Stori:: SITAMSAHAU FRANC
Mtunzi :: FRANCO SAMUEL
:: 0768800687
Episode no 8
Ilipoishia Episode ya 7....
"Hivi kwanini nimekuwa mjinga hivi, kwanini skubadili jina? Kweli mie mjinga" niliwaza. Walitangaza Irene Paul ajitokeze sikwenda, wakaanza kukagua tiketi moja baada ya nyingine!!
Zilibaki siti tatu wanikute, nilihisi haja ndogo ikiachia bila break, walikuwa wakitishia iwapo watampata na hakujitokeza basi wangemfanyia kitu kibaya, nilikosa uvumilivu kwa woga nikafikiri nijitokeze..Sauti moja ilinambia jitokeze ma sauti nyingine ikinanbia jikaze tu.........
Sasa songa nayo polepole....
Ukaguzi uliendelaea huku siti tatu zikibakia, nilianza kutetemeka na huku akili ikiniambaia nijitokeze tu lakini nikagundua nimechelewa. Askari wale walitisha sana na kufanya nione kifo kikiwa karibu kabisa..
Nilichukua ticket yangu iliyokuwa mfukoni mwa lile gauni langu la kiislamu huku mikono ikitetemeka mno. Kuishika tu tiket ililowa kwa jasho, askari alinifikia na kunipiga jicho kali mno, nilijikuta nikizidi kupoteza tumaini na ujasiri wa kutokamatwa.
"Wewe lete ticket acha kuzubaa kama kuku mwenye kideri" aling'aka afande kwa sauti ya ukali iliyopasua ngoma za masikio yangu huku kukiwa na harufu fulani ya kama sigara sijui ndio bange ama pombe hivi kifupi alitisha mno na macho yake mekunduku tanibihi ya majogoo yaliyopigana kwa muda mrefu.
Nilitoa tiket huku mkono ukitetemeka kwa woga na kisha nikavuta pumzi ndefu huku nikimuangalia askari yule usoni kwa kujiamni. Macho yake mekundu hayakunifanya nimuogope, ila nilijivika ujasiri kama Rambo kwenye movie yake ya Commando.
"unani tumbulia mimacho unaona nimefanana na bibi yako eet?" alisema askari yule ambaye kwa haraka nilibaini alikuwa ni mkorofi mno.
Nillikaa kimya akasoma tiketi kwa umakini mkubwaa...
"afande Irene Paul huyu hapa, amejikausha kama paka shume mtoto hatari sana huyu."
Maaskari wengine waliacha kukagua na kunisogolea huku mwingine akinikamata na kunyanyua msobemsobe juu kwa juu yaani utadhani nilikuwa na kilo mbili hivi kwa jinsi alivyoni ning'iniza kama pazi na jogoo.
"Acha kufanya hivyo mshikeni kwa adabu huyo ni binti"

Aliongea sheheikh mmoja aliyekuwa abiria kwenye lile basi na kusimama kuja kunitetea. Sasa niliona thamani ya hijab na kujistiri vema jinsi kunavyosaidia. Askari walimwangalia na kuanza kumpiga sheikh wa watu wakati huo mie niliteremshwa nje na askari wa kike aliyeonekana ana hasira kwani hata jicho lake tu lilioneehsa kiasi gani alikuwa amechukia hasa kutokana na sheikh kutaka kunitetea.
"yaani huyu Sheikh ni mjinga. Mjinga sana. Anafikiri matukio aliyofanya binti ni ya kitoto? Huyu zaidi ya Al Qaeda au sijui ni Mvietinamu" aliongea askari huku akiwangalia wenzake waliokuwa wakigawa dozi kwa Sheikh asiye na kosa kabisa.
Ndani ya basi waliendelea kupigana na nilishuhudia yule sheikh akiwapa kipigo cha maana na kumsukuma askari mmoja aliyendoka nje kama gunia la mkaa. Abiria walianza kupiga Makelele huku wengine wakimsaidia sheikh yule kuwapiga askari. Wakati huo nilikuwa nikitafuta namna ya kuweza kutoroka, lakini sikuona hata pa kukimbilia ukizingatia pale mahali bado palikuwa mjini.
Askri aliyekuwa nami kuona vile alianza kunikamata kwa nguvu ili anifunge pingu lakini abiria wakatoka nje na kufanya aogope kwani walikuwa wengi huku wakipiga Makelele hali iliyofanya watu wengine kutoka pale mjini wakusanyike kushuhudia nini kinaendelea eneo lile.
