Monday, October 16, 2017

SITAMSAHAU FRANC 5....

>>>>>>STORY: STAMSAHAU FRANC
>>>>>MTUNZI: Franco Samuel-0768800687
           Episode #5.
  


Tangazo.. Kupata mpangilio na mfululizo mzima wa stori hii na nyingine ya KISASI LAZIMA tembelea link hii hapa http://francosamuel.blogspot.com kisha bonyeza home chagua simulizi na utazipata zote kwa mtiririko mzuri kabisa bila kukosa kipande.....

 
Ilipoishia Episode ya 4………
Irene: kwani hapa wapi? Alafu we manaume unafanya nini kitandani kwangu? Nilijua ni Franc kumbe siyo”  mara akaanza kulia kwa sauti. Amando hakuwa na la kufanya zaidi ya kumpiga kofi Irene kwani ameshaharibu. Mlangoni james aliendelea kugonga na Amando hakujua cha kufanya, alijua sasa ndio mwisho wa maisha yake na binti Yule aliyemuokoa…James aliamua kuvunja mlango na kuingia ndani akiwa na bastola mkononi na kukutana uso kwa uso na Amando na binti ambaye James alihisi kama Alisha wahi kumona ila hamkumbuki vizuriii………………

Songa nayooooooo
Amando na Irene hawakuwa na chakufanya zaidi ya kuwa kimya kwani James alikuwa na gadhabu kubwa sana. Irene akaamka huku akitetemeka lakini Amando akamvuta na kumrudisha kitandani ile Irene  anatua tu risasi zilimiminwa kifuani mwa Amando na palepale akapoteza maisha. Irene alibaki haamini na akili yake sasa ilikaa vizuri kwa kuwa mara ya kwanza hakukumbuka yuko wapi akakumbuka jinsi alivofukiwa kwenye kaburi na kumuona Amando kama shujaa pekee aliyekubali kuokoa maisha yake, japo hakuelewa vizuri amekujaje tena duniani. 


James alisogea na kuanza kunikamata nilijitahidi kujiokoa ili nikimbie ila alikuwa na nguvu sana. Aliniburuza chini na kunipeleka sehemu ya juu ya lile jumba na kule niliona sehemu iliyotengenezwa kama bembea. Alinifunga kamba na kuniacha pale bila huruma na kulikuwa ndio kunakucha. Nilimshukuru Mungu kwani sikuamini kama niko salama kwa yaliyokuwa yamenitokea kwa muda ule wote. Nilitumia muda kidogo kumshukuru Mungu na kuomba neema zaidi ili niweze kupona jaribu lile, anga lilipambazuka na sasa nilianza kuuona mji wa Iringa. Sikuelewa pale pailikuwa wapi na nitatokaje ila kulikuwa kumetulia sana na nyumba zilionekana ziko vizuri sana maeneo yale.

Niliendelea kushangaa huku na kule na kubahatika kuona barabara.Pale barabarani magari kadhaa mazuri yalipita na Ilionyesha tofauti na barabara zingine ile haikuwa bize sana.  Kuna mtu alikuwaa akipita huku akiongea na simu na nilijaribu kusikiliza kwa makini  mno nikapata kusikia akisema yupo Gangilonga. “ahh kumbe huku ni Gangilonga? Nilikumbuka jinsi Marehemu Franc alivokuwa amenieleza enzi za uhai wake kuwa Ngangilonga ndio eneo lenye watu wenye peda kwa mkoa wa iringa. “kumbe wanapata pesa kwa njia kama hizi? Kweli Mungu awasamehe na kuniokoa mimi.” Niljisemea mimi Irene na nikiwa katika kusema hayo kwenye lile ghorofa dirishani niliona mtoto mdogo akinianagalia kwa huruma sana.
 
