Tuesday, October 31, 2017

USIWE Mwanamke wa Hivi...

USIWE MWANAMKE WA HIVI... 

Usipime kwa Macho,  Wenzako wameteketea...

Inaanzaia hapa story  nzima...


Umekutana nae facebook.

Unaangalia picha zake za wasifu!

Anakutumia ujumbe inbox.

Unamjibu vizuri kwa furaha.

Ni mwanaume mtanashati, msafi na HB..

Anaendesha LIMOUSINE MPYA..
Anakutongoza,  unakubali.

Unapanga tarehe ya kukutana.

Unavaa vizuri,  bila nguo za ndani.

Unajipulizia perfume nzuri,  unanukia.

Makeup  safi,  uso unang'aa unajiangali kwa kioo.

Unaridhika,  umependeza wow, unatingisha kiuno.

Anakupeleka lunch, Plaza hotel.

Anakupeleka kwenye vinywaji, New City pub.

Mnafurahi wote wawili.

Anaishika mikono yako kimahaba.

Unafurahi mno jinsi anavyokushika inakupa wazimu

Unamwangalia na kutabasamu.

Anakuangalia kwa jicho la  huba na kutabasamu.

Unajikuta kwenye hisia nzito za kimapenzi.

Kama vile unamfahamu toka utoto.

Anakuchukua kukupeleka kwake.

Wow!  Ghorofa zuri,  upepo mwanana wa kiyoyozi.

Unaingia chumbani.

Kwa raha anakukaribisha kitandani.

Unalala ukiwa na furaha mno.

Anaanza kukubusu kimahaba.

Unafurahi,  unambusu, unaruhusu tayari afanye!

Ohh raha sana, unalalamika! Na macho unafumba, kwa utamu

Unajua ni makosa,  ila unahisi utamu.

Unamuuliza kuhusu kinga,  anajibu umechelewa.

Unakubali, hupendi kumsumbua.


Anaendelea na shughuli,  utamu mpaka kisogoni.

Anakwambia anakupenda,  kimahaba unajibu.

Nakupenda pia.

Anatoka kukuletea maji, anakusaidia kukunywesha.

ohh unajiona ni malkia.

Asante unamwambia.

Unajiona  ni maalum mno kwake.

"Huyu ndio mwenyewe" unajisemea nafsini.

Unavaa vinguo vyako!

Tena hakusaudii kuvaa.

Kama alivo saidia kuvua, hujiulizi! ?

Anakusindikiza stendi ya tax.

Anakubusu shavuni na kusema

" nimeridhika na uwepo wako"

Anakupa pesa.

Unatabasamu na kumwambia.

"tutaonana kesho mume"

Anakaa kimyaa

Taksi inaondoka, safari kurudi kwenu.

Unatabasamu pekee kwenye taksi.

Unafika nyumban unamwambia nimefika salama.

Yuko online ila hakujibu.

Unaanza kumchukia,  wallah unaumia

"AMESHAKUBLOCK"

****     ***    ***

Dakika,  masaa,  siku,  wiki,  miezi inapita!

Unahisi homa,  uchovu,  huna nguvu,

Unapungua uzito,  ndoto za ajabu.

Unaamua kwenda hospitali.

Unapimwa  Afya.

Dakika zinapita

Daktari anakuja!

Moyo unadunda unataka kuchomoka!

Anafungua kinywa chake....

"pole una HIV +  na  UJAUZITO"

"KIUIPI?!!?"


Unajiuliza.

Humuelewi daktari.

Ukweli inakuuma.

Unaenda nyumbani.

Muoga

umechanganyikiwa.

unafika stendi ya basi

unalala kila seehehhemu, huna tumaini,  huna hisia.

Unaona kifo kinakuja karibu.

unaangalia juu angani unamuomba Mungu

Huo ndio mwisho wako.

###  jjj  ###  ***
Usiwe msichana wa hivi,  usingalia uzuri wa nje na vitu
 anavyomilki
ISHI MAISHA HALISI

USIIGIZE,
USIIGE,
USIFUATE MKUMBO,
USIJILINGANISHE NA FULANI.

KUWA MWANAMKE WA thamani
THAMINI MAISHA YAKO.

Kuwa msivhana wa heshima.

Kwa Wasichna wote
na wavulana wote....r
anco Samuel

jicho lionalo mbali

franco samuel  stories..

No comments:

Audio