Niliangalia kwa umakini na nikaona upenyo na kisha kuanza kutimua mbio kuelekea mitaani. Nilikimbia mno bila kugeuka nyuma, Nilifurahi kwani nyuma sikusikia sauti za mwizi ama mhalifu. Nilijua kama sauti hizo zingeoigwa basi wananchi wenye hasira kali wangenikamata na kuniteketeza kabla sijafika popote. Kila nilipopiga hatua nilihisi viatu vikinichelewesha hivyo nikawa navivua huku nakimbia. Niliongoza uchochoro mmoja na kuafauta njia ambayo ilianza kuingia porini.
Nilizidi kuongeza spidi huku nikikatisha mashamba ya mahindi na miembe mingi. Sikuogopa chochote nilichotaka ni kukwepa mkono wa sheria kwani nilijua nikikamatwa tu basi llazima ningefia jela kwani watu walio kuwa wameuwa Iringa mjini huku mimi nikua wawili lazima ningefungwa tu na hakuna aliyejua zaidi yangu Mimi. Binafsi sikuua kwa kukusudia ni hasira tu za yaliyonikuta. Nikiwa nakimbia huku pumzi zikinibana nilijiona mumwagaji damu mkubwa na mikono yangu ilikuwa michafu kwa kufanya matukio kama yale. Hii yote sababu ya penzi. Penzi la Franc ambaye hata sikuongea nae neno moja. Kweli Mapenzi yana nguvu sana. Nilijisemea huku nikikaza hatua...
Pumzi ilikuwa ikinibana kila nilipokimbia na kuongeza hatua. Nilifika mahali nikahisi damu ikinuka puani kwa jinsi nilivyokimbia, nilichoka, jua lilikuwa kali mnooo kiu ilinikamata, mwili ulichoka hasa ukizingatia nilikuwa nimedhoofu mno kwa mateso niliyoyapitia toka niondoke Dar kumfuta Franc Iringa mjini.
Nilifika sehemu nikageuka nyuma sikuona mtu yeyote, kulikiwa na miti hapa na pale, na nyasi ndefu. Nilijiangalia na kuona nimechubuka chubuka usoni kwani niliposhika uso nilikutana na damu. Sikujali sana Pia hijab yangu ilikuwa imechanika chanika na kulowa damu hivyo nikaitupa palepale. Pia nguo zangu zilikuwa zimechanwa chanwa kwa miiba na miguu ilikuwa ikivuja tu damu.
"Kwa jinsi nilivyochoka sidhani kama Franc angefufuka leo angekubali kuendelea nami" nilijisemesha na nafsi yangu huku chozi la mahaba likinitoka.
"Franc anakupenda ulivyo Irene, hana tabia hizo yule ni mwanaume" sauti ingine ilinijibu na kufanya nione tumaini jipya kabisa.
Nilitembea pole pole na kuanza kuona wanyama kwa mbali niliona twiga wakila majani yaliyojuu ya miti.
"daa hii si mbuga kweli, nitatokaje humu, mimi si nitauliwa na wanyama" niliwaza sana kugundua kuwa nilikuwa kwenye mbuga ya wanyama. Niligeuka nyuma na kuona kwa mbali kundi la tembo. Uoga ulinizidi kwani niliambiwa kuwa tembo huweza kuhisi harufu ya mtu mita miatano. Nilizidi kukimbia ila nisijue naenda wapi na nitatokaje ndani ya mbuga ile.
Nilitembea umbali mrefu na kushuka kibonde fulani chenye ukijani kisha nikakutana na kimto, nilifakamia maji mpaka nikapaliwa. Nilikukunywa maji mengi nikahisi kile kimto kingekauka. Nilijiosha uso na miguu. Niliwashwa sana kutokana na michirizi na mikwaruzo ya miiba. Baada ya zoezi la kunawa nilitembea na kukaa pembeni palipokuwa na mti mzuri na upepo mwanana huku nikibembelezwa kwa sauti nzuri za ndege waliokuwa wakipumzika kwenye matawi ya mti ule wenye kivuli kimfaacho mwadamu.

Nilitafakari maisha yangu yote, nikatafakari Ukuu wa Mungu mwema kwa kunikirimia uzima. Nikakumbuka ndoto zangu za kuwa mwanasiasa, nikakumbuka Franc akiwa kwenye kabati kule mochwari niliumia sana kwani Franc niliyempenda ndiye kimekuwa chanzo cha mateso haya, nikisali na kumuombea Franc wangu alale pema huku nikimuomba Mungu anitoe katika mbuga ile salama kwani kulikuwa na wanyama wakail kama simba, chui, fisi faru na nyoka wakubwa.
