Friday, October 27, 2017

SITAMSAHAU FRANC 11

Stori. :: SITAMSAHAU FRANC
Mtunzi ::  FRANCO SAMUEL 
              :: 0768800687
Episode no 11
Ilipoishia.......


"nini utasema nikuelewe? Wewe usitukoseshe pesa siye"
"hapana si hivyo, sikilizeni" alisema Lau mara nikashuhudia Kris akimtandika Lau ngumi ya usoni, kweli ulikuwa ugomvi mkubwa!

Akili sasa ilikaa sawa,  nikajilaumu kwa kujifanya mkweli mithili ya bikira Maria! Niliinuka fasta ili nichomoke lakini Rama alikuwa akiniangalia kwa jicho la hasira huku akisogea mlangoni mwa handaki lile... 
Sikuwa na pakutokea,  Lau mwokozi wangu alikuwa akiugulia maumivu ya kupigwa... 
Niliduwaa nisijue cha kufanya,  ukweli umeniponza, nilinljilaumu mno...
Sasa songa nayo mwenyewe…. …

Sikuwa na cha kufanya zaid tu nilizidisha dua kwa Mungu na kujiona kumbe nilikuwa na maadui wengi mno ambao walikuwa wakinizunguka kila kona.  Sikuwa na pa kwenda kwani tayri Rama alikaa mlangoni tena akiniangalia kwa macho yaliyomtoka pima na ukali!

Sekunde kadhaa ni kama nilipoteza Fahamu nilijiweka sawa na kuamua kutembea kwenda alipo Lau ili nimsaidie bado niliamini ndiye wa kuniokoa ndani ya lile handaki,  kabla sijamfikia Kris aliendelea kumpiga huku akitukana ovyo utafikiri si watu waliofanya kazi pamoja 
Sikujua nilipata wapi nguvu nikajikuta nimeparua Kris usoni na akawa analalamika macho  na kuacha kumpiga Lau. Nilimuinua Lau  ili tumkabili Rama amliyekuwa akituangalia mithili ya mtu aliyepotea mtaa.  
"pole sana Lau"
"asante,  tutafute namna ya kutoka ha..... 
Kabla hajamalizia, Rama alimrukia Lau nakuanza kumpiga wakati huo Kris alikuwa akigalagala chini chini kwa maumivu.
Niliamua kumsaidia Lau kama kawaida mbinu yangu kuu kwa adui huwa ni moja tu,  kumpoteza macho nilihangaika lakini Rama akaudaka mkono wangu na kunitupilia mbali nilibweka kama toto la mbwa koko. 

Nilijaribu tena safari hii nilifanikiwa kuparua jicho Moja na kumfanya Rama aache kumpiga Lau aliyekuwa akihema kwa kasi mithili ya majogoo yapiganavyo.
 "inuka twende Lau"
Niliona hainuki ikabidi nimwinue tukaanza kutoka 
"Lau unamsaliti bosi wako kisa huyo mwanamke,  nenda tu ila huyo huyo atakuua tu" alisikika Rama wakati tukiufikia mlango. 
"lazima niseme kwa bosi kabla hamjavuka hili pori mtakuwa mmekamtwa tu" aliongezea Kris... 
Lau hakujali tulianza kukimbia kuelekea kusikojulikana ila Lau akaomba kurudi kwenye ile nyumba
"Irene naomba nirudi kule"
"urudi kufanya nini?"
"nataka nikawafungie ndani ili wastoke njee kupiga simu kwa kuwa ukiwa mule ndani network haiishiki kwahiyo wakitoka nje lazima wapige simu kwa bosi Na hatutavuka hili pori watatukamata tu"
"mhh ukirudi wakakukamata au kupiga risasi?
"hapana hawawezi kufanya hivyo"
"hapana Lau ukumbuke ukiwafungia ndani watakufa na njaa,  sipendi iwe hivyo acha twende Mungu pekee anajua safari yetu"

Nilipatawa na huruma sana juu ya kuwafungia Rama na Kris ndani kwani wangekufa kwa kukosa chakula.  Nilifurahi kwa kuwa Lau alikubali na tukaanza kukimbia,  mwanzoni tulitumia njia ambayo ilionekana 
watu wachache Walishawahi kuapita,  jua lilikuwa kali,  ukizingatia sijaoga na ndio nimetoka kula nilitoa jasho mno. 
Lau pia alikuwa akitweta tu na kuhema kama boko nikajiuliza ina maana mwili huu niliojua ni wa kimazoezi kumbe ni bure kabisa! 

