>>>>>>STORY: STAMSAHAU FRANC
>>>>>MTUNZI: Franco Samuel-0768800687
Episode #7
Ilipoishia Episode ya 6………
Sikujibu, niliacha kula na kuanza kutoka ili nikimbie, nilijua kashanifahamu, ila nilipofika getini sikuweza kufungua, na alikuwa akija kwa spidi kali mnooo…masiniki mimi sikujua nitatokaje na pale palikuwa wapi…………….
Songa nayo kwa raha zako...
Mzee alikuwa anakuja kwa spidi sana, sikuweza kufungua geti kwakuwa nilikuwa mgeni. Maisha yangu yalikuwa yameingia katika mtihani mwingine mgumu zaidi. Mama alikuwa ameniambia basi kesho ningerudi kwetu Dar, ndoto iliyeyuka na kuzimika gafla kama mshumaa kwenye upepo mkali na kiza kinene cha kutisha. Nilijaribu kufungua geti ila ikashindikana na cha ajabu sasa mzee alichomoa bastola.
Mke wake alimsihi asinipige risasi mzee alionekana kupuuza huku akizidi kunikaribia na nikiwa katika tahamaki na taharuki ile mara kijana wa Yule baba akamkamata baba yake na kuanza kumnyang’anya ile bastola. Nilipata ahueni kuwa kumbe Mungu alituma mtetetzi wangu kwa kipindi kile, nilijaribu kukwea uzio ili niruke ila ulikuwa mrefu na juu ya uzio kulikuwa na chupa zilizochongoka sana.
Nilibaki nimesimama huku nikitetetemeka machozi yakinitoka sana pia kamasi zilinitoka bila kupenda , mama Yule aliniangali kwa huruma na wakati huo baba na kijana waligeuka kupigana, kijana alipigana kwaajili yangu. Niliumia kwa kuwa ni mimi nimesababisha ndugu wanapigana. Mama alikuja pale getini na kufungua geti na haraka haraka nikatoka nje akanishika mkono nilijaribu kuukwepa ila akaung’ang’ania na kunipa kitu Fulani. Nilipopokea akaniachia na kuanza kukimbia, niliendelea kukimbia ovyo ovyo bila kujua kule kulikuwa wapi na wapi nilikuwa naelekea, niliona tofauti kubwa kati ya Jiji la Dar na Iringa, kwani magari yalikuwa machache sana, na watu wachache walionekana wakitembea wakirudi makwao.
Nilizidi kukimbia mwili wote ukawa unatoa jasho na nikawa nimechoka sana. Nilienda kando ya barabara na kuanza kutembea polepole na mbele yangu kulikuwa na dada mmoja na kaka wameongozana kwa haraka nilijua ni wapenzi. Niliamua kuwa simimisha na kuwauliza pale ni wapi wakajibu kuwa ni Kihesa kisha nikamuuliza stendi kuu wapi akaniambia ninyooshe na barabara. Nilishukuru na niakaangalia ni nini hasa Yule mama alinipa kipindi kile naondoka. Nilifurahi kwani alikuwa amenipa hela shilingi 30,000/= nilimshukuru na kumuombea Salama huko alilko na nikamuomba Mungu awajalie wepesi ili wasiendelee kugombana kwaajili yangu.
Nilitembea kidogo ikaja daladala nikapanda na tukaendelea na safari ya kuja mjini. Nilikuwa nimekaa dirishani siti ya mwisho kabisa, na nilibahatika kukiona tena kihenge cha Mkoa wa Iringa. Hofu ilitanda mno na nikaanza kuogopa nikikumbuka yaliyonikuta kule Gangilonga.
Kidogo tu gari lilisimamishwa, nilichungulia nje na kuona askari wa barabarani wakiwa pale nje. Mmoja aliingia ndani na kusema kuna mtu wanamtafuta ni binti, amefanya mauaji na muda si mrefu ametoroka alikuwa anataka kufanya mauaji mengine Kihesa. Moyo wangu ulidunda gafla na kijasho kikajaa mwili na askari Yule akaendelea kusema kuwa abiria wote washuke chini ili waweze kukagua kama muuaji yupo mle ndani….
Nilifikiri niruke kupitia dirisha la daladala ila lilikuwa dogo. Tayari abiria walikuwa wakishuka, kwa haraka nikafiiri na kuamua kuvua khanga na kujifunika uso kama dada wa kiislamu. Nilijikaza na kusimama kushuka ila nikajiuliza kama watahoji kwanini si hijabu ingekuwaje? Kwa haraka nikajijibu kuwa kama nitatua chini wakanistukia basi natimua mbio, ila nikawaza je wakinipiga risasi? Sikupata majibu ya haraka kwa wakati ule..
“we dada shuka haraka washangaa nini?”
ali amrisha askari kisha nikashuka. Walianza kumulika usoni kwa tochi kali mmoja baada ya mwingine. Pembeni nilimuona mzee mmoja nikachunguza vizuri kisha nikagundua kuwa ni Yule baba ninayemkimbia toka kihesa. Sasa nilikuwa natetemeka tu. Miguu yangu ilikuwa haina ushirikianao kabisa, nilitembea polepole huku nikitetemeka na kumulikwa usoni, na Yule baba alikuwa akinisogelea!
Aliniangalia nikakaza macho, askari akaniruhusu niende. Niliondoka kupanda gari ila nikahisi kuna mtu ananifuata kwa nyuma, nguo yangu ilivutwa na nilipogeuka nilishangaa kuona ni Yule baba. Sijui nilipata wapi ujasri wa kukasirika…
“we baba vipi unanizalilisha! Unanishika mimi ni mkeo? Hebu niache niende zangu!”
kwa maneno yale mzee aliogopa na kuniacha, gari likaondoka na tukafika stendi nikashuka ila sikuwa na pakulala. Kwa kuwa niliogopa hata sikuona haja ya kuomba msaada. Nililala banda la kusubiria abiria, huku mbu wakifaidi damu yangu na kelele zao kuwa ndio wimbo wa kunibembeleza. Hii yote kwaajili ya Franc niliyempenda sana, asijue kuwa nampenda…
Niliamka asubuhi nikiwa nimechoka, na nikiwa sina raha. Nilichukua pesa kidogo na kununua hijab kisha nikaivaa nikawa kama binti wa kiislamu. Sasa haikuwa rahisi kwa mtu kunifahamu na hata nilipotembea niliinamia chini.
Niliamua kukata tiketi ya basi na nikaondoka, pembeni yangu alikuwa amekaa mzee akisoma gazeti. Nilibahatika kuona kichwa cha habari
“MAUAJI YA KUTISHA YAFANYIKA IRINGA.
Muuaji ni binti mdogo, anasakwa na polisi.
Yasadikika alienda kutekeleza mauaji mengine Kihesa
Polisi wadai muuaji ni zaidi ya Ninja!”
Muuaji ni binti mdogo, anasakwa na polisi.
Yasadikika alienda kutekeleza mauaji mengine Kihesa
Polisi wadai muuaji ni zaidi ya Ninja!”
Nilistuka kwani pia picha zangu zilikuwepo nyingi zikiwa zimepamba ukrasa wa mbele wa gazeti lile. Niliogopa na kuzidi kuficha uso wangu Na muda mwigi niliinamia chini..
Gari lilitembea na Hatimaye tulikuwa Morogoro. Tulifika sehemu na kusimama, watu wengine walishuka kununua vitu vya kudakua, Sikuona hata raha ya kula chochote, niliomba tufike salama. Tukiwa bado pale nilimuuliza mtu mmoja kwenye lile gari na akaniambia ni stendi ya msavu ila hana uhakika, sikupenda sana kuendelea kuuliza kwa kuwa niliogopa!! Sio muda kuna askari walikuja na kudai kuna mtu wanamtafuta hivyo abiria wote waingie kwenye basi. Abiria walitii amri wakaingia wote, moyo wangu ulijawa na wasiwasi mwingi mno.
"yaani nimefika huku kote nataka kukamatwa tena"
Nilijiona mwenye mkosi mno, askari walisema wanamtafta binti anaitwa Irene Paul inasadikika kapanda gari za asubuhi za kwenda Dar. Iliniuma nilijua nmeshakwisha kwani tiketi niliiandikisha jina hilo hilo Irene Paul...
"Hivi kwanini nimekuwa mjinga hivi, kwanini skubadili jina? Kweli mie mjinga" niliwaza. Walitangaza Irene Paul ajitokeze sikwenda, wakaanza kukagua tiketi moja baada ya nyingine!!
Zilibaki siti tatu wanikute, nilihisi haja ndogo ikiachia bila break, walikuwa wakitishia iwapo watampata na hakujitokeza basi wangemfanyia kitu kibaya, nilikosa uvumilivu kwa woga nikafikiri nijitokeze. Kuna roho ikanambia jikaze, sauti mbili ziliendelea kuoingana ndani ya kichwa changau... Nilikosa maamuzi kabisa........... .
Itaendelea
usikose episode ya 8
nini kilimkuta binti Irene?
nini kilimkuta binti Irene?
maoni yako muhimu
Pia usisahau kushare na kuinvite friends wasome story hii na zingine zinakujia....
2 comments:
Welcome for your comment
Thanks a lot mate wangu My God bless you
Post a Comment