Monday, October 9, 2017

Mwanamke Akiambiwa "Nakupenda.. " nini Humjia Kichwani?


"NAKUPENDA SANA"

 "pokea moyo wangu!"  

 

 Ni maneno matamu asemayo mwanaume kwa mwanamke sikioni na kuvuruga mfumo mzima wa ufahamu wa Mwanamke! 

 

 Mara nyingi mwanamke anapoambiwa na mwanaume NAKUPENDA,  Moyo Wa mwanamke hufurahi na mwanamke huwaza mbali zaidi kuliko mwanaume!!  Mwanamke akiambiwa nakupenda moja Kwa moja huwaza; Kutambulishwa,  kutolewa posa,  send off-kitchen part,   ndoa, honeymoon, jinsi atakavyoringa,   watoto,  Jinsi atakavyo tengeneza familia na huyo kaka watoto wao watakuweje,  itakuwaje huo ndio moyo Wa mwanamke mara zote huwaza familia zaidi!. 

 

 Lakini mwanaume ni tofauti saana anaposema nakupenda (kwa wale waliotamani)  yeye hufikiria pafupi sana kamab vile mtakutana saa ngapi amalize haja zake, kama  hotel gani ama gest gani,  je utakuwa mkali zaidi ya yule aliekuwa naye kipindi cha nyuma au laa!   Na mwanaume anayetaka tu kukutumia huwaza atakuachaje hasa yule aso na mapenzi ya dhati-mwenye tamaa za mwili tu!   

  Mwanaume usipige ndege kwenye kichaka cha miiba kama hujui njia ya kumuokota,  ukamuacha akioza, bora aishi kuliko kufa bila kuliwa!   Mwanamke acha kujirahisi,  kama hakuelewa mapenzi ya dhati basi  hapo ndipo moyo  wake hujeruhika nakujisikia vibaya,  kujikataa, hujidharau na kujiona Hana tena thamani.   Mbaya zaidi Mwanamke huumia pale anapoona yule jamaa kesho anafunga ndoa na mwanamke mwingine!! Kiukweli  maumivu ya huyu Dada Mungu asipoingilia Kati anaweza Fanya maamuzi mabaya zaidi kuliko ambavyo ungedhani. 

   Wapo wengi wapo katika hali hii,  Mungu aponye mioyo ya wanawake woote waliojeruhiwa Kwa namna moja au nyingine!  Wema Wa Mungu ukawazunguke, ewe Mwanamke uliye katika mateso, tambua  ipo nafasi ya kuanza upya!  Upo muda utapata furaha yako na faraja ya kweli, haijalishi kakuacha na mtoto ama laa!   

  Tambua Mungu mwema   akafuta maumivu yote, atakuongoza katika njia mpya,  mkabidhi leo akuongoze, amua Leo kukung'uta mavumbi,  ukaanze upya na Mungu atakupa kilicho bora zaidi!.  Upendo wa Mungu umejaa na hakika utapata aliyebora zaidi! . 

 Hakuna kukata TAMAA dada,  wewe wa thamani! Unastahili kupendwa!  Take care Mwanamke....  

Na Franco Samuel Jicho 👀 lionalo mbali.... 


No comments:

Audio