Friday, October 13, 2017

SITAMSAHAU FRANK EPISODE #4

STORY: STAMSAHAU FRANC

MTUNZI: Franco Samuel-0768800687

           Episode #4.

Ilipoishia………
Nililia sana, nilimkumbuka mama yangu na baba yangu nikamkumbuka Franc amabye sasa ningeenda kuungana nae huko ahera, sasa nilikuwa nakosa hewa ya kupumua mbavu zilibana na jasho liliongezeka nilihema kwa nguvu na haja ndogo ikanitoka. Mauti ilikuwa inanijia na malaika mtoa roho alikuwa amefika, “jamani nakufa huku naona,  Franc nipokee nakuja mimi Irene Mpenzi wako nakupenda sana” nilijisemea…..
 Songa nayooooo…………
………………………………

Nililia kilio kikuu mno, sikuona tena muujiza mbele yangu,  mwili utota kwa jasho na kukosa hewa, sasa taabu ilizidi kila nilipojaribu kuvuta hewa ili nipumue, nilihisi macho yakilegea polepole na ukungu ulitanda mbele ya macho yangu masikio yalikuwa yakiunguruma kweli kaburi linatisha sana giza lilikuwa nene. Nilianza kuhisi kama usingizi mzito wenye ndoto za kutisha na moyo wangu ulidunda polepole mno kiasi cha kutoelewa nini kilichoendelea kabisa....                                     ****************************************************************************

James aliamrisha wenzake wamchukue Boss na kumpeleka chumba cha matibabu ndani ya jumba lile. Walifanya hivo na tayari madaktari special waliendelea kumtibu Boss wao kwa utulivu wa hali ya juu, walimuwekea mashine ya kunyoosha tumbo kwani alikuwa ameumizwa vibaya na hasa sehemu ya korodani. Pia walibaini ya kuwa kutokana na kuparuliwa macho jicho moja lilikuwa limeharibika vibaya hali iliyolazimua abadilishwe au litolewe ili awe na jicho moja. Waliingia stoo ila hakukuwa na sapea hivo ikabidi ang’olewe jicho na kubaki nalo moja. Hali hii ilimfanya James kuumia sana kwani hakika alimepnda sana Boss….

James:“Amando jiandae nenda ukamlete Yule askari hapa haiwezekani alete mtu kichaa sasa anataka kumuua boss wetu mtukufu, akipona boss lazima uuawe tu”  aliongea James kwa sauti ya ukali mnoo.

Amando: sawa mkuu naenda ila saizi bado usiku mkuu.

James: utaenda asubuhi. Nawapa ruhusa wote mwendeni mkapumzike mimi nabaki na boss na  nawasimamia madaktri ili wamtibu boss wetu vizuri!

“Sawa mkuu” walijibu Amando na wenzake kisha wakaondoka kuelekea vyumbani kwao kulala.

Amando wakati anaenda kulala aliwaza sana juu ya maisha yale magumu na ya kutisha anayoishi. Aliwaza atajibu nn kwa mola siku akifa, kuwaza kule kulitokana na picha ya binti Irene waliyemzika mzima mzima. Moyo ulimuuma na hatimaye akajikuta akisema
“naenda kumuokoa Yule binti bora nisaliti ila niokoe maisha yake nipo tayari kufa na Mungu nisamehe kwa yote. Ila nahishi atakuwa amesha kufa muda wote ule”. Alingalia saa ilikuwa saa kumi muda ule,
""Ahha kumbe muda haujaenda sana lazima nikamuokoe binti wa watu na nitaacha rasmi kazi hii hakuna haja ya kuishi kifahari wakati moyo wangu hauna amani kabisa”  

Alijisemea Amanda na   baada ya kujiweka sawa alitoka moja kwa moja kuelekea shemu ile waliyo kuwa wamemzika Irene, wakati anakaribia mara akakutana na James aliyekuwa akizurula zurula..

James: “amando uanenda wapi?

Amando: ahaah nili --- nataka nikachukue lile jambe pale nje watu wasije kujua wakija kututembelea ghafla” alijibu kijasiri...

