Monday, October 23, 2017

Saikolojia. Fahamu Makundi Manne Ya Tabia za Binadamu.

SAIKOLOJIA : PATA KUFAHAMU MAKUNDI MANNE YA TABIA ZA BINADAMU.
Wataalam wa mambo ya saikolojia na maumbile wamezisoma tabia mbalimbali za binadamu na hatimaye wamewagawanya binadamu katika makundi makuu manne yenye kategoria kuu mbili. Kategoria hizo ni

1. Introvant: watu wenye uwezo mkubwa kiakili na wanaotafakari mambo kwa kina
hapa kuna makundi mawili
1.Melancolin 2. Fragmetic

2.      Extrovants: wana uwezo wa kawaida kiakili na hawana tafakari za kina katika mambo yao
Hapa kuna makundi mawili
1. Sanguine 2. Colerick
Na sasa tuangalie tabia za kila kundi na mienendo yao


1.MELANCOLIN
Watu wa kundi hili (females and males) wana sifa zifuatazo
-wana uwezo mkubwa kiakili (high intelligence Quotient)
-ni wagunduzi wa mambo makubwa ya kisayansi
-wanamudu vizuri masomo ya sayansi na hesabu
-ni watu wenye pole pole na wasio na maneno mengi
-wana hisia kali za upendo na ni kundi linalosadikika kuwa na upendo wa dhati
-Wanawajali sana wenzao hasa wanapokuwa katika shida na matatizo(i.e ndio maana hawa huwa waombaji –wanamaombi wazuri sana kiimani)
-Wana huruma sana na hawapendi kuona wengine wakionewa
-Wanajitolea kwa haraka na kwa dhati katika mambo ya wengine
-Huondoa uchungu wao kwa machozi (wakiumizwa hulia haraka, hasa kwa upande wa wanawake/wasichana)
-Hawajiamini kwa mambo wanayoyafanya (hata wakiwa darasanu si wepesi wa kunyoosha vidole ili kujibu maswali)
-Wanahesabu kushindwa kuliko kufanikiwa (mfano akitaka kuanzisha duka; badala ya kuwaza itakuwaje nikipata faida wanawaza itakuwaje kama duka litaibiwa ama kuungua moto, kwa maswali hayo anajikuta hata anafikia katika uamuzi wa kuahirisha uanzishaji wa mradi huo)
-Wakata tamaa wanapokosolewa.
-Wanapenda sana kutiwa moyo kiuhalisia.
-Wanapenda kusoma, kusikiliza, na kusimulia mambo yenye tafakari na uchambuzi wa kina (hawapendi umbea)
-Wanapotoa mawaidha mahubiri ama ushauri wengi(wanaosikiliza) huwa wanaguswa nao na hubadilika haraka kutokana na mawaidha hayo ama ushauri ama mahubiri hayo
-Hawapendi kuvunja taratibu, sheria za eneo husika.
-Wanapenda usafi na mpangilio mzuri wa vitu vyao
-Ni wa vumilivu sana katika hali mbalimbali (mfano wanapoonewa ama kuumizwa)
-Hawapendi kufuatilia mambo ya wengine pasipo sababu za msingi.
-Ni kundi mojawapo linaloathiriwa sana na magonjwa ya mashinikizo kutokana na kuwa wanawaza sana
-Ni wagumu wa kusahau na hiyo imewasababishia kuwa wagumu wa kusamehe
-Wanaumia sana wanapokosea ama kushindwa jambo Fulani
-Wanajeruhika mioyo yao kirahisi (i.e wakiingiwa na pepo wabaya si rahisi kuwatoka kwa sababu ya kutunza uchungu kwa muda mrefu mioyono mwao)
-Wana busara na hekima nyingi
-Ni watu ambao wakiishika imani fulani wanajitahidi kuitimiliza sheria yote.
-Ni wepesi wa kutubia makosa yao na kutubu kwa ajili ya wengine.
-Wana aibu nyingi sana hasa kwa watu wasiowafahamu wala kuzoeana nao
-Ni kundi la watu wanoridhika haraka
-Masikini wengi kiuchumi duniani ni wa kutoka katika kundi hili kutokana na uoga wao wa kuanzisha mambo kwa kuhofia kushindwa
-Watoto wanaozaliwa katika kundi hili inasadikiwa ni wengi huwa na ndoto za kufanikiwa mapema lakini ni wachache mno ambao huweza kutimiliza ndoto zao kutoka na uoga wa kuanzilisha mambo mapya.
-Kundi linalopenda amani na utulivu
-Wanaogopa sana matatizo, vikwazo na changamoto
-Katika familia baba na mama wakiwa melancolin upo uwezekano mkubwa kwa watoto kuharibika maadili kwa sababu hawa melancolin si wepesi wa kuadhibu
-Mara nyingi hupenda kuonesha sura za tabasamu hata kama wapo katika matatizo makubwa
-Hawapendi kumueleza kila mtu mambo yao binafsi
-Ni kundi la watu wenye marafiki wachache
-Wakati mwingine hupenda kujikataa.
-Ni waaminifu na wasema ukweli
-Wanapenda kusaidia wengine kupita hata uwezo wao
-Ni waaminifu sana kwa mambo ya kawaida na yale ya kiimani
-Hawapendi kujionesha mbele ya macho ya watu
-Hawa hawafai kuwa viongozi (si wazuri sana) kwa sababu wanapenda kusikiliza na kutafakari kila wanachoshauriwa hivyo hujikuta kuwa wanayumba kimisimamo. (mfano kama mkurugenzi/mwenyekiti wa eneo Fulani akiwa ni melancolin yafaa sana msaidizi wake awe ni colerick
-kingine kinachowanyima sifa ya kuwa viongozi wazuri ni kutokuwa na uwezo wa kujieleza kwa kujenga hoja zenye ushawishi mkubwa [Musa wa biblia alikuwa ni mmoja ya watu wa kundi hili, alikuwa hajiamini, anakata tama mapema, mlalamishi, asiyeweza kujieleza, licha ya kupewa msaidizi na Mungu bado tabia zake zilimuathiri na akajikuta anakosa nchi ya ahadi-Kaanani]
-Wanauhesabu upendo wa dhati kutokana na mambo wanayofanyiwa na sio kuambiwa (wanafurahia sana vitendo kuliko maneno}
-Kwa upamnde wa wasichana inasemekana kuwa ndio ambao wanasumbuliwa zaidi na maumivu ya hedhi, na kujifungua
Mifano ya watu wa kundi hili: Musa (wa biblia) Yesu Kristo, Bob Marley, Celin Dion

