Tuesday, October 17, 2017

Maamuzi katika Mahusiano

Maada ya leo: Siri ya Mahusiano na Maamuzi ya mambo..

na Franco Samuel

Picha kwa hisani ya mtandao Fb


Kuna watu wanashindwa kuelewa kuwa mahusiano ni makubaliano baina  ya watu wawili. Lakini pia maamuzi ya mahusiano ni ya watu wawili. Mahusiano mara nyingi ya kaiafrika  yamevunjika kutokana na  kua taasisi yenye watu wengi wanaohusika katika uchaguzi na ushauri...
Kuna ndugu wa karibu kama wazazi,  shangazi, wajomba kaka na dada wanakuwa wana maamuzi makubwa sana kuhusu mahusiano ya sisi vijana. Wengine kupitia maamuzi yao yasiyo na tija wamesabababisha mahusiano yaliyokuwa na tija na muelekeo mzuri  kuvunjika na kuleta athari kubwa kwa wawili wapendanao. Wapo wengi wamekumbwa na kadhia hii.  Kuna wengine walipeleka wachumba kutambulisha ila ndg wakakataa kata kata kuwa hafai.  Hali hii huwa fedheheha na huumiza sna wahusika wote wawili.. Pengine na wewe uliwahi kuk0umbwa na kadhia hii nini uliamua?

Ijapo kuwa ushauri wa ndugu na wazazi ni muhimu ila maamuzi binafsi ya wapendanao ni muhimu zaidi. Kuna watu saa hizi wapo kwenywe wakati mgumu, umempenda mtu ila mama baba na ndugu hawataki hata kumuona... Hutakiwi kukata tamaa.  Kumbuka uko na akili ya maamuzi hivyo unaweza kuwa imara ukashikiria msimamo wako na ukawa nae kwa kuwa wewe ndiye utaishi naye...
Hakuna kitu kizuri kama kukaa na mtu unayempenda na mnapendana hata kama dunia nzima wanawachukia maisha yatakuwa mazuri tu. Ni wakati wako kijana kutafakari na kuona umuhimu wa maamuzi yako kuliko kusikiliza tu mzazi.
Hata kama  mzazi ana maono ya mbele juu ya maisha ila wewe ni muhimu kulinda mahusiano yako kwani hakuna kitu hata kimoja kilichowahi kuwa kizuri au kumpendeza kila mtu chini ya jua.  Hakuja wahi tokea mtu akapendwa na watu wote chini ya jua, haijawahi tokea, kumbuka nabii pia hakubaliki kwao wewe  nani utake kila kitu kiwe sawa? Tafakari fanya maamuzi yenye tija.. Hakika utafurahi hata kma watu wako against you decisions... Love is joy,
#wants_to_see_you_change_everyday
Franco Samuel

No comments:

Audio