STORY: STAMSAHAU FRANC
MTUNZI: Franco Samuel-0768800687
Episode #6.
Ilipoishia Episode 5………
Sasa askari Yule alitembea kwa madaha akinifuata nilipo huku akiwa kanigeuzia bastola yake ili anipige, nilijukuta naburuza matako ili kukwepa ila alizidi kunisogelea, sikuona msaada kwani kwa muda ule wote hakukuwa na mtu mle ndani zaidi yangu na yeye wengine wote walikuwa marehemu. Leo ndio mwisho wangu niliwaza na sasa alikuwa amenifikia kabisa, naam hatua tatu tu zilikuwa zimebakia….
Songa nayooooooooooooo…………………..…………
Nilihisi ndio mwisho wangu kwa kuliona jua siku hiyo na tayari nilijiburuza mpaka mwisho wa ukuta na hapakuwa na nafsi tena ya kuendelea kujificha kama wahenga wasemavyo mbio za sakafuni huishia ukingoni. Aliniangalia sana kwa hasira huku akishilia trigger vizuri tayari kwa kuachia risasi. Chumvi ilijaa mdomoni ila kimoyomoyo nilimuomba Mungu atende tena muujiza kama alivonisaidia, kwa ujasiri nikajikuta naropoka
“wewe dada, hunihurumii mtoto wa mwanamke mwenzio? Uliniuza nimepona bado tu wataka kuniua kwani nimekukosea nini mimi? Mbona nateseka sana juu yako? Tafadhali nisamehe niache nirudi kwetu niko pekee wazazi wananitegemea!”
nilijua kwa kusema vile atanisamehe na kunihurumia ila haikuwa hivo badala yake akajibu:
“wewe ni kiumbe wa ajabu sana, mpaka sasa nakuogopa kwani umeponaje katka jumba hili, najua muda si mrefu, polisi wataingia hapa na utakamatwa, huwezi kuikwepa kesi hii ya kuua watu wote hawa, na naelewa utasema mimi nimekuuza hivo ili kujilinda lazima nikuue tu!”
Alimaliza kuongea nikawa natetemeka mara ghafla simu yake ikaita, alipoichukua tu niliitumia nafasi hiyo vizuri kwa kuchukua sturi iliyokuwa karibu na kumarushia ikampata kichwani na akadondosha ile bastola, niliruka haraka na kuiokota na kuielekezea kichwani kwa Yule askari huku nikisema anipe simu bila shuruti alikuabali kisha nikaibamiza simu yake chini.
Nikiwa bado nimemsonta kwa bastola nikaanza kutoka huku nikisema ole asubutu kunifuata. Sikujua mtoto wa kike anilipata wapi ujasiri kama ule, sasa nilikuwa nimetoka na kumfungia mle ndani askari mzima aliniogopa.
Mtihani uliokuwa umebakia ilikuwa namna ya kutoka katika lile jumba, niltembea huku na kule huku nikiwa nimeshikilia bastola, nilicheki upande wa barabara na kuona kuna gari linakuja ila sikuona sehemu ya kutokea, haukuwa na lift wala ngazi za kushukia chini. Nilishangaa sana ghorofa lile, nilifikri kidogo na kuamua kuchukua kamba iliyokuwa inatumika kuanikia nguo kisha nikaifunga kiunoni na kuifunga kwenye nguzo mojawapo ndani ya lile jingo, nikajiviringisha na kufumba macho kisha nikajirusha, nilitua chini na kuhisi maumivu makali sana ya mgongo, na mguu.
Nlifungua kamba haraka haraka na kuanza kutoka pale, na tayari gari la polisi liliuwa linafika, nilijibana seahemu na kuwaona wakishuka na bila hata kuchunguza wakaingia ndani ya lile jengo. Nilibahatika kuona ukuta wake, kuna sehemu Paliandikwa Freemanson Min Office, moyo ulidunda sana na niliona neema kubwa sanaa kupona katika jengo lile. Niliamua kutoka pale ili nikimbie ila ile natoka tu kumbe dereva alikuwa anafungua mlango wa gari, alimasura anione. Nilijibanza pale kisha akaingia ndani na hatimaye nilitembea kwa kunyata kupitia kwenye maua na kuburuta hadi kuikuta barabara. Kutokana na kuburuta nilikuwa nimechafuka sana na miguu ilikuwaimechubuka magotini, damu zikotoka.
Niltembea kufuata barabara ila nikipita pembezoni na kuanza kukata chochoro. Nilipita sehemu na kuona kihenge cha mkoa wa Iringa ila sikujua stendi ni wapi. Niliongoza kufuata barabara na watu walinishanga kwani nilionekana kama chizi, hakuna hata aliyenihurumia.
Nilifikri sana na nilihisi kiu, uzuri wangu ulipotea ndani ya muda mfupi , kutokana na kulawza muada mrefu nilikuwa nimesha chelewa chuo. Sikuwa hata na shilingi na kutokana na jua la mda ule kiu ilinitesa sana. Niliaamua kwenda niombe maji nyumba flani iliyokuwa karibu. Wote walinikimbia mama na watoto wakinicheka na kuniita chizi, niliumia sana mtu nina degree leo naitwa chizi kisa akiwa Franc, kwa hali ile niliamini hata Franc angefufuka basi asingenitamani kabisa!