Tuliacha njia ile baada ya Lau kusema kama tungeifuata basi rahisi kukamatwa hivyo tukaingia porini kuanza kutengeneza njia yetu,  nilimfuata lau tu kwa nyuma kwakuwa sikuwa nikujua,  nilichoka mno lakini ningefanyaje!  Haya yote kwaajili ya franc mwanaume nilyempenda,  nilijiona wa kwanza duniani kuwa na mikosi. 
"lazima nilipe kisasi,  siwezi kuacha lazima niwaue wote na mwisho nitajiua pia nikakutane na franc" nilikuwa nikiwaza huku tukiendleaa kukimbia.

Ilikuwa tamabarare ndefu huwezi kuona ilipoishia,  ubaya zaidi hakukuwa na sehemu ya maji kabisa masikini sisi tutakufa na kiu.  Nilihisi kuchoka nikamwomba lau tupumzike kwa kutembea, alikubali sasa tulienda mwendo wa wastani na jua nalo lilikuwa likiutafta machewo yake kwa kasi kubwa
"lau unauhakika tutafika vijiji vya karibu?
"ndio nina uhakika kabisa usiogope upo na kamanda"
"maana jua linaenda angalia ishakuwa jioni"
"tunafika ni kule mbele japo inatakiwa tukimbie zaidi"
"Sawa basi tuanze kukimbia bwana"
"twende hivi hivi nahisi kiu kali mno"
"me too lakini jikaze hakuna maji huku"

Tulikaza mwendo na kufanikiwa kuliona bonde,  tumaini la kupata maji liliongezeka sana,  ili bidi tukimbie kwakuwa palikuwa na mteremko kidogo.
Kweli palikuwa na maji kwenye kibonde kile,  japo pembezoni vilitapakaa vinyesi vya wanyama kuashiria walikunywa maji yake Sikuogopa nikajiinamisha upesi kunywa maji.
Lau pia alifanya hivyo,  tukanywa maji na kuosha nyuso zetu.  
"Lau naomba nikaoge ukae hapa unisubirii sijaoga siku ngingi mno"
"ahh unawaza kuoga tena kwenye vita kubwa kama hii? "
"sasa nifanyaje,  naoga mara moja"
"sawa nenda, fanya upesi nakaa hapa kwenye jiwe"
Niliondoka fast na kushuka chini kidogo ili Lau asinione. Akili ikanambia vipi akija akubake itakuwaje? Ahh potelea mbali nampa tu,  mbona niliyemtunzia kashapotea sasa nasubiri nini!  Hapana simpi mpka nifunge ndoa heshima kwa wazazi" nilijikuta nawaza hayo "aaah hivi mie chizi badala ya kuoga nawaza upuuzi" nilisema kwa sauti na kuanza kuvua nguo nioge. 

Nilimalizia ya mwisho na kuingia majini kuoga  nguo zikiwa kando ya kile kijito, nilianza kuoga miwasho ilizidi sana kutokana na ngozi kuchubuka na sikuwa nasabuni,  nilijikuna sana kama mtu mwenye upele. 

Nikiwa katika kuoga nilihisi kama watu wanaongea hivi,  kugeuka nikakutana na nyani wakubwa wakiwa wamechuka nguo zangu,  mmoja mkubwa wakiume alikuwa katangulia anakuja kwangu niliruka upesi na kuanza mbio kupanda kwenda kwa Lau. 

