Friday, October 27, 2017

SITAMSAHAU FRANC 12...

Stori. :: SITAMSAHAU FRANC
Mtunzi ::  FRANCO SAMUEL 
              :: 0768800687
Episode no 12
Ilipoishia......


Aliondoka mwenyeji yule ambaye kiumri nilihisi tulilingana.  Aliliingia chumbani na nilikuwa makini mno
"baba kuna wageni ila nmeona dada ni km yule muuaji anayetafutwa,  njoo uwaone wapo sebuleni" niliisikia sauti ile ya chini. Lau pia alisikia...... Nilikosa  nguvu nikajutia uamzi wa kukubali kwenda kwa balozi 
"kumbe hata huku kijijni wanajua juu yangu hadii sura?" nilijiwazia.... 
Mlango Wa chumbani ulifinguliwa... Amani ikapotea... 
Sasa endelea... 

Mlango ulifunguliwa kijana akiwa wa kwanza kutoka.  Nilikuwa na wasiwasi sana,  mzee alifuata nyuma akiwa kavalia kikoi kiunoni akiacha tumbo lilinenepa kihasara likiwa wazi kabisa. Alituangalia kwa jicho la kichovu kuashiria  usingizi ulikuwa ukimchukua. 

Alitembea polepole, huku akishikilia mlango utafikiri kalewa hivi, alitufikia na kutuangalia sana. 
Niliona aibu kwa kuwa nilikuwa sijavaa vizuri, ila sikuwa na jinsi
"nyie akina nani? " aliongea kwa sauti ya kukoroma na kivivu
"mzee Shikamoo, sisi ni wananchi tumekuja kupata hifadhi tulikuwa tunasafari tumechelewa" alijibu Lau wakati huo niliinamisha kichwa chini. 
"ahh mnaenda wapi?"
"kesho tukiamka tunaenda mjini ili tuendelee na safari"
"kwani mmetokea wapi? Na ni akina nani nyie? "
Aliuliza swali hili huku akinitazama, niliona Lau akikunja sura kuashiria swali lile lilikuwa gumu kulimeza, alionesha hakuwa na majibu! 
"mmekaa kimya jibuni"
"mzee kama nilivyosema tunasafiri kama unatupa hifadhi sema"
"nitawapaje hifadhi hamtaki kujitambulisha? "basi kama huwezi tuache tuende
"nimeshawajua Tayari,  wewe binti 
Alinisonta nikiwa nimeinamisha kichwa chini, akaendelea
"wewe ni muuaji mkubwa mno, tumeona kwenye taarifa,  nadhani umejileta sehemu salama kabisa ili nikufikishe kwa police "
Niliinuka na kumshika Lau ili tuondoke, kiukweli ilikuwa balaa lingine,  tulitoka bila kuongea neno, tukimuacha akiwa anchukua simu.
"napiga simu police sasa hivi" alisikika akisema wakti huo Lau akipambana kufungua geti lile la mitimiti. 
Aliahamgaika halifunguki ikabidi tuvunje ili tutoke,  lilivunjika tukatoka mbio na kuanza kukimbi, mzee alipiga kelele na kupiga filimbi kuashiria hatari,  mitaani watu walisikika wakitoka huku kelele za kulikoni zikishika hatamu. 

Tulikimbia na kujibanza kwenye ukuta flani,  nikaona nyumba moja nje wameanika nguo!
Wazo la kuiba nguo ya kuvaa lilinijia nikamweleza Lau 
"Lau nataka nikachukue ile nguo pale nivae
"hapana usifanye hivyo utaleta balaa
"liwalo na liwe bwana acha niende
"no usiende subiri 
Nilimchukia Lau kwa kunizuia, watu walikuwa wengi huku wakiongea kulikoni kulikoni waliendlea kukusanyika kwa balozi kama ujuavyo kijijini walivyo na ushirikiano. 

