Monday, October 23, 2017

SITAMSAHAU FRANC 9..


Stori.   :: SITAMSAHAU FRANCMtunzi ::  FRANCO SAMUEL               :: 0768800687Episode no 9

Ilipoishia......

LAU hakuwa na jinsi,  aliunyanyua mwili wa Irene na kuanza kutoka nje kwenda kuutupa.  Irene Paul Binadamu mwenye thamani aliyepitia mengi kisa likiwa ni penzi la Franc leo anatupwa bila huruma kama mbwa porini tena bila hata Wazazi na ndugu kujua chochote, inauma sana!!  Lau alitembea pole pole huku Rama na Kris wakimuangalia,  Lau aliendela kutembea huku mwili legevu wa Irene ukiwa begani pake. Akiwa kaubeba  Lau alitafakari juu ya  mwili wa Irene. Kama binadamu aliumia kwani kutupwa bila kaburi wala ndugu kujua ni ina uma mno.. Mwili ulikuwa begani mwake tayari kwenda kuutupa bila kaburi ...

Masikini binti Irene ndiyo anatupwa kama mnyama!...Dunia haina huruma,  walimwengu wabaya ...uwiiii uwiii 
Songa nayo.....

Lau aliendela kutembea na hatimaye kufika nje ya kambi na kuuweka mwili wa Irene Paul chini huku akitafakari vitu kadha wa kadha juu ya tukio lile. Wakati anauweka mwili ule alihisi kama kuna mstuko fulani hali hii ilimfanya aushike mkono wa Irene na kuutikisa, kama alihisi Akiwa hai vile,  alitikisa mwili mzima na kushangaa Irene akikohoa kwa mbali, haraka haraka aliuparamia mdomo wa Irene na kuanza kupulizia pumzi kisha Irene akapata Fahamu kwa mbali.

Alimnyanyua upesi na kutembea akienda ndani huku akiita..

"Rama ameamka kumbe alikuwa kazimia tu, mtengeeni uji fasta!"

Aliingia na kumlaza kwenye malazi yake ya nyasi na kuendelea kumshughulikia ikiwemo kupiga piga misuli na kumpepea ili azidi kuimarika. Hatimaye Irene alikuwa akifumbua macho yake japo alikuwa hajui ni wapi yupo.

Rama alikuwa akipika uji wakati Kris mtaalamu wa masuala ya IT alikuwa akitengeneza vifaa vyake ili waweze kujua ni nini kinaendelea, kiufupi kila mmoja alionekana kufurahi kurudi upya duniani kwa binti yule ambaye alikuwa kawaachia kitendawili kikubwa kisichotdguka juu ya ujio wake kule porini!  Walikuwa na shauku ya kujua ni nani na kipi kimemfikisha katikati ya pori ya hifadhi, sehemu ambayo hata wao hawana uzoefu nayo licha ya kuwa wawindaji kwa muda mrefu.

Lau alimnywesha uji binti Irene aliyevipokea vijiko kama mtu mwenye njaa ya miaka mitatu,  kadri alivyokunywa ndivyo alivyozidi kuimarika na ndivyo tumaini la akina Lau, Kris na Rama kutaka kujua yule ni nani lilizidi kuongezeka!!

Kris alimaliza kazi yake ya ufundi na tayari ilikuwa saa 2 usiku,  japo kwa eneo walilokaa kuna umeme kama mchana,  na aliunganisha moja kwa moja wakaanza kuona taarifa ya habari, tayari Irene alikuwa vizuri japo hawakutaka kumuuliza maswali,  alionekana mwenye mawazo na soni kweli pale alipo kaa kwa kuwa hakuna hata mtu aliyemjua. 

"BINTI MUUAJI ATOKOMEA PORINI,  asababisha fujo kubwa, baadhi ya wananchi na abiria washikiliwa, zaidi tujiunge na mwandishi wetu wa habari aliyeko mkoani Morogoro; "Binti mmoja anayefahamika kwa jina la Irene Paul amefanikiwa kutoroka mikononi mwa jeshi la polisi na hii imetokea baada ya baadhi ya abiria kutaka kumsaidia wakati alipokuwa akikamatwa na jeshi hilo!  Tukio hili la kiaina yake limetokea leo mchana maeneo ya karibu na Mikumi ambapo binti huyo alikuwa akisafiri kwenda Dar baada ya kufanya mauaji ya kutisha mkoani iringa!  Hata hivyo jeshi la polisi limefanikiwa kuwatia mbaroni baadhi ya wananchi walimsaidia binti huyo hatari na watahusika kulisaidia jeshi kumpata binti huyo aliyetokomea maporini." Ilimalizika Ripoti hiyo iliyomuweka akili sawa Irene na kumfanya ajue kuwa ni yeye, japo hakuna picha yake iliyooneshwa, uoga ulimzidia mno akaanza kutetemeka.