"Lau  lauuu nisaidie eeeee
nilikimbia ovyo ovyo, nilimkuta na kujishikisha kwake huku akinishangaa nikiwa uchi kabisa! 
Nilijifikiri sikuona pa kuficha, mkono mmoja nikaweka kifuani kuficha maziwa yangu na mwingine kiunoni huku nikibana mapaja yangu!
"kuna nyani wamechukua nguo zangu"
"ahh wapo huko chini? 
"ndiyo,  wamechukua
"ngoja nikupe hii
LAU alivua tisheti lake na kunipa,  kisha akaenda kule chini, na kuwakimbiza nyani,  walikimbia na nguo zangu zote wakiacha ya ndani tu.
nlivaa tisheti la Lau na kwa urefu wake lilifika magotini. Lau alikuja akiwa kashika chupi yangu na kunipa huku akiwa na aibu
"mkosi kweli wamebakiza hii tu"
Asikwambie mtu nilihisi aibu mno,  nikaipokea nikawaza nivae pale pale au laaa! Ama kweli maisha hubadilika mimi niliyezoea kubadili nguo kama hizi hata 3 kwa siku leo navaa moja wiki nzima!  Nilisikitika sana, kiukweli nilichoka mno!  Niliivaa hivyo hivyo japo hata rangi ilipotea kabisa ila sikuwa na jinsi,  Lau alishudia nikiiivaa! 
"vipi mbona kama una mawazo sana? 
"ahh basi tu Lau sijui yatakwisha lini.... 
Tulianza Kutembea na tayari kigiza kilianza kuingia, Lau akiwa na fulana na mie nikiwa na tisheti tu ndani hali iliyofanya maziwa yangu madogo yaelee hewani kwani tisheti lilikuwa kubwa sana. 

Tulitembea,  tulimbea tukatembea na nikahisi kuchoka. Nilizidi kujikaza ila uvumilivu ukanishinda
"Lau nimechoka tupumzike hapa kesho tumalizie safari"
"hapana tutazingirwa 
"Lau ila mwenzio nimechoka
"Jitahidi Irene tunakalibia si unasikia sauti za mziki,  angalia taa ile" Alionesha japo sikuona macho yangu hayakuona kabisa ila sauti nilisikia za miziki
"basi njoo nikubebe
nilikuwa nimchoka sikuweza hata kukataa.  Lau aliinamisha mgongo wake nikapanda akaniweka mabegani kama mtoto mdogo nkishikilia kichwa chakehe huku mapaja yangu Yakigusa shingo yake. 

Nilihisi aibu ila sikuwa na jinsi,  alitembea kwa kasi sana na kila tulipoenda hatua kadha; taa ambazo mwanzo sikuziona sasa niliziona, sauti za miziki hata watu pia ziliongezeka Kusikika. 

Tuliikuta njia na moja kwa moja kuongoza njia siyo muda tuliingia kijijini na ilikuwa saa 3 usiku nikiwa bado mabegani mwa lau huku nikimwomba Mungu atujaalie mema. 
"nishushe nitembee mwenyewe
"sawa nakushusha
Nilishuka na tukatembea,  tulimkuta mtu mmoja na kumuomba atuoneshe kwa balozi
"Nyie kina nanin?alihoji 
"sie wageni tunataka hifadhi
"sawa ongozeni hii njia mkifika mbele kuna maduka mawili,  na nyumba. Ile nyumba ndiyo ya balozi. 
Kwa kuwa kulikuwa na umeme haikuwa ngumu kubaini ile nyumba,  tulifika na kugonga! 
"karibu ingia" ilisika sauti ya kiume
lau alisukuma geti ila lilikuwa limefungwa,  
"nakuja kufungua" Ilisikika sauti kutoka ndani

tulisimama kidogo na hatimaye geti lilifunguliwa tukaingia,  geti likafungwa mwenyeji yule alituangalia sana
"karibu ndani
"asante" Alijibu lau,  muda wote nilikuwa kimya. tulipewa viti na kukaa. 
"ngoja nimwite baba"
Aliondoka mwenyeji yule ambaye kiumri nilihisi tulilingana.  Aliliingia chumbani na nilikuwa makini mno
"baba kuna wageni ila nmeona dada ni km yule muuaji anayetafutwa,  njoo uwaone wapo sebuleni" niliisikia sauti ile ya chini. Lau pia alisikia...... Nilikosa  nguvu nikajutia uamzi wa kukubali kwenda kwa balozi 
"kumbe hata huku kijijni wanajua juu yangu hadii sura?" nilijiwazia.... 
Mlango Wa chumbani ulifinguliwa... Amani ikapoteai.  
Itaendelea... ...

No comments:

Audio