Saturday, November 4, 2017

Ushauri kwa Vijana

Ikiwa wewe ni kijana na Una umri wa kuanzia miaka 22+na Kuendelea
Soma hapaujifunze maisha ya hekima na namna  bora ya kuishi na kufanikiwa ungali kijana... 

 
1. Kama uko shule au chuo soma na usicheze ukifeli unajipotezea muda.

2. Jifunze kuweka akiba ya pesa.  Pia jifunze kuwa na matumizi mazuri ya pesa,bajeti vizuri na jiwekee akiba bank au popte unapoona panafaa.


3. Jitengenezee good character yaani tabia yako njema ili uwe tofauti na wengine.. Jitofautishe na wengine, uwe mfano bora


4. Jifinze kufanya kazi tofauti tofauti. Fanya hiki ama kile ili angalau uweze kuishi popote kwani dunia inabadilikaa na huwezi jua kesho yako

5. Anza kununua na kumiliki vitu kama kitanda godoro vyombo na ardhi au kiwanja.  Kumbuka msingi mzuri wa maisha ni fikra za ujana na kujiwekea mali


6. Kama utaweza kapange ujifunze maisha. Anza kujitegemea ili kujipa confidenece na maisha.


7.  Weka falsafa yako katika maisha na uiishi.  Falsafa ni dira ya kukuongoza. Mafano unataka kumiliki nini katika maisha?  Unataka mke au mume wa aina gani?  Aina gani ya maisha unaipenda?  Hiyo ndiyo falsafa...


8. Tengeneza mahusiano yaliyotulia na weka malengo. Jichagulie kijana au binti aliyemzuri katika wengi,  kijana au binti wa moyo wako, mpende... Kipindi hiki ni cha kuwa na mwenza aliyetulia kama unafikiri kuoa au kuolewa. Ukicheza ukafikisha 30 bila kuwa na mtu maaalumu basi utaoa au kuolewa bora mradi ila siyo na mtu wa ndoto yako..


9. Kuwa na marafiki imara,  jichagulie katika wengi marafiki kadhaa waliotulia wenye nidhamu ya maisha na wanaopenda uende mbele. Kijana chunga marafiki ulionao wengi leo wanajuta ba urafiki m'baya uliowapoteza... a


10. Kumbuka ibada na kumshukuru Mungu.  Kipindi hiki ni cha misukosuko na mihemko mingi. Usiache mafundisho ya imani yako,  usimsahau Mungu.  Mshukuru Mungu kwa uhai na kila jema au baya likupatalo.


11.  Jitume katika kazi,  watu waliofanikiwa wanajua thamani ya juhudi na kujituma.  Usikate tamaa hata kama unapata kidogo. Fanya kazi kama vile kesho haipo. Matunda utayaona


12. Zingatia kujiweka safi.  Kuwa msafi na mtanashati huanza na ubongo,  muonekano wako ndivyo watu watakavyo kuchukulia. Jiweke safi na jitunze..


13. Kula kwa afya,  wengi wanachukia miili yao. Wanauchukia aidha unene au wembamba,  ila ukila kwa afya,  ukafanya mazoezi unatengeneza afya bora ya sasa na baaadae..


14. Vaa kwa heshima,  usivae kama mcheza disko au teja.  Kumbuka thamani yako kwa Mungu.  Kwanini uvae nguo za machukizo mbele yake! Kwanini ukubali kuwa wakala na kutumiwa na shetani kuwaaangamiza wengine kwa kuvaa ovyo?  Vaa kwa heshima..


15. Pendelea kusafiri maeneo tofauti na ujifunze!  Asafiriye hupata maarifa na hujifunza mengi.  Penda kusafiri,  tembelea maeneo tofauti utakuwa na mengi ya kujifunza.


16. Kumbuka kupumzisha mwili.  Kuishi kwetu kupo katika chembe ya uhai iliyopo mwilini. Upe mwili na ubongo chakula chake cha kupumzika.  Nenda maeneo yatakayofanya mwili na akili vipumzike angalau kila baada ya miezi kadhaa..


17.  Jifunze kuamua mwenyewe.  Usisubiri kila kitu kumshirikisha mtu ndio uamue.  Jifunze kuwa mwamuzi wa mambo yko mwenyewe haijalishi kwa gharama ipi.  Watu wawe washauri ila ubaki kuwa mwamuzi mwenyewe.


18. Kuwa mtu wa kutunza siri. Jitahidi kuwa na shingo nzito na akili yenye kuweka siri.  Usiwe mtu wa kusema kila uonacho au uambiwacho.


19. Jfunze na zitawale hisia zako.  Hisia ziwe za hasira,  mapenzi au ugomovi zitawale na utaishi miaka mingi. Asiye tawala hisia zake hata awe mkubwa bado ni mdogo...


20.  Jitolee kwaajili ya wengine,  fundisha kemea saidia.  Unaweza kufundisha kupitia facebook wasap nk.  Kemea ukiona mtu anafanya kitu kibaya, saidia wenye shida wakumbuke wagonjwa yatima wazee na wenye mahitaji.  Wewe ni yatima,  mzee,  au muhitaji wa kesho.. Weka akiba ya wema


21 Jenga mazingira ya kuishi na watu vizuri.  Usijione mzuri au hb sana ukadharau wengine.  Ishi na kila mtu kwa upendo hata kama wankuchukia..


22. Tunza muda,  muda ni mali huwezi kuurudisha,  kuusimamisha au kuuzuia.  Ukishapotea ndio basi tena. Tambua thamani ya muda na fanya vitu kwa wakati..


23. Pendlea kusoma hasa vitabu vya dini,  kuhusu mali,  elimu,  mchumba,  afya,  maisha,  uongozi,  hekima, busara,  utu, uchaji,  utii,  maarifa,  utajiri,  heshima,  uvumilivu,  matumaini,  upendo,  na kila kitu vimo katika  Biblia na Qur'an ..soma uchote hekimaa... 


24. Acha kujifunza matumizi ya pombe, sigara , dawa za kulevya. Kama unatumia jitahidi uache,  kama unajifunza acha na kma kuna mtu anakushawishi kataa.  Afya ni mali na mtaji usichoshe na kuumiza uhai wako kwa pombe sigara na madawa ya kulevya...


Inafaa ukishare  kwa wengine wajifunze  maarifa haya..
Maisha ni maamuzi yako wewe, 
Kuamua kufanikiwa au kushindwa,
kuamua utajiri au umasikini yote ni mipango na hutokana na fikra zako..
#wants_to_see_you_change_everyday.. Well said... Sharee share
Franco Samuel....

1 comment:

Unknown said...

Shukran sana🙏
Ubarikiwe sana

Audio