Stori:::: SITAMSAHAU_FRANC
MTUNZI: Franco Samuel-0768800687
MTUNZI: Franco Samuel-0768800687
Episode ya 2
Ilipoishia episode namba 1
Ilipoishia episode namba 1
Niliamua kuchukua begi langu na kuondoka, tayari kurudi Dar kwani niliyemfuata alikuwa katangulia mbele ya haki. Wakati nakaribia na geti la pale mochwari mbele yangu kulikuwa na askari wawili wakiwa wamebeba karatasi Fulani na virungu na walikuwa wakitembea haraka sana. Mmoja alionekana kunikazia sana macho mpaka nikaogopa kisha akampa ishara mwenzake, naye akaniangalia na haraka walifungua lile karatasi na kuchukua kitu wakati huo sasa tulikaribiana kabisa kukutana.
Sasa endelea kuinjoyi.....
Afande mmoja akanisimamisha alinisimamisha, nilibabaika kidogo
Afande: "unafanya nini hapa? " alihoji kwa sauti ya kikali kidogo
Irene: "‘nilikuwa hapa kwenye msiba ule uliondoka” aliniangalia kisha akaniuliza
Afande: "unaitwa nani?"
Irene: “Naitwa Irene James”, wakati najibu afande alitikisa kichwa kisha akaongezea swali lingine, sikuwa na budi kujibu
Afande: "wewe ni mwenyeji wa wapi?"
Irene: "mimi kwetu Dar!”
Afande:“haa kwenu Dar vizuri!”
Kisha askari mwingine akachukua bahasha na kuifungua, alito picha na kuionesha, nilistuka sana, ilikuwa ni picha yangu niliokuwa nimemtumia Franc, na nguo ni zilezile nilizokuwa nimevaa, imechapishwa kwenye karatasi kubwa huku maneno "MOST WANTED" yakiwa juu ya picha ikifuatiwa na namba za simu kwa mawasiliano kwa yeyote atakayeniona. Askari alinaingalia sana na wakati huo pole pole nilihisi kabisa kukosa nguvu, afande akafungua kinywa chake na kusema kwa ukakamavu.
Afande: “Irene unakesi ya kujibu dhidi ya kifo cha Franc na kuanzia sasa upo chini ya ulinzi, hutakiwi kubisha na lolote utakalofanya litachukuliwa kama ushahidi mahakamani!”
Sasa nilikuwa nipo ktk hali nyingine kabisa, nilihisi haja ndogo ikija bila break, jasho jembamba lilinitoka mgongoni hata vidole pia vililowa. Afande alichukua pingu na kunifunga, sikuwa na la kufanya nililia sana hasa nikakumbuka kuwa nilidanganya nyumbani. Afande alichukua simu yake na kupiga na sio muda sauti ilijibu wakaongea huku nikisikia
“haloo mkuu tayari tumefanikisha kumpata mhusika kwani alikuwa hapahapa Iringa kwa hiyo tutakuja nae kituoni mda si mrefu”. Upande wa pili ulionesha kufurahi sana, afande alikata simu na kuninyang’anya kila kitu. Simu yangu pamoja na zawadi za kipenzi changu Franc zilichukuliwa, na sikuwa na njia yeyote ile ya kuwasiliana. Nilielewa kuwa nyumbani walijua mimi niko chuo nasoma kama nilivo tumwa na wazazi ila la hasha nilikuwa naingia Central Police Iringa kujibu shitaka la kuhusika na kifo cha Franc. Nilipelekwa pale kituoni na kuambiwa nahusika sana na kifo cha Franc, ila sitakiwi kueleza chochote ili kulinda upelelezi mpaka ndugu wa Franc wamalize msiba na ndio kesi itaanza rasimi. Nililia sana, nilimuomba Askari mmoja niliyemuona kama anahuruma minitarafu kwa muonekano wake anisaidie simu nimpigie mama. Hakika usimuamini mtu kwa muonekano Askari yule aliniitikia kwa kofi la kushoto lilionipeleka chini sakafuni na kujikuta nikibusu sakafu kisha kikafuata kizunguzungu kikalk mno, Japo nilijitahidi kukikabili ili niinue ila masikini wa Mungu mimi Irene nilishindwa na kuhisi kama ukungu machoni na Sikuelewa kilichoendelea kabisa.
