Simulizi : SITAMSAHAU FRANC
Mwandishi:FRANCO SAMUEL EPISODE YA 13
ILIPOISHIA..
Alikimbiza sana nikiwa nimeshikilia tumbo lake, upepo ulisababisha macho yangu yatoe machozi. Niligeuka kwa kuibia sikuona tena gari la polisi, tulikuwa tumeliacha mbali mno na hata wangekuja na spidi gani wasingalitukuta mimi na Lau wangu ambaye hakika nilimuamini sana!
Hatimaye tulianza kuingia katika kijiji na kadri tulivosongo tuliona kumbe hakikuwa kijiji ila mji kabisa.
Nilivuta pumzi kubwa nikimshukuru Mungu wangu na kuona alikuwa mwema kwa yote. Kwa mbali nilihisi njaa ikiuma tumbo lilikuwa likidai chochote ili lilidhike.
Lau alizima pikipiki na kupaki pembeni ya barabara tulisogelea mgahawa fulani ulikuwa pale ili tule lakini mimi sikuwa na hela. Tuliingia ndani ila kwa nje king'ora cha polisi kilisikika na nilichungulia nikaona likipaki pale tulipoacha pikipiki yetu.
Yaani nilinyong'onyea kabisa...
Nilikosa nguvu sana, nilishuhudia askari wakishuka na bunduki huku wakija kwa kasi pale mgahawani. Lau aliniangalia na kunipa ishara fulani ya kuashiria hatari, Tayari askari walikuwa wakikaribia mlangoni!!
Tulibaki tumeduwa tu tusijue cha kufanya.
SONGA NAYO...
Kwa haraka Lau alinipa ishara ya kunitaka niiname chini, nilifanya hivyo kisha akanionesha nisimame nilifanya hivyo na kuelekea sehemu ya ndani ya ule mgahawa na kujificha nyuma ya magunia ya mkaa, ile napoteza tu kichwa, nilisikia amri ikitaka wote tutoke mle! Ilikuwa taharuki kubwa iliyofanya kila mtu aache kula, wakatio huo Lau aliingia kwenye gunia na kujikunyata kama mzigo kisha kulala chini.
Askari waliamuru watu wote watoke nje na kwa amri ile waliitii, ilisikika miguu ya askari akitembea mule ndani akaja upande wangu na kupitia upenyo wa magunia yale nilimuona akimkanyaga lau ndani ya gunia, ni kama alistuka na kuinama kuangalia ila akapita na kuja mpka pale kwenye magunia kisha akarudi pale kwenye meza na kuanza kula vyakula vilivyoachwa na wateja. Ilionesha alikuwa na njaa kali mno ndani ya tumbo lake, nilimshuhudia akitoka huku nje sauti ya mama akilalamika sana ilisikika kwa uhafifu kwenye ngoma za masikio yangu
"mniache mimi mgahwa wangu nalisha watoto baba yao alikufa na hao watu siwajui" kwa malalamiko yale ilionesha kabisa alikuwa ni mmiliki wa mgahawa ule. Niliumia sana roho ya huruma ilinijia nikifikiri taabu apatazo mama ambaye akaachiwa watoto tena wanaosoma baada ya mumewe kufariki, hakika iliniuma sana.
*********** ************** ***************** ***********
*********** ************** ***************** ***********
Jiji kuu Dar Es Salaam. Usiku...
Kituo cha Polisi Osterbay jijini Dar Es Salaam askari watatu wakiwa kwenye sare zao walikuwa wakifanya kikao cha kupeana mikakati. Kila mmoja alionekana makini mno huku wakisikilizana kwa usikivu mkuu. Kilichokuwa kikijadiliwa ni kuhusu taarifa walizozipokea jioni. Taarifa hiyo ilitoka kwa mama mmoja ambaye alijieleza kupotelewa na mwanae wa kike wa pekee tangu akiwa chuo kipindi cha likizo.
