Showing posts with label Simulizi. Show all posts
Showing posts with label Simulizi. Show all posts

Wednesday, November 8, 2017

Simulizi SITAMSAHAU FRANC EPISODE 15

11/08/2017 11:57:00 AM 0
Story::::           SITAMSAHAU FRANC
Mwandishi ::   FRANCO SAMUEL
Whatsapp ::    0768800687
Episode ya 15.....

 Ilipoishiae Episode iliyopita...

Taarifa zilipelekwa kwenye ubongo wa nyuma kisha mbele na kumbukumba za ubongo zikanambia hao ni Rama na Kriss wale wa kule porini. Lau aliniangalia na kunipa ishara fulani kama wanenavyo wahenga kuwa waswahili wa pemba hujuana kwa vilemba. Bila kuchelewa nikamuona kondakta akitoka kwa hasira na kumkwida Kriss ambaye alimuangalia tu kondakta bila kumfanya lolote. Kondakta kuona vile kwa hasira alimpiga Kriss Ngumi ya uso, Kriss wala hakutikisika badala yake alimtandika kondakta kofi moja lilompeleka chini kama gunia la viazi na kumfanya apige ukelele wa maumivu makali mno.

Walimuacha  kondakta akiugulia maumivu na kimadaha Kriss na Rama wakaanza kuja kwenye basi. Sijui nani aliwaonesha kuwa tuko kwenye hili gari, nilijikuta nikiwaza bila jibu. Nilijua tu ni mimi na Lau ndio mawindo yao. Na kweli wametupata. Hakuna pa kukimbilia. Abiria walianza kupiga mayowe ya hasira huku wakiwa hawajui nini kinaendelea.  Mimi,  Lau,  Rama na Chriss ndio tulikuwa tunaujua mtanange mzima.

Songa nayo hapaa


Rama alionekana mwenye hasira nikakumbuka maneno ya Lau kuwa huwa hana utani hasa awapo kazini.  Ulikuwa mtihani mwingine wa kuukabili mimi na Lau, kwa misuli waliyokuwa nayo akina Rama na Chriss sikuzani kama tutaweza na niliona mwisho umefika wa maisha yetu.
"Lau tukubali tu yaishe acha tu watukamate. Maana sioni tumaini  la kuokoka hapa kabisa" nilimwambia Lau kwa sauti ya kukata tamaa. Lau aliniangalia bila kisema chochote kile,  Wakati huo walikuwa wanaingia kwenye basi. Kwa muonekano wa macho yao mekundu nilibaini wamevuta kitu cha Arusha au kama sio hivyo basi wana hasira kali mno.

"We msaliti toka nje faster na tusipotezeane muda" alifoka Rama huku akimkazia Lau macho yake mekundu.  Sasa watu wakawa wakiangalia picha lililoibuka bila hata director wakiwa hawajui mwanzo wake. Lau alikausha kama hajasikia,  Rama kuona vile akatifuta pale kwenye siti. Kriss muda wote alikaa mlangoni.  Nilichungulia nje akili ikanituma kuruka kupitia dirisha. Wakati nikijianda kuruka Rama alimkamata Lau na kuanza kumtoa nje kwa nguvu,  kabla hajafika mlangoni kondakta alikuwa kaamka na kuanza kumshambulia Kriss aliyekuwa mlangoni. Mapigano yale hayakumuacha kando dereva kwani nae aliachia usukuni kwankulizima gari na kuanza kumshambulia Kriss akiwa na lengo la kumuokoa kondakta wake aliyeonekana kuzidiwa na makonde yenye ujazo aliyotupiwa na jitu lenye mwili wa mazoezi Kriss.

Rama akiendelea kumlazimisha Lau ashuke huku akimshikilia alipokea teke la tumbo lilimpeleka chini na kumfanya aisalimu lami. Teke hilo lilirusha na Lau kwa ustadi kabisa na Rama hakutarajia kama angepokea teke la tumbo toka kwa adui yake Lau. Kudondoka tu gari lilipita nusura limgonge ila akalikwepa kwa ustadi na haraka. Watu kwenye basi walibaki wakishangaa,  huku akina mama wakifumba macho wasione kinachoendelea. Baadhi ya abiria kama kawaida wakachua simu na kuanza kupiga picha huku wengine wakirekodi video ya filamu iliyoanza bila hata muongozaji.

Rama alijitahidi kuamka ila Lau akamshindilia kwa ngumi ya uso na kumfanya aendelee kulala pale chini. Wakati huo Kriss alionekana mtata kwa kuwasambazia kipigo Kondakta na dereva. Masikini kondakta uso wake ulivimba pima kama mtu aliyeng'atwa na nyigu.  Niliwashangaa baadhi ya wanaume wakiwa kimya ndaninya basi bila kwenda kuamlia ugomvi. Akili ikanituma kushuka nikainuka na kushuka haraka ila nilipofika mlangoni nilipigwa kikumbo cha tumbo na Kriss aliyeoneka bado ana utawala mpambano ule.

Tumbo lilizizima kwa maumivu ya kikumbo kisichotarajiwa toka kwa Kriss. Lau akanipa ishara ya kuondoka pale.  Sikujua hata kwa kwenda,  tayari watu wengine walishuka na kuafanya wapita njia  kukusanyika. Rama aliinuka na kuanza kumshambulia Lau kwa makonde ya ngumi za uso,  tumboni na kifuani. Kweli ilikuwa kutesa kwa zamu. Lau  alipigwa ngumi nyingi mfululizo nikashuhudia akidondoka chini. "sasa nimekwisha leo siponi kabisa" nilijisemea na jasho likanitoka licha ya kuwa ile ilikuwa ni   asubuhi kabisa.
Dereva bado alipambana na Kriss akafanikiwa kumkata ngebe kwa ngumi ya uso. Rama alimsogelea Lau pale chini na kuanza kuinama ili amsulubu vema adui wake lakini wakati akiinama alikutana na teke la uso kutoka kwa Lau. Teke lilimfanya akadondokee mgongo na kisogo na kuugulia maumivu.

Niliona kama Lau amefufuka vile, aliinuka na kunishika mkono tukaanza kukimbia. Mbele kidogo kulikuwa na  magari mengi. Watu wakawa wanatushangaa tu. Niligeuka nyuma nikamuona Kriss akija kwa kasi ya ajabu, spidi ya Lau ilikuwa ndogo nikaanza kumvuta. Mbele kidogo tukaikuta taxi,  bila maneno Lau alifungua mlango na kuzama ndani bahati nzuri dereva alikuwa ndani na gari likuwa limewashwa.

"Ondosha gari haraka kijana Kuna hatari" alisema Lau huku akihema. Kuona vile dereva hakuwa na ubishi aliondosha gari kwa sipidi kali sana. Nilichugulia kupitia tinted na kumuona Kriss akilikaribia gari,  aliiruka gari na kutua nyuma huku akijaribu kujishikiza vizuri.
"Lau Kriss huyo nyuma ya gari kashikilia kweli" nilimstua Lau akiwa anahema huku damu ikimtoka puani.
"Oya dereva piga break fasta na ondosha gari" dereva alipiga break,  hali ile ilifanya Kriss kukosa balance akagonga kioo na kudondoka kisha gari likaendlea. Tabasamu likachanua usoni. Nikamuona Lau bonge la shujaa. Nikamuangilila,  usoni amevimba huku akitoka damu puani. Niliumia sana, kweli mapenzi kitu kingine, mateso yote haya kisa penzi la Franc..

"Lau pole sana,  nitakupa kitu kizuri tukipona katika hii hatari" niliongea kwa unyonge ila Lau akaonekana kukoroma tu na ni kama alikuwa hasikii ninachoongea!  Nikawaza hivi akiuliza hicho kitu kizuri nitajibu nini,  sikupata jibu.Nilimfuta damu, kwa kutumia tisheti,  wakati huo dreva akiwa kimya akiendesha gari kuitafuta Dar Es Salaam katikati ya mji. Alipoona natumia tisheti,  alipunguza mwendo na kutupatia kiboksi cha first aid.  Nilichukua na kufungua nikatoa pamba na iodine tincture na kunza kufuta ili damu ingande isiendelee kuvuja. Lau alilalamika kwa maumivu kisha akatulia kidogo.
"Nawapeleka wapi maana hata sijui tunakoenda" aliuliza dereva.  Sikuweza kujibu,  kwani sikujua anapokaa Lau japo kwetu ni Osterbay meeneo ya Masaki. Nilimstua Lau na kumuuliza wapi dereva atupeleke akamwambia dereva atupeleke Ubungo External. Dereva aliendesha gari na kujitahidi kuzikabili foleni kwa kupita njia za mkato zaidi. Haikuchukua muda, tulifika maeneo ya Ubungo External huku Lau akiomba dereva aingize gari ndani zaidi ili tusionwe na watu.