James: nice una akili  sana kalitoe” aliongea james na kuingia ndani. Amando alifurahi na kujipongeza kwa uwezo wake wa kutunga sababu iliyokubalika na mkuu wake na sasa alienda haraka haraka akaanza kulifukua lile kaburi, alifanya kwa umakini kuhakikisha. hakuna hata chembe ya sauti inayosikika pindi anapolichimba lile kaburi,  haikuchukua muda akawa amemaliza na kufanikiwa kulitoa nje jeneza. Alitoka ndani ya kaburi na kulivunja jeneza haraka akitaka kumuokoa Irene, alimtoa na kusikiliza mapigo ya moyo.

Masikini Amando alilia machozi kwani Irene alikuwa hapumui wala moyo wake haukusikia ukipiga. Alijaribu kuyafunua macho ya Irene na kuyaona yakiwa yamejaa weupe na kugeukia juu mbinguni. Alimliza Irene pale chini na kufukia kaburi haraka haraka kama kawaida kisha akambeba Irene ili aende nae chumbani. Alitembea kwa uangalifu huku akihakikisha hakuna anaye muona, japo alielewa kuwa atakamatwa tu kwani jumba lile lililindwa na CCTV camera. 

Hatimaye aliingia chumbani na kuanza kufungua zile kamba ambazo Irene alikuwa amefungwa, akamlizia na mdomo na kumlaza Irene kitandani kisha akaenda stoo ya vifaa na kuiba pacemaker kifaa maalumu kinachotumika kustulia mapigo ya moyo pindi mtu anapokuwa amefariki muda si mrefu. Alirudi haraka na kufunga  mlango akafungua switch na kuweka voltage ya kutosha, alifungua shati la Irene upande wa kushoto na kuweka mashine ila hakustuka. Aliongeza voltage na kupiga kifuani pa Irene lakini bado, akapiga mara ya tatu, kidogo Irene akastuka, haraka akaacha mashine na kuanza kupulizia okisijeni mdomo mwa Irene mapigo ya moyo yakarudi, sasa Irene alikuwa anahema kwa mbali, Amando huku akitikwa na machozi ya furaha aliendelea kupulizia na mapigo ya moyo ya Irene yakaimarika japo mwili ulikuwa wa baridi mno na alikuwa akinuka sana kutokana na mkojo.

 Alichemsha maji na kumchukua Irene na kumuogesha aliweza kuuona uzuri wote wa Irene, akamrudisha chumbani na kumvika nguo zake yeye kwani za Irene. Akapika uji na kuanza kumnywesha Irene, alimnywesha na baada ya muda kidogo macho ya Irene yalikuwa yanaanza kufumbuka na kurudi hali ya kwaida. Alimuosha mdomo na kumuweka vizuri kisha kumrudisha kitandani na kufua nguo zote za Irene na kuzianika mule chumbani.  


Baada ya muda Irene alianza kukohoa kwa nguvu sana kama mtu aliyepaliwa na kitu, Amando alimfuata na kumtuliza kisha akamuuliza unaitwa nani? Irene hakujibu alibaki akimwangalia kwa macho yaliyo legea, wakati akiendelea kumhoji Irene ili ajue namna ya kumsaidia mara mlango uligongwa kwa fujo kweli,

“Fungua Mlango haraka na utuambie ni nani uko nae humo ndani!” Ilikuwa ni sauti ya ukali mno ya James iliyomstua Irene na kujikuta akiitika “MIMI” hali iliyomfanya Amando awe katika wakati mgumu akiwaza namna ya kujiokoa yeye na Irene.

James: Amando unaleta dharau kwa kumtuma mwanamke aitike sio nimesema fungua!

Irene: kwani hapa wapi? Alafu we manaume unafanya nini kitandani kwangu? Nilijua ni Franc kumbe siyo”  mara akaanza kulia kwa sauti. Amando hakuwa na la kufanya zaidi ya kumpiga kofi Irene kwani ameshaharibu. 

Mlangoni james aliendelea kugonga na Amando hakujua cha kufanya, alijua sasa ndio mwisho wa maisha yake na binti Yule aliyemuokoa…James aliamua kuvunja mlango na kuingia ndani akiwa na bastola mkononi na kukutana uso kwa uso na Amando na binti ambaye James alihisi kama Alisha wahi kumona ila hamkumbuki vizuriii………………

Je nini kitamsaidia Amando ambaye kajitolea kumsaidia Irene?
Itaendelea pia kitabu cha stori hii na zingine kinakujia…

No comments:

Audio