Friday, October 27, 2017

Ushauri: Mambo 26 ujifunze

Mambo 26; Muhimu kujifunza.... 

 Na Malenga wa Ubena

 ©Raymond Mgeni 2017 

0676559211

1: Ubongo ni msuli wahitaji mazoezi kama ulivyo mwili unavyohitaji mazoezi yakutosha ili uwe imara na ukakamavu.

2. Kuna nguvu katika kujiandaa mapema katika maisha yetu,

3. Kila mwanadamu amepewa wajibu wa kugusa maisha ya mtu mwingine na kuishi kwa kutegemeana kwa vipaji, ujuzi na hata maisha kwa ujumla

4. Mazoea na kuchukulia mambo kikawaida ni adui wa kwanza wa kuzuia mtu kuwa na ubunifu

5. Elimu inayokosa kukabiliana na changamoto za kawaida za maisha ina walakini mkubwa sana

6. Kuna nguvu kubwa sana ya kufanya jambo kila siku pasipo kuacha, na ndivyo nidhamu ya mambo inahitaji kufanyika kila siku pasipo kuacha au kuishia njiani

7. Pamoja na wingi wa maarifa na taarifa nyingi katika ulimwengu huu, bado imekua kuna watu walio nyuma katika kusogea mbele kwa kukosa jambo moja muhimu nalo ni KUTOCHUKUA HATUA

8. Maisha yanayokosa malengo yanafananishwa na Nyumba ilokosa mlango na hukosa dira na pengine huzaa madhara pia

9. Ugumu wa jambo lolote lile kipimo cha pekee kabisa ni katika MUDA WA SUBIRA

10. Mazingira halisi kama uwepo wa miti hutoa somo kubwa sana katika maisha yetu, hasa somo la Subira na kuhimili misukosuko ijapo hali ya tofauti ya kimazingira

11. Anga linatufundisha kukubali hali tofauti tofauti katika maisha yetu na kuwa tayari katika kupokea ukweli huo, Anga moja ila hubeba uangavu mchana na giza wakati wa usiku

12. Thamini kila hatua ya maisha kabla ya kuhama katika hatua hiyo, kama ni kijana thamini ujana wako, kama ni mtu mzima thamini utu uzima wako kabla siku haujakuhama

13. Akili ni Kama Bustani upandacho ndicho huvunwa na wewe ndiye mtunza bustani kuhakikisha magugu na mapando yaso katika bustani unayang’oa

14. Siri ya kupata mawazo mengi ni kupanua wazo moja kuwa wazo lingine, na ndani ya lingine zua jingine.

15. Ukiruhusu utulivu wa ndani wa akili unaruhusu mazingira ya kupata mawazo na majibu ya changamoto unazopitia, wengi huwa hawapati mawazo mapya sababu hawana muda wa utulivu akilini mwao

16. Uhai ni mfano wa jani mtini laweza dondoka toka tawini kwa upepo au uzee wake

17. Kuchukua Hatua ndogo ndogo kila siku ni kujenga kichuguu kikubwa kama walivyo mchwa huanza kidogo kidogo ila ajabu yao ni mwonekano wa ukubwa wa kichuguu

18. Kabla ya kuanza kufanya jambo au kutengeneza kitu kuwa na macho kwa wateja wako wanataka kitu gani kutoka kwako.

19. Tunafanya vitu au mambo sababu hatupendi kujiingiza matatizoni au pengine tunafanya mambo tuonekane kwa vile watu wanataka tuwe, au tunafanya kwa kuheshimu hisia za watu na mwisho tunafanya ili kupokea pongezi fulani.

20. Ushairi hubeba Maisha halisi, na hujumuisha visa na matukio ya kila siku ya watu waishivyo na kuenenda

21. Kifo kipo karibu nasi, Muda wowote hutokea. Hivyo nafasi ya kuwa mzima ni ya pekee sana na si ya kubeza au kupuuza.

22. Wazo jipya ni gurudumu la maendeleo kukupa hatua zaidi ya kusonga mbele

23. Kuna Mambo madogo madogo tunayoyapa nafasi yenye kuharibu mambo makubwa tunayotamani kuyafikia. Vidogo vina nguvu ya kuangusha vikubwa. Kufuli kubwa hufunguliwa na Ufunguo mdogo

24. Kumbuka kuna Mambo dunia haitataka ujue Ukweli, na kutokujua ndipo hutumia kukuhadaa.

25. Usahaulivu wa mashaka, hofu na vitisho vya ulimwengu hutuletea Furaha na amani katika Maisha yetu.

26. Ng’ombe hajui thamani ya mkia wake mpaka umekatika, Na ndivyo katika maisha yetu kuna mambo mpaka yapotee ndipo akili hufunguka na macho huona thamani

Nikutakie tafakari njema sana kwa haya nilojifunza na kuendelea kuchukua hatua kila siku kwa nafasi ya uzima na afya. Nikutakie tafakari njema pia ya mwezi huu uendapo mwisho kabla ya Novemba.


Na Malenga wa Ubena
©Raymond Mgeni 2017
Mgeniraymond@yahoo.com
0676559211

Chukua Hatua, Ushindi ni Haki Yako

No comments:

Audio