MAISHA MAPYA NA YENYE FURAHA BAADA YA KUSALITIWA NA KUVUNJIKA KWA MAHUSIANO….
Leo nitazaungumzia namana gani mtu anaweza kuishi baada ya kuachana na mpenzi wake au kuvunjika kwa uhusiano. Maisha baada ya mahusiano kuisha yamekuwa magumu sana miongoni mwa watu ambao tayari walishaonja joto hili kali ya kuumizwa na mapenzi. Kiufupi kwa aliyekuwa ampenda na kudhamiria huumia sana na huhisi kama hakuna tumaini tena katika safari ya mapenzi kwa ujumla.
Ulisahawahi pengine kujiapia kuwa siatapenda tena ua hata kufikri kujiua kwaajili ya kusalitiwa ama kuvunjika kwa mahusiano ya mpenzi? Ama ushawahi sikia mtu akisema yeye basi hatopenda tena ama umejisemea mimi mapenzi basi?
Kama jibu ni ndio au ulishwahi kumbana na maumivu ya kuachwa leo nitakufundisha mbinu kadhhaa ili uwe na furaha tena. Acha kujiapiza hutapenda tena wakati una moyo, acha kulia irejee furaha yako kwa kusoma haya mambo ninayokuandikia hapa. Fanya yafuatayo ili uwe na furaha:
1: Kubaliana na hali halisi: yaani kubali ukweli kuwa mmeshaachana na unatakiwa kuwa huru, kuna watu wameachana ila bado moyoni mwao wameweka mtu ambaye yeye hata hayupo miyoni mwao. Kumbuka ndugu kukabiliana na maji yapande milima ni kazi kubwa sana namaanisha kulazimisha mtu aliyesema muachane ni kazi na ipo siku utakuja kuumia zaidi.
2: Uspendelee kuonana au kuongea na Yule aliyekusaliti: simaanishi msiongee ila kuna wakati mtu anaweza kupata hasira au kujhisi vibaya sana kwa kuendelea kuongea naye. Kuachana na mtu haimaanishi kuwa maadui ila usipende sana kuongelea tena mambo ya mahusianao na mtu ambaye tayari kakusaliti.
3: Pendelea kukaa na marafiki na kujichanganya na watu, hapa ni muhimu pia marafiki wasiwe watu wa kukupa stress au wnaopenda kuzungumzia habari za kauchana na kukucheka, usipende kuwa na marafiki wa aina hii kwani hukatisha tamaa zaidi. Usipende kukaa chumbani pekee kwa kuwa utakuwa ukifikiria sana na utakuwa na msongo wa mawazo juu ya hilo na kuchukua maamuzi magumu kama kunywa sumu au hata kukijtia kitanzi. Pia waweza kuwa eleza watu wa muhimu kwako ili wawe na msaada juu yako kama utashindwa kufanya mambo yako vizuri mfano wazazi au watu auanwaoamini sana.
4: Kubali kusamehe: msamehe na mwache aende ili uwe na fursa nyingine mpya katka maisha. Roho au moyo usiosamehe huumia zaidi. Ili kuwa na furaha samehe na jisikie huru kabisa. Kwa kutoa msamaha una ruhusu Moyo wako kuwa huru kabisa.
5: Futa kumbukumbu na viashiria vya mtu uliye achana nae, mfano picha au namba za simu nk. Kama kunapicha mlipiga pamoja na zinakufanya ukumbuke mambo Fulani ya nyuma yanayoumiza moyo basi ni vizuri ukazifuta. Wengi huwa hawapendi kuona picha kwakuwa hukumbushia tukio linaloweza kukuumiza zaidi. Waweza kubakiza picha chache zisozo kuumiza, pia jitoe urafiki nae mfano fb kwa kuwa unaweza kuzikuta post zake zikazidi kukuumiza zaidi na zaidi.
6:Jifunze madhaifu yako na maweza yako na kujikubali ulivyo: jiulize una mapungufu gani yaliyopelekea kuachana? Je ulikosea wapi ili iwe rahisi kuanza mahusiano mapya! Kumbuka tunajifunza kupitia makosa na kama hujakosea bado hujajifunza kitu. Pia jikubali kuwa wewe unaweza kwaajili ya mahusiano mapya.