*** *** ****** *** ****** *** ****** *** ****** *** ****** *** ****** *** ******
Nilikuja kustuka na kujikuta nipo na watu wenye mavazi meupe, nilihisi kama nipo mbinguni na malaika. Baada ya kupepesa macho huku na kule kwa shida nilianza kutambua mahali pale palikuwa hospitali kwani kuna watoto walikuwa wakilia, haikupita muda alikuja nesi na askari wa kike aliyevalia nguo za kiaskari nyeupe!
Nes: “pole sana Irene!” aliongea nesi kwa huruma mno nilibaki namwangalia tu. Nilimuangalia pia askari aliyekuwa pembeni yangu kwani alionesha kunihurumia pia.
Nesi: Irene unanifahamu’ sikujibu chochote kabisa kwani Sikuwa na uhakika kama namfahamu. Nilihisi ile sura haikuwa ngeni ndipo nikaanza kukumbuka siku ile nilipopigwa kofi na kisha kudondoka sakafuni, nikijitahidi kuinuka ila nikashindwa. Nilikumbuka japo sikujua ilikuwa ni lini na muda gani umepita nikiwa pale hosipitali.
"’atakuwa bado hayuko sawa’ alisema nesi na kisha kuondoka akiniacha mimi na askari wa kike ambaye nilihisi alikuwepo siku ile nikipigwa kofi na kupoteza fahamu. Nilimuangalia askari kwa huruma mno kisha akanisogelea na kuniuliza kulikoni. Nilimueleza kila kitu kilichotokea baina yangu hadi kupeleka kifo cha Franc, aliumia mno huku akiahidi kunisaidia.
“mdogo wangu nakuonea huruma sana, ila si kesi kwako kwani siyo wewe uliyemgonga so nikutoe wasiwasi kuwa utakuwa salama na mimi kama msichana mwenzako nipo tayari kukusaidia Irene’ sikujua namna ya kumshukuru ila tayari nilishapata ahueni kwa maneno yake. Aliongeana na mimi na kunambia akija daktari nisijibu chochote ili usiku anitoroshe niende kwetu. Nilikubali na kumuuliza kwani niko hospital siku ya ngapi, alijibu ni wiki ya pili sasa. Niliumia sana kwani tayari chuo kilikuwa kimeshafunguliwa na usaili ulikuwa unakaribia kuisha. Alinieleza pia kuwa mama wa Franc alikuja mpka nilipokuwa nimelazwa na aliniombea tu nipone kwani yote ni mipango ya Mungu. Kidogo nilifurahi na wakati nataka kuongea mara mlango ulifunguliwa, aliingia nesi na kuniuliza maswali ila sikujibu kama alivokuwa ameniambia askari. Nesi alimwambia askari
“bado akili yake haiko sawa kabisa, nilimungalia tu kisha akendelea kusema
“ afande muangalie maendeleo yake mimi mpaka kesho”. Nesi aliondoka zake.
Usiku wa manane baada ya kulala nilistuliwa na afande akaniambia niamke ili tuondoke, niliwaza sana nitaenda wapi, na itakuwaje? Je nikienda chuo si nitakamatwa vilevile? Wakati naduwaa na kuwaza afande alinistua tena na nilijaribu kuinuka kitandani ila sikuwa na nguvu kabisa, nilijitahidi nikaweza ila nilihisi maumivu makili ya kichwa upande wakulia.
Tulitoka na kutembea taratibu kama vile wagonjwa wanaoenda kupunga upepo. Getini tulikutana na kigingi kwani mlinzi hakutaka kuturuhusu kabisa, tulimwambia tuna punga upepo na afande akalegeza msimamo na akakubali. Tulitoka na kutembea hadi Mtaani ambapo niliona kibao kimeandikwa Uhindini, wakati huo askari alikwa akichati na simu nilihisi anachati na mpenzi wake kitu kilichofanya nimkumbuke Franc. Tukiendelea kutembea usiku ule tulivu, tulipishana na mbwa koko waliokuwa wakipigana na kubweka wakitafuta riziki zao za kila siku na hakukuwa na watu wala magari. Ukimya ulitanda mno nikaamua kumuuliza mwenyeji wangu ni wapi tunaelekea na alijibu
“nakupeleka kwetu ili nifanye mpango urudi dar!’ nilipata faraja na tumaini jipya kwani nilimuona askari yule kamu muokozi aliyetumwa na Mungu.
“nakupeleka kwetu ili nifanye mpango urudi dar!’ nilipata faraja na tumaini jipya kwani nilimuona askari yule kamu muokozi aliyetumwa na Mungu.