Kwa udadavuzi ilionekana kama mama ni mzembe kwani muda mrefu umepita toka likizo. Ijapo mama alieleza kuwa hakujua kama mwanae kapotea ni ukimya wa mwanae huyo ndio uliomstua sana. Maelezo yaliyosomwa yalionesha kuwa binti aliyepotea ni Irene Huang. Mwanadada wa chuo cha Dar Es Salaam. Kulingana na maelezo ilionesha kuwa mama yake mjane hakupata taarifa mapema.
Askari wale waligana majukumu. Mmoja alipewa jukumu la kwenda kutafuta habari juu ya kutoweka kwa binti huyo katika chuo kikuu cha Dar Es Salaam. Mwingine alipewa jukumu la kwenda kutafuta taarifa za mawasiliano yake tangu siku anapotea. Huyu alitakiwa kujua nani aliwasiliana na Irene siku ya mwisho na maeneo gani alikuwa akiwasiliana nae kupitia simu. Askari wa mwisho alipewa jukumu la kuhakikisha anampeleleza zaidi mama yake na Irene ili ajaue sababu za kupotea na wapi wanahisi yupo. Baada ya majadiliano hayo yaliyodumu takribani nusu saa kila mmoja alitawanyika na kuendlea na majukumu mengine wwakisubiri kesho kufanya kile walichopangiana.
Wakati huo nyumbani kwa mama Irene , ilikuwa ni majonzi tele. Mama alikuwa akilia hasa alipotazama picha ya bintie ukutani. Alivuta kabati la nguo na kutoa albamu ya picha. Akianza kuangalia moja baada ya nyingine. Alikutana na picha ya mwanaume, akiwa kavalia suti. Kuiona picha ile kulileta kilio kikubwa mno. Ilikuwa picha ya marehemu mumewa baba Irene. Mawazo zaidi yakamjia, akikumbuka jinsi alivyoishi na mumewe huyo kwa upendo. Picha hii ilimfanya akumbuke kifo cha kutatanisha cha mumewe kilichotokea muda sio mrefu. Machozi na simanzi vilimfika shingoni mjane huyu na kumfanya alie sana. Aliwaza juu ya binti yake kipenzi Irene, mtu pekee aliyekuwa kabakia katika hii dunia. Mawazo yake yakapingana, huenda mzima huku roho nyingine ikimwambia huenda kafariki. Alilala juu ya meza tena bila kula kabisa kwa maumivu ya uchungu wa mwananae..
******** ********* ********* *********** ***********
Nilisikia kipila kile cha polisi kikiondoka kwa kwasi na watu wote waliokamatwa katika mgahawa, ukimya ulitawala sana nilimuangalia Lau kwenye lile gunia na kumuona akiwa mkimya pia, sikutaka kuwa na papara ya kuinuka nilisubiri mpaka Lau akiamka ndio niamke. Kutokana na kujibana vibaya pale kwenye magunia bila Lau kuamka nilihisi maumivu ya makali sana ya miguu ila nikajikaza, haukupita muda niliona Lau akianza kujitoa ndani ya lile gunia.
Alitoka nikatoka pia na kumuangalia usoni Lau alikuwa akivuja damu nyingi puani, ilikuwa kawaida yangu kustuka mno nionapo damu
"Lau pole kuna nini"
"Yule askari alinikanyaga puani, kiatu chake kigumu sana nilihisi maumivu makali mno, kama nisingekuwa imara hakika ningepiga yowe la maumivu"
"Pole sana, ndio maana nilimuona askari kama kastuka kitu vile"
"Ndio niliamua kujikaza kwa kuwa sikuwa na namna ya kufanya, nadhani kile kiatu kingetua kwenye mwili wako ungepiga ukelele wa maumivu"
"Pole sana" nilimwambia Lau na kuanza kumfuta Damu zile puani, wakati huo wote Lau alikuwa kimya, nilimaliza na kuhakikisha hazitoki tena kisha nikachukua maji ya baridi yaliyokuwepo ndani ya mgahawa ule na kamkanda Lau kwenye paji lake la uso.