Hatukujua kwa kwenda kabisa kwa kuwa ugeni na kijiji kile ulitufanya kutindikiwa na kutojua hata pa kukimbilia kanisa. 
"Lau tunafanyaje na tunaenda wapi?
"yaani sijui hata kwa kwenda kwa kuwa sikijui kabisa kijiji hiki.. 
"daa leo basi tumekwisha
"ila wait tiluone nini kinaendelea hapa... 

Niliona kama Lau hakuwa mnjanja aliyejua mbinu za kukwepa kama nilivyofikiri. Nilishaanza kukata tamaa, tuliskia king'ora cha police kwa mbali na king'ora kile kiliashiria gari lingefika si muda.  Baridi nayo ilipenya mithili ya misumari,  nilihisi kutopona tena. 

"naenda pale nikakuchukulie nguo angalia kama kuna mtu nistuwe sawa?  
"aha sawa nenda
Lau alienda jwa mwendo wa kunyata na kuifikia kamba akachukua nguo na kunirushia niliokota na kuvaa ile suruli, ilikuwa kubwa wenyewe wanaitaga sixteen GB. Niliifunga hivo hivyo nikisubiri lau arudi, hakutokea, dakika ikapita, zikawa dakika 5 haji na haonekani
"ameamua kunikimbia nini!  Nitafia hapa leo mimi huku ugenini" nilijisemea kwa kukata tamaa.  
Niliamua kumfata na kumkuta pembeni kidogo ya ile nyumba palikuwa na pikipiki ni kama alikuwa akiiyengeneza hivi
"wewe unafanya nini? 
Alistuka sana kiukweli, 
"ahha umeamua kinifata huku
"nilijua umenitoroka mimi jamani
"hapana nafanya maarifa hapa ili tuondoke
"sawa " tuliongea kwa sauti za chini mno kiasi cha kutosikika kwa mtu yeyote. 

Nilitumia upenyo huo kuchagua suruali nzuri na kuivua ile kubwa kisha nikaivaa ile ndogo. Nilibadilisha mbele ya Lau kwani tayari sikuna cha kuogopa. Wakati huo alikuwa akikata nyaya fulani kwenye ile pikipiki kisha akaanza kuisukuma polepole. 
"unataka kuipeleka wapi?  Nilimhoji
"we subiri
"mbona umeikata nyaya? 
"ngoja tutoke hapa kidogo utajua tu

Polepole tulifika barabarani na akaniambia nipande pikipiki, kisha akainama na kugusisha nyaja,  ngoma ikaunguruma.  Nilitabasamu mno kiukweli nilifurahi
"nilikata nyaja ili tupige shoti iwake! 
"ahaa kumbe ndio wanavyofanyaga wezi? 
"yeah,  sema kingine tushukuru Mungu hakuifunga usukani. 

Alipanda na kuanza kuendesha huku akinisihi nimshikilie yeye kwa nguvu kwani angeendesha mwendo wa hatari. 
Gari la polisi lilisikika likiwa karibu mno ikabidi tuingie mitaani ili lipite,  na kweli lilipita kuelekea kule kwa balozi.

Lau aliendesha ila kilikuwa kitendawili wapi tuelekee. Aliendesha kifuata kule ambako gari la polisi limetokea 
"nadhani huku walikotokea polisi ndio mjini" alisema lau huku akiendesha pikipiki ile... 

Tulitembea nikiwa nimemshikilia lau kwa nguvu kwani mwendo aliotembea ulikuwa wa hatari mno na kila alipofikia sehemu za kuteremka ali weka free. Tulifika mahali na kuona nyuma kuna taa ikitumulika na nyuma yetu kuna pikipiki ikitufuata

Lau alizidi kuongeza mwendo huku akisema ni bora twende mbele kuliko kukamatwa kizembe kizembe. Pikipiki ile nayo ilizidi kutufuata na sasa nilijua wameshatufahamu.  King'ora pia kilisikika kuashiria gari la polisi lilikuwa likija pia.

Tulikuwa maporini kwa haraka nilijua ni sehemu inayotenga kijiji kimoja na kingine.  Bado mwendo ulikuwa mkubwa mno ambao aliendesha. Na kile tulifanikiwa kuwaacha mbali wale watu wa pikipiki na gari la police. 