"natamani sana kujua juu ya binti huyu,  japo ningeiona sura yake, kuna jambo zito Bosi wetu alituambia" alisema Rama

"mwisho utajulikana tu,  ila sidhani binti mdogo vile angeweza kufanya mauaji ya kutisha na kuzizima namna ile,  nadhani kuna watu wapo nyuma yake au wanazunguka pazia ili kuonekana ni gule binti kumbe siyo" aljiubu Kris...

"Lau pika supu ya maana tule, pia ili huyu mgeni apate nguvu ajitambulishe tumjue vizuri" alisema Rama huku akimwangalia irene ambaye alijaa uoga chungu nzima!

Ukimya ulitawala sana, hakuna aliyesema zaidi ya vyombo kulalamika vilipogonganishwa na mpishi wa siku hiyo, supu iliiva vema na kuwekwa tayari ili watu wapate kula na kunywa!

"jamani karibu tuleni" alisema Lau huku akimkabidhi Irene bakuli la  Nyama.
Walikula,  Irene alionekana  akila kwa kasi kweli Kweli wote walikuwa kimya tu midomo ilifanya kazi ya kutafuna nyama na chapati.
"nikuongezeee? " alisema Lau huku akimwangalia Irene usoni, irene aliitikia kwa kutikisa tu kichwa kukubali kuongezewa,  bakuli lilijazwa akalimaliza tena, Lau akaomba kumuongezea ila safari hii Irene akakataa kuongezewa!

"binti usiogope kwanza pole sana,  tulikustua tusamehe sana" alisema Kris
"pia jisikie huru sisi tutakusaidia tunataka kujua wewe ni nani umekujaje huku na nini kimekusibu?  Aliongezea Rama!

Swali la Rama liliamsha kengele ya akili kichwani mwa  Irene na kumfanya akumbuke Aliyoyapitia siku ile huku akikumbuka akiwa anasali pale mtoni hadi anavyodondoka! Alama ya hatari iligonga kichwani alipokumbuka juu ya taarifa ya habari na jinsi watu wale walivyokuwa na hamu ya kujua muuaji ambaye ni yeye! Alikuwa amefahamu jina la mmoja Lau baada ya kusikia Rama akilitaja!

Irene aliamua kukaa kimya bila kujibu chochote kile, Rama aliamuru walale huku wakimpa Irene sehemu ya kulala, na wakigawana majukumu.
"kesho mie na Kris tutaenda kazini, Lau utabaki na huyu mgeni,  muuliza vizuri na umjue vema tukirudi tujue taarifa zake" alisema Rama huku akielekea sehehemu ya kulala...
Kila mmoja alielekea sehemu ya kulala, na Irene alilala pia,  wenyeji wake walilala na maramoja wakaanza kukoroma.

"Lau amka unisaidie nakuomba" niliongea kwa upole huku nikimtingasha pale alipokuwa amelala,  kiukweli nilibanwa na haja si mchezo,  sikujua pa kwenda ndani ya nyumba ile tulivu, ilikuwa usiku mno wote wakikoroma.

"Lau amka basi" nilimsihi na kwambali akaamuka na kufikicha macho yake na kuniangalia

"ehee sema dada"

"naomba unisaidie nijue choo ilipo"

"aahh Samahani sana tulisahau kukuonesha"

"bila Samahani" alisimama na kuanza kutembea kuelekea ndani ya vyumba na kunionesha mlango,  njee kwa mbali nilisikia wanyama wakiunguruma na wangine wakibweka kwa kufukuzana,  nilihisi kama tupo chini yaani kwenye handaki.

Nilifanya shughuli zangu na kurudi kulala,  nilipitiwa na usingizi mzito wenye ndoto nzuri kwani niliota nikiwa nimeonana na Franc, wakati nataka kumsalimia mara mtu akanizua, nilichukia na kustuka kuona Lau akiamsha nikabaki nimezubaa kwa aibu na soni usoni mwangu.
"kumekucha Dada amka" niliamka kiuvivu nikichukia kwanini anikatishe na ndoto yangu ile nzuri. Niliangalia na kuona bado taa zimewashwa

"mbona bado usiku,  taa zinawaka"

"noo kumekucha saa 2 asubuhi mda huu twende nje ukaone kwani jana ulikuwa hujitambui" niliinuka na kuanza kutembea hatimaye tulipanda ngazi na kutokea Nje juu ya kilima mwamba umetobolewa na kutengenezwa mlango,  Huwezi kujua kirahis kama utapita eneo hilo kuwa ndani kuna nyumba nzuri yenye kila kitu...

