Tuesday, December 5, 2017

Madhara ya Kujichubua

Madhara ya kujichubua

Urembo na kuwa na ngozi yenye mvuto  ni kitu ambacho karibia kila mtu anapenda. Siku hizi imekuwa kawaida kukutana na mtu akiwa kajipendezesha hasa uso. Hii ni kwasababu wengi tunaamini uso ndio kitu cha kwanza kuonwa na watu yaani face is introduction for everyone 


Katika baadhi ya sehemu duniani watu wanaamini kuwa ngozi angavu huashiria uzuri, utajiri na uwezo(kifedha) alionao mtu. Katika baadhi ya sehemu watu wenye ngozi nyeusi huchukuliwa kuwa wapo chini ya kiwango, hii hupelekea watu hawa kutumia ving´arisha ngozi kama krimu, vidonge au nyenzo zingine kubadilisha ngozi zao. Idadi inazidi kukua maradufu ya matumizi ya ving'arisha ngozi, na siku hizi hata wanaume wapo tofauti na zama za kale ambapo mabinti walishika usukuni.

 Tafiti zinaonyesha kwamba wavulana na wasichana hupendelea kutumia bidhaa zinazong´arisha ngozi ili waweze kupata hadhi nzuri katika kundi la familia zao, na jamii. Kwa kweli,hata matangazo yanayoonyeshwa kwenye televisheni mbalimbali huonyesha kitu hiki.

Mambo hayo yote huwa na athari kubwa juu ya mawazo ya vijana wa kiume na wakike ambayo hupelekea kuwafanya wachague chochote wanachomudu kati ya krimu au vidonge.

Je kuna madhara kujichubua...?

  • Jibu ni rahisi tu, ndiyo yapo tena sana kama sio leo basi kesho kwa wewe unayetumia! Nimekuandikia hapa madhara yasome uelewe mtu wangu..u anaeyejichubua anaweza kupata kansa ya ngozi, chunusi, uvimbe katika ngozi, ngozi kuwa nyembamba na kukosa uimara katika uvutikaji yaani stretiching ambapo mtu huyu akipata ajali sio rahisi kushona kwa kuwa ngozi hukatika tu! 
  • Kuongezeka kwa hamu ya kula na uzito, wengi wameongezeka uzito bila kujijua hii inatokana na baadhi ya krimu ama vidonge kuongeza hamu ya kula
  • Kutokwa na mabaka na mavipele makubwa ambayo siyo rahisi kupona na hufanya mtu akose mvuto na raha, wapo wengi wako katika hali hii. U
  • Ugonjwa wa pumu kutoka na krimu ama vidonge kuathiri mapafu na mfumo wa upumuaji. K
  • Kupata watoto wenye kasoro baadhi ya madini na viambata vilivyopo kwenye ving'arisha ngozi huathiri mbegu na mfumo wa uzazi hivyo kuathiri aina ya watoto mtu atako zaou
  • Kupata matatizo ya akili na kuharibika kwa ini, ini huaribika kutokana na kushindwa kukabili sumu ya dawa ambazo mtu katumia. K
  • Kuharibika kwa mishipa ya fahamu pamoja na figo kutokana na kiwango kikubwa cha zebaki(mercury) kilichomo katika krimu, Osteoporosis(kupungua kwa uzito wa mifupa ambapo huongeza hatari ya kuvunjika kwa mifupa)

Kuungua kwa uso na kubaki na ngozi yenye makovu makovu na isiyovutia.. 
Baadhi ya madhara haya huonekaa mara moja na mengine hujitokeza kadri mtu anavyotumia ving´arisha ngozi na kadiri anavyozidi kuzeeka. 
Waweza kupendeza leo ila ukawa unajichimbia kaburi la mateso hapo baadae, kumbuka fainali uzeeni na siku zote kujikubali ulivyo ndio silaha ya kwanza. 
Waweza kushare maarifa haya kuokoa wengine



No comments:

Audio