Story: SITAMSAHAU FRANC
mwandishi :FRANKO SAMUEL
EPISODE YA 14
ILIPOISHIA.....
Lau alibaki kimya, sio muda tukiwa na Lau pale kizuizini wakikataa kufungua geti, radio call ya askari yule iliita, wakaongea
"Hallo sagent, ni koplo John Kifaruhande hapa"
"Ndio Afande, nawapa taarifa kuwa kuna watu wawili mwanaume na mwanamke yule muuaji mkubwa wametoroka huku Kihorogota, wanatumia pikipiki kuanzia saa hizi pikipiki zote zikaguliwe na magari pia"
"sawa mkuu, tutalitekeleza vizuri!"
"msifanye upuuzi hao watu ni hatari mno, pia kuna mpunga mrefu mno"
"sawa sawa kamanda" maongezi hayo yalisikiwa vema mno na mimi na Lau kwenye ile radio call.
Baada ya maongezi askari alikata ile radio call na kutuangalia kwa kupokezana kisha akatwambia kwa usalama wetu tumfwate ndani.
Akili yangu iliamka na kuwa Tayari Kwa Mapambano, miguu ikawa mizito kwa mimi kusimama kuingia kituo cha polisi. Askari hakukawia, alinipiga konde la kichwa kwa ugumu wa ngumi ile nilihisi kutishwa gunia la viazi kichwani ikifuatiwa na kizunguzungu...
Songa nayo...
Nilihisi kizunguzungu kikali, wakati huo Lau aliniangalia kwa Jicho la kunionea huruma, alishuka kwenye pikipiki na kwa haraka, alirusha teke kali kwenye tumbo la askari yule teke lile lilimfanya atue chini kwa kupiga magoti, ngumi kali ikatua kwenye kichwa cha askari yule na kufanya adondoke chini. Aliongezewa ngumi ya shavu, damu zikamruka kisha Lau akainyang'anya bunduki yake aina ya SMG na akaniamrisha nipande pikipiki.
Alipanda na kuwaamrisha askari waliomzunguka kuwa warudi nyuma na mmoja afungue geti haraka huku akikoki ile bunduki.
Walikuwa wapole sana, mmoja akafungua geti, tukatoka lakini niliwaza sana kuwa wangenirushia tu risasi. Lau alisimamisha pikipiki na kuwaambia ole warushe risasi, kisha akaweka bunduki yao chini na kuondoka kwa kasi ya ajabu.
Nilishikilia kwa nguvu mno nikiwa naogopa kuwa lazima warushe risasi na zitanipata mimi kwani ndiye nilyekuwa nyuma. Bado pikipiki ilienda kwa kasi huku nikisali kuomba toba kwani nilijua askari wale wasingetuacha tupotee mikononi mwao wakati wamepewa taarifa ya kutukamata.
Nikiwa ninefumba macho na tukizidi kutoka pale kituoni. Baada ya mwenda wa dakika kadhaa nikisikia mlio mkali paa!!..ikifuatiwa na muungurumo .
Pikipiki iliyumba huku na kule na kukosa muelekeo. Lau alijitahidi kuiweka sawa lakini spidi ile kali ilifanya iwe ngumu. Tuliyumba yumba mithili ya walevi waliokunywa ulanzi na kushindwa kujitambua. Ufundi wa Lau ulishinda, pikipiki ikatulia. Tulishuka na Lau akaanza kuniuliza kma niko salama. Aliamini nimepigwa risasi. Haikuwa hivyo bali ulikuwa ni mlio wa tairi la pikipiki la nyuma lilikuwa limepasuka.
"ohh shit, what the hell is this? " kimombo kilimtoka Lau huku akiangalia pikipiki ile.
"Lau tuondoke tu hapa watatufuta! Hujui askari wanafikiri nini. Pia wanaweza kupiga simu vituo vya mbele tukakamatwa kizembe wakati tumekwepa mishale mingi. Njia sahihi ni kutembea kwa mguu tukatize porini porini. Sio barabara tena" nilimshauri Lau.
Tuliitelekeza pikipiki pale pale na tukakubaliana tukaanza kutembea. Giza nalo lilizidi kutoweka kwa kasi kupisha jua lililokuwa likipenyeza anga za mashariki.Moyo ulitulia nikamuona Lau ni mtu na kijana pekee aliyedhamiria kweli toka moyoni kuyaokoa maisha yangu. Nilimuangalia kwa macho ya kumkubali sana japo alionekana mtu mwenye kuwaza kitu fulani katika kichwa chake. Nikahisi huenda huenda anayodhamiri nyingine ila hataki kuweka wazi kwangu.
"Naenda nae tu hivyo hivyo nikifika mjini tu namtoroka atajua mwenyewe namuomba Mungu anigikishe mjini salama nipande basi." nilijisemesha moyoni huku tukitembea nayo anga ilizidi kupokea miale ya jua na kufanya ndege waruke huku na kule kufurahia ujio wa siku mpya. Ukimya ulitawala huku kila mmoja akinyanyua hatua zake. Niliamua kuvunja ukimya kwa kumuuliza Lau swali la kichokozi.
Nilimuuliza kwanini yuko katika mawazo akajibu wasiwasi wake ni juu ya Rama na Kriss kwani bila shaka watakuwa katika mawindo mazito ya kutusaka hivyo tungetakiwa kuwa makini sana na sio sauala la mchezo hukua akisisitiza kuwa kuwa Rama huwa hapuuzii pindi apewapo amri na mkuu wao wa kazi.
Maneno ya Lau yalinifanya niwe na hamu ya kujua huyu mkuu ni nani na kwanini anataka kuniua mimi? Nilifikiri nikaona bora nimuulize Lau ili anieleweshe vizuri.
"Lau kila mara umekuwa ukitaja neno Mkuu na huyu mkuu ni nani?" swali langu lilimfanya Lau aliyekuwa kama kasinzia hukua akitembea kustuka na kuniangalia kisha akasema.
"Irene, kuna siri nzito sana juu ya suala hili, mkuu wa nchi kabisa anahusika na kifo cha mpenzi wako Franc na kama hutakuwa makini utakufa pia. Nilikueleza hapo awali kuwa ripoti ya Franc juu ya utafiti wake ilibaini uzembe na baadhi ya viongozi kuhusika kwenye uwindaji na upotevu wa wanyama na hivyo kufanya viongozi kumstukia na kumuua.
Pia wewe unatafutwa kwani ukaribu wako na Franc unawapa wasiwasi kuwa huenda alikushirikisha hivyo ukaja kufunua siri zao na siri za kifo chake Franc. Sijui kama Franc alikuambia hili au laa. Istoshe wale watu waliotaka kukutoa sadaka kule mjini Iringa wanaogopa kwani hata mheshimiwa ni mshirika mkubwa wa chama kile cha kishetani.
Inasadikika kuwa mheshimiwa enzi za ujana wake kabla ya kuwa kiongozi, alioa mke na kumtaka mkewe awe katika kile chama cha kishetani lakini mke akakataa. Kulingana na masharti ilibidi atoe kafara na wakati huo yeye na mke walikuwa wakikaa Iringa. Walikuwa na na watoto mapacha wakike na wakiume. Mkuu aliombwa na chama atoe mtoto wa kiume, ili awe na nguvu na uwezo. Kuna mtu alimuhurumia mkewe kwa kuhofia kupoteza mwanae wa kiume, akampaa taarifa juu ya mipango ya mumewe. Aliyetoa taarifa alikuwa ni mmoja ya watu wa karibu na mheshimiwa. Mkewe aliona bora ampe mtu mtoto wake wa kiume. Mtu huyo ambaye alipewa mtoto alikimbia na mtoto angali mchanga na kwenda nae maeneo ya Kilolo. Mpaka leo hii ninapokwambia haijulikani kama mtoto ni mzima au laa na umri wake ni sawa na wetu mimi na wewe."
"Na huyo mke yuko wapi sasa?" niliongezea swali jingine.
"Sikia, baada ya kumtorosha mtoto wake wa kiume, inasemekana alitoroka na kuelekea jiji la Dar Es Salaam. Pia inasemekana aliolewa na mtu mwingine na kuishi huko. Japo hakupata kuzaa nae mtoto. Ila huyo mtoto wa kike wa kumkuta anajua huyo mwanaume ndiye baba yake halisi. Ila ukweli wote anaujua mama na baba. Pia babu alinimbia kuwa huenda huyo baba alishauliwa kwani Mkuu hawezi kukubali kuona mtu aliyempenda akiwa na mkewe na mwanae."
"Lau wewe upo kama mimi kiumri ulijulia wapi mambo haya?"
"Ninaye babu yangu kule nyumbani anaitwa Simbayavene ni mzee ila anajua mambo ni hatari, alishiriki hata mpingo ya vita vya maji maji si mchezo. Babu alinisimulia yote na alidai kuna kitu ataniambia nikikua kwani mimi pia jina langu halisi naitwa Kamkosi, akasema nalo lina historia pia. Hivyo inabidi nifuatilie kwa umakini ili nijue kabla ya babu yangu aliyenilea haukata"
"Ahh sawa kabisa, sasa kwanini huyu mheshimiwa anaabudu mashetani?"
"Irene rafiki yangu, tambua kuwa nguvu za kuitawala dunia na wanadamu pamoja na kumiliki utajiri hutoka kwa miungu na hasa dini ya kifreemasoni. Karibia viongozi wakubwa wa kidunia maraisi, mawaziri, wakurugenzi na wengine wengi hupata nguvu ya nyota ya kuongoza kupitia Freemason. Pia kuna wahuburi wakubwa maarufu duniani na hapa Tanzania ni washirika wakubwa wa dini hiyo na hawa huogopwa na waumini kwani kwa kuombea kwao huponya watu ila si kwa nguvu za uweza wa Mwenyezi Mungu ama Yesu bali kupitia mkuu wao wa kuzimu Lucifer."
Aliongea Lau maelezo yake yaliyofungua ubongo wangu na kufanya niwe na shauku ya kujua zaidi. Japo tuliongea kwa sauti za chini mno huku tukiikanya ardhi bila huruma. Tulitembea na kulikuwa kukizidi kupambazuka.
Tulitokea katika barabara na basi likatokea, walisimamisha tukapanda na kuendlea kupiga stori. Lau alizidi kuniambia mengi utafikiri alikuwa mwanachma wa Freemasons. Wakati tukipiga stori kuna abiria mmoja alikaa pembeni yetu alionekana kufutilia kwa kina mno mazungumzo yetu. Kila nilipojaribu kumuangalia alificha uso wake na kufanya nisimjue vizuri. Niliwaza sana juu ya viongozi wa dini kuhusishwa na dini ya kishetani, sikuustaajabu sana kwani nilishawahi kusikia habari hizi kuwa wahuburi wengi wenye uwezo mkubwa hupata nguvu hizo kupitia njia hii japo sikufuatilia ila nilijihakikishia ukaribu wangu na Lau ungenipa nafasi ya kufahamu mengi zaidi.
Nilitafakari maelezo ya Lau kuhusu vyote alivyosema na kuona nipo kwenye mtihani mkubwa tena mzito! Kwa maelezo yale nilihisi hata kuhangaika kwangu kuwakwepa ni bure kwani freemansons wanaona popote ulipo. Alama yao ipo kwenye noti ya dolla ambapo ukichunguza vizuri utaona alama ya jicho kwenye pembe tatu likiitwa All See Eye yaani jicho lionalo popote. Haya yote nilifunuliwa na Lau. Tuliendelea na safari. Tayari jua lilikuwa limeshachomoza huku gari lile likiendelea kukata barabara na kufanya watu watulie wakimpa nafasi dereva uwezo wake wa kuliendesha gari lile.
