Sunday, October 8, 2017

Mapenzi na Ushauri

+
Imani kubwa!

 Mwanamke ni jasiri sana! Anaweza kupewa mimba na aliyempa akamkata! Ataumia sana! Atateseka moyoni, bado wazazi na ndugu watamfukuza na kumwona hafai kabisa. Atakosa pa kukaa,  wengine hupewa hifadhi na marafiki!  Haitoshi kanisani atatengwa na kwenye kwaya ataonekana hafai.  Kwenye jumuiya ya vijana atatengwa! Anaishi kwa shida kukuosa mlo kamili,  bado anajpa moyo ipo siku yatakuwa sawa! 


 Bado baadhi ya marafiki zake watamponda, watamuona malaya,  marafiki wachache watabaki naye wakimfariji. Miezi tisa atasubiri hajakata tamaa,  leba ataingia. Faraja yake pekee ni mtoto wake kucheza tumboni.   Atajifungua kwa maumivu makali, tena wengine kwa opresheni. Bado kwa upendo atampa jina la ukoo babake na mtoto!  Furaha yake kubwa ni kuona mtoto wake mkononi akicheza.

Wakati mwingine huwa nawahurumia sana personally, ama kweli hakuna kama mama!  Wakati baba akila raha na vimada wengine yeye yuko biza mara auze nyanya mara mkaa ili mtoto aishi!  Huyo ndiye mwanamke ana imani kubwa hata akitengwa!   Wanawake hongereni Mungu mwema awape hitaji la moyo na kuwafanya muishi kuona na kufaidi matunda ya mateso yenu.

Mungu mwema awape baraka zote wanazostahili

 Inafaa ukashare kuonyesha ujasiri wa mwanamke

Franco Samuel

No comments:

Audio