Nilisimama na kumkumbatia huku nikifikiri mbali sana juu ya yote ninayopitia, hakika nilimwamini sana Lau, ule usemi wa mwalimu wangu wa chuo wa kusema don't trust any one ukaja kichwani ila nikaupotezea haraka, kumbatio lile lilinipa joto mwanana kwenye kifua kilichojitenga vema na chenye mazoezi cha Lau. Nilihisi niko mbali mno, nikamkumbuka Franc, nilimuangalia Lau kwa macho fulani ya hamasa yaani ya kuonesha kuwa nilifurahia sana kumkumbatia, Lau alisogeza mdomo wake karibu na wa kwangu nilihisi macho yangu yakipoteza nguvu ya kuona na kujikuta yakijifumba taratibu kama mlevi mwenye usingizi.
Nikiwa sioni nilipokea busu zito mdomoni na kufanya nihisi kupigwa ganzi mwili mzima, kitendo kile kilifanya nimpe Lau ulimi wangu naye akafanya hivyo kweli tulikuwa ulimwengu mwingine.
Kama haitoshi, Lau alishusha mkono wake na kugusa kiuno changu, nilihisi raha sana nilizidi kumkumbatia zaidi kwani mwili wake ulikuwa wa joto sana, mkono wake haukuishia hapo Lau aliupandisha taratibu, ukatua kwenye kifua changu na kukutana na matiti yangu madogo, nilijikuta nikilalamika polepole kwa kuguswa na mikono yake yenye joto kwenye maziwa yangu madogo kwani sikuwa hata na brazia katika mwili wangu. Mshike mshike patashika, ilitawala. Kila mmoja akijaribu kumuonesha mwenzake uwezo wake katika tasnia ya mapenzi..
Ilikuwa vurugu patashika nikiwa kwenye ulimwengu mwingine kabisa, akili ikanihama sikujali mazingira tuliyokuwepo. Kweli mapenzi yana nguvu ya ajabu na hisia zina sumaku ya asili haijalsihi uko wapi. Nilistuka baada ya kuhusi mkono wa Lau ukiwa umetua kwenye kifungo cha suruali yangu na ikiwa imefunguka huku vidole vyake vikitalii maeneo yale, kustuka kule hakukuwa kwa kutisha haukupita muda Lau alinibusu. Bado mikono yake ilinipa raha ajabu. Aliongezea busu lenye ujazo na kuniachia huku akinitazama kwa macho yake yaliyojaa mahaba. Macho yangu yalijaa mahaba kiasi cha kutoona vyrma. Lau alisitisha zoezi lile na kukata utamu njiani huku akitahadharisha kuwa tupo kwenywe hatari hivyo ni vema tuache kile tunachofanya.
Nilimuachia kishingo upande na kuona kama muuaji aliyeziibua na kuchokonoa hisia zangu za mapenzi na kuniacha katika kiu kuu ya tendo. Mwili ulikuwa ukitetemeka na macho yangu yalikuwa hayaoni vizuri hadi nilisahau kuwa pale palikuwa mghawani na tulienda kwa lengo moja tu nalo ni kula. Ni kama njaa ilinipotea hivi. Lau aliniacha pale chinj na kuingia ndani ya ule mgahawa akatoka na sahani la wali na chupa ya chai, alimimina chai na tukaanza kula, sikuwa na hamu akili yangu yote ilikuwa kwake nikimungalia kwa kuibia kila nilipopata nafasi ya kumuangalia, kuna kipindi macho yangu yaligongana na yake
"Irene unajisikiaje?"
"Niko kwaida tu" nilidanganya ila ukweli niliumia sana kwa kiyendo chake cha kuniacha na hisia kali za mapenzi, nilishindwa kumwambia tu kwa kuwa nilikuwa mwanamke.
"Kula au hupendi chakula? Jitahidi tuondoke hapa kwani si salama"
"Saa tano hii tutaenda wapi Lau wangu? "
"Tukikaa hapa kunauwezekano wa askali kurudi, pia huu mgahawa Rama na Chriss wanaujua vema kwa kuwa kila mara huwa tunakuja hapa tukitoka kule." alisema Lau akameza funda la chakula kisha kuendelea kuongea.