****************
Jiijini Dar Es Salaam. Asubuhi
Hali ya hewa na utulivu ulitanda jijini Dar huku pilika pilika za watu na magari wakiwahi makazini zikishika nafasi yake. Huyu alikuwa akienda huku na huyu akienda kule.Mlio wa alamu ya saa iliyoashiria saa 12 za asubuhi ulitosha kukatisha usingizi wa mama yake Irene. Aliamka na kusali kidogo akimshukuru Mungu kwa uhai na uzima. Katika sala yake hiyo pia alimshukuru Mungu kwa kumfanya mvumilivu huku akiomba mwanae Irene awe mzima wa afya. Alitandika kitanda na baada ya hapo usafi ukafuta. Alipika chai na kishindwa kuinywa kwani kutokana na mawazo alijikuta akifanya kazi muda mrefu tena kwa pole hivyo muda ukawa umemuishia. Ni muda wa kuonana na askari wa kituo cha polisi cha Osterbay jijini Dar Es Salaam juu ya kuootea kwa mwanane Irene.
Huko Osterbay kituo cha Polisi majira ya Asubuhi.
Askari wa kwanza kama walivyo ahidiana jana aliamka mapema na kuwahi kwa mkuu wake ili kupewa kibali cha kwenda chuo kikuu cha Dar Es Salaam kupepeleza habari za awali. Mkuu alimuandikia kibali na kumruhusu. Aliondoka tayari kwenda Mlima. Alifika na kupokelewa na walinzi. Akijitambukisha kama ndugu wa Irene. Walinzi walianza usumbufu wa hapa na pale. Mwishowe aliwaonesha kitambulisho na wakamruhusu aingie. Alienda moja kwa moja hadi jengo utawala na kuomba kuonana na mlezi wa wanafunzi mabwenini na kuoewa taarifa kuwa Irene alikuwa akikaa hostel za mabibo hall five chumba namba A 6.
Askari mwingine alikuwa kaenda Tanzania Communication Regulation Authority TCRA kuomba kibali cha kufuatilia mawasiliano ya simu yaliyofanywa na Irene kabla ya kutoweka jijini Dar Es Salaam. Alipewa vibali vya kuingia katika ofisi za mitandao yote ya simu. Namba alizopewa awali na mama yake zilionesha kuchati kawaida na marafiki zake. Pia rekodi za mawasiliano ya mwisho yalikuwa ni simu iliyopigwa kwa mama yake. Maelezo yake yalikuwa hataenda rikizo kwa kuwa ni muda mfupi. Lakini central tracking system ilionesha network yake ya mwisho kutumia ilikuwa mkoa wa Iringa manara wa posta. Imei ziliiingizwa na ilionekana simu yake ilikuwa ikitumiwa na mtu aliyekuwa Mufindi huko Iringa, ijapo laini yake ilikuwa haipatikani kabisa.
Upande wa mama Irene..
Askari wa kike aliyekuwa kavalia sare ya kipolisi alikuwa akimhoji mama irene Masawali kadhaa. Swali lililokuwa gumu ni kwanini hakuwahi kutoa taarifa mapema kituo cha polisi. Mama Irene alijibu kuwa hakuwahi kuwa na wasiwasi na mwanae. Hata hivyo alipata taarifa kutoka kwa marafiki zake wakimuuliza kwanini kwanini Irene hapatikani na kachelewa shule. Kwa maelezo yale askari alipata kujua kuwa Irene hakumuaga mtu yeyote yule. Swali lingine ilikuwa kama Irene alishawahi kuugua magonjwa akili nk. Mama Irene alijibu haijawahi kutokea kabisa. Pia askari alitaka kujua kama Irene alikuwa na Matatizo ya kisaikolojia kama kutendwa au kuachwa na mpenzi au kushindwa masomo. Mama Irene alijubu kuwa hawezi kuwa msemaji sana kuhusu mahusiano ya mwanae kwani hakuwahi mshiriksha chochote. Pia aliongezea kuwa alijua Irene alikuwa single na si vinginevyo. Kuhusu masomo alisema mwanae alikuwa akimueleza kujitahidi hivyo hadhani kama kinaweza kuwa chanzo chake. Askari aliongezea swali lingine, kuhusu baba wa Irene na uhusiano na ndugu wengine. Swali hili lilimfanya mama Irene akae kimya kwa muda bila kusema neno. Ilionesha lilikuwa swali gumu kwake..