Mbele kidogo tulishuka na tukatembea nikimfuata Lau. Hatua kadhaa mbele yetu kulikuwa ilikuwa nyumba  chakavu na kuukuu ya muundo wa zamani. Alitoa ufunguo na kuanza kufungua kitasa kilicholeta mgomo kwa muda kutoka na kutu. Afadhali kwani watu walikuwa wachache na niliona tulikuwa sehemu salama kabisa..Alifanikiwa kufungua kitasa na kunikaribisha ndani nikaingia, aliongoza moja kwa moja chumbani na bada ya muda alitoka na noti za hela na kwenda kumkabidhi dereva.
Akarudi na kuja kukaa kwenye sofa,  nilijkutaa nikimkumbatia kwa nguvu na kumbusu Lau kwenye paji la uso. Sikujali majeraha na michubuko aliyonayo..
*****
Askari aliyekuwa akifanya uchunguzi TCRA aliridhika na taarifa na kugundua kuwa mara ya mwisho simu ya Irene ilitumika huko Iringa mjini na sasa simu hiyo ilikuwa ikitumika na mtu mwingine aliyeko Mufindi. Japo laini ya Irene ilikuwa haijatumika muda mrefu. Aliridhika na taarifa akamua kurudi kituoni Osterbay majira ya saa tano na nusu asubuhi.
Askari aliyekuwa chuoni,  hostel ya Mabibo Hall 5 Chumba A6 alikuwa akipiga stori na wadada waliokuwa hapo chumbani. Stori za hapa na pale ziliwavuta wadada hao na kufanya wajikute wakitoa ubuyu bila kujua.

"Eti hivi humu mnakaa watatu tu?" alihoji asakari akiwa kavalia nguo za nyumbani.
"Hapana bwana tupo na mwenzetu ila kwa sasa hayupo hapa chuoni" alijibu moja ya wananafunzi hao

"Yuko wapi na saaizi ni muda wa masomo"

"Kutoka tufunge aliondoka bila kuaga. Baaada ya chuo kufungua akawa hajaja. Muda ukaenda kimya bila simu,  tulipiga simu yake haipatikani. Na bahati mbaya hatukuwa na namba za Wazazi. Pita pita katika notsi board ndio tukaona  jina lake likiwa ilimebandikwa kama moja na wanafunzi waliochelewa kusajiliwa hivyo,  asingeendelea na masomo.  Juzi juzi tumepata taarifa kuwa mwenzetu kapotea na haonekani" alijieleza mwanadada.

"Kibaya zaidi,  Irene hakuwa mtu wa kujichanganya na watu sana.  Pia wakati mwingi alipenda kukaa pekee na sio mtu wa kuongea sana. Hatujui yuko wapi, nini kimempata na kwao hatukujui" aliongezea dada mwingine..

"Okay sawa,  kwanini hamkutoa taarifa mapema?" alihoji askari

"Isingekuwa rahisi kwa kuwa hatukujua yuko wapi. Ujue wakati mwingine mtu anaweza chelewa maybe kakosa ada na some other reasons so haikuwa rahisi kwa sisi kujua hilo" alijubu mwanafunzi mwingine.

"Mie niwaambie ukweli, nipo nafanya upelelezi. Tumepewa taarifa na mama Irene kuwa mwanaye hapatikani.  Mbaya zaidi mumewe yaani baba Irene amefariki kifo cha kutatanisha mno. Kwahiyo nashukuru kwa taarifa zenu. Naondoka!"  Masikitiko na majonzi zikawajaa wadada waliokuwa wakikaa na Irene,  nyuso zikajikunja ila askari akawapa moyo kuwa Irene yu mzima. Aliwatuliza  na kuondoka zake tayari kurudi kituoni kitoa taarifa.

Askari aliyekuwa akimpeleleza mama Irene alimuuliza kuhusu uhusiano wake na ndugu wengine. Mama Irene aliona swali lile kama gumu sana. Alafikiri na kumweleza askari kuwa amekuwa akiishinna watu. Japo mumewe alikufa kifo cha kutatanisha baada ya kupotea kwa siku tatu na kisha mwili wake ukaja kupatikana ukiwa umeharibika kabisa hali iliyolazimu kuzikwa kwa haraka. Alieleza siku zote tokea mumewe apotee hakumtaarifu binti kwani aliogopa kumchanganya na masomo.  Baada ya kupatikana kwa mwili ndio nikampigi simu na iikiwa likizo hakupatikana, nikajua labda ubize na chuo. Ikanilazimu kuja na chuo pia wakasema hayupo. Hata waliokaa nae chumba kimoja wakadai kutojua alipo. Maelezo ya mama Irene yalijitosheleza na kumwacha askari pasi na walakini.

"Pole sana kwa matatizo,  mwanao atapatikana akiwa mzima wa afya kabisa. Sisi tutajitahidi. Nakuomba uende nyumbani ila acha simu namba ya simu tutakupigia" alisema askari na kumkabidhi mama Irene kijitabu kidogo akaandika namba na kuondoka huku chozi likimtoka

"Mume wangu kafariki kwa kifo cha kutatanisha na mwanangu huonekani, mwaniacha na nani huku ugenini?" alijisemea mama Irene huku chozi likizidi kutiririka.

*******    ******* **********
Niliendelea kumbusu Lau na kumkubatia kwa muda. Uso wake bado ulivimba baada ya muda tulisitisha zoezi la kukumbatiana huku Lau akinambia tupike. Alinionyesha jiko lilipo katika nyumba yake hiyo chakavu kwa nje ila kwa ndani ikiwa ni nzuri. Kama mtu angepita tu kwa nje hata asingejua kama ndani kuna vitu vya thamani kiasi kile. Kulikuwa na masofa mazuri,  kabati,  flat Screen TV kubwa ya maana na pia vyombo vya thamani sana. Ijapo vumbi lilivamia kwa kuwa muda ulipita bila mtu kukaa mle kwenye nyumba. Kweli Lau alikuwa vizuri. Niliwasha jiko la gesi na kupasha maji. Niliingia Karibu kila chumba isipo kuwa alichokuwa Lau, vyumba vyote vilikuwa ni self contained. Baada ya maji kupata uvugu vugu nilimwita Lau na kumkanda kanda. Kidogo uso wake ukapungua uvimbe uliokuwapo na akawa amebakia ni michubuko na majeraha madogo.

Nikaweka maji na kumuomba akaoge. Allikubali kufanya hivyo na wakati huo nikafanya fanya usafi wa nyumba. Nilipukuta vumbi illotanda kila mahali ikifuatiwa na deki. Lau baada ya kutoka kuoga alipiga simu na kuongea na mtu. Sio muda gari ilikuja na kushusha baadhi ya vitu vya kula. Nilipika chai ya maziwa nikamwita mezani tukala. Njaa ilikuwa kali sana. Niljikuta nikila chapati kama sio mtoto wa kike hadi Lau akanishanga. Baada ya kula nikamwomba niende kuoga. Sikujua hata nikioga nitavaa nguo gani.

Niliingia bafuni moja ya vyumba vya mle ndani nikawa naoga. Nilisikia mtu akigonga mlango. Nilijihisi vibaya sana maana niijua ni Lau tu. Aligonga kisha akasema baada ya kuona niko kimya.

"Nimekuletea taulo Sorry nilisahau kukupa muda unaenda kuoga." alisema na kisha nikasikia hatua za miguu zikitembea kuashiria alikuwa kaondoka. Bila kuchelewa nilifungua mlango nusu na kulichukua taulo. Nilioga haraka baada ya kupata wazo la kumpigia mama.
Nilitoka bafuni na kuelekea chumba alichonionesha Lau. Nilifurahi sana baada ya kukuta nguo mpya,  gauni,  kibrazia kidogo kama vile alinipima mimi na chupi. Pia kulikuwa na mafuta ya kupakaa pale. Nilimshukuru Mungu ila nikawa naona aibu. Nikajiuliza Lau kajuaje size ya nguo zangu. Nilienda mbali zaidi na kufikiri huenda nguo hizi alimnunulia mpenzi wake. Wivu ukanikaba nikiwaza akija huyo mtu wake itakuwaje. Lakini tena zilikuwa mpya kabisa  zikinukia dawa za dukani,  liwalo na liwe nilisema. Kisha nikaanza kujipaka mafuta. Nilidondosha taulo na kujiangalia kwa kioo kilichokuwa mbele yangu. Nilikuwa nimepungua sana na kupauka.

