Madhara ya kujichubua
Urembo na kuwa na ngozi yenye mvuto ni kitu ambacho karibia kila mtu anapenda. Siku hizi imekuwa kawaida kukutana na mtu akiwa kajipendezesha hasa uso. Hii ni kwasababu wengi tunaamini uso ndio kitu cha kwanza kuonwa na watu yaani face is introduction for everyone
Katika baadhi ya sehemu duniani watu wanaamini kuwa ngozi angavu huashiria uzuri, utajiri na uwezo(kifedha) alionao mtu. Katika baadhi ya sehemu watu wenye ngozi nyeusi huchukuliwa kuwa wapo chini ya kiwango, hii hupelekea watu hawa kutumia ving´arisha ngozi kama krimu, vidonge au nyenzo zingine kubadilisha ngozi zao. Idadi inazidi kukua maradufu ya matumizi ya ving'arisha ngozi, na siku hizi hata wanaume wapo tofauti na zama za kale ambapo mabinti walishika usukuni.
Tafiti zinaonyesha kwamba wavulana na wasichana hupendelea kutumia bidhaa zinazong´arisha ngozi ili waweze kupata hadhi nzuri katika kundi la familia zao, na jamii. Kwa kweli,hata matangazo yanayoonyeshwa kwenye televisheni mbalimbali huonyesha kitu hiki.
Mambo hayo yote huwa na athari kubwa juu ya mawazo ya vijana wa kiume na wakike ambayo hupelekea kuwafanya wachague chochote wanachomudu kati ya krimu au vidonge.
Je kuna madhara kujichubua...?




