Monday, November 13, 2017

Simulizi fupi: USIMDHARAU USIYEMJUA


Soma simulizi fupi ya kusisimua
 "Usimdharau usiyemjua undani wake"
 

Msichana mmoja alikuwa amempenda kijana mmoja mtanashati na mcha Mungu.. Malengo yao ilikua waje kuoana baada ya muda. Kijana huyu alijitoa sana kwa binti huyu
hadi wenzie wakamuona mjinga, lakini ukweli ni kuwa alimpenda msichana yule
kwa dhati. Alimtafutia kazi alipomaliza chuo, alimshauri kuhusu mipango ya maisha na alikua akimuombea kila  alipopata nafasiya kuomba.
 

Siku moja binti alikua anasherehekea siku yake ya kuzaliwa...hivyo akaalika marafiki zake, na watu wengine muhimu akiwemo mpenzi wake. Wageni wote walifika kwa wakati isipokua yule kijana alichelewa kidogo... Hivyo msichana akatumia muda ule ambao mpenzi wake hajafika kuwaeleza wageni  namna yule kijana alivyokua wa muhimu kwake..

Akamsifia sana, akasema atamvalishapete ya uchumba soon, na akasema siku hiyo ya birthday yake anategemea zawadi kubwa sana kutoka kwa huyo mpenzi wa nafsi yake.

Baadae kijana akaingia na kuketi high table.. Muda wa zawadi ulipofika watu wakamtunza binti zawadi mbalimbali na kijana akawa wa mwisho... Hivyo wageni wote wakawa na hamu ya kutaka kujua zawadi aliyoleta hasa baada ya yule msichana kumsifia sana.

Kijana akaamka na kutoa mfuko.. kila mtu akataka kujua kilichokua ndani ya mfuko..mara kijana akafungua mfuko na kutoa mkate..!!Lahaula... watu wote wakastaajabu..mkate??? Lakini kabla hajasema lolote kuhusu ule mkate, yule msichana akaanza kulia.. akapandwa hasira kwa kuwa mpenzi wake amemuaibisha..!!Akiwa analia kwa kwikwi, akamkwida shati na kumvua tai yake, akamwagia juisi, kisha akauchukua ule mkate na kuutupa.!!

Maskini..yule kijana akaukimbilia ule mkate na kuuokota.. Kisha akarudi hightable na kusema "baby nakushukuru kwa yote..Huenda umenidharau kwa kuwa nimekuletea zawadi hii ndogo kwenye siku yako muhimu kama hii. Lakini kamaungetambua thamani ya zawadi hii,usingefanya haya.."

Kisha akafungua ule mkate na kutoa vituviwili alivyoficha ndani ya mkate.. Kwanza akatoa ufunguo wa gari, ambalo alikuwa amemnunulia mpenzi wake na alitaka amkabidhi siku hiyo ya birthday. Kisha akatoa pete ya uchumba na kusema
"Nilimuomba Mungu anipe mwanamke atakayenipenda katika hali yoyote. Nilipanga leo nikuvalishe pete hii ili kuelekea ndoto yetu ya ndoa....Lakini kwa kuwa uliangalia nje, uliona mkate, badala ya pete hii ya thamani iliyokua ndani.. Naamini mwanamke niliyemuomba kwa Mungu bado sijampata.. Nashukuru kwa yote uliyonifanyia, nimekusamehe, nawe naomba unisamehe kama nimekukwaza.."

Kisha akachukua mkate wake, huyooakaondoka. Msichana akaomba msamaha lakini ilikua too late..

MORAL OF THE STORY..!
Usidharau kitu/mtu kwa kumtizama nje.. Mungu huangalia thamani ya kitu ndani lakini Wanadamu huangalia nje.. Thamani ya kitu/mtu ipo ndani na si rahisi kuonekana..
Usiwe mwepesi wa kuhukumu kwa kutizama umbo la nje.. Wale wanaokudharau leo na kukuona mkate, ipo siku watagundua haukua mkate wa kawaida... kuna vingi vya thamani ndani yako.
Wote wanaokudharau leo ipo siku watakusalimia kwa heshima..!!

No comments:

Audio