SIMULIZI YA KUFUNDISHA..
WAKUMBUKE WAZAZI WAKO..
soma mpaka mwisho utajifunza..
"Irene mama yako ni mgonjwa sana. Tunahitaji msaada wako tafadhali. Pia mama alitueleza kuna kitu anataka kukwambia angetamani uje akuone. " iliongea sauti kwenye simu ya Irene aliyekuwa Meneja katika kampuni kubwa la kibiashara.
"Sawa nitaaangalia ili niondoke kuja. Ila bado niko bize sana. Kampuni bado wananitegemea." aling'aka kwa sauti ya maudhi huku akizungusha kiti chake hapo ofsini.
Aliwaza na kuona hakuna haja ya kwenda. "Mbona pesa nilitoa, dawa nilinunua, wanataka aje huku mjini kufanya nini? Kwani kule hakuna hospital? Kwanza akija watu watanichukuliaje" alijisemesha Irene binti mrembo, mwenye mwili uliojigawa vema kabisa ukitenga kiuno, maziwa na vingene mahala pake. Kila mtu alikriri Irene alikuwa binti mzuri sana tena aliyeumbika
*** **********************************************
"drii driii driii" ulikua mtetemo wa simu ya Irene. Aliingalia na kugundua ni namba ile ya jirani iliyompigia asubuhi kueleza habari za mama yake. Allingalia kwa wasiwasi na kuamua kupokea simu ile..
"Halo Irene. (kisha kwa utulivu) Samahani na pole, mama yako hatunaye tena duniani, Mungu kampenda zaidi. Pole sana Irene. Pole mno" iliongea simu ya jirani kwa upole kisha ikakata mithili ya mtu aliyeishiwa salio au dakika kwa simu yake..
"Mama mama yangu kwanini kwanini... Umeniacha mie sina raha! Nabaki yatima.. Uwiiiii " alilia kwa sauti sana Irene. Alikuwa akijibamiza huku na kule.
Alimpigia simu mchumba wake Allen akimweleza kifo cha mama yake mzazi. Allen alionekana kutokujali sana. Akampigia rafiki yake Martha ambaye alihuzunika ila akasema hata msindikiza kwani alikuwa na safari mkoani.
Akamoigia Joyce rafiki wanayefanya kazi pamoja. Joyce alidai hangekwenda msibani kwani alikuwa anaenda kumwona mama yake kijijini ili amsalimie!
Akaona bora amoigie Esta waliyekutana nae saloon kisha kuwa marafik wakubwa wakienda sehemu za starehe kama bar disko na kadhalika. Kwanza Esta limjibu yuko bize, kwa jinsi alivyomjibu Irene aligundua Esta alikuwa kifuani mwa mwananaume wakiendelea kupeana maraha ya dunia...
Kilikuwa kipindi kigumu sana kwake. Akakumbuka marehemu baba yake aliyedondokewa na mti kipindi cha uhai wake akihangaika kupata ada yake ili amalize chuo. Akakumbuka jinsi mama yake alivyokuwa akimsihi amkumbuke. Akakumbuka siku akiindoka mama yake akiuza kitanda na godoro kule kijijini ili atimize pesa yake baada ya kukosekana. Akakumbuka mama yake alikuwa akilala kwenye viroba vya mifuko chini.
Aliangalia nyumba yake kubwa ya kifahari yenye kila kitu machozi yakamtoka. Mpaka saa 8 usiku alikuwa akigalagala kitandani hana mfariji wala hapati usingizi.
Alipitiwa usingizi na kustuka tahamaki ilionesha saa 12 asubuhi. Aliwahi sokoni pekee na kununua vitu. Akarudi na kuvipanga katika gari yake tayari kwa safari ya kwenda kijijini.
Alipiga simu kwa Allen mchumba wake ila akajibiwa sitakwenda kwani mie hata kwenu hawanifahamu. Pia hukuwahi nambia kama mama anaumwa aliongezea jibu la nyongeza Allen. Kila siku niko nawe unanificha. Majibu ya Allen yalimzidishia machungu. Irene aliona dunia chungu kaachwa pekee. Alifunga mageti na kuoanda gari safari ya kwenda kijijini ikaanza.
Alikuwa pekee yake kwenye gari machozi yakimtoka huku akiendesha. Baada ya mwendo wa masaa kadhaa njiani alisimamishwa na akina mama wanne waliovalia vitenge na kutanda vichwa vyao. Aliwaza asisimamishe kwani aliona wanamchelewesha msibani. Akaamua asimamishe na kuwasikiliza.
"Hujambo binti, tunaomba msaada tunaenda msibani kijiji cha jirani. Tafadhali tusogeze ili tuwahi msiba hata ukituacha njiani sawa"
Bila kujibu Irene alionesha ishara ya kuwa waingie na walipoingia safari ikaanza. Walikaa kimya kidogo kisha mama mmoja akasema
"Yaani unaambiwa huyo mama marehemu alikuwa na mtoto mmoja tu wa kike. Toka aende huko mjini hajawahi kumkubuka"
"Sio hivyo tu nasikia mwanae huyo anayo kazi nzuri na jumba kama hekalu ila hakutaka hata mama yake afike na kutia baraka. " alidakia mama mwingine.
" Kwa kweli mabinti zetu wangejua tunavyoteseka wasingefanya haya. Baba yake alidondokewa na mti akihangaika kumtafutia pesa lakini binti kakuwa kageuka wala anaona mama yake mzee kama takataka. Ila hawa mabinti wakumbuke kuwa nao watazeeka. Siku ipo" alikandamiza mama mwingine na kufanya Irene alie kimya kimya machozi yamtoke na kuvuruga utulivu wa uendeshaji gari. Yamkini kina mama hawa hawakujua wanaongea na Irene. Hawakujua binti wanayemsema ndiye huyo....
Walifika kijijini. Irene alilia sana. Tofauti na misiba mingine ambayo watu wa mjini huja kumsindikiza rafiki yao kwa wingi Irene alikuwa pekee. Rafiki wa kumfariji alikuwa ni Flora waliyesoma nae akaishia lasaba na kukaa kule kule kijijini. Irene alilia sana. Akaangalia kajumba kadogo ka udongo ulimo kuwa mwili wa mama yake..aliingia kwa kuinama maana ukuta ulikuwa mfupi.
Alilia sana baada ya kuona mwili wa mama yake mzazi ukiwa umelazwa chini. Hata nguo za mama yake zilikuwa mbaya zilizochoka sana. Mwili wa mama yake ulikuwa umekonda sana. Alilia sana akajirusha huku na kule ila Flora na watu wengine wakamshikilia kwa nguvu.
Baada ya muda alitoa nguo mpya alizomnunulia mama na kuwapa watu wamvike. Walimvika ila hazikutoshaa. Viatu vilimvuka. Simanzi kubwa ilitanda msiba ule, nguo zilikuwa saizi ya mama ila hazikutosha. Viatu namba ile ile ila kila alipovikwa vipya vilishindwa kutosha. Akivikwa vya zamani vinatosha. Machozi yalimtoka mno irene. Uzuri ukampotea....mwili wa mama yake ulikataa vitu vipya, yamkini kama angemnunulia mama akiwa mzima ingekuwa raha kwake..Wakamzika mama kwa nguo zake za zamani. Irene alilia sana tena sana hakuna maelezo ya kilio chake na huzuni yake...
Baada ya mazishi siku ya pili, shangazi akaja na kumkabidhi Irene karatasi akimweleza kuwa iliandikwa na mama yake. Karatasi ile ilisomeka
"Mwanangu mpendwa Irene. Najua hunipendi kwa kuwa mimi sio mzuri, sina afya ni mchafu na sivutii. Hupendi hata nije kwako. Nilisikia umenunua gari na kujenga nyumba. Pia nilisikia una mchumba na marafiki. Nilisikia una kazi nzuri na una heshimika sana.
Ni kweli u mzuri hayo yote sababu yangu! Ombi langu niliomba uje nikuone. Mimi hata nisingekaa kwenye nyumba yako. Nilijua mimi ni wa kufa. Kukuona kwako kungefanya niishi... kungenipa tumaini jipya kabisa...
Mwanangu, kazi, marafiki na utajiri ni sababu ya mimi na baba yako. Unakumbuka kifo cha baba yako akihangaika ili usome!? Mwanangu Irene sitakulaumu ila nalaumu elimu uliyopata na kufanya uwe mpuuzaji..
Mwanangu ipo siku hao marafiki watakukimbia, kazi hutakuwa nayo gari litaharibika, mchumba atakuacha, ila ishi na watu vizuri. Nakuacha yatima Irene. Nilitamani nikuone ili niishi tena kuona wajukuu zangu ila umekuwa mgumu wamwili na roho. Nilijua kukuona kungenipa nguvu mpya na tumaini jipya..
Nakutakia maisha mema.
Mama yako Sarah Sikapenza"
Barua ile ilimuhukumu moja kwa moja Irene. Mchumba wake hakuwepo, marafiki hawakuwepo pale. Hakuwa na raha tena. Akiwa katika kulia simu yake ikaita. Alikuwa ni Allen akipiga simu. Akapokea na kuweka simu sikioni.
" haloo Irene pole na msiba. Nakupa taarifa kuwa nyumba yako imeteketea yote nadhani ni hitilafu ya umeme." Lilikuwa ni pigo lingine kwa irene hakuamini.
Alilia sana na sio muda akapigiwa simu. Alikuwa ni mkurugenzi mkuu wa kampuni aliyokuwa akifanyia kazi, mkurugenzi alieleza kuwa kulikuwa na hasara katika kampuni hivyo apishe kidogo kufanya uchunguzi. Tayari iliiashiria huenda atakosa kazi.
Alilia mno akabembelezwa asitulie. Alipanda gari na kuanza safari ya kurudi mjini. Alifika kwake na kushudia majivu na masizi tu ya nyumba yake ile. Akiwa pale mwenye huzuni na kukata tamaa walikuja polisi wa ukaguzi. Waliangalia enoeo zima la nyumba iliyoteketa na pia gari lake likaonekana kukosa kadi halisi ya mnunuzi kwani Irene alitumia njia ya mkato. Gari lilichukuliwa na kupelekwa kituoni.
Hakuwa na kwa kwenda zaidi ya kwa Allen mchumba wake aliyempenda sana Allen naye alikuwa kama vile hamuoni akidai hana kazi wala nyumba hivyo hawezi kuendelea kuwa na yeye kwa kuwa hana kazi wala pa kuishi. Mapenzi yalikuwa yameisha. Irene alichanganyikiwa. Hakuna cha Joyce Esta wala Martha, marafiki wote walipotea ghafla.
"Hata mchumba wangu hanitaki kweli mama umenilaani" alilia kwa huzuni mno.....
Siku tatu baadae Irene alipatikana amejiua kwa kitanzi. Ndio alijiua kutokana na msongo wa mawazo. Akazikwa na historia ya familia ikawa imesha..
.......................................................................................
Wakumbuke wazazi wako wewe kijana uliyeko mjini...
Uziri wako si kitu mbele ya mzazi wako, kumbuka hata bibi alikuwa binti mrembo tena zaidi yako...
Tambua ipo siku marafiki watakuacha pekee, hivyo ishi kwa akili..
Baraka za mazazi ni muhimu, ishi na wazazi vema..
Epuka mzazi asikupe laana na lazi zake, kwani hakika utaumia sana...
Fanya hima kumsaidia mzazi wako, yeye ndiye kakuleta duniani kwanza... hiyo iwe nira yako...
Mali, utajri na kazi ni vitu vya kupita, thamini uhai kwanza... uhai uhai ni kila kitu..
Kijana baba yako na mama yako wanataka kukuona. Lini uliwaona na kuwasalimia..? panda basi uende kule kijijini kapokee baraka zako
Hata angekuwa mchafu, chizi, amekonda, hana uzuri bado atabakia kama mzazi wako.... ulinyonya, ukilia na kulala katika kifua chake kilichofifia kwa uzee..
Share share share..
Franco Samuel
No comments:
Post a Comment