"Mungu asante Leo naenda kuonana na mama yangu kipenzi."  Nilijisemea na kuchukua chupi ili nivae. Sijamaliza kuvaa mlango ukagongwa na kufunguliwa kwani nilikuwa nimeegesha tu. Nikazubaa tu kama kuku mwenye kideri na kukodoa macho mlangoni kucheki nani alikuwa akiingia. Ni Lau ndio alikuwa akiingia. Alistuka baada ya kuniona nikiwa karibu uchi kwani nilikuwa nimevaa chupi tu. Nikaanza kujificha kwa kuokota taulo haraka huku mkono mmoja nikijitahdi kificha manyonyo yangu madogo Lau asiyaone.

"Lau sijavaa bwana naomba usibiri please" nilisema baada ya kuhakikisha taulo imenikaa vyema. Bado alisimama mlangoni bila kusema kitu. Ubongo kitu kingine kabisa, nikahisi pengine anataka penzi.  Nikamuona mjinga, anawaza penzi wakati mimi hata wazazi sijui wanaendeleaje..nikiwa katika kuwaza Lau akasema..

"Sorry sana ila nilikuwa nataka.. nataka nikwambie kitu kimoja hivi" aliongea kwa kukata kata sauti yake sikujua sababu yake ni nini. Kwa sauti yake ya uoga nikahisi kabisa kuwa fikra zangu za kumuhisi akinitaka kimapenzi zilikuwa sahihi.  Sikujibu chochote nikabaki kimya tu. Nadhani alipoteza point baada ya kuniona nikiwa vile bila nguo.. "ila nahangaika nini,  mbona alishaniona toka kule porini,  pale mgahawani alinishika shika shida ninil? " niliona yuko sahihi kutaka penzi langu ila muda haukuwa sahihi kwani mimi fikra zangu zote zilikuwa kwa wazazi na kufika nyumbani.

"Ukimaliza kuvaa njoo chumbani kwangu tafadhali" alinistua Lau na kunitoa kwenye mawazo yangu ya kijinga. Alifunga mlango na kuondoka kuelekea chumbani kwake. Nikavaa huku nikiwaza huko chumbani kuna nini? Kama kuna cha kuongea si tukutane tu sebuleni? Mawazo mengi yaliniandama hadi nikahisi kichwa kuuma.  Nikatoka baada ya kuvaa na kwa hatua za uoga nikaanza kutembea kuelekea chumbani kwa Lau. Nilifika mlangoni na kuchungulia nione anafanya nini. Alikuwa akibonyeza kicharazio cha kompyuta mpakato yake. Nikawaza anataka nini kwangu? Liwalo na liwe niliamua baada ya kufikiri kwa dakika kadhaa kisha nikagonga mlango kwa woga
"ngo ngo ngoo"
"Ingia tafadhali" alisema Lau akiwa ndani ya chumba chake kunikaribisha.. Nikashika kitasa tayari kuufingua mlango wa chumba cha Lau.

Itaendelea..
Je Lau anataka nini kwa Irene?
Tuseme ndio anataka malipo ya msaada aliompa Irene?
Wanaume Mungu anawaona...
Bado kuna mengi utayajua.
Usikose  iko hapa 1 6...http://francosamuel.blogspot.com

Saturday, November 4, 2017

Simulizi KISASI LAZIMA 1

11/04/2017 08:38:00 PM 0
RIWAYA:KISASI LAZIMA
mwandishi : Franco Samuel
WhatsApp : 0768800687

Episode 1...
Picture arts kwa hisani ya Mtandao 
 

Alikuwa akifanya mazoezi mazito na magumu mno tofauti na siku zingine. Mwili wake uliojengeka vizuri kwa mazoezi ulitoa jasho kila sehemu na kufanya nguo alizovaa kuloa na kunata mwilini hali iliyofanywa mwili ujichore kama wacheza vigodoro na khanga moko waliomwagiwa maji.  Alidhamiria kupiga push ups mia tatu na kisha kufanya zoezi la target kwa muda ili kujihakikishia uwezo wa kulenga shabaha.

Alizipiga push ups kwa staili tofauti tofauti na mwili ulizidi kuloa jasho chapachapa. Baada ya hapo alichukua bastola yake aina ya Berretta na kupakia risasi kisha kulenga kwenye mchoro wa mtu uliokuwa umewekwa ukutani. Alipiga risasi ya kwanza ikatua kichwani kwenye ile picha. Rusasi ya pili ilitua kwenye kifua upande wa kushoto na kulenga moyo moja kwa moja. Risasi ya tatu ilitua kwenye paji la uso na kufanya tobo kubwa mno kwenye ile picha kubwa... 


Alichomoa magazine na kujaza risasi kisha akarirudia zioezi lile na kufanikiwa kurudia mule mule. Safari hii risasi ya mwisho ilipiga kelele sana na kufanya watu waamke. Huyu ni Immanuel Huang kijana wa umri wa maika 20. Kijana mdogo ila hatari sana ndani ya taifa la Tanzania kutokana na uwezo wake. Licha ya kutafutwa kwa muda muda mrefu na vyombo vyote vya usalama kuanzia police, mashushu na watu wengine hakuna aliyejua yuko wapi na wapi anaishi. Hakuna aliyekuwa na uhakika kama Immanuel Huang alisoma au hakusoma. Hakuna aliyekuwa na uhakika kama Immanuel Huang alikuwa na wazazi ama laa. Ilibaki kitendawili kikubwa mno hasa jina lake la pili la Huang kwani siyo jina halsia la kitanzania. Wengi walijua kuwa kuna siri kubwa ila nani angezitoa siri za kijana huyu?  Kwa matukio na vitu alivyofanya watu walimuogaopa na yeye alijiita Imma The Boy... The silent Killer...

*** ***
Mlio wa risasi ya mwisho ya Imma The Boy ulimuamsha binti mrembo aliyekuwa kapiga usingizi wa asubuhi. Baada ya kukurupuka binti yule alitazama huku na huku na kupapasa kitandani kama vile alikuwa akimtafuta mtu. Aliinuka alikiwa kavalia nightdress ya rangi nyeupe iliyoangaza na kuonyesha mwili wake ulioumbika vema. Binti alikuwa mrembo, mwenye macho ya ujazo wa wastani  na kiuno kilichojengeka vema kabisa. Mviringo wa kifua chake chenye  maziwa magumu na chchu  zilizosimama wima kama vifuu vya nazi vilivyochongwa ulifanya aonekane mariddadi zaidi na kumtia miadi mwanaume yeyote ambaye angepita  katika upeo wake.  Alitembea kiuvivu na kufanya makalio yalikaa vema kwenye nyonga yake kutiskika kwa step huku akielekea mlangoni. Miayo ilimjia kivivu akipiga miayo kuashiria alikuwa kusawiri uchovu wa usingizi. Alitembea kila hatua kwa umakini ili asisikiwe na mtu. Alifika mlangoni mwa jumba lile zuri na kukishika kitasa polepole alizungusha ili kufungua mlango. Alizungusha bila mafanikio akagundua kuwa mlango ulikuwa umefungwa kwa nje. Kidogo alipigwa na butwa na kuanza kuangaza huku na kule ndani ya chumba kile kizuri kilichojaa vifaa vya thamani kubwa mno. 


Ghafla mlango ulifunguliwa na aliyeingia haukuwa mwingine bali ni Immanuel Huang "Imma The Boy " kama wengi walivyozoea kumuita. Alikuwa kashika bastola yake aina ya Berretta na alipoinasa sura ya binti yule mrembo aliyekuwa kazubaa aliificha mashine yake kwa nyuma na kuichomekea haraka kwenye sarawili yake ya mazoezi.


Alitembea haraka na kumkumbatia binti ikifuatiwa na busu zito lililotua kwenye paji la uso wa binti yule. Zawadi ya busu ilimfanya binti azizime kwa hisia na kumrudishi Imaa The Boy busu la mdomo. Ndimi zao zikatekenyanya huku wakizidisha utundu kwa kunyonyana midomo yao. Walibaki wakikumbatiana kwa muda huku mikono yao ikitalii maeneo tofauti ya miili yao. Sauti ya pumzi kupanda ilisikika na binti alionekana kuhema sana mathalani ya mtweta kilima afikapo katika kilele kikuu juu ya mlima. Pole pole walikokotana kimahaba na kuingia kwenye chumba kidogo ndani ya chumba kile kilichokuwa kimeandikwa Bathroom. Wakiwa wamekumbatiana bado,  Imma alimtoa binti mikononi mwake na kuvua nguo zake zilizokuwa zimelowa kwa jasho la mazoezi  na kubaki kama alivyozaliwa. Alibonyeza kitufe kimoja kwenye  ukuta na maji ya bomba ya mvua yalianza kutiririka. Yalitoa mvuke na hii iliashiria yalikuwa ya moto. 