2: FLAGMETIC
-Wana uwezo mkubwa kiakili baada ya melancolin
-Uwezo wao katika utendaji wa mambo inasemekana ni kati ya asilimia moja na sitini
-Ni mabingwa wa kuahirisha mambo (mfano kama akitaka kwenda kupalili shamba, akafika na kukuta kuwa majani ni -machache atabeba zake jembe na kurudi nyumbani hata kama ni msimu wa kupalilia)
-Wanapenda sana kupuuzia mambo ikiwa hawakuyaelewa ama kuyaona kwa macho yao wenyewe
-Hawapendi kukubali ama kusifia mafanikio ya wenzao
-Ni kundi la watu wabishi sana na ambao ni mahiri wa kujenga hoja kwa jambo wanalolitetea
-Katika ushindani hasa wa hoja huwa hawakubali kushindwa kirahisi (anaweza kusema mti ni gari akajenga hoja akazitetea na wote mkakubali hata kama ni kwa shingo upande)
-Mawakili majaji na mahakimu mahiri duniani ni wale wanaotoka katika kundi hili
-Ni watu wanaopenda kutafiti na kufuatilia mambo mbalimbali ndio maana maongezi yao mengi hatawaliwa na mifano na takwimu halisia
-Wanapenda kufuatilia mambo ya wengine pasipo hata msingi wowote (wanapenda sana ushushushu)
-Wapelelezi mahiri hutoka katika kundi hili
-Ni watu wasioumizwa kufanya makosa
-Hawapendi kuwaamini wenzao
-Ni wepesi wa kupokea lakini ni wagumu wa kutoa ama kujitolea kwa mambo mbalimbali
-Wanatafakari mambo kwa kina na kuyatolea uamuzi wa uhakika
-Mapenzi (love affairs) si kitu kinachowaumiza sana (kundi linaloongoza kwa kuwa single na ambalo ni rahisi kukubali talaka pale inapotokea migogoro katika ndoa zao)
-Wanasamehe haraka sana kwa sababu hawajali (they don’t care)
-Ni wagumu wa kuomba msamaha (i.e mara zote hutaka kuonekana kuwa wapo sahihi) ndio maana hupoteza nguvu za Mungu kirahisi (imani zao zikipoa huwa si rahisi sana kuamka)
-Ni wagumu wa kupokea mambo mapya hasa yahusuyo imani na sera, vile vile si rahisi kuachana na imani ama sera walizozipokea
-Si watu wanaojali muda na ratiba
-Ni rahisi kukatisha mahusiano ya aina yeyete pindi wanapogundua kusalitiwa ama kurubuniwa.
-Hawaogopi kumkosoa mtu ama kumuumbua hata kama ni hadharani
-Hawaumizwi na maneno ya watu dhidi yao
-Ni wasuluhishi wazuri wa migogoro ya kijamii na ya kimataifa na wenye ushawishi wa kina (i.e karama ya utele kwa neno la upatanisho ipo kwao)
-Ni kundi linalifanya mambo mengi lakini kwa ufanisi wa wastani
-Ni kundi la watu ambao sio wakereketwa wa masuala ya usafi na unadhifu (i.e kimavazi na kiutaratibu)
-Wakianzisha jambo huweza kuliachia njiani bila kulimaliza na wala wasiumizwe na kukwama huko
-Ni watu wasiopenda vurugu hasa demokrasia ya ushuluhishi wa hoja inapokwama
-Wapo tayari kusalimisha chochote walicho nacho ilimradi wabakie na amani (wanafahamika kama peace makers)
-Watu waliojaa dharau na ambao muda wote huona wao ni bora kuliko wengine katika mambo yote
-Hawapendi kuelekezwa na mara nyingi eidha huwadharau viongozi wao ama hutengeneza mitazamo na hoja za kupinga matendo, kujitolea na maagizo ya viongozi wao.
-Wanapenda kutekeleza maagizo wanayopewa uso kwa uso na sio yale ya jumuia
-Wakiwa viongozi huweza kujikuta wakichukiwa na watu hasa pale watakapoendekeza tabia yao ya kutojali haja na matakwa ya wale wanaowaongoza.