Nilimuangalia pia ila hakuonesha kuogopa alizidi kuniangalia tu. Nilibaiani alikuwa ni wakiume kwa jinsi ya muonekanao wake, hali nikiwa katika kuangalia mara James akaja na kundi la wenzake wengi mno wakiwa na silaha yaani bastola na mishale. James aliwaeleza wenzake kuwa nilikuwa nimefukiwa ila kwa usaliti wa Amando nikapona, japo amemuua Amando kwa mkono wake. Alisema sasa ilikuwa ni zamu yangu mimi kuuuawa na kuhakikisha kuwa safari hii siponi kabisa.


Waliweka vibao vya kulengea shabaha yaani target na kuanza kulenga shabaha, nilishangaa sana, walikuwa wako vizuri mno kwani hakuna hata mmoja aliyelenga pembeni, ila nilishanga zaidi kwani risasi za silaha zao hazikutoa kelele kabisa, nikakumbuka mafunzo ya jkt kuwa huenda ilikuwa wameweka sound proof yaani kitu cha kuzuia sauti ili hata wakipiga risassi  nyumba ya jirani wasisikie kabisa.
Walikoka moto na kuchemsha maji ya kutosha huku visu na masufuria vikiletwa wakisema lazima wanile nyama siku ile. Nilisali sana na kutubu dhambi zangu zote na kumuomba Muangu anaijalie  mwisho mwema ili niende kuungana na Franc Mpenzi wangu. James alinisogelea na kuniweka kwenye kitanzi huku akisema leo ndio mwisho, alinipiga lkofi na kunitemea mate yaliyonuka moshi wa sigara, niljisikia viabya sana, aliendelea kusema kuwa  akifyatua tu kiti basi lazima nife na kila mtu atapita kunizawadia risasi moja moja ya hadi nitakapokufa. Aliniambia niombe dua ya mwisho, nikafanya hivo kwa uchungu mkuu na kisha kiti kikafyatuliwa na nikaanza kuning’inia huku kamba ikikaba koo na kushindwa kupumua. Walijipanga tayari ili kunipiga risasi wakati huo kamba ilinizungusha huku na kule na kufanikiwa kumuona Yule mtoto niliyemuona dirishani akiniangalia huku machozi yakimtoka. Nilkuwa napumua kwa shida sana kiasi cha kuhisi kufa kabisa na mkojo ulinitiririka miguuni bila mbreak wote waliona wakacheka sana, sasa nilikata tamaa ya kuishi tena na niliona walimwengu wakiwa ni watu wa ajabu kabisa na wasio wa kuwaamini katika maisha.
James alihesabu moja mpaka tano na kuamuru wa kwanza apige risasi, nilifumba macho, kufumbua nikajikuta nimedondoka chini kwenye kile kitanzi na kushuhudia akina jeames na wenzake  wakainguka chini kama magunia kwa risasi zilizokuwa zikiwapata bila kumuona mpigaji. Niljikaza ili niinuke na mbele yangu alikuwa Yule mtoto nilyemuona dirishani akiwa na bunduki huku akiniangalia kwa huruma akiwa kalengwa na machozi machoni. Hakuongea kitu akanifungua kamba kwenye shingo, nilishiaka shingo na ilikuwa ikitoa damu, kamba ilikuwa imenikata.
Nilijaribu kuongea ili nimwambie asante ila ikashindikana sababu koo liliuma kweli kweli.  Alinitembeza hadi ndani na kunikanda kwa maji kisha kunipa uji na baadae chakula. Nilimuangali tu baada ya kushiba kisha nikaamua kuomba aniruhusu niondoke, alikataa akisema Yule askari wa kike aliyeniuza kaipata habari kuwa nilipona hivo ili kupoteza ushahidi bado ananitafta ili aniue kwani aliogopa mimi kwenda kushtaki. 

“masikini ananitaka tena. Istoshe simfahamu kabisa hivi kwanini mimi nateseka hivi siku  moja imekuwa na mateso zaidi ya mzee aliyeishi miaka 100! Inaniuma sana” 

nilijiseamea na kisha kumshukuru mtoto Yule aliyeonekana ana umri wa miaka kama 10.  

Nilipepesa macho pembeni na kuona gazeti kisha nikaliomba, alinipa na kulifungua nikakutana na habari iliyohusu kuopotea kwangu na  picha yangu ilikuwa pale niliumia sana  kwani nilijua wazazi wangu hawana furaha yeyote kwakuwa mimi ndio mtoto wao pekee. Nilitokwa machozi na kisha Yule mtoto akaniambia nisilie kwakuwa atanifikisha Dar kwa wazazi wangu bila wasiwasi, sikumuamini kabisa ila akanisihi nikakubali kumridhisha tu moyoni nikiwa sina hata asilimia moja ya kumuamini.  Alinisimualia juu ya yeye kuamua kuniokoa kuwa ni kutokana na baba yake kuwa na tabia za kutoa kafara ili utajiri wake uendelee kitu amabcho yeye toka apate akili hakukipenda hasa pale alipomtoa mama yeke mzazi, kaka yake na mdogo wake, alainiambia kuwa nilikuwa mtu wa kipekee kupona ndani ya jumba lile na  haijawahi kutokea kabisa, nilimshukuru na kidogo nilianza kumuamni, aliniambia anaitwa Frank na sasa nitakuwa dada yake kwani hakubakiwa na ndugu yeyeote isipokuwa mm amabye ameniokoa kwa wakti ule…..

Irene:  “ nini unaitwa nani?” nilistuka saana

Frank :“ Frank Albert Marc, Yule mzee uliyemjeruhi jana ni baba yangu na tayari kashapoteza maisha!”

Nilistuka kwa kuwa jina lilifanana na Franc Yule mpenzi aliyefanya yanikute yote haya, nilibaki nikimchunguza nikidhani labda atakuwa Franc Yule wa kwangu ila haukuwa mwenyewe, hali nikiwa katika kuchunguza mara mlango ukagongwa na sauti ya mwanamke nilyehisi kama namfahamu ilisikika ikibisha hodii, nilimuona Frank mwenyeji wangu akiogopa sana, sikuja ni nani ila woga ulinijaa ghafla mno.
Frank alichukua bastola na kunikabidhi ila sikujua namna ya kuitumia nilijaribu kukumbuka vile tulifundishwa jkt ila nikaona muundo wake  ni tofauti na SMG, SR, na LMG. Yeye aliniambia nijibanze ukutani na nishikilie silaha vizuri nilifanya hivo, kisha akanyata polepole kwenda kufungua mlango. 

Niliiona sura ya mgeni Yule alikua ni askari Yule aliniuza na kwa kudanganya kuwa alitaka kuniokoa, nilipatwa na hasira kubwa mno na kujikuta nafyatua risasi tatu mfulululzo zilizomapata Frank na akadondoka chini na kumuacha adui wangu akiwa hai, nilikamua trigger ila hakukuwa na risasi tena ndani, askari Yule aliniangalia kwa daharua na Frank alikuwa anakata roho, masikini nilikuwa nimeua tena, kwanini sikuzuia hasira zangu, nilikumbuka usemi wa wahenga hasira hasara, sasa askari Yule alitembea kwa madaha akinifuata nilipo huku akiwa kanigeuzia bastola yake ili anipige, nilijukuta naburuza matako ili kukwepa ila alizidi kunisogelea, sikuona msaada kwani kwa muda ule wote hakukuwa na mtu mle ndani zaidi yangu na yeye wengine wote walikuwa marehemu. Leo ndio mwisho wangu niliwaza na sasa alikuwa amenifikia kabisa, naam hatua tatu tu zilikuwa zimebakia…………………..………………


Usikose sehemu  Ya 6 ya SITAMSAHAU FRANC
UTABURUDIKA...... PIA NAKULETEA STORY MPYA INATWA
KISASI LAZIMA
Unasubili nini? Hujachelewa njoo http://francosamuel.blogspot.com

No comments:

Audio