Binti hakuchelewa, alifungua kifungo cha kifuani kwenye nguo yake. Aliiachia ikadondoka chini na kubaki kama alivyokuja duniani. Uzuri wake ulionwa na Imaa ambaye ndani ya muda mfupi alianza kuhema huku wote wakiyasogelea maji na kukumbatiana. Maji yaliwatiririkia huku wakipakana sabuni na miili yao ikigusana sana. Haukupita muda kila mtu alikuwa akihema na hakuna aliyeongea chochote. Ni lugha za ishara na vitendo ndio ziliendelea ndani ya chumba kile. Imma alionekana kuvamia kifua cha binti na kuminya minya maziwa yake ya mviringo yaliyogawanyika vema katika kifua cha binti. Walioga kwa mtindo wa kukumbatiana na kufanya kila mtu awe na adhiki na mwenzake. Imaa hakukawia baada ya kuridhika alimuinua binti na kum'beba juu na kutoka naye kisha kum'bwaga kitandani. Michezo ya hapa na pale ilitawala na hakika walionekana kunogewa kweli asubuhi ile huku Imma akionekana kuwatayari kulila tunda lake.

 Dakika kadhaa mbele kitanda kilikuwa kikipiga kelele na kulalamika kwa kuzidiwa na shughuli iliyokuwa ikiendelea. Sio cha Imma wala binti wote walihema kwa nguvu huku waking'ang'aniana mithili ya majogoo yaliyopigana muda mmreu. Walikuwa katika ulimwengu mwingine kabisa wa mahaba huku kila mmoja akijitahidi kumuonesha uwezo mwenzake katika tasinia ya mapenzi. Binti alikata chake kiuno mithili ya mwendo wa feni bovu likigomagoma kuzunguka kisha spidi ikaongezeka haraka kama mcheza mziki wa dance wa zamani Yondo Sister.  

Pindua huku na kule kulifanya jasho ziwatoke wote huku sauti za kulalamika zikizidi kuwatoka bila kupenda. Yess ohhhhh there u fuck me..... Ohhhh that is sweet ....do it harder baby huku vidole vyake virefu vikizidi kutalii kifuani mwa Imma The Boy aliyekuwa kama anafumba macho.  Maneno yote yalimtoka binti huku akizidisha spidi ya uzungushaji wa kiuno chake. Binti yule huku akiwa kama kapagawa alipitisha mkono wake kwenye mto aliokuwa kauegemea wakiwa wanaendelea na shughuli na chini ya ule mto alichomoa bastola. Huku akiendelea na shughuli ile nzito ya kupeana mahaba, aliichomoa Pistol ile na kuisonta kifuani pa Imma. Imma kuona hivyo aliruka kwa kumsukuma binti haraka kama vile hakuwa kwenye ile shughuli ipotezayo nguvu na akili za mtu. Kwa sekunde kadhaa wote walibaki wameduwaa..

"Mary John Kihwana!  U have made a mistake! Yes a big mistake my dear! U think am not clever? Yaani "Mary John Kihwana! Umekosa sana. Umefanya kosa kubwa mno. Unafikiri sina akili? " ni maneno ya ukali aliyoyatoa Imma huku shoka lake la maangamizi likisinyaa kwa kasi ya ajabu. Imma aliendelea kusema.. 

"Umekuja kwangu ukijitambukisha kama Angel John. Nilijua na kukutambua kuwa wewe ni Mary John Kihwana. Najua misheni yako. Na mimi mtu akija kwenye anga zangu huwa simwachi salama. Nakupa dakika mbili,  fanya maamuzi sahihi and I promise you will pay for this. No regrets,  make proper decision"

Maelezo ya Imaa yalimstua mno binti na kumfanya adondoshe bastola yake bila hata kupiga risasi. Imma alimwacha Mary Joh Kihwana afikiri ili ampe jibu. Alivuta kabati pale chumbani na kuchukua suruali tayari kwa kuivaa. Akiwa kainama kuvaa suruali alipokea teke moja lililomdondosha chini na kufanya apige ukelele wa maumivu. Aligeuza kichwa chake na kukutana na bastola ikimsonta pale chini alipotua huku akiwa hajui cha kufanya. Aliyemsonta si mtu mwingine bali ni binti mrembo hatari sana tena akiwa uchi kwa jina la Angel John ijapo Imma alimjua kama Mary John Kihwana!! 

Imma alipata maumivu makali mno kwenye kichwa chake kutokana na lile teke. Pia wakati anadondoka alidondokea kichwa hivyo ni kama akili haikuwa sawa.  Kwa sekunde takribani 30 hakujua afanye nini na binti alimkazia macho huku akikoki mashine na kuishika vema trigger tayari kwa kufyatua risasi. Ulikuwa wakati mgumu mno kwake. Hakuamini kama binti aliyemuamini alikuwa ni shushushuu aliyetumwa kumwangamiza. Akakumbuka mazoezi yake. Akili ni kama ilifanya kazi mara kumi sasa. Alijifyatua pale chini kwa mfumo wa kuteleza na kumpiga binti mateke ya kumzoa miguu yake yote miwili. Mateke yale yalimpleleka binti moja kwa moja chini na kufanya iiasalimie sakafu bila kupenda. Wakati akidondoka bastola yake ilidakwa na Imma aliyejiona ni bonge la shujaa. 

Haraka imma aliinuka na kuanza kumshambulia binti kwa ngumi za uso za mfululizo na  zisizo na idadi wala hesabu. Muda mfupi uso wa binti ulituna pima kama mtu aliyeng'atwa na nyuki huku baadhi ya sehemu zikipasuka na kutoa damu. Macho yake mazuri sasa yalikuwa hayaonekani. Zoezi hili lilifanyika kimya kimya kiasi kuwa hata mtu wa chumba cha jirani asingeweza kutambua chochote. Ngumi zile zenye ujazo ziliendelea kutua usoni mwa binti yule na damu nyingi zikamtoka mdomoni. 

 Imma aliporidhika kuwa kamdhoofisha adui wake alisimama na kumbeba kisha kufungua kichumba kidogo ndani ya kile chumba. Ndani kulikuwa na silaha tofauti.  Pia kulikuwepo na kiti cha umeme. Alimfunga binti yule kwenye kamba kubwa na kuwasha taa kali mno zilizomkabili binti usoni. Alianza kumhoji masawali lakini Mary alikuwa kama kala gundi mdomoni mwake kwani hakujibu chochote.  Kofi na ngumi ziliendelewa kupigwa usoni mwa Mary bila huruma. Mwishowe Imma alichukua camera yake na kupiga picha. Pia ali rekodi video akimtesa Mary na kisha kufunga mlango wa chumba kile. Alichukua kompyuta yake na kuweka video na zile picha...
.Itaendelea... 

Kuna nini kati ya hawa watu?
Ni nani kamtuma Angel ama Mary John Kihwana kumwangamiza Imma The Boy?
Je huu ndio mwisho wa maisha ya Imma? Ni kosa gani Imma The Boy kalifanya? 
Huu ni mwanzoo tuuuu...
Usikose no 2..

Simulizi SITAMSAHAU FRANC 14

11/04/2017 08:00:00 PM 0
Story: SITAMSAHAU FRANC mwandishi :FRANKO SAMUEL EPISODE YA 14

ILIPOISHIA.....


Lau alibaki kimya,  sio muda tukiwa na Lau pale kizuizini wakikataa kufungua geti, radio call ya askari yule iliita, wakaongea

 "Hallo sagent, ni koplo John Kifaruhande hapa"
 "Ndio Afande,  nawapa taarifa kuwa kuna watu wawili mwanaume na mwanamke yule muuaji mkubwa wametoroka huku Kihorogota, wanatumia pikipiki kuanzia saa hizi pikipiki zote zikaguliwe na magari pia" 
"sawa mkuu,  tutalitekeleza vizuri!"
 "msifanye upuuzi hao watu ni hatari mno,  pia kuna mpunga mrefu mno" 
"sawa sawa kamanda" maongezi hayo yalisikiwa vema mno na mimi na Lau kwenye ile radio call.
 Baada ya maongezi askari alikata ile radio call na kutuangalia kwa kupokezana kisha akatwambia kwa usalama wetu tumfwate ndani. 

 Akili yangu iliamka na kuwa Tayari Kwa Mapambano,  miguu ikawa mizito kwa mimi kusimama kuingia kituo cha polisi. Askari hakukawia,  alinipiga konde la kichwa kwa ugumu wa ngumi ile nilihisi kutishwa gunia la viazi kichwani ikifuatiwa na kizunguzungu...
Songa nayo... 

Nilihisi kizunguzungu kikali,  wakati huo Lau aliniangalia kwa Jicho la kunionea huruma,  alishuka kwenye pikipiki na kwa haraka,  alirusha teke kali kwenye tumbo la askari yule teke lile lilimfanya atue chini kwa kupiga magoti,  ngumi kali ikatua kwenye kichwa cha askari yule na kufanya adondoke chini. Aliongezewa ngumi ya shavu, damu zikamruka kisha Lau akainyang'anya bunduki yake aina ya SMG na akaniamrisha nipande pikipiki. Alipanda na kuwaamrisha askari waliomzunguka kuwa warudi nyuma na mmoja afungue geti haraka huku akikoki ile bunduki. 
  Walikuwa wapole sana,  mmoja akafungua geti,  tukatoka lakini niliwaza sana kuwa wangenirushia tu risasi. Lau alisimamisha pikipiki na kuwaambia ole warushe risasi, kisha akaweka bunduki yao chini na kuondoka kwa kasi ya ajabu. 
Nilishikilia kwa nguvu mno nikiwa naogopa kuwa lazima warushe risasi na zitanipata mimi kwani ndiye nilyekuwa nyuma. Bado pikipiki ilienda kwa kasi huku nikisali kuomba toba kwani nilijua askari wale wasingetuacha tupotee mikononi mwao wakati wamepewa taarifa ya kutukamata.

 Nikiwa ninefumba macho na tukizidi kutoka pale kituoni. Baada ya mwenda wa dakika kadhaa nikisikia mlio mkali  paa!!..ikifuatiwa na muungurumo .
Pikipiki iliyumba huku na kule na kukosa muelekeo.  Lau alijitahidi kuiweka sawa lakini spidi ile kali ilifanya iwe ngumu.  Tuliyumba yumba mithili ya walevi waliokunywa  ulanzi  na kushindwa kujitambua.  Ufundi wa Lau ulishinda, pikipiki ikatulia.  Tulishuka na Lau akaanza kuniuliza kma niko salama.  Aliamini nimepigwa risasi. Haikuwa hivyo bali ulikuwa ni mlio wa tairi la pikipiki la nyuma lilikuwa limepasuka. 

"ohh shit,  what the hell is this? " kimombo kilimtoka Lau huku akiangalia pikipiki ile. 

"Lau tuondoke tu hapa watatufuta! Hujui askari wanafikiri nini. Pia wanaweza kupiga simu vituo vya mbele tukakamatwa kizembe wakati tumekwepa mishale mingi. Njia sahihi ni kutembea kwa mguu tukatize porini porini. Sio barabara tena" nilimshauri Lau. 

Tuliitelekeza pikipiki pale pale na tukakubaliana tukaanza kutembea. Giza nalo lilizidi kutoweka kwa kasi kupisha jua lililokuwa likipenyeza anga za mashariki.Moyo ulitulia nikamuona Lau ni mtu na kijana pekee aliyedhamiria kweli toka moyoni kuyaokoa maisha yangu. Nilimuangalia kwa macho ya kumkubali sana japo alionekana mtu mwenye kuwaza kitu fulani katika kichwa chake. Nikahisi huenda huenda anayodhamiri nyingine ila hataki kuweka wazi kwangu.
"Naenda nae tu hivyo hivyo nikifika mjini tu namtoroka atajua mwenyewe namuomba Mungu anigikishe mjini salama nipande basi." nilijisemesha moyoni huku tukitembea nayo anga ilizidi kupokea miale ya jua na kufanya ndege waruke huku na kule kufurahia ujio wa siku mpya. Ukimya ulitawala huku kila mmoja akinyanyua hatua zake. Niliamua kuvunja ukimya kwa kumuuliza Lau swali la kichokozi. 
  Nilimuuliza kwanini yuko katika mawazo akajibu wasiwasi wake ni juu ya Rama na Kriss kwani bila shaka watakuwa katika mawindo mazito ya kutusaka hivyo tungetakiwa kuwa makini sana na sio sauala la mchezo hukua akisisitiza kuwa kuwa Rama huwa hapuuzii pindi apewapo amri na mkuu wao wa kazi.

Maneno ya Lau yalinifanya niwe na hamu ya kujua huyu mkuu ni nani na kwanini anataka kuniua mimi? Nilifikiri nikaona bora nimuulize Lau ili anieleweshe vizuri.

"Lau kila mara umekuwa ukitaja neno Mkuu na huyu mkuu ni nani?" swali langu lilimfanya Lau aliyekuwa kama kasinzia hukua akitembea kustuka na kuniangalia kisha akasema.

"Irene, kuna siri nzito sana juu ya suala hili, mkuu wa nchi kabisa anahusika na kifo cha mpenzi wako Franc na kama hutakuwa makini utakufa pia. Nilikueleza hapo awali kuwa ripoti ya Franc juu ya utafiti wake ilibaini uzembe na baadhi ya viongozi kuhusika kwenye uwindaji na upotevu wa wanyama na hivyo kufanya viongozi kumstukia na kumuua.
Pia wewe unatafutwa kwani ukaribu wako na Franc unawapa wasiwasi kuwa huenda alikushirikisha hivyo ukaja kufunua siri zao na siri za kifo chake Franc. Sijui kama Franc alikuambia hili au laa.  Istoshe  wale watu waliotaka kukutoa sadaka kule mjini Iringa wanaogopa kwani hata mheshimiwa ni mshirika mkubwa wa chama kile cha kishetani.
Inasadikika kuwa mheshimiwa enzi za ujana wake kabla ya kuwa kiongozi, alioa mke na kumtaka mkewe awe katika kile chama cha kishetani lakini mke akakataa. Kulingana na masharti ilibidi atoe kafara na wakati huo yeye na mke walikuwa wakikaa Iringa. Walikuwa na na watoto mapacha wakike na wakiume. Mkuu aliombwa na chama atoe mtoto wa kiume, ili awe na nguvu na uwezo.  Kuna mtu alimuhurumia mkewe kwa kuhofia kupoteza mwanae wa kiume, akampaa taarifa juu ya mipango ya mumewe. Aliyetoa taarifa alikuwa ni mmoja ya watu wa karibu na mheshimiwa. Mkewe aliona bora ampe mtu mtoto wake wa kiume.  Mtu huyo ambaye alipewa mtoto alikimbia na mtoto angali mchanga na kwenda nae maeneo ya Kilolo. Mpaka leo hii ninapokwambia haijulikani kama mtoto ni mzima au laa na umri wake ni sawa na wetu mimi na wewe."


"Na huyo mke yuko wapi sasa?" niliongezea swali jingine.

"Sikia, baada ya kumtorosha  mtoto wake wa kiume, inasemekana alitoroka na kuelekea jiji la Dar Es Salaam. Pia inasemekana aliolewa na mtu mwingine na kuishi huko.  Japo hakupata kuzaa nae mtoto. Ila huyo mtoto wa kike wa kumkuta anajua huyo mwanaume ndiye baba yake halisi. Ila ukweli wote anaujua mama na baba. Pia babu alinimbia kuwa huenda huyo baba alishauliwa kwani Mkuu hawezi kukubali kuona mtu aliyempenda akiwa na mkewe na mwanae."

"Lau wewe upo kama mimi kiumri ulijulia wapi mambo haya?"

"Ninaye babu yangu kule nyumbani anaitwa Simbayavene ni mzee ila anajua mambo ni hatari,  alishiriki hata mpingo ya vita vya maji maji si mchezo. Babu alinisimulia yote na alidai kuna kitu ataniambia nikikua kwani mimi pia jina langu halisi naitwa Kamkosi, akasema nalo lina historia pia. Hivyo inabidi nifuatilie kwa umakini ili nijue kabla ya babu yangu aliyenilea haukata"


"Ahh sawa kabisa, sasa kwanini huyu mheshimiwa anaabudu mashetani?"

"Irene rafiki yangu, tambua kuwa nguvu za kuitawala dunia na wanadamu pamoja na kumiliki utajiri hutoka kwa miungu na hasa dini ya kifreemasoni. Karibia viongozi wakubwa wa kidunia maraisi, mawaziri, wakurugenzi na wengine wengi hupata nguvu ya nyota ya kuongoza kupitia Freemason. Pia kuna wahuburi wakubwa maarufu duniani na hapa Tanzania ni washirika wakubwa wa dini hiyo na hawa huogopwa na waumini kwani kwa kuombea kwao huponya watu ila si kwa nguvu za uweza wa Mwenyezi Mungu ama Yesu bali kupitia mkuu wao wa kuzimu Lucifer."

