NJIA NZURI ZA KUONDOA MSONGO WA MAWAZO.
Na Franco Samuel
Jifunze baadhi ya njia nzuri ambazo unaweza kuzitumia kukabilina na msongo wa mawazo. Kwa sababu kila mmoja wetu yupo tofauti na vitu vinavyoleta msongo wa mawazo ni tofauti, hakuna njia moja sahihi ya kuleta mabdailiko kwako.
Zifuatazo ni njia za kutumia:
1: Kukwepa Vyanzo Vya Msongo Wa Mawazo: Si rahisi kukwepa kila chanzo cha msongo wa mawazo na ni vibaya kukwepa chanzo cha msongo wa mawazo ambacho inabidi ukikabili. Jifunze kusema hapana:
Wakwepe watu wanaoksababishia msongo: Kama kuna mtu anakusababishia msongo wa mawazo kila wakati, punguza muda wa kukutana naye au vunja kabisa mahusiano naye.
Dhibiti mazingira mabovu: Kama habari za jioni za kwenye TV zinakukera, zimisha hiyoTV na kama msongamano wa magari kwako ni kero, chukua njia nyingine isiyo na msongamano hata kama ni ndefu zaidi.
Kwepa mada zinazokupa maudhi: Kama mada za dini au siasa hukupa maudhi, acha kushiriki kwenye mada hizo. Kama kila siku unalumbana na watu fulani kuhusu mada fulani, acha kuanzisha mada hizo au tafuta kisingizio cha kuondoka mada hizo zinapoanzishwa.
Chunguza ratiba yako: Itazame kwa kina ratiba yako, majukumu yako na kazi ulizojipangia kwa siku. Kama mambo ni mengi mno, yagawanye kwenye makundi ya yale ambayo ni lazima yafanywe na yale ambayo ni muhimu kufanyika.
2. Badili Mazingira ya chanzo:Kama inashindikana kukwepa chanzo cha msongo wa mawazo, badilisha mazingira yake. Jaribu kufikiria ni nini cha kufanya ili chanzo hicho kisijitokeze tena hapo baadaye.
Onyesha hisia zako: Kama kuna kitu au mtu anakukera, mweleze wazi kabisa kwa njia ya kistaarabu. Kama husemi, unajenga chuki na kuiacha hali ikibaki pale pale.
Usilee matatizo: Usilikalie lile linalokukera, liseme wazi na chukua hatua mara moja ya
3. Badilika Kuendana Na Chanzo: Kama huwezi kukibadili chanzo cha msongo wa mawazo, wewe badili mtazamo wako kuhusu chanzo hicho:
• Rekebisha viwango vyako: Moja ya sababu ya kujipa msongo wa mawazo ni kutaka kila kitu kiende sawa kwa kiwango cha hali ya juu. Usijiweke kwenye mtego wa kushindwa kwa kujiwekea viwango vya juu kiufanisi. Jiwekee viwango vinavyowezekana kwako na kwa wenzako na jifunze kukubali matokeo ambayo hayakufika kiwango lakini siyo mabaya.
•
Yakumbuke mazuri yako: Msongo wa mawazo ukikunyemelea, chukua muda kidogo kushukuru kwa yale yaliyo mazuri katika maisha yako, ikiwa ni pamoja na vipawa nyako vizuri na vyenye nguvu. Hili litakusaidia kukupa mtazamo tofauti wa mambo yaliyo mbele yako.
4. Kubaliana Na Yale Ambayo Huwezi Kuyakabili: Vyanzo vingine vya msongo wa mawazo huwezi kuvibadili wala kuvizuia. Huwezi kukizuia kifo cha mtu wa karibu yako, wala ugonjwa mkubwa, au mporomoko wa uchumi wa nchi. Hapa inafaa kukubaliana na hali ingawa ni vigumu.
Usijaribu kudhibiti kisichowezekana: Vitu vingi sana katika maisha yetu vipo nje ya uwezo wetu – hasa tabia za watu wengine. Kuliko kung’anga’nia na kugombana nao wabadili tabia, fikiria zaidