Mwanamke ukiwa na Sifa hizi ni rahsi sana Kuachwa...
Kulingana na utafiti wa kisaikolojia na masuala ya mahusiano, wataalamu wanatanabahi kuwa kama mwanamke utakuwa na sifa hizi ni rahsi mno kuachika. Hii inatokana na mapendeleo ya wanaume wengi kupenda mwanammke wa sifa fulani. Sifa zinachukiwa na wanaume wengi ni hizi zifuatazo..
1. Matumizi mabaya ya Fedha. Moja ya eneo ambalo mwanamke anatakiwa kuwa vizuri sana ni matumizi ya fedha yaani bajeti. Unaweza kupewa pesa nyingi kama mtego. Mwnaume anakuwa anakuchunguza aone unatumiaje na kwa muda gani. Mwananaume hupenda mwanamke mwenye kupangilia bajeti nzuri na asiwe wa matumizi makubwa. Unapewa milioni moja unarudi hakuna hata ulichonunua cha maana..
2. Wivu uliopitiliza. Mwanaume hupenda uhuru. Hata kama amekuoa hapendi umchunge sana na kuwa na wivu uliopindukia kiasi cha kumchunga kama mtoto mdogo. Japo wivu ni kiashiria cha upendo ila ukizidi huwa ni kero mno kwa wanaume. Fanya kila kitu kiwe mid...
3. Urembo na kujipamba kupitiliza. Japo urembo na kujipamba humvutia mwananaume ila kujipamba na kuwa kama mwanasesere sio poa. Yaani kucha za bandia ndefu kma jini makata. Umejipamba hadi unakuwa mbaya tena huvutii. Kujpanda sana ni kiashiria cha uvuvi hasa kutumia muda mwingi kwenye kioo..
4. Hutulii yani kiguu na njia. Mara upo kwa Mary, upo kwa Beny upo kwa Binamu kaka wa Kigamboni. Hapa mwananaume anakuwa na wasiwasi na wewe. Mwanamke tulia kidogo usiwe mtembezi sana kama kuku wa kienyeji...
5. Maneno mengi, yaani muongeaji sana. Mwnamke unaongea utafikiri umemeza loud speaker. Hupumziki maneno mengi hadi unapitisha kiwango, mwanamke anatakiwa kuwa mtulivu... Muongeaji wa wastani tena kwa sauti ya kike ile ya kubembeleza!
6. Vsingizio vingi kila mara. Unaambiwa njoo huku mara umesingizia hili. Mumeo anataka miezi sasa, wewe umegeukia huko. Visingizo visivyo na maana. Wewe ni mchumba wa mtu anakuita mwende hata out kila siku zikifika ksingizio mara kiatu kimekatika umesahau jana kakununulia...
7 Unataka kumwongoza mwanaume. Mwnaume hupenda mwanamke submissive anayejishusha no matter how. Sasa wewe unataka kumpanda kichwani na kumuongoza! Lazima ndoa yako au mahusiano yako yaende mrama. Elekeza mwananaume kwa hekima sio kumpanda kichwani ili umuongoze..
8. Una tabia za luba kuganda sana. Uhuru ni kitu chema. Kumganda sana mwanaume huchukulia km mateso fulani kwake. Km humpi uhuru na unamganda sana kufikia hatua ya yeye kutojisikia vema basi jua unaweka rehani penzi lako..
9. Unasifia boyfriend aliyepita. Kosa kubwa sana hili. Hata km mwananaume uliyenaye yukoje ni kosa la jinai kumwaga sera na sifa za boyfriends zako waliopita. Kufanya hivyo ni kumfanya ajione dhaifu na njia pekee atakayo tumia ni kuachana....
10. Mashoga chungu mzima tena wasio na maana. Hakuna binadamu asiye na marafiki ila aina ipi ya marafiki ulionao ndio swali la msingi... Miluzi mingi humpoteza mbwa uwanja wa vita ndivyo ilivyo kwa mwanamke mwenye marafiki wengi wasio na msingi kwani humo wapo watakao kushauri vibaya na kukupoteza kabisa. Kuwa na limit ya marafiki na chagua walio bora ili uishi kwa furaha...
11. Hujishushi, kujishusha ni kuacha jambo lipite kukiwa na mgongano. Baadhi ya wanawake wa kileo hata ukiongea naye hasikilizi aelewe bali anasikiliza akujibu. Ikiwa wewe ni jeuri na hutaki kushindwa yaani hushuki kila mgogoro mdogo ukitokea wewe unapanda juu tu. Basi tambua na elewa tu kwa hakuna mwananaume ataye ishi na chama cha upinzani ndani.. Mwanamke staha....
....maoni yako Muhimu...
Like
Share...
Franco Samuel
Like
Share...
Franco Samuel
No comments:
Post a Comment