Aliongea Lau maelezo yake yaliyofungua ubongo wangu na kufanya niwe na shauku ya kujua zaidi. Japo tuliongea kwa sauti za chini mno huku tukiikanya ardhi bila huruma. Tulitembea na kulikuwa kukizidi kupambazuka. 

Tulitokea katika barabara na basi likatokea, walisimamisha tukapanda na kuendlea kupiga stori. Lau alizidi kuniambia mengi utafikiri alikuwa mwanachma wa Freemasons. Wakati tukipiga stori kuna abiria mmoja alikaa  pembeni yetu alionekana kufutilia kwa kina mno mazungumzo yetu. Kila nilipojaribu kumuangalia alificha uso wake na kufanya nisimjue vizuri. Niliwaza sana juu ya viongozi wa dini kuhusishwa na dini ya kishetani, sikuustaajabu sana kwani nilishawahi kusikia habari hizi kuwa wahuburi wengi wenye uwezo mkubwa hupata nguvu hizo kupitia njia hii japo sikufuatilia ila nilijihakikishia ukaribu wangu na Lau ungenipa nafasi ya kufahamu mengi zaidi. 

Nilitafakari maelezo ya Lau kuhusu vyote alivyosema na kuona nipo kwenye mtihani mkubwa tena mzito!  Kwa maelezo yale nilihisi hata kuhangaika kwangu kuwakwepa  ni bure kwani freemansons wanaona popote ulipo.  Alama yao ipo kwenye noti ya dolla ambapo ukichunguza vizuri utaona alama ya jicho kwenye pembe tatu likiitwa All See Eye yaani jicho lionalo popote. Haya yote nilifunuliwa na Lau.  Tuliendelea na safari. Tayari jua lilikuwa limeshachomoza huku gari lile likiendelea kukata barabara na kufanya watu watulie wakimpa nafasi dereva uwezo wake wa kuliendesha gari lile.
**************** 

Jiijini Dar Es Salaam. Asubuhi
 Hali ya hewa na utulivu ulitanda jijini Dar huku pilika pilika za watu na magari wakiwahi makazini zikishika nafasi yake. Huyu alikuwa akienda huku na huyu akienda kule.Mlio wa alamu ya saa iliyoashiria saa 12  za asubuhi ulitosha kukatisha usingizi wa mama yake Irene.  Aliamka na kusali kidogo akimshukuru Mungu kwa uhai na uzima. Katika sala yake hiyo pia alimshukuru Mungu kwa kumfanya mvumilivu huku akiomba mwanae Irene awe mzima wa afya.  Alitandika kitanda na baada ya hapo usafi ukafuta. Alipika chai na kishindwa kuinywa kwani kutokana na mawazo alijikuta akifanya kazi muda mrefu tena kwa pole hivyo muda ukawa umemuishia.  Ni muda wa kuonana na askari wa kituo cha polisi cha Osterbay jijini Dar Es Salaam juu ya kuootea kwa mwanane Irene.
Huko Osterbay kituo cha Polisi majira ya Asubuhi


Askari wa kwanza kama walivyo ahidiana jana aliamka mapema na kuwahi kwa mkuu wake ili kupewa kibali cha kwenda chuo kikuu cha Dar Es Salaam kupepeleza habari za awali.  Mkuu alimuandikia kibali na kumruhusu. Aliondoka tayari kwenda Mlima. Alifika na kupokelewa na walinzi. Akijitambukisha kama ndugu wa Irene. Walinzi walianza usumbufu wa hapa  na pale. Mwishowe aliwaonesha kitambulisho na wakamruhusu aingie. Alienda moja kwa moja hadi jengo utawala na kuomba kuonana na mlezi wa wanafunzi mabwenini na kuoewa taarifa kuwa Irene alikuwa akikaa hostel za mabibo hall five chumba namba A 6. 

Askari mwingine alikuwa kaenda Tanzania Communication Regulation Authority TCRA kuomba kibali cha kufuatilia mawasiliano ya simu yaliyofanywa na Irene kabla ya kutoweka  jijini Dar Es Salaam. Alipewa vibali vya kuingia katika ofisi za mitandao yote ya simu. Namba alizopewa awali na mama yake zilionesha kuchati kawaida na marafiki zake. Pia rekodi za mawasiliano ya mwisho yalikuwa ni simu iliyopigwa kwa mama yake. Maelezo yake yalikuwa hataenda rikizo kwa kuwa ni muda mfupi. Lakini central tracking system ilionesha network yake ya mwisho kutumia ilikuwa mkoa wa Iringa  manara wa posta. Imei ziliiingizwa na ilionekana simu yake ilikuwa ikitumiwa na mtu aliyekuwa Mufindi huko Iringa, ijapo laini yake ilikuwa haipatikani kabisa. Upande wa mama Irene..

Askari wa kike aliyekuwa kavalia sare ya kipolisi alikuwa akimhoji mama irene Masawali kadhaa.  Swali lililokuwa gumu ni kwanini hakuwahi kutoa taarifa mapema kituo cha polisi.  Mama Irene alijibu kuwa hakuwahi kuwa na wasiwasi na mwanae.  Hata hivyo alipata taarifa kutoka kwa marafiki zake wakimuuliza kwanini kwanini Irene hapatikani na kachelewa shule. Kwa maelezo yale askari alipata kujua kuwa Irene hakumuaga mtu yeyote yule. Swali lingine ilikuwa kama Irene alishawahi kuugua magonjwa akili nk. Mama Irene alijibu haijawahi kutokea kabisa. Pia askari alitaka kujua kama Irene alikuwa na Matatizo ya kisaikolojia kama kutendwa au kuachwa na mpenzi au kushindwa masomo.  Mama Irene alijubu kuwa hawezi kuwa msemaji sana kuhusu mahusiano ya mwanae kwani hakuwahi mshiriksha chochote.  Pia aliongezea kuwa alijua Irene alikuwa single na si vinginevyo. Kuhusu masomo alisema mwanae alikuwa akimueleza kujitahidi hivyo hadhani kama kinaweza kuwa chanzo chake. Askari aliongezea swali lingine, kuhusu baba wa Irene na uhusiano na ndugu wengine. Swali hili lilimfanya mama Irene akae kimya kwa muda bila kusema neno. Ilionesha lilikuwa swali gumu kwake.. ***      ****     ****         ****    *****

 Irene na Lau Wakiwa kwenye gari.. 
Gari liliendelea kutembea huku kukiwa kumekuchwa na hali ya jua ikitawala. Nilichungulia dirishani na kuona tulikuwa tupo maeneo ya Chalinze. Nilijawa na furaha sana, tumaini la kuwaona baba na mama yangu likawa kubwa sana. Nilijikuta nikipatwa na huzuni ghafla kuanza kuliona jiji la Dar, nikakumbuka kuwa  sikuwa mwanafunzi wa chuo tena. Kweli ngoswe penzi kitovu cha uzembe. Iliniuma sana kwani penzi la kijana  Franc lilikuwa limetia doa jeusi maisha yangu yote. Machozi yalinilenga lenga nikulimuangalia Lau aliyekuwa akisinzia kwa usingizi. 

Nikiwa bado kwenye dimbwi la mawazo nilistushwa baada ya gari kufunga break kali na za ghafla zilizofanya abiria kuhama viti na kugonga siti za mbele. Taharuki ikaanza kwani abiria walilaani dereva kuendesha bila ustadi, huku wengine wakitukana matusi "msenge huyu" na kumzomea. Kila mtu aliongea lake lakini mimi na Lau macho yetu yalikuwa mbele kubaini hasa nini kilikuwa chanzo cha dereva  kufunga break kali vile tena kwenye kona. Macho ya Lau yaliamka huwezi kudhani kama ndiye aliyekuwa akisinzia muda sio mrefu. 


Mbele ya basi letu, walisimama wanaume wawili walioshiba vizuri kwa mazoezi, nilifuta macho yangu na kuwaaangalia vizuri, sura zile hazingukwa ngeni kabisa machoni pangu, hali ile ilinifanya nifikiri kwa kasi ili niwakumbuke vizuri na upesi

Taarifa za za viumbe niliowaona zilipelekwa kwenye ubongo wa nyuma kisha mbele na kumbukumba za ubongo zikanambia hao ni Rama na Kriss wale wa kule porini. Lau aliniangalia na kunipa ishara fulani kama wanenavyo wahenga kuwa waswahili wa pemba hujuana kwa vilemba. Bila kuchelewa nikamuona kondakta akitoka kwa hasira na kumkwida Kriss ambaye alimuangalia tu kondakta bila kumfanya lolote. Kondakta kuona vile kwa hasira alimpiga Kriss Ngumi ya uso, Kriss wala hakutikisika badala yake alimtandika kondakta kofi moja lilompeleka chini kama gunia la viazi na kumfanya apige ukelele wa maumivu makali mno. 

