi lazima upost. Mara nasafiri, mara ulaya mara nakula piza kumbe unaponea majimbi huko kijijini, mara nyumba nzuri kumbe umeitwa kwa wenyewe kusutwa, huo ni upuuzi sana. Kuna siku utapost naenda mp kwa akili yako fupi!

*9. Ni mtu wa maneno maneno* yani we kila unachokiona unaongea na kuropoka ropoka tu hauna break! mwanamke gani? Utafikiri kasuka, hujawahi ona kitu ukanyamaza, maanake utakuwa ukiropoka hata mbele za watoto.

.*10. Huna mawazo ya malengo* endelevu yani we kwenye kichwa chako kumejaa umbea tu sijui leo Wema Sepetu amefanya nini? Sijui Kim, Lupita amefanya vile na upuuzi mwingine. Sijui leo sitaki ugali nataka piza, nimechoka kula hapa twende hotel, binti kwa hali hii utaona km umelogwa na aliyekuloga kafa!

11 Mizinga.* Yani siku ya pili tu baada ya kukutongoza unaanza " honey nataka galaxy" Htc" Huawei" mara baby nimeona nguo nzuri mara ooh baby yaani njaa inauma'' , utasindikiza harusi za wenzio hadi upigwe alama..

12. Umezoea vitu feki, ngozi umeibadili km rangi mbili, yaani wewe kila kitu ni feki, macho, kope kucha makalio yasompangilio vyote vyaMchina, alafu unaringa mie mzuri! Endelea kujiremba kama mwanasesere uone mwisho wako! Usoni mweupo km mwarabu koko vidole na viwiko rangi mbili, chezea ngozi yako fainali uzeeni!

13. Hujui bajeti! Unapewa laki tano uende shoping, unarudi na vigsuni vya ajabu, badala ya kufanya vya msingi.

14. Una matusi matusi na maneno ya ovyo ovyo mithili ya chizi, siku hizi unakuta binti anataja kiungo chake kile kinachofichwa na chupi wala hata haoni haya! Haoni haya wala soni usoni kujisifia kwa boyfriend wake kuwa kila mtu anamuogopa kwa matusi mtaa mzima. Hapa subiri neema na rehema ya Mwenyezi Mungu kuolewa!

15. Mvivu hupendi kazi na kujishughulisha, unakuta mwanaume atahangaika huku na kule apate riziki wewe hata kupika hutaki, unaogopa kuchafua kucha feki na kuupa uso jasho! Unawaza habari za house girl hata hujaposwa! Maisha ni kujituma km hujui hili paki pembeni acha wenzako waolewe wanaojua kujituma na kutafta!

16. Una makundi ya ovyo ovyo na kulewa! Sidhani km mwanaume mwenye serikali timamu katika kichwa chake ataoa au kwenda kutambulusha mlevi kwao! Wewe kila pombe unabwia; chimupumu, bia balimi Heineken nyingine hata baba yako hakuwahi kunywa ila wewe ndio star! Una makundi ya ovyo ovyo wanopenda starehe, kukicha kiguuu na njia kufata umbeya, hapa subiri kusindikiza Send off za wenzako Mpka visigino vipinde!

17. Huna chembe ya heshima na adabu; kuna mabinti wengine wanajua kuheshimu mtu mpka awe na mamilioni. Haheshimu hata wazazi wake, nani atakuamini? Jua kila kitu huenda na heshima! Heshimu uheshimiwe na uthaminiwe

Waswahili husema, "Kama mzuri, Olewa"

Jihadhari na tabia hizi.

zimepoteza wengi

Wanajutia kiburi na ufedhuli wao

Usiige watu

Ishi wewe km wewe
#want_to_see_you_change_everyday

Franco Samuel

Audio