3.SANGUINE
-Wana uwezo wa kawaida kiakili (mara nyingine mdogo)
-Ni wacheshi sana
-Watu walio na maneno mengi na wasiopumzika kuongea
-Wanajisikia raha sana pale wanapokuwa wakiongea na watu wengine wakiwasikiliza
-Wanapenda kuanika mambo yao binafsi mbele ya wengine
-Waigizaji wa kuchekesha wengi ni wakutoka katika kundi hili
-Wanapenda sana kujisifu na kujikweza
-Wanapenda sana kusifiwa hata kwa mambo ambayo hayana uhalisia
-Wanataka sana kuonekana mbele ya watu kwa kila jambo wanalolifanya.
-Wanavipaji vingi vizuri lakini wanahitaji kusifiwa na kuhamasishwa ndipo huvionesha kwa uhakika
-Wana hisi za zima moto (i.e wanahamasika haraka na kusahau haraka. Ikitokea ajali huwa watu wa kwanza kujitokeza eneo la tukio na kuanza kutoa msaada; lakini akiondoka pale anasahau kila kitu na hata kama ametumwa akalete ambulance, anaweza kuanza kufanya shughuli zake nyingine)
-Muda wote wako nadhifu (ni wakereketwa wa masuala ya usafi na unadhifu)
-Wana kiherehere sana.
-Wagumu wa kuelewa na wepesi wa kusahau
-Ni vinyonga katika tabia zao (wanuwezo wa kuigiza tabia zisizo zao kiuhalisia na watu wasiowajua wasiwagundue kirahisi)
-Wanashawishika haraka sana kupokea mambo mapya lakini ni rahisi kuyaacha
-Wasichana wa kundi hili si rahisi kurubuniwa kimapenzi kwa silaha ya ushawishi wa maneno, kwa sababu na wao wana maneno mengi
-Ni kundi linaloathiriwa sana na love affairs (i.e wao ni multiple lovers-ni kawaida kumkuta sanguine akiwa na wapenzi zaidi ya mmoja: __inasemekana kutokana na maneno yao mengi na ufundi wa kuigiza hisia na tabia wavulana wanaume wa kundi hili huwanasa wasichana kirahisi bila kutumia mtaji mkubwa.)
-Wawapo kwenye jamii hukubalika sana hasa kutokana na ucheshi wao na ukarimu walio nao.
-Wanapenda sana kuwasaidia watu ingawa ni kwa kujionesha
-Ni wahamasishaji wakubwa na wenye ushawishi wenye kukubalika kirahisi
-Ni kundi la wainjilisti wanaoongoza kwa kurudisha kondoo wengi kwa Bwana (wengi wana karama za kuhubiri kwa mvuto na ushawishi wa pekee)
-Hawaumii wanapokosolewa, ama wanaposhindwa jambo
-Ni kundi la watu waoga sana (wanajiamini sana kwa maneno lakini kivitendo ni kunguru)
-Si watunzaji wazuri wa siri (waropokaji)
-Wanapenda kujaribu kila jambo linalokuja mbele yao
-Wanaamini kuwa wao ndio watu bora kuliko wengine
-Wanapenda sana kusimulia mambo ya wengine
-Hawana aibu hata mbele ya watu wasiowafahamu wala kuwazoea
-Wanaume wa kundi hili huamini kuwa walizaliwa kwa ajili ya kuwasaidia wanawake
-Ni wavivu wa kufanya kazi, wanapenda sana starehe na anasa na ndoto za kufanikiwa kwa miujiza huwa zimewatawala (wanapenda kuwaza jinsi ya kupata bahati nasibu, kuzawadiwa fedha na hata kuokota fedha ama madini)
-Ni watu wasiojua namna ya kupanga na kuimudu bajeti kwa ustadi)
-Ni watu wa mipango isiyoona mbali (wakurupukaji) (Ministers of emmergency affairs)
-Ni wazuri katika kusifia(i.e wanazikubali kazi za wengine kirahisi na kwa dhati)
-Kutokana na porojo zao hujipatia marafiki wengi na hivyo kuwa maarufu
-Wanapenda kusikiliza na kusoma vitu ambavyo havina uchambuzi wa kina.
Mfano ni Petro mtume wa Biblia: alipenda kujaribu kila kitu (alipomwona Yesu anatembea juu ya maji alitaka na yeye kufanya hivyo) alipenda kufahamu kila kitu (aliuliza habari za siku za mwisho) alipenda kujionesha kuwa ni jasiri (aliahidi kuteswa na Yesu), alikuwa ni muoga sana (alimkana Yesu mara tatu kwa kuhofia kuteswa na wayahudi), alikuwa ni mwinjilisti wa kutumainiwa (alihubiri siku ya Pentekoste), alikuwa ni mwepesi wa kukubali pindi anapokosolewa (alikiri makosa baada ya kuonywa na Paulo juu ya upotoshaji wake wa kuhubiri kuwa hakuna wokovu kwa wasiotahiriwa)