Tulikaa kwenye jiwe huku nikiangalia vilima na mabonde kwa mbali,  ukimya ulitawala, kisha nikaamua kuvunja ukimya kwa kumuuliza Lau maswali
"Lau jana nilisikia mkiongea habari ya binti muuaji ikoje hiyo Habari!?" kwanza alionekana kushangaa mimi kutaja jina leke

"Haa umejuaje jina langu!?  Pia siwezi kukuambia mpaka nijue wewe ni nani na huku umekuja kuja kufanya nini?"

"hicho tu? Na nikikwambia utaniambia ukweli? kuhusu jina lako nikisikia rafiki yako akilitaja"

"ahaa una kariri fasta,  ndiyo nitakuleza kila kitu"

"mimi naitwa Natasha Maureen, nilipotea huku baada ya kufukuzwa na fisi wakati nikiwa shambani na nakumbuka mara ya mwisho nimeona watu watatu na mlio mkubwa ndipo sikuelewa kilichoendelea!" niliamua kudanganya kwa ujasri.

"pole sana dada,   ndio maana umechubuka chubuka na kuumia,  Mungu mwema kakuokoa!  sasa upo kwenye mikono salama"
"Asante Sana, niambie kuhusu  Irene"

"ohh hausahau tu, ni historia ndefu sana"
"nisimulie hata kama itakuwa ya masaa 12"
"masaa 12 si watatukuta hata kupika sijapika,  enyiweyi sikiliza,  mimi naitwa Laurian Angelo Mkosi, nilizaliwa Kilolo,  huko Iringa vijijini,  nilikulia huko na kusoma mpaka kidato cha nne lakini sikufanikiwa kwenda mbele. Nilihangaika kutafta kazi sikupata ndio kuna jamaa akaniunganisha huku,  ninayokuambia ni siri itunze dada Natasha!  Shuleni  nilikuwa na rafiki yangu niliyempenda sana,  Tulisoma pamoja ila yeye alifaulu na kwenda kidato cha tano Hatimaye chuo. Aliitwa Franc Samuel kwa sasa ni marehemu, Mwenyezi Mungu mlaze pema!  Huyu rafiki yangu alisomea mambo ya maliasili chuoni hivyo akiwa mwaka wa mwisho alifanya tafiti (research) na kugundua jinsi gani viongozi wanazunguka nyuma ya pazia na kufisiri nyara za serikali, inasemekana baada ya kutolewa tu repot ile wengi waliogopa hivyo kuamua kutafuta mbinu ya kumuua.  Hata hivyo ilibainika kuwa kuna binti kwa jina Irene Paul alikuwa mpenzi wa karibu mno ambaye huenda alijua kila kitu juu ya kifo chake kwani hata siku aliyekufa alikuwa anaenda kuonana nae na  ndiye anayesadikika  Kufanya mauaji kulipa kisasi!!  Binafsi natamani kumfahamu binti ili niungane nae nilipe kisasi kwa wote waliohusika kuplan kifo cha Rafiki yangu franc kwa kumgonga na gari hasa nikimkumbuka mama yake kule kijijini!  Wasi wasi wao mkubwa ni kuogopa huyo binti asije kuripot kwenye usalama kwa kuwa wanafikiri anajua yote juu ya Franc na kifo chake ndiyo maana wanataka akikamatwa tu wamuue hima!!"
alimalizia Lau kwa ushujaa na hisia kali. Sasa  alikuwa amenihamisha na kurudisha jeraha la mapenzi yangu kwa Franc liloanza kupona,  nilikuwa nimejua kila kitu.

Niliwaza na kutafakari kwa kina mno nisijue cha kufanya,  nikahisi machozi yakinilenga ila nikajitahidi Lau asijue,  nilifikiri  cha kufanya Nisikione kwani  tayari nilishamdanganya jina Lau, nilifikiri kumwambia ila nikaogopa, hasira zilinipanda mimi Irene na kuona kulipa kisasi ndiyo suluhu pekee hasa nikimkumbuka Franc..... "lazima kisasi mateso yote haya, chuo nimekosa"niliwaza.

lakini pia niliwaza kama Lau atakuwa ananidanganya ili nikamatwe ingekuwaje, nilibaki njia panda juu ya nini niamue, nimwambie lau ukweli,  au nifiche tu...

je ataamua kujitambulisha?
ungelikuwa wewe ndiye Irene ungeamua nini?
Na ungekuwa wewe je Ungelipa kisasi?

Usikose episode ya 10...

No comments:

Audio