Sunday, November 5, 2017

SIFA ZA MWANAMKE ANAYEFAA KUOLEWA

JE  WAZIFAHAMU ZIFAHAMU SIFA ZA MWANAMKE ANAYEFAA KUOLEWA?..

Ukiwa kama kijana na mwanaume mwenye ndoto za kupata mke bora katika siku hizi za kisasa za sayansi na teknolijia, tambua kuwa sio kazi nyepesi kuchangua mtu wa kuanza nae uchumba hadi kufikia ndoa yenye furaha ya amani ya moyo. Wanaume wengi wamejikuta katika mkanganyiko mkubwa hasa linapokuja suala la kutafta mchumba au mwenza wa kumuoa na kuanzisha maisha na familia. Kijana wa kiume anaweza kuanzisha uhusiano na msusruru wanawake ila linapokuja suala la kuoa basi lazima kidogo atulize kichwa kwa kuwa ndoa si lelemama kwani ni jukumu ambalo sio la kukurupuka.


Leo nimekuletea hapa baadhi tu ya sifa za masingi ambazo mwanamke anatakiwa awe nazo kama unataka kuoa. Ikumbukwe kuwa mwanamke unayetaka anaweza asiwe na sifa zote unazozitaka ila unashuuriwa kutofuata moyo pekee ili kuwa na maisha ya ndoa yenye upendo na amani. Tuanze moja kwa moja kwa kuzitaja sifa hizi;

  1.  Tabia njema: uzuri wa mwanamke amabye anafaa kuwa mama wa  watoto na familia unapimwa kwa tabia. Hii ina maaana kuwa mwanamke ambaye mwanaume unataka kuingia nae katika ndoa ni sharti awe na tabia njema kwani atakuheshimu na atalea vema watoto. Tumekuwa  tukiona wanaume wana date na wanawake wazuri wazuri wa kila aina ila akitaka kuoa  lazima aangalie yupi ana adabu na tabia njema ili ndoa yake isiwe ya vitimbi. Si maanishi wazuri hawaolewi ila kuwa na tabia njema ni kigezo kikubwa cha mwanamke kuolewa kwahiyo mwanamke  jitahidi kutengeneza tabia yako kuwa njema na ya staha kwa mwanaume ili kujipa nafasi nzuri ya kuolewa.  
  2. Mwanamke mwenye kushika dini, kuna wanawake wengi wazuri sana ila hawashiki dini. Tunaamini kuwa anayaeshika dini huwa na heshima kwa mumewe kwa kuwa hata dini inafundisha hivyo. Japo si wote wanaoshika dini huwa na heshima ila aghalabu wanawake waliolelewa katika dini huwa na hashima sana kwa waume zao. Pia ni rahisi mtu huyu kuwafundisha watoto njia njema na salama katika ulimwengu huu wa kisasa.
  3. Heshima na adabu, hapa hekima inahitajika kujua yupi anaheshima. Ukiwa kama mwanaume na unakuta mwanamke mwenye heshima basi jitahidi kuwa makini kwani wanaweke wengine huigiza tabia ili tu waolewe. Wapo wanawake wazuri kama malaika ila tabia zao ni kama shetani yaani ni wazuri ila hawana hata chembe ya heshima, kuanzia mavazi yake si ya heshima, sijui nguo zimechanika chaninka au nguo za kulalia anavaa mchana na za machana usiku. Kama anashindwa kuwa na heshima hata juu ya mwili wake atakuheshimu wewe mwanaume? So badilika dada yangu ili usiseme ulizaliwa na mikosi huolewi kumbe unajitakia tu.
  4. Anaye vaa kwa staha na heshima; mwanamke avae kwa staha sio anavaa kama mhuni au kahaba fulani hivi. Mwanamke usivae tu kisa fasheni au kwa kuwa fulani kavaa,  au ili uoneshe kuwa una sahpe na vitu kam hivyo. Unavaa nguo mpaka ukipita kwa watu unajistukia mwenyewe? Aina ya nguo hizo zinafanya wanaume watamani na wengine wanaweza kujua ni mhuni kupitia tu nguo ulizo vaa hata kama si tabia yako. Usiseme unavaa kuendana na wakati. Mwanamke anayevaa nguo ambazo hazimpi uhuru akitembea hawezi kuwa mwanamke bora kama mke wako. Mwanaume unamnunulia mchumba vinguo vya ajabu akivaa na kupita mtaani wahuni wanamtamani  wanamtongoza na hawezi kukataa. Usilalamike chanzo ni wewe.

Suala la maadili  ni muhimu mno  katika mavazi, SIKUHIZI MWANAMKE AKIVAA STARA ATAITWA MSHAMBA NA AMEPITWA NA WAKATI. LAKINI AKIVAA NUSU UCHI ATAITWA MTOTO MKALI wa mjini.  Mimi siamini kama ili mwanamke aonekane mrembo zaidi ni lazima avae nusu uchi. Wakati huohuo asilimia kubwa ya wanawake walio olewa ni wale wanaojisitiri vema!!

5: Anayependa na kuwaheshimu wazazi, ni wajibu wa mwanamke kuwapenda wazazi wake na wa upande wa kiume. Unadate na binti unakuta hata wazazii wake hawapendi na hata wakwako hawapendi wala kuwa heshimu, huyo ni jipu muache kwani ipo siku mama atakuja kukutembelea badala ya kupikiwa atamgeuza mamamkwe housegirl. Acheni heshima za kinafiki.

6: Awe na mapenzi ya dhati na anayejua kupenda, wengi wameumi sana kwa kupenda au kupenda kisa mtu anakitu Fulani aidha fedha au mali. Kumbuka furaha na upendo wa kweli hautokani na mali au pesa, mwamke asikupendea kwa kuwa una pesa au wewe ni meneja, ukifirisika lazima uone dunia kama kuzimu vile.  Ewe binti usimpende mtu sababu ya pesa au uatajiri kwani hivi vitu vinapita, jali utu na thamni ya mtu si mali au cheo chake. Kuna watu wnapesa ila ndoa zao ni machungu mnoo..bora maskini anayepata upendo kuliko tajiri mwenye machungu ya moyo.

7: Kauli njema  na za adabu, chunguza  kauli zake je za kutia moyo au kukatisha tamaa? Yaani awe mtu wa kukutia moyo wewe mwanaume,  anakuongelesha kwa heshima sio anakuwa mkali kama askari wa zamu wa jeshii la zimamoto. Ndio maana mwanaume alioa akiwa bonge gafla anaconda na kuwa kma mbu wa kiangazi, kauli zinafanya wanaume wanakimbia uhusiano, utasikia naenda kwa Jeni rafiki yako, yes ataenda kwa kuwa wewe hujui kuongea na mpenzi wako vizuri. Binti ichunge kila kauli uitoaye pindi uwapo  na boyfriend au mchumba wako.

8: Mwenye malengo na mtazamo wa kimaendeleo, siku hizi wnawake wameamka sana wanapenda kuendeleo,  awe mtu mwenye mipango ya mbele ya namna ya kuendesha familia na kufanikiwa, awe anashirikiana nawe katika kutekeleza miapngo ya maendeleo na si kung’ang’ania nywele na mawigi ya  elfu 70 wakati mnaishi nyumba ya kupanga, huyo mwogope kama ukoma.

9: Asiwe mtu wa makundi sana na starehe, ktk vitu vinavyofanya mwanamke akakosa adabu ni makundi. hatukatai kila mtu anazungukwa na watu ila makundi mengine yanabomoa, utasikia “we mjinga mwanaume mmoja pekee atakusaidia nini”. Kuwa makini na makundi ambayo mchumba au boy/girlfriend anaishi nayo. Kuna wanawake vichwa vyao vyawaza kubomoa uhusiano wa wengine, wanawaza pombe, mziki, starehe na kulewa, hayo makundi yaogope kama ukoma.


10: Asiyependa kuiga, utasikia “beby nataka simu kama ya Mwajuma ile Iphone 7”  au si jui gauni la Angel. unajua boyfriend wako hana uwezo ila unaiga kwakuwa fulani anayo, huo ni ujinga. Mwanaume muepuke mara moja binti kama huyu kwani ipo siku utashindwa kumnunulia na atakuacha. Mwanamke bora haigi kila kitu…

 11. Asojivunia uzuri wake, mwanaume unakutana binti kauli zake tu ni kukutishia eti mzuri mi sana! Mimi nasemaga hata Cleopatra alikuwa mzuri ila alimtii mumewe, wewe nani hata ujidai na uzuri wako? Uzuri huo ni nini? Eti nina kiuno! Sio kweli kabisa, Ndio maana kuna mwanasaikolijia alisema mwanaume ukitaka kuishi kwa stress “oa mzuri sana”  simaanishi usiwe na mwanamke mzuri ila asiwe wa kujivunia uzuri wake. Waswahili wana sema “kama Mzuri Olewa” so usipende sana kutumia uzuri kama silaha okay…

12: Anasikiliza na kukutii, mwanamke bora huwa anakuwa msikilizaji, anahoji vizuri na kwa utulivu, sasa unakuta mtu ni  mchumba tu hata hujamaliza ulicholikuwa unaongea kasha dakia, majibu ya ovyoovyo, hiyo ndoa lazima iwe ya kibondia na kwa wenye miili midogo kama yangu utakonda bure ufe uache wazazi na watoto...

13: Usafi, kiufupi wanawake wameumbwa na hulka ya usafi, awe mtu wa kupangilia vitu vizuri anavaa kwa unadhifu kiasi hata ukitembea nae njiani huogopi kumtambulisha. Usafi huu ni wa ndani na nje, kumbuka mwili wa mwanamke ni tofauti na wa kiume, km hapendi usafi saa hizi na hamna watoto itakuwaje majukumu yakiongezeka? Ndio pale unampeleka rafiki yako kwako na kukutana na viatu juu ya meza….

14: Asiwe mtu wa ugomvi, tuanaamini kuwa mwanamke aliumbwa mpole na mnyeynyekevu, awe angalau mtu wa kushuka hata ukimkosea, ili kwa kinywa chake asiharibu ndoa na uhusiano. Unakuta mwanamke mgovi kitu kidogo tu maneno mengi mpaka mtaa wa  tatu wanasikia. Hapa mwanamke ujue una lazimisha mwanaume atafute kimada anayejua kutuliza kinywa chake!.

15: Mchapa kazi, simaanishi awe ameajiriwa au awe na kazi ila namanisha anayewza kutimiza majukumu yake vizuri na kwa wakati. Sio unamnunulia mboga mapema, unarudi kazini unakutahata vyombo vya jana hajaosha na kupika hajapika. Mwanamke usiwe mtu wa kupangiwa majukumu jiongeze, ukiona nguo chafu fua, usisubiri kuambiwa. Ukitekeleza majukumu vizuri lazima upendwe tu….

16. Mdomo wa heshima,  mwanamke mpenda maneno mengi si vema ukawa nae makini,  i mean chaumbeya,  hapa jua kutofautisha kati ya muongeaji na maneno mengi..

Binti zingatia haya ili uolewe, wanaume wamebaki wachache n wanawake kila siku wanaongezeka_fact
Hizi ni chache kati ya nyingi, azotakiwa kuwa nazo, ruksa kuongeza kwa kukoment na kushare ili watu wajue …..
#wants_to_see_you_change_everyday
Franco Samuel

No comments:

Audio