4. COLERICK
-Wana uwezo wa kawaida kiakili
-Ni wa wakali na wakaidi
-Hawana huruma wala unyenyekevu
-Watu wasiopenda kudharauliwa ama kuonewa
-Wanapenda kuwatawala wenzao muda wote
-Ni viongozi kwa asili ya kuzaliwa
-Wanawaza kufanikiwa pekee na wala sio kushindwa
-Watu wasiokata tamaa mapema
-Wanajiamini kupita kiasi
-Hawana uoga ni majasiri sana
-Hisia zao hasa za upendo, mapenzi hazionekani kwa uwazi(hidden emotions)
-Kundi la watu wenye nguvu nyingi
-Ni madikteta
-Hawapendi kabisa kupingwa wala kukosolewa
-Watu wa kulipiza visasi
-Watu wa vitendo kuliko maneno
-Ni waonevu, wanapenda dhuruma na ubabe
-Ni watu wakulazimisha mambo hata kama hayawezekani
-Huwa wanatumiwa sana kwa ajili ya kuzima ghasia, uasi ama kuanzisha jambo lenye upinzani eneo fulani
-Wanafaa sana kuwa viongozi kutokana na uhodari wao wa kuwaongoza watu kwa sera za ushawishi wenye mlengo -wa kiukandamizaji
-Hawajui kubembeleza
-Hawaongei wala kucheka ovyo
-Wanapotenda jambo huwa wanawaza namna ya kunufaika na hata kama akimsaidia mtu anawaza namna ya kurudishiwa hicho alichokitoa
-Ni kundi la watu matajiri sana duniani hasa kutokana na uimara wao katika kuthubutu kutenda mambo na hali zao za kutoogopa hasara
-Si watu wanaopenda suluhu na amani
-Unadhifu na usafi wao ni wa wastani
-Hawapendi starehe kwa wingi
-Ni watu wanaoweza kufurahia mazingira yenye dhiki na shida
-Siku zote huwa wanatafuta kufanya mambo ya kihistoria ili wakumbukwe hata baada ya kufariki
-Wanafurahia kushuhudia na kutazama hadithi, matukio na filamu zilizosheheni ukatili na za kutisha
-Mifano ya watu wa kundi hilo: Idd Amin, Hitler, etc

