Thursday, October 19, 2017

Ushauri Bora kabisa...

 Soma hapa ujifunze dada na kaka yangu, madhara ya sogezena tuishi....


"Tulikaa wote kwa miaka miwili.  Hakuna cha ndugu aliyejua nakaa na mwanaume!  Nadhani umbali toka kwetu na wazazi walipo pia ilifanya tuwe hivi kwani wazazi wangu walikuwa  kijijini.  Nilimpenda sana na kumwamini. Mwaka wa pili nilipata ujauzito. Hakunielewa kabisa. Mbaya zaidi aliniacha pekee nikiteseka!  Niliwaeleza wazazi wangu waliumia sana! Sasa hivi sijui yuko wapi! Wasichana wenzangu sio vizuri kabisa. Saizi nalea mtoto na wazazi wangu kwa shida." shuhuda toka kwa binti...


Mahusiano yamekuwa magumu sana katika kizazi hiki cha sasa kutokana na mifumo iliyopo.   kukuta watu wakikaa kama mume na mke bila hata wazazi kujua! Lakini swali la msingi ni hili nani alaumiwe mzazi au sisi vijana?

Je itakuwaje umekaa na mtu mara akaumwa kazidiwa sana pengine hadi Kuukata kama mnavyoita kwa lugha ya kileo?  Fikiri utampeleka wapi au utaeleza nini? 

Kuna madhara makubwa sana ya kuchukuana na kukaa na Mwanaume au mwanamke  bila kukuoa,  kutoa mahari wala wazazi wenu kujua.   Kufanya hivyo ni kinyume na maadili pia hata vutabu vitakatifu vinazuia.

Waathrika Wakubwa zaidi wa sogezena tuishi huwa ni wanawake kwanini?


  • Kwanza kabisa kuna ishu ya mimba.  Unaweza kuta wamekaa wote ila mwanamke akabeba mimba jamaa anamkataa! Huo ndio unakuwa mwisho wa kukaa

  •  Kwa kufanya hivyo mwanamke unajishushia thamani. Imekuwa kawaida kwa vijana wa kileo kuishi maisha ya sogezena tuishi, sasa akikuacha na umekaa naye miaka kadhaa siyo rahisi kupata mtu mwingine wa kujenga nae future.  Mwananaume huwa na kigugumzi kuwa na mtu aliyedumu na mtu kwa miaka kadhaa.  Hujiuliza mwenzangu alishindwa nini? 

  • Swali liko hapa je atakuoa?   Siku zote  mwanaume huwa sio mtu wa hasara sana linapokuja suala la kuoa kwa kuwa kwake age is not a matter!  Kwa mwanamke age is everything. Unavyozidi kuchelewa mmewekana ndani ndio na chance zinapungua km nia ni kuolewa baadae!    

  • Jitahidi kufikri mara mbili tatu kabla hujaikubali sogea tuishi kwani kunamengi yanaweza kutokea ikiwemo mimba,  ugonjwa na kupotezeana muda...

Kwa upande wa mwanaume...
Duniani mwananaume ameumbwa kama flexible na anaweza kuoa hata akiwa na miaka mingi  pengine  49 tena anaoa kigori wa miaka 18. Tukiingia kwenye law of comperative advantage utakuta mwananaume ndiye mwenye unafuu asilimia 75 hata kama mahusiano yatavunjika...

Dada,  kaka kama anakupenda, ni vema mkatambulishana huko kwenu. Hata bila kwa kutoa posa tu. Au hata kuwaona ili siku tatizo likitokea uwe na pa kuanzia kusema... Kumbuka matatizo hayana hodi.  Hakuna mwenye mkataba na Mungu juu ya maisha yake...
Ichunge thamani yako
Fanya maamuzi sahihi sasa..

No comments:

Audio