Nilimuona lau kama shujaa kwani tayari tulikuwa tumeiepuka hatari ile. Lau aliendesha na ghafla pikipiki ikazima 
"mungu wangu kuna nini? Nilihoji
"nahisi mafuta yamekata 
"daa tunafanyaje sasa na huku porini
"sijui hata ila tutatokaje hapa

Ilibidi tushuke na kuisukuma pembeni ile pikipiki kisha tukaingia porini kujificha kwani waliokuwa wanatufukuzia walikuwa karibu, tuliingia kwenye kichaka kimoja na kukaa kimya kulikuwa na upenyo na tuliweza kuona ile pikipiki ikiwa na watu wawili,  walifika na ule taa ya mbele ilionyesha pikipiki yetu iliyopaki pembeni. Walipunguza mwendo na kushuka 
"oya wameenda wapi? 
"sijui watakuwa upande gani 
"umeona pikipiki yenyewe kumbe hawa ni wezi
"ndiyo na plate namba ni ile ile aliyolalamika jamaa kuwa imeibiwa! 
Yalikhwa ni maongezi ya wale watu yakiashiria walikuwa wakituwinda

"inamaana wamegundua tayari?" nilimhoji Lau kwa sauti ya kunong'ona
"inawezekana kabisa 

Walienda upande wa pili wa barabara huku sisi tukiwa upande mwingine. Pikipiki yao ilikuwa ikiunguruma huku taa ikiwaka. Nilishangaa gari la polisi halaifiki tu kwa jinsi walivyokuwa wakitufukuzia. 
"wameenda kule,  chakufanya hapa ni kwenda fasta tukapande ile pikipiki yao na kuondoka"
"Lau inawekanaje hiyo"
"sifa wepesi Irene,  kwa kuwa ipo on ni kupanda na kutimua kwa kasi"

Moyo wangu ulidunda kwa wasiwasi mkubwa. Nilijina ni dhaifu na nisingeweza kufanya tukio lile la kishujaa. 
"twende sasa wameenda mbali, twende kabla ya gari la polisi kufika"
"Lau naogopa sana"
"jikaze twende

Alinishika mkono tukaanza kutembea fasta fasta, tulifikia pikipiki na kupanda haraka kami electron za umeme zisafirijo. 
"shikilia kwa nguvu" alisema Lau 
Sikujibu nilimshikilia na akaiondoa pikipiki kwa kasi kama vile inataka kupaa.  Alikimbiza mno, nyuma niliwashuhudia wale watu wakijaribu kufukuzia huku gari la polisi nalo likija ka kasi kubwa mno. 

Alikimbiza sana nikiwa nimeshikilia tumbo lake,  upepo ulisababisha macho yangu yatoe machozi.  Niligeuka kwa kuibia sikuona tena gari la polisi,  tulikuwa tumeliacha mbali mno. 
Hatimaye tulianza kuingia kijiji na kadri tulivosongo tuliona kumbe hakikuwa kijiji ila mji kabisa. 
 Nilivuta pumzi kubwa nikimshukuru Mungu mwema kwa yote.  Kwa mbali nilihisi njaa ikiuma tumbo lilikuwa likidai chochote ili lilidhike.  

Lau alizima pikipiki  na kupaki pembeni,  tulisogelea mgahawa fulani ulikuwa pale ili tule lakini mi sikuwa na hela. Tuliingia ndani ila kwa nje king'ora cha polisi kilisikika na nilichungulia nikaona likipaki pale tulipoacha pikipiki yetu. 

Yaani nilinyong'onyea kabisa... 
Nilikosa nguvu sana,  nilishuhudia askari wakishuka na bunduki huku wakija kwa kasi pale mgahawani.  Lau aliniangalia na kunipa ishara fulani. Tayari askari walikuwa wakikaribia mlangoni!! 
Tulibaki tumeduwa tu tusijue cha kufanya ....

Usikose namba 13....

No comments:

Audio