Niliikuta round about kwenye clock tower na kuona garden watu wakiwa wanapumzika. Wengine walikuwa na wapenzi wao, nilihisi wivu kwani hakika bado penzi la Franc lilidumu ndani ya Moyo wangu. Niliingaia ndani ya ile garden na kulikuta bomba amabalo kwa haraka nilijua lilitumika kumwagilia maua ya pale. Nilkunywa yale maji bila hata kuogopa, nilipukuta nguo zangu na kuosha uso pia, watu walionekana kunishangaa tu, Iliniuma sana.
Nilitembea kufauta barabara ya kutokea pale garden. Mwendo wangu ulikuwa wa legelega na goigoi mno. Nilitokezea barabara ya soko kuu nikakumbuka siku ya kwanza nilivyoletwa na yule dada kuja kuthibitisha kama ailyekuwa kafariki ni Franc kweli, nilihisi kukosa hamu kabisa na kumbukumbu ya Franc akiwa Mochwari ndani ya kabati ikanijia, nikahisi kizunguzungu kikali kikivamia kichwa changu, macho yakakosa nguvu kabisa na giza totoro likatanda mbele ya upeo wangu!
Nilistuliwa na honi kali ya gari na kucheki nilikuwa kati kati ya barabara. Gari lililo nipigia honi lilikuwa ni defender ya polisi ile niliyokuwa nimeicha kule Gangilonga. Nilitoka ndani ya barabara upesi na defender ikapita kwa spidi kuelekea kule kilipo kituo kikuu cha Polisi cha Mkoa wa Iringa. Sasa akili ilikaa sawa nikahisi kuanza kutafutwa tena. Ilinibidi niende stendi haraka, ili kama nikifanikwa nipande gari na kwenda Dar. Ila sikuwa na hela hata sent moja, nilifika stendi na kwa jioni ile hakukuwa na gari kabisa, ilinibidi nizurule stend nikiwa sijui pa kulala wala pa kula.
Tayari ilkuwa jioni na watu walizidi kupungua pale stendi. Mabasi ya mikoani yalifika na kushusha abiria mengine yakiondoka na mengine kupaki pale. Pia abiria wengine walikuwa na wapenzi wao wakifutahi sana. Ile ilinipa wivu mno. Jioni iliingia kwa kasi mno na nikafikiri sana nini nifanye. Maamuzi yaliyonijia ni kwenda moja ya duka la karibu na stendi ambapo walikuwa wanafunga.
Katika duka lile alikuwepo mama na kaka mmoja, nikawa salimia. Walijibu kwa uchangamfu mno. Nilimuita mama pembeni na kumueleza kwa kudanganya kuwa nilikuwa nimeibiwa kila kitu hivyo nahitaji pa kulala na kesho niondoke. Aliniangalia na kusikitika sana! Muonekano wangu wa kuchoka ulimfanya akubali kunisaidia, nilimshukru sana! Nilijisemea kweli watu Iringa ni wema sana hasa Wahehe kama nilivyokuwa nikisikia. Tuliondoka kwa kupanda teksi ambayo kwa haraka niligundua ni ya yule mama kwani aliiendesha mwenyewe.
Tulifika kwao japo sikujua ni wapi kisha akanipa nguo alizo sema ni za watoto wake ambao wako shule. Nilipewa maji na kuoneshwa bafu ili nioge. Niliingia nikaoga na kuzifua nguo zangu kisha nikaitwa sebuleni kula kwani muda ulikuwa umeenda tayari.
Wakati tunakula TV iliwashwa ili tuangalie taarifa ya habari ya saa mbili za usiku Msomaji alinza kwa mbwebwe zote
“MAUAJI YA KUTISHA YATOKEA MKOANI IRINGA”
Huku picha mbalimbali zikipita na nikastuka saana baada ya kuona picha zangu tofauti tofauti na iliyoonekana vizuri ni ile nikiwa na bastola kipindi kile natoroka katika lile jengo. Wote tuliokuwa pale mezani tulibaki kuangalia luninga na baada ya muda wakaanza kuniangalia sana mimi. Baba yao alinikazia sana macho nilishusha uso wangu ila akazidi kukaza macho yake.
Taarifa ikasomwa vizuri huku wakisema
muuaji ni binti ambaye alifanikiwa kukimbia kabla ya polis kufika enoe la tukio na hivo zawdi nono itatolewa kwa atakayefanikiwa kukamatwa kwa muuaji.
muuaji ni binti ambaye alifanikiwa kukimbia kabla ya polis kufika enoe la tukio na hivo zawdi nono itatolewa kwa atakayefanikiwa kukamatwa kwa muuaji.
Baba aliniangalia na kisha nikashuhudia akiingiza mkono mfukoni na kuchua simu yake kisha akatoka nje. Nilisikia akipiga simu huku akisema yukoje na akarudi huku akiningalia sana…kiukweli nilishiba ghafla na sikuona tena ladha ya chakula, baba yule aliingia na kusema
“we binti unatokea wapi?
Sikujibu, niliacha kula na kuanza kutoka ili nikimbie, nilijua kashanifahamu, ila nilipofika getini sikuweza kufungua, na alikuwa akija kwa spidi kali mnooo…masiniki mimi sikujua nitatokaje. Sikujua pale nilipokaribishwa na mama mkarimu palikuwa wapi!
Nilibaki getini nikiwa nimeduwaa tu...………….
Nilibaki getini nikiwa nimeduwaa tu...………….
Itaendelea….
Je ataurudi tena mikkoni mwa polisi?
Na kama ni hapana nani atamsaidia?
Usikose sehemu ya 7
No comments:
Post a Comment