Thamani ya Maisha yako
"Mwalimu aliingia darasani na kuwaonesha wanafunzi noti ya fedha ya shilingi elfu kumi. Ilikuwa mpya kutoka bank. Akawauliza wanafunzi kuwa ile noti ina thamani gani, wote wakajibu elfu kumi!
Akachukua noti nyingine ya elfu kumi iliyochoka mno, imepoteza rangi na kupauka. Ikaonekana kuanza kuchanika chanika. Akauliza thamani yake wanafunzi wakajibu ni elfu 10.
Akachukua noti ile mpya na kuikunja kunja na kuifinyanga. Ikajikunja mno, ikawa haijanyooka kama awali. Akawaonesha wanafunzi, wakajibu jibu lilelie la elfu kumi.
Akachukua noti nyingine ya elfu kumi imechoka na kuungwanishwa na gundi aina ya soltep. Wanafunzi wakajibu thamani ni ile ile ya 10
Mmejibu vema wanafunzi wangu, upya, usafi, kuchafuka, kuchoka na kuchachanika chanika kwa noti ya elfu kumi hakuharibu thamani yake. Ukiwa nayo mpya ni elfu kumi iwe imechoka au imechanika ni elfu kumi... "
Kisha mwalimu akamalizia kwa kusema..
"Katika maisha usiige
Tambua thamani yako na uitenze..
Changamoto na vikwazo visikushushe thamani bali iwe njia ya kuonesha thamani ya maisha yakoo...
Kumbuka kuwa na maisha mabaya sio kukosa thamani. Jithamini kwanza wewe mwenyewe...
Kuumia na kuteseka moyo wako kusikufanye ukose thamani na kuona maisha hayana thamani.
Kutendwa na kuachwa kusifanye uchukie na kuona huna thamani.. Nashangaa wengine hufikia hatua ya kukatisha uhai na maisha yao yenye thamani kubwa..
Kukataliwa, kunyanyaswa na kuteswa kusikunyime thamani... Jitengenezee thamani yako..
Kila mtu na maisha yake, uijue thamani yako... Usiige ya wengine..
Kukosa kitu fulani kusikufanye uone hauna thamani...
Siku zote kuishi ni thamani..
Tambua thamani ya maisha yakoo...
#Wants_to_see_you_change_EveryDay.
Franco Samuel
Friday, October 27, 2017
Thamani ya maisha yako....
Tags
# Mapenzi na Ushauri
About Admin
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Mapenzi na Ushauri
Labels:
Mapenzi na Ushauri
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment