Tuesday, October 24, 2017

SITAMSAHAU FRANC 10...SIMULIZI

Stori.   :: SITAMSAHAU FRANC

Mtunzi ::  FRANCO SAMUEL          

 WhatsApp :: 0768800687

Episode no 10
Ilipoishia.......


Niliwaza na kutafakari kwa kina mno nisijue cha kufanya,  nikahisi machozi yakinilenga ila nikajitahidi Lau asijue,  nilifikiri  cha kufanya Nisikione kwani  tayari nilishamdanganya jina Lau, nilifikiri kumwambia ila nikaogopa, hasira zilinipanda mimi Irene na kuona kulipa kisasi ndiyo suluhu pekee hasa nikimkumbuka Franc..... "lazima kisasi mateso yote haya, chuo nimekosa"niliwaza. 

lakini pia niliwaza km Lau atakuwa ananidanganya ili nikamatwe ingekuwaje, nilibaki njia panda juu ya nini niamue, nimwambie lau ukweli,  au nifiche tu... 
Songa nayo...

Niliwaza sana mpaka Lau akanistukia,  kumbe kulikuwa na siri nzito iliyopelekea kifo cha Franc wangu,  nilijua ni ujio wangu kumbe ilikuwa imepangwa." nilijiwazia

Bado niliogopa kusema kuwa mimi ni nani,  japo kiduchu niliyameza maneno ya Lau na kuona ni mtu aliyemfahamu vema Franc. Nilitafakari na kuona ni bora niulize walijuaje ana uhusiano na huyo binti Irene Paul.

"Lau eti walijuaje ana uhusiano na huyo binti Irene ? "
"kuna wataalamu wa IT walifanya kazi na kudukua taarifa za mawasiliano yake. Kwa hiyo kila kitu alichokuwa akifanya kilikuwa kinafahamika ndiyo maana hata picha za binti zilichapishwa akiwa iringa!"  nikakumbuka siku ile pale mochwari. 
"sawa bosi wenu anasemaje juu ya huyo binti Irene kama akifanikiwa kumkamata? "

"anadai akimkamata tu na akijiridhisha kuwa Irene anajua kuhusu franc na kila kitu basi ni lazima afe ila kama hajui hajasema ata mfanya nini"

"oky sawa,  vipi sasa kuhusu aliyemgonga kuna mtu alikamatwa!"

"ujue kuwa ile  ilikuwa ni planned mission kwahiyo walichokifanya ni kumhusisha Irene na ndio maana baada ya kifo Irene alikamatwa ila inasadikika alikimbia,  na mpka leo wanamtafuta kwa kuwa wanamwogopa"

"ohh sawa kwa hyo wewe ulinambia upo tayari kulipa kisasi kwanini unataka kufanya kufanya hivyo? Na je unaweza kulipa kisasi bila ushirikiano na Irene?"

"nataka kulipa kisasi kwa kuwa yule ni ndugu yangu. Nimesoma nae,  pia napenda kumfahamu Irene ili nimuokoe kwa kuwa hawa watu ni hatari,  akikamatwa tu unaweza usisikie tena taarifa zake,  watamfinya moja kwa moja!"

"je wewe unaona bosi wako yuko sahihi?"

"siwezi kujua,  ila nikikutana na Irene na akasema ukweli nitajua nani ni sahihi kati ya bosi na Irene!l

"sawa nashukuru sana kaka Lau, mie nahis maumivu ya miguu na kichwa"

"twende ndani nikusaidie"

Tuliingia ndani ya ile nyumba yetu ya  chini ya ardhi kisha akanilaza kwenye kitanda changu cha nyasi pale chini! Kichwani mwangu niliwaza sana juu ya mustakabali Mzima wa tukio lile,  Niliona Lau ni mtu wa kipekee kwa jinsi alivyokuwa amejibu maswali yangu.  

Halmashauri ya ubongo wangu iliniambia mwambie ukweli huyo ndiye mwenyewe wa kukusaidia,  kuna kisauti kilinijia kikisema no usimwamini usiyemjua,  kiukweli nilikuwa katika lindi zito la mawazo. 

Lau alichemsha dawa fulani kwenye sufuria na kisha akatia chumvi nikiwa namwangalia,  alikuwa mrefu,  mweusi kawaida, mnene kiasi na mwili wake ulijengeka vizuri, kiufupi muonekano wake ni mwili wa kimazoezi. 

Alinijia pale  nilipolala na kuweka dawa kwenye bakuli kubwa kisha kunikanda vizuri,  nilifurahi sana. Alinishika polepole na kila aliponiwekea dawa hakusahau neno "pole" toka nianze kukutana na mateso ni siku pekee niliyoiona ya furaha.  Alihamia miguuni na kuikanda kwa dawa,  vidonda na michubuko ilizizima kadri chumvi ilivyoingia na kufanya nihisi maumivu makali mithili ya mishale ikipenyeza ndani ya mwili. Alinipa pole na kunifuta jasho usoni kwani maumivu yale yalifanya uso utoe kijasho chembamba.  Aliniangalia kwa huruma mno,  nilijawa na soni usoni nikakwepesha macho!

Alinifunika vizuri na kuondoka,  hali hii ilifanya nimwamini mno na kuona ni bora niseme ukweli.  Niliamua kumuita...

"lau kaka naomba nikwambie ukwe......."

Niliamua kukatisha kuna kitu kiliniambia usiseme
"naam nakuja kukusikiliza"
Alinisogelea na kukaa pembeni yangu,  kiukweli alikuwa na upendo sana.

"ukwe.. Ndio nini niambie"
"Lau kaka yangu ni lini mtanipeleka kijijini?" niliamua kubadilisha maada,  japo bado nilona bora niseme,  asikwambie mtu siri inatesa moyo bora kuisema,  ndiyo maana wengi hawakai na siri. 
"ukishapona tu tunakupeleka."

"mimi naomba wewe unipeleke"

"kwanini mimi siyo Kris ama Rama"

"nimekuamini ndiyo maana"

"ahaa sawa,  ila mkuu wetu ni Rama atakachooamua sawa,  so akisema twende na mimi ni sawa"

"nitafurahi sana nikienda na wewe"

"nitafurahi pia! Nikuulize swali?"

"yeah uliza tu" nilistuka hadi akagundua .

"vipi mbona umestuka sana,  hupendi maswali au huniamini? "

"ah. Hapana nakuamini sana tu" niliongea kwa woga,  nilihisi amenitambua kuwa mimi ni Irene kwani aliniangalia macho fulani hivi

"kule una kaa kijiji kipi,  matogole ua vile vya karibu na msavu au Likule? "

Kiukweli swali lile lilinipa wakati mgumu mno,  sikuwa nikijua chochote juu ya vijiji wala kata,  mbaya zaidi alikuwa ananikazia macho kinoma. Nilihisi kijasho,  nikaone bora. nifunguke Ukweli Na liwalo na liwe kwanza nimepitia mateso mengi na hata nihangaike mie ni mtu wa kufa...

"Lau kaka yangu, nimekuamini sana, nmesikiliza maelezo yako, nimekuuliza maswali mengi  umejibu! Umeniambia upo tayari kushirkiana na binti Irene Paul.  Irene Paul ni mimi nimepitia mengi mno mpka hapa,  sijui cha wazazi wangu na niliua watu wawili tu bila kukusudia,  kwahiyo nisaidie ni mimi Irene Paul" nilimaliza huku machozi  yakilenga machoni. 

Lau aliniangalia na hakuamini,  niliona akiwa kastuka sana,  sikujua amepokeaje kwani hata pale alipokaa alianza kusogea pembeni

"kweli wewe ni mwenyewe au unadanganya? "

"ni mimi lau,  Irene Paul, aliyetoroka jana polisi ni mimi ndiyo maana nmeumia hivi,  maisha yangu ni ya mateso mno" machozi yalinitoka! 

"pole usilie Irene,  nyamaza mie nitakusaidia! Kwahiyo franc alikuwa ndiyo mchumba wako,?"

"kiukweli nilimpenda na sikuwa nimemwambia,  siku niliyokuja kumwambia ndiyo aliyouliwa na nilibahatika kuona maiti yake tu,  nikikumbuka inaniuma mno" nililia kwa kwikwi. 

"pole usilie,  mie nipo" Lau alinifuta machozi na sasa nilikuwa nahisi kupendwa, niliona thamani yangu ikirudi japo nfsi iliulaumu moyo kwa kushindwa kubeba siri nzito, wakati moyo ukilaumu nafsi kwa kumuamini haraka Lau.  Neno la don't trust anyone lilikuja katika ubongo,  nilijaribu kulipotezea ila bado lilinijia tu,  furaha ikapotea nikajuta kutoa siri. 

Lau aliondoka pale na kupika na siyo muda Rama na wenzake wakaja,  ila hawakuwa na chochote kile
"oyi vipi na leo kapa" lau alisema baada ya Rama na Kris kufika

"no tumepata bonge la dili,  tumepeleka pale kilimani" 

"nikajua na leo kapa"

"leo imekuwa bahati huoni tumerudi mapema? "

"ni kweli,  karibuni chakula tayari"

Walikaa kuanza kula nikiwa bado pale kwenye kitanda changu cha nyasi,  nafsi na moyo vikisutana kwanini nimetoa siri, Lau alikuja na kunishika mikono akaniamsha na kinipeleka pale, wote waliangalia jinsi Lau alivyonishika nihisi aibu na kusema asinishike niliogopa,  nilivumilia nikajikongoja taratibu na kakaa. 
"Shikamooni"
"ahh unatuzeesha bwana" Rama 
"salimia za mchana au za kazi" akadakia Kris 
"sawa poleni na kazi "
"salama za kushinda na unaendeleaje?" alusema Rama. 
"Naendelea vema kabisa" muda wote Lau aliningalia nilikosa kujiamini. 

"sawa tule kwanza, "
Tulikula vitu vilivyofanania na viazi na nyama,  hata sikujua ni nini! Sikula sana Kwa kuwa uoga uliniingia na moyo uliuma mno ni kwanini nilisema ukweli,  nafsi na moyo vilishindana Nikawa na hofu kuu. 
Niliondoka na kwenda kulala pale pale,  bado Lau kila alipopata upenyo wa kuibia aliniangali, macho yake yalijaa huruma,  nilifarijika! 

Nililala ila nikakumbuka nina siku 3 sijaoga,  nikaamua nitulie nisubiri Lau ale akimaliza niombe kuoga angalau nisafishe mwili na kutoa uchovu.  Kweli mateso kitu kingine nilikuwa nmeshapoteza mvuto. 

Walimaliza kula na nikamsikia Rama akisema
"Lau huyu binti ni nani? "
Moyo wangu ulidunda mno,  nilitetemeka na nikamwangalua Lau ambaye aliniangalia pia
"anaitwa Irene Paul, ni mwenyewe ambaye bosi amekuwa akimsema kila mara! "
Kris na Rama waligeuka Kwa pamoja kuniangalia,  kiukweli nilikosa amani, niliulaumu moyo kwa kutotunza siri!
"Ahaa safi sana dili limekamillika sasa,  bosi wetu atafurahi" alisema Rama kauli iliyofinya moyo wangu na kuufanya uumie kama umepigiliwa misumari ya moto. 
"sio hivyo Rama kuna kitu nitawaeleza wote kuhusu Irene ili mjue" alisema Lau kwa umakini. 
"nini utasema nikuelewe? Wewe usitukoseshe pesa siye"
"hapana si hivyo, sikilizeni" alisema Lau mara nikashuhudia Kris akimtandika Lau ngumi ya usoni, kweli ulikuwa ugomvi mkubwa!

Akili sasa ilikaa sawa,  nikajilaumu kwa kujifanya mkweli mithili ya bikira Maria! Niliinuka fasta ili nichomoke lakini Rama alikuwa akiniangalia kwa jicho la hasira huku akisogea mlangoni mwa handaki lile... 
Sikuwa na pakutokea,  Lau mwokozi wangu alikuwa akiugulia maumivu ya kupigwa... 
Niliduwaa nisijue cha kufanya,  ukweli umeniponza, nilinljilaumu mno... 
Utaendelea... 
Haya ukweli umemwangamizaa.... 
Tukutane keshooo
Katika Episode ya 11...

No comments:

Audio