Tuliendelea kutembea na tukaikaribia njiapanda fulani, nikaona kwenye ukuta pameandikwa kitanzini, niliyasoma maandishi hayo kwa ugumu kutokana na mwanga hafufu eneo hilo. Tukiwa hapo njia panda ya kwenda Kitanzini mara walitokea wanaume wanne walioshiba vizuri sana. Miili yao iliyokuwa mirefu na kujaa misuli ilidhihirisha wazi kuwa walikuwa ni watu wa mazoezi makili, nikiwa katika kushangaa tahamaki wakanikamata na kunifunga mdomo ili nispige kelele. Nilijitahidi kujinasua ila sikuweza kabisa, walikuwa na nguvu mno sasa niliona kifo kipo karibu ila sikuogopa kwani nilijua naenda kuungana na Franc wangu.
Kwa muda mfupi niliamini watu ni wanafiki sana na wasaliti mno, nilijua hili kupitia yule askri aliyenisaliti, nilimsikia akuongea na wanaume huku akiwaambia ‘najua huyu atatufaa sana kwa ile kazi yetu, nimemtoa huko hospitali kwa kuwa hakuwa na wazazi wa kumsaidia na hana kesi sasa mchukueni na mkafanye kama kawaida mi malipo yangu niyakute kwenye akaunti” alionge askari Yule niliyedhani ni mwokozi wangu sasa aligeuka adui nilikumbuka usemi wa mwalimu wangu wa chuo aliokuwa akipenda kuutumia kila atufundishapo "Don’t trust anybody" yaani usimuamini mtu yeyeote yule. Askari Yule aliniangalia na kusema "Bye Irene sina jinsi nenda tu liwalo na liwe ila nisasamehe sana” nilitamani kuongea ila sikuweza kwakuwa nilifungwa mdomo. Walinibebaba juu kwa juu na kukatisha mitaa ambayo sikuijua na sikuelewa wananipeleka wapi na kufanya nini.
Niliendelea kusali kimoyo kimoyo kila aina ya sala iliyonijia niliiona iko sawa, zaidi niliomba kifo chema ili nikakutane na Franc mpenzi wangu. Hakika asingekuwa Franc haya yote yasingalinikuta niliumia sana na machozi yalinitoka bila hata kupenda macho na sura yangu vilitia huruma mno, sikijua wanaume wale walikuwa na moyo wa aina gani kwa mimi nisiye na kosa kabisa. Hatimye tulifika wakanishusha na kuniingiza katika jumba Fulani na kunilaza sakafuni, jumba lile lilikuwa kubwa na zuri sana kiasi kwamba sikujua tulipoingilia wala pa kutokea, ukatani kulikuwa na alama na michoro ya kutisha yakiwemo mafuvu ya vichwa vya biandamu na wanyama wa kutisha kama dubu na picha iliyonitisha ni ya kiunzi cha mtu ila kichwani kikitoa damu mbichi huku macho yakitoa damu na mdomo ukitoa moto, kiufupi palitisha. Pia kulikuwa na picha ya dragon anayetoa moto ikiambatana na kichwa cha mbuzi na pembe za kondoo mbili zilizochorwa kwa ustadi mkubwa. Vyote hivyo vilikuwa vimepakwa rangi nzuri mno na ya kumetameta iling'aa vema kabisa. Nikiwa napepesa macho na kushangazwa na maajabu ya jumba lile.
Mmoja wa wale wanaume aliondoka kwa kuwaaga wenzake akisema anenda kumwita boss. Mlango ulifunguka kisha akaja mwanaume wa makamo aliyeshiba vizuri. Alikuwa akitembea kimadaha na baadya ya kunifikia pale sakafuni nilipokuwa nimelala kwa dharua akaniangalia mno. Macho yake yalitisha na alionekana mwenye hasira sana. Baada ga kuniangalia na kuridhika alitikisa kichwa chake na kusema kwa jinsi nilivolegea siwezi kufaa kwa sadaka ya siku ile labda kesho. Wakati nikishusha pumzi kumshukuru Mungu kunipa nafasi ya kuishi tena, nilipigwa kofi moja kali sana, kofi hilo liliyumbisha kichwa changu na kukosa balance…
nilijikuta nikidondoka kama gunia kwenye sakafu…
Ndio kwanza tupo episode ya 2
Usikose episode ya 3 pata uhondo wote hapaaa...
No comments:
Post a Comment