Ningali katika hali ya kusali ni kama nilisikia kitu kikitembea nyuma yangu, mwili ulistuka mno nikahisi atakuwa fisi au chatu akinimvizia animeze, nilijaribu kugeuka ile nageuka nilikutana na bundiki 3 zikiwa zimeelekezwa upande wangu na watu watatu waliosimama wima sikuongea neno nilisikia tu mlio paaah!! Mwili ulikosa nguvu, macho yakipigwa ukungu nilijihisi mzito mno nikatua chini kama gunia sikujua chochote....
**************** ********* *****************
**************** ********* *****************
"Oya kwanini umepiga bwana Rama? " Ilikuwa sauti ya kiume ikisemakwa ukali
" Kris kama angekuwa adui je? "
"binti mdogo kama huyu hawezi kuwa na jeuri hiyo"
"hawezi, hawezi nani Kukudanganya wewe Lau? Angefikaje huku ndani kabisa ambako hata sisi ni nadra kufika? " alikazia Rama kwa ukali kidogo
"haya kwahiyo tunafanyaje?" Kris
"mwacheni hapo hapo" Rama
"hapana tumchunguze kama tukiweza tumchukue" Lau kwa huruma..
"umchukue uende nae wapi?" Rama
"kambini kwetu " Lau
"unamwaminije mtu huyu? " Rama
"Nyie tumchukue tu kama yu hai tutajua cha kufanya" Lau
Yalikuwa ni mabishano ya vijana ambao walikuwa ndani ya mbuga hiyo. Walikuwa katika harakati za kusaka mawindo na ndipo walipomuona binti akisali, Rama aliamua kupiga risasi hewani ili kumstua binti lakini wakajikuta wamefanya makosa kwani Irene alizimia kabisa. Kifupi wao ni wawindaji haramu na hawakuogopa kitu licha ya serikali kuweka sheria na ulinzi mkali.
"Lau beba huyu twende nae" Rama sasa alionekana kulainika, na akaichukua bunduki ya Lau ili aibebe.
"tuharakishe asije poteza maisha bila kujua yeye ni nani na anataka nini huku" bado Rama aliamrisha.
"ni kweli mkuu, twene fasta" alisema Kris
walitembea na kufika sehemu ya kambi yao ndani ya ule msitu na kuingia ndani.
Walijaribu kumwagia maji Irene ila hakustuka kabisa. Walichemsha maji na kumkanda lakini bado, Irene hakustuka. Walihangaika kwa muda muda mno, Lau ndiye aliyeonesha ubindamu zaidi kwani kuna dawa aliichukua akidai alipewa kipindi babu yake akiwa hai kuwa ikipuliziwa puani mwa aliyezimia basi angeamka lakini masikini binti Irene hakuamka.
"Oi mtu huyu ameshakufa, Tukamtupe huko nje" alisema Rama
"daa binti wa watu hata hatumjui kabisa" Kris alijibu
"tunamtupaje bila kaburi" Lau aliongea kwa sauti ya huzuni..
"wewe utachimba kaburi mpka saa ngapi" Alijibu Rama
"Ila huyu ni Binadamu jamani si mnyama" Lau bado alionesha ubinadamu..
"we beba katupe huko nje bwana tusikae na mikosi hapa, angalia leo hatujapata windo lolote na unataka huo mkosi ulale hapa?" Rama alisema akionesha kuanza kukasrika jioni ile
"mimi nilifikiri tubebe tupeleke kule kijiji cha karibu na kutelekeza mwili ili watu waokote wajue ni nani na wamwazike, hatujui kesho yetu na sisi." bado Lau alisisitiza
"muda huo haupo mimi kma mkuu wenu naamua katupe huo mzoga kule nje" Rama alionesha hasira yake.
LAU hakuwa na jinsi, aliunyanyua mwili wa Irene na kuanza kutoka nje kwenda kuutupa. Irene Paul Binadamu mwenye thamani aliyepitia mengi kisa likiwa ni penzi la Franc leo anatupwa bila huruma kama mbwa porini tena bila hata Wazazi na ndugu kujua chochote, inauma sana!! Lau alitembea pole pole huku Rama na Kris wakimuangalia, Lau aliendela kutembea huku mwili legevu wa Irene ukiwa begani pake. Akiwa kaubeba Lau alitafakari juu ya mwili wa Irene. Kama binadamu aliumia kwani kutupwa bila kaburi wala ndugu kujua ni ina uma mno.. Mwili ulikuwa begani mwake tayari kwenda kuutupa bila kaburi ....
Masikini binti Irene ndiyo anatupwa kama mnyama!...Dunia haina huruma, walimwengu wabaya ...uwiiii uwiii machozi yanitoka.. Kwaheri Irene....
Usikose episode ya 9....
No comments:
Post a Comment