Walimuacha  kondakta akiugulia maumivu na kimadaha Kriss na Rama wakaanza kuja kwenye basi. Sijui nani aliwaonesha kuwa tuko kwenye hili gari, nilijikuta nikiwaza bila jibu. Nilijua tu ni mimi na Lau ndio mawindo yao. Na kweli wametupata. Hakuna pa kukimbilia. Abiria walianza kupiga mayowe ya hasira huku wakiwa hawajui nini kinaendelea.  Mimi,  Lau,  Rama na Chriss ndio tulikuwa tunaujua mtanange mzima...
Itaendlea..

Usikose episode ya 15

Simulizi SITAMSAHAU FRANC 13

11/04/2017 07:54:00 PM 0

Simulizi : SITAMSAHAU FRANC  

 Mwandishi:FRANCO SAMUEL EPISODE YA 13


ILIPOISHIA..

Alikimbiza sana nikiwa nimeshikilia tumbo lake,  upepo ulisababisha macho yangu yatoe machozi.  Niligeuka kwa kuibia sikuona tena gari la polisi,  tulikuwa tumeliacha mbali mno na hata wangekuja na spidi gani wasingalitukuta mimi na Lau wangu ambaye hakika nilimuamini sana!
Hatimaye tulianza kuingia katika kijiji na kadri tulivosongo tuliona kumbe hakikuwa kijiji ila mji kabisa. Nilivuta pumzi kubwa nikimshukuru Mungu wangu na kuona alikuwa mwema kwa yote.  Kwa mbali nilihisi njaa ikiuma tumbo lilikuwa likidai chochote ili lilidhike. 
Lau alizima pikipiki  na kupaki pembeni ya barabara tulisogelea mgahawa fulani ulikuwa pale ili tule lakini mimi sikuwa na hela. Tuliingia ndani ila kwa nje king'ora cha polisi kilisikika na nilichungulia nikaona likipaki pale tulipoacha pikipiki yetu.
Yaani nilinyong'onyea kabisa... Nilikosa nguvu sana,  nilishuhudia askari wakishuka na bunduki huku wakija kwa kasi pale mgahawani.  Lau aliniangalia na kunipa ishara fulani ya kuashiria hatari, Tayari askari walikuwa wakikaribia mlangoni!! Tulibaki tumeduwa tu tusijue cha kufanya.
SONGA NAYO... 

Kwa haraka Lau alinipa ishara ya kunitaka niiname chini,  nilifanya hivyo kisha akanionesha nisimame nilifanya hivyo na kuelekea sehemu ya ndani ya ule mgahawa na kujificha nyuma ya magunia ya mkaa,  ile napoteza tu kichwa,  nilisikia amri ikitaka wote tutoke mle! Ilikuwa taharuki kubwa iliyofanya kila mtu aache kula,  wakatio huo Lau aliingia kwenye gunia na kujikunyata kama mzigo kisha kulala chini. 

Askari waliamuru watu wote watoke nje na kwa amri ile waliitii,  ilisikika miguu ya askari akitembea mule ndani akaja upande wangu na kupitia upenyo wa magunia yale nilimuona akimkanyaga lau ndani ya gunia,  ni kama alistuka na kuinama kuangalia ila akapita na kuja mpka pale kwenye magunia kisha akarudi pale kwenye meza na kuanza kula vyakula vilivyoachwa na wateja.  Ilionesha alikuwa na njaa kali mno ndani ya tumbo lake,  nilimshuhudia akitoka huku nje sauti ya mama akilalamika sana ilisikika kwa uhafifu kwenye ngoma za masikio yangu

"mniache mimi mgahwa wangu nalisha watoto baba yao alikufa na hao watu siwajui" kwa malalamiko yale ilionesha kabisa alikuwa ni mmiliki wa mgahawa ule. Niliumia sana roho ya huruma ilinijia  nikifikiri taabu apatazo mama ambaye akaachiwa watoto tena wanaosoma baada ya mumewe kufariki,  hakika iliniuma sana.
***********      **************         *****************           ***********

Jiji kuu Dar Es Salaam. Usiku...
Kituo cha Polisi Osterbay jijini Dar Es Salaam askari watatu wakiwa kwenye sare zao walikuwa wakifanya kikao cha kupeana mikakati.  Kila mmoja alionekana makini mno huku wakisikilizana kwa usikivu mkuu. Kilichokuwa kikijadiliwa ni kuhusu taarifa walizozipokea jioni. Taarifa hiyo ilitoka kwa mama mmoja ambaye alijieleza kupotelewa na mwanae wa kike wa pekee tangu akiwa chuo kipindi cha likizo

Kwa udadavuzi ilionekana kama mama ni mzembe kwani muda mrefu umepita toka likizo. Ijapo mama alieleza kuwa hakujua kama mwanae kapotea ni ukimya wa mwanae huyo ndio uliomstua sana.  Maelezo yaliyosomwa yalionesha kuwa binti aliyepotea ni Irene Huang. Mwanadada wa chuo cha Dar Es Salaam.  Kulingana na maelezo ilionesha kuwa mama yake mjane hakupata taarifa mapema. 
  Askari wale waligana majukumu.  Mmoja alipewa jukumu la kwenda kutafuta habari juu ya kutoweka kwa binti huyo katika chuo kikuu cha Dar Es Salaam. Mwingine alipewa jukumu la kwenda kutafuta taarifa za mawasiliano yake tangu siku anapotea. Huyu alitakiwa kujua nani aliwasiliana na Irene siku ya mwisho na maeneo gani alikuwa akiwasiliana nae kupitia simu. Askari wa mwisho alipewa jukumu la kuhakikisha anampeleleza zaidi mama yake na Irene ili ajaue sababu za kupotea na wapi wanahisi yupo. Baada ya majadiliano hayo yaliyodumu takribani nusu saa kila mmoja alitawanyika na kuendlea na majukumu mengine wwakisubiri kesho kufanya kile walichopangiana

Wakati huo nyumbani kwa mama Irene , ilikuwa ni majonzi tele. Mama alikuwa akilia hasa alipotazama picha ya bintie ukutani.  Alivuta kabati la nguo na kutoa albamu ya picha.  Akianza kuangalia moja baada ya nyingine.  Alikutana na picha ya mwanaume, akiwa kavalia suti. Kuiona picha ile kulileta kilio kikubwa mno. Ilikuwa picha ya marehemu mumewa baba Irene. Mawazo zaidi yakamjia,  akikumbuka jinsi alivyoishi na mumewe huyo kwa upendo. Picha hii ilimfanya akumbuke kifo cha kutatanisha cha mumewe kilichotokea muda sio mrefu. Machozi na simanzi vilimfika shingoni mjane huyu na kumfanya alie sana. Aliwaza juu ya binti yake kipenzi Irene,  mtu pekee aliyekuwa kabakia katika hii dunia. Mawazo yake yakapingana, huenda mzima huku roho nyingine ikimwambia huenda kafariki. Alilala juu ya meza tena bila kula kabisa kwa maumivu ya uchungu wa mwananae.. ******** ********* *********    ***********    ***********

Nilisikia kipila kile cha polisi kikiondoka kwa kwasi na watu wote waliokamatwa katika mgahawa,  ukimya ulitawala sana nilimuangalia Lau kwenye lile gunia na kumuona akiwa mkimya pia,  sikutaka kuwa na papara ya kuinuka nilisubiri mpaka Lau akiamka ndio niamke.  Kutokana na kujibana vibaya pale kwenye magunia bila Lau kuamka nilihisi maumivu ya makali sana ya miguu ila nikajikaza, haukupita muda niliona Lau akianza kujitoa ndani ya lile gunia. 
  Alitoka nikatoka pia na kumuangalia usoni Lau alikuwa akivuja damu nyingi puani, ilikuwa kawaida yangu kustuka mno nionapo damu
 
"Lau pole kuna nini"
  "Yule askari alinikanyaga puani,  kiatu chake kigumu sana  nilihisi maumivu makali mno,  kama nisingekuwa imara hakika ningepiga yowe la maumivu"
  "Pole sana,  ndio maana nilimuona askari kama kastuka kitu vile"
  "Ndio niliamua kujikaza kwa kuwa sikuwa na namna ya kufanya,  nadhani  kile kiatu kingetua kwenye mwili wako ungepiga ukelele wa maumivu"
  "Pole sana" nilimwambia Lau na kuanza kumfuta Damu zile puani,  wakati huo wote Lau alikuwa kimya, nilimaliza na kuhakikisha hazitoki tena kisha nikachukua maji ya baridi yaliyokuwepo ndani ya mgahawa ule na kamkanda Lau kwenye paji lake la uso.
Nilisimama na kumkumbatia huku nikifikiri mbali sana juu ya yote ninayopitia, hakika nilimwamini sana Lau, ule usemi wa mwalimu wangu wa chuo wa kusema don't trust any one ukaja kichwani ila nikaupotezea haraka,  kumbatio lile lilinipa joto mwanana kwenye kifua kilichojitenga vema na chenye mazoezi cha Lau. Nilihisi niko mbali mno, nikamkumbuka Franc, nilimuangalia Lau kwa macho fulani ya hamasa yaani ya kuonesha kuwa nilifurahia sana kumkumbatia,  Lau alisogeza mdomo wake karibu na wa kwangu nilihisi macho yangu yakipoteza nguvu ya kuona na kujikuta yakijifumba taratibu kama mlevi mwenye usingizi.