*** **** **** **** *****
Irene na Lau Wakiwa kwenye gari..
Gari liliendelea kutembea huku kukiwa kumekuchwa na hali ya jua ikitawala. Nilichungulia dirishani na kuona tulikuwa tupo maeneo ya Chalinze. Nilijawa na furaha sana, tumaini la kuwaona baba na mama yangu likawa kubwa sana. Nilijikuta nikipatwa na huzuni ghafla kuanza kuliona jiji la Dar, nikakumbuka kuwa sikuwa mwanafunzi wa chuo tena. Kweli ngoswe penzi kitovu cha uzembe. Iliniuma sana kwani penzi la kijana Franc lilikuwa limetia doa jeusi maisha yangu yote. Machozi yalinilenga lenga nikulimuangalia Lau aliyekuwa akisinzia kwa usingizi.
Nikiwa bado kwenye dimbwi la mawazo nilistushwa baada ya gari kufunga break kali na za ghafla zilizofanya abiria kuhama viti na kugonga siti za mbele. Taharuki ikaanza kwani abiria walilaani dereva kuendesha bila ustadi, huku wengine wakitukana matusi "msenge huyu" na kumzomea. Kila mtu aliongea lake lakini mimi na Lau macho yetu yalikuwa mbele kubaini hasa nini kilikuwa chanzo cha dereva kufunga break kali vile tena kwenye kona. Macho ya Lau yaliamka huwezi kudhani kama ndiye aliyekuwa akisinzia muda sio mrefu.
Mbele ya basi letu, walisimama wanaume wawili walioshiba vizuri kwa mazoezi, nilifuta macho yangu na kuwaaangalia vizuri, sura zile hazingukwa ngeni kabisa machoni pangu, hali ile ilinifanya nifikiri kwa kasi ili niwakumbuke vizuri na upesi.
Taarifa za za viumbe niliowaona zilipelekwa kwenye ubongo wa nyuma kisha mbele na kumbukumba za ubongo zikanambia hao ni Rama na Kriss wale wa kule porini. Lau aliniangalia na kunipa ishara fulani kama wanenavyo wahenga kuwa waswahili wa pemba hujuana kwa vilemba. Bila kuchelewa nikamuona kondakta akitoka kwa hasira na kumkwida Kriss ambaye alimuangalia tu kondakta bila kumfanya lolote. Kondakta kuona vile kwa hasira alimpiga Kriss Ngumi ya uso, Kriss wala hakutikisika badala yake alimtandika kondakta kofi moja lilompeleka chini kama gunia la viazi na kumfanya apige ukelele wa maumivu makali mno.
Walimuacha kondakta akiugulia maumivu na kimadaha Kriss na Rama wakaanza kuja kwenye basi. Sijui nani aliwaonesha kuwa tuko kwenye hili gari, nilijikuta nikiwaza bila jibu. Nilijua tu ni mimi na Lau ndio mawindo yao. Na kweli wametupata. Hakuna pa kukimbilia. Abiria walianza kupiga mayowe ya hasira huku wakiwa hawajui nini kinaendelea. Mimi, Lau, Rama na Chriss ndio tulikuwa tunaujua mtanange mzima...
Itaendlea..
Usikose episode ya 15
No comments:
Post a Comment