"Wanaweza kutoka kule wakitufuta na kuja kutukuta hapa tukawa matatani. Kumbuka nia yangu ni kulipa kisasi kwa rafiki yangu Franc na wewe, hapo ndio roho yangu itatulia tuli! "
"Sasa tunaenda wapi? "
"Tutoke tutajua cha kufanya"
Lau aliingia sehemu kwenye ule mgahawa na kutoka na koti na sweta, alinikabidhi sweta na yeye kuvaa koti kubwa kisha akanikumbatia tena, sikupenda kwa kuwa alitaka kuamsha mwili wangu ulioluwa ukipowa kwa kunyimwa penzi lake.
Aliniachia na kunishika mkono, tukaanza kutoka na kukata mitaa, kadhaa kwa kutembea kwake ilionesha Lau alitambua vema mitaa ile.
Tulifika sehemu nje ya nyumba Lau, aliangaza huku na huko kisha akaingia ndani na kutoka pikipiki, kama kawaida alifanya ujanja wake ikawaka, tukaanza safari usiku ule
"Tunaenda wapi usiku huu"
"Nataka tufike mahalia ili pa kupanda basi ili kesho twende Dar"
"Tutafika salama kweli? "
"Mumgu mwema, pia Upo na mimi Lau hutakiwi kuogopa kitu kabisa siwezi kufanya kosa"
"Haya twende baba" nilimjibu na kumshikilia vyema, tukaendelea na safari. Ilikuwa ndefu mpka nikahisi usingizi na kulala nyuma ya mgongo wa Lau, sikuhofia kudondoka kwa kuwa barabara Ilikuwa ya lami na Lau aliendesha kwa mwendo wa kawaida....
Nilistuka baada ya kumulikwa na mwanga mkali usoni, macho yangu yaliyojaa usingizi yalifumbuka haraka na Kwa ukali wa mwanga ule sikuona chochote kile.
Niliyafikicha macho, nikasikia sauti ya amri ikiniamuru nishuke. Nilishuka na kwa sekunde kadhaa kuamsha akili yangu iliyohisi zile ni ndoto, kumbe hazikuwa ndoto, tulikuwa tupo kwenye kizuio cha polisi yaani mizani.
"Kwanini mnamnyanyasa abiria wangu?"
Alisikika Lau kwa ukali akiwa kwenye ile pikipiki wakati huo nikitua chini huku Lau akiwa kainamisha kichwa chini.
"Usiku huuu mnaenda wapi?
"Nampeleka huyu mteja akawahi basi la Dar kwani ana haraka"
"Huna helmet, hujavaa nguo nzito, abiria pia hana helmet! Iko wapi leseni yako ya udereva? "
Aliongea askari aliyeoneka machachari kweli, lau aliingiza mkono wake mfukoni na kisha kuchomoa leseni na kwa kabidhi. Askari aliingalia, wakati huu macho yangu yalurudi kawaida kabisa na niliona vizuri, bado askari yule kiherehere akahoji
"Huja renew leseni yako, what the hell you idiot" alikuwa mkali huku akionge kwa kuchanganya kiswahili na Kiingereza.
Lau alibaki kimya, sio muda tukiwa na Lau pale kizuizini wakikataa kufungua geti, radio call ya askari yule iliita, wakaongea.
"Hallo sagent, ni koplo John Kifaruhande hapa"
"Ndio Afande, nawapa taarifa kuwa kuna watu wawili mwanaume na mwanamke yule muuaji mkubwa wametoroka huku kihorogota, wanatumia pikipiki kuanzia saa hizi pikipiki zote zikaguliwe na magari pia"
"sawa mkuu, tutalitekeleza vizuri!"
"msifanye upuuzi kuna mpunga mrefu mno"
"sawa sawa kamanda" maongezi hayo yalisikiwa vema mno na mimi na Lau kwenye ile radio call, askari yule alikata ile radio call na kutuangalia kwa kupokezana kisha akatwambia kwa usalama wetu tumfwate ndani.
Akili yangu iliamka na kuwa Tayari Kwa Mapambano, miguu ikawa mizito kwa mimi kusimama kuingia kituo cha polisi. Askari hakukawia, alinipiga konde la kichwa kwa ugumu wa ngumi ile nilihisi kutishwa gunia la viazi kichwani ikifuatiwa na kizunguzungu...
Itaendelea
Usikose 14
Usikose 14
No comments:
Post a Comment