Nikiwa sioni nilipokea busu zito mdomoni na kufanya nihisi kupigwa ganzi mwili mzima, kitendo kile kilifanya nimpe Lau ulimi wangu naye akafanya hivyo kweli tulikuwa ulimwengu mwingine. Kama haitoshi, Lau alishusha mkono wake na kugusa kiuno changu, nilihisi raha sana nilizidi kumkumbatia zaidi kwani mwili wake ulikuwa wa joto sana, mkono wake haukuishia hapo Lau aliupandisha taratibu, ukatua kwenye kifua changu na kukutana na matiti yangu madogo, nilijikuta nikilalamika polepole kwa kuguswa na  mikono yake yenye joto kwenye maziwa yangu madogo kwani sikuwa hata na brazia katika mwili wangu. Mshike mshike patashika,  ilitawala. Kila mmoja akijaribu kumuonesha mwenzake uwezo wake katika tasnia ya mapenzi.. 

Ilikuwa vurugu patashika nikiwa kwenye ulimwengu mwingine kabisa,  akili ikanihama sikujali mazingira tuliyokuwepo. Kweli mapenzi yana nguvu ya ajabu na hisia zina sumaku ya asili haijalsihi uko wapi. Nilistuka baada ya kuhusi mkono wa Lau ukiwa umetua kwenye kifungo cha suruali yangu na ikiwa imefunguka huku vidole vyake vikitalii maeneo yale,  kustuka kule hakukuwa kwa kutisha haukupita muda Lau alinibusu. Bado mikono yake ilinipa raha ajabu. Aliongezea busu lenye ujazo na kuniachia huku akinitazama kwa macho yake yaliyojaa mahaba. Macho yangu yalijaa mahaba kiasi cha kutoona vyrma. Lau alisitisha zoezi lile na kukata utamu njiani huku akitahadharisha kuwa tupo kwenywe hatari hivyo ni vema tuache kile tunachofanya


Nilimuachia kishingo upande na kuona kama muuaji aliyeziibua na kuchokonoa hisia zangu za mapenzi na kuniacha katika kiu kuu ya tendo.  Mwili ulikuwa ukitetemeka na macho yangu yalikuwa hayaoni vizuri hadi nilisahau kuwa pale palikuwa mghawani na tulienda kwa lengo moja tu nalo ni kula. Ni kama njaa ilinipotea hivi. Lau aliniacha pale chinj na kuingia ndani ya ule mgahawa akatoka na sahani la wali na chupa ya chai,  alimimina chai na tukaanza kula,  sikuwa na hamu akili yangu yote ilikuwa kwake nikimungalia kwa kuibia kila nilipopata nafasi ya kumuangalia,  kuna kipindi macho yangu yaligongana na yake
  "Irene unajisikiaje?"
  "Niko kwaida tu" nilidanganya ila ukweli niliumia sana kwa kiyendo chake cha kuniacha na hisia kali za mapenzi, nilishindwa kumwambia tu kwa kuwa nilikuwa mwanamke. 
  "Kula au hupendi chakula? Jitahidi tuondoke hapa kwani si salama"
  "Saa tano hii tutaenda wapi Lau wangu? "
  "Tukikaa hapa kunauwezekano wa askali kurudi,  pia huu mgahawa Rama na Chriss wanaujua vema kwa kuwa kila mara huwa tunakuja hapa tukitoka kule." alisema Lau akameza funda la chakula kisha kuendelea kuongea.
  "Wanaweza kutoka kule wakitufuta na kuja kutukuta hapa tukawa matatani. Kumbuka nia yangu ni kulipa kisasi kwa rafiki yangu Franc na wewe,  hapo ndio roho yangu itatulia tuli! "
  "Sasa tunaenda wapi? "
  "Tutoke tutajua cha kufanya"

Lau aliingia sehemu kwenye ule mgahawa na kutoka na koti na sweta,  alinikabidhi sweta na yeye kuvaa koti kubwa kisha akanikumbatia tena,  sikupenda kwa kuwa alitaka kuamsha mwili wangu ulioluwa ukipowa kwa kunyimwa penzi lake. Aliniachia na kunishika mkono, tukaanza kutoka na kukata mitaa,  kadhaa kwa kutembea kwake ilionesha Lau alitambua vema mitaa ile.
  Tulifika sehemu nje ya nyumba Lau, aliangaza huku na huko kisha akaingia ndani na kutoka pikipiki, kama kawaida alifanya ujanja wake ikawaka, tukaanza safari usiku ule
  "Tunaenda wapi usiku huu"
  "Nataka tufike mahalia ili pa kupanda basi ili kesho twende Dar"
  "Tutafika salama kweli? "
  "Mumgu mwema,  pia Upo na mimi Lau hutakiwi kuogopa kitu kabisa siwezi kufanya kosa"
  "Haya twende baba" nilimjibu na kumshikilia vyema,  tukaendelea na safari.  Ilikuwa ndefu mpka nikahisi usingizi na kulala nyuma ya mgongo wa  Lau, sikuhofia kudondoka kwa kuwa barabara Ilikuwa ya lami na Lau aliendesha kwa mwendo wa kawaida.... 

Nilistuka baada ya kumulikwa na mwanga mkali usoni,  macho yangu yaliyojaa usingizi yalifumbuka haraka na Kwa ukali wa mwanga ule sikuona chochote kile. Niliyafikicha macho, nikasikia sauti ya amri ikiniamuru nishuke. Nilishuka na kwa sekunde kadhaa kuamsha akili yangu iliyohisi zile ni ndoto,  kumbe hazikuwa ndoto,  tulikuwa tupo kwenye kizuio cha polisi yaani mizani. 

"Kwanini mnamnyanyasa abiria wangu?"
  Alisikika Lau kwa ukali akiwa kwenye ile pikipiki wakati huo nikitua chini huku Lau akiwa kainamisha kichwa chini. "Usiku huuu mnaenda wapi? "Nampeleka huyu mteja akawahi basi la Dar kwani ana haraka" "Huna helmet,  hujavaa nguo nzito,  abiria pia hana helmet!  Iko wapi leseni yako ya udereva? " Aliongea askari aliyeoneka machachari kweli, lau aliingiza mkono wake mfukoni na kisha kuchomoa leseni na kwa kabidhi. Askari aliingalia, wakati huu macho yangu yalurudi kawaida kabisa na niliona vizuri,  bado askari yule kiherehere akahoji "Huja renew leseni yako, what the hell you idiot" alikuwa mkali huku akionge kwa kuchanganya kiswahili na Kiingereza. Lau alibaki kimya,  sio muda tukiwa na Lau pale kizuizini wakikataa kufungua geti, radio call ya askari yule iliita, wakaongea.
  "Hallo sagent, ni koplo John Kifaruhande hapa"
  "Ndio Afande,  nawapa taarifa kuwa kuna watu wawili mwanaume na mwanamke yule muuaji mkubwa wametoroka huku kihorogota, wanatumia pikipiki kuanzia saa hizi pikipiki zote zikaguliwe na magari pia"
  "sawa mkuu,  tutalitekeleza vizuri!"
  "msifanye upuuzi kuna mpunga mrefu mno"
  "sawa sawa kamanda" maongezi hayo yalisikiwa vema mno na mimi na Lau kwenye ile radio call, askari yule alikata ile radio call na kutuangalia kwa kupokezana kisha akatwambia kwa usalama wetu tumfwate ndani.

Akili yangu iliamka na kuwa Tayari Kwa Mapambano,  miguu ikawa mizito kwa mimi kusimama kuingia kituo cha polisi. Askari hakukawia,  alinipiga konde la kichwa kwa ugumu wa ngumi ile nilihisi kutishwa gunia la viazi kichwani ikifuatiwa na kizunguzungu...

Itaendelea
Usikose 14

Audio