*SI TABIA ZOTE ZA KUNDI LAZIMA ZIANGUKIE SEHEMU MOJA
MAMBO MUHIMU UNAYOPASWA KUFAHAMU

-Kila mtu amezaliwa na tabia fulani zinazomfanya awe katika kundi fulani
-Huwezi kujibadilisha kundi
-Kujifahamu kundi lako kunakuwezesha kurekebisha madhaifu uliyonayo na kuimarisha mazuri uliyonayo. Pia inakusaidia kuwatambua watu wengine hivyo kuwa makini namna ya kuishi nao
-Inawezekana kabisa kujifahamu upo kundi gani na pia kwa kusoma na kutazama ni rahisi kutambua makundi ya wengine

*NITATAMBUAJE MIMI NI WA KUNDI GANI
?
-Watu wengi wana tabia za makundi zaidi ya moja
-Kwa wale tabia zaidi ya asilimia themenini kutoka kundi fulani hao wanaitwa pure (i.e pure sanguine etc)
-Kama una tabia kutoka kundi zaidi ya moja, unaunganisha majina ya makundi mawili yenye tabia nyingi zaidi, unaanza jina la lile lenye asilimia nyingi zaidi
**Mfano: flag-coleick; cole-flagmetic, flag-colerick , sangu-melancolic, melanco-sanguine: etc

KUJIFAHAMU NI HEKIMA

No comments:

Audio