7: Acha kuwaza mtazamo hasi (negative attitude) kuna watu mpaka leo bado anasikitika na kuaona watu wote ni wasaliti. Huo ni mtazamo mbaya na hufanya mtu asipende tena. Aliye kusaliti ni mmoja tu, usiichukie dunia nzima, wapo wanaoweza kukupenda mpka ukajihisi ni mfalme, kwanini uwachukie wote wakati aliyekusaliati ni mmoja tu? Ama mtu anajiona yeye basi hana bahati nani kasema huna bahati? Acha mawazo potofu na uishi kwa furaha kabisa ukiamini kuwa ipo siku utapendwa zaidi.
8:Baada ya muda pata mpenzi mpya, usikae ukiumia wakati moyo unao, irejesha fuaraha yako kwa kupata mtu mpya uanendana nae. Hutakiwi kukataa ukipendwa tena, mfano, una miaka 20 tu unakata tamaa ya kupata mpenzi tena, je uataweza kuishi miaka 50 bila kuwa na mahusiano? Jibu ni hapana na haiwezekani, hivo haraka iwezekanavo pata mtu mpya kabisa wa kukufanya usahau na usirudie makosa ya kipindi cha nyuma.
*****************NJIA MBAYA WANAZOTUMIA WATU WAKIaCHANA AU UHUSIANO UKIVUNJIKA***************************************
Kuna watu wanatumia njia zisizofaa kurejesha furaha pindi mahusiano yanapoisha. Njia hizi huwa hatari na huathiri afya ya muhisika na pengine kuathiri maisha yake yote hadi kupelekea kufa. Tafadhali usitumie hizi njia
1: Kunywa pombe na vilevi, unakuta mtu alikuwa hanywi akiachana tu basi anakunywa sana, hilo ni tatizo kwa kuwa ukinywa uta sahau tu, pombe ikiisha unarudi katika hali ya kawaida. Pia unauchosha mwili kwa pombe kali wakati usio wake.
2: Kufanya ngono, mtu akiachana na mpenzi wake basi anakuwa wa moto kweli, mara yuko na huyu mara huyu kama vile anamkomesha aliyeacahana nae! Jua tu unajikomesha Kumbuka kuna magonjwa siku hizi, na pia unauchosha tu mwili wako.
3: Kukataa kula au kula sana, unatakiwa ule kwa afya na ufanyee mazoezi, usikate kula japo chakula huwa ni kichungu ila jikaze ule tu na uwe na amani. Usile sana kwani huathiri tumbo na mfumo wa kumeng’enya chakula.
4: Kutolala au kulaa sana, hapa utaathiri mwili wako ila lala kawaida tu. Wengine hutumia muda mwingi kuangalia TV au komputa kwa muda mrefu sana.
5: Kujaa hasira na kubwatukia kila mtu, yaani unakuwa mkali kama mbogo , haifai.
6: Kulia lia na kunung’unika sana. Mtu kila siku yeye ni kulia tu, utalia mpka lini rafiki yangu? Kila kitu kina mwisho na ipo siku utapata furaha.
7: kutangaza kila sehemu: mara fb moyo sukuma damu, mara sijui nini ila jua sio kila mtu lazima ajue kuwa umeachika. Pia kutangaza sifa za mtu uliyeachana nae haifai kabisa….
Mwisho: kuvunjika kwa nyundo hakumanishi mwisho wa uhunzi, nikimaanisha kuachana hakumaanishai huatapenda tena, bado una wakati mzuri kabisa wa kupenda na kuw ana furaha yako katika maisha haya.
Kwa wale wanao waacha wapenzi wao: tambua kuwa chozi la mtu lina thamani sana na ipo siku yatakukuta nawewe pia. Sio vizuri sana kwani hakuna aliyekamilika. Maumivu ya kuachwa na unaempenda ni makali mno na haufanya mtu asiwe na amani tena.
Kwa mnaopendana ni vizuri kudumisha upendo wenu vizuri ili usiumie baadae.
Love is sweet
Love is enjoyable
Love is fantastic : post by Franco Samuel 2017
usiasahu kulike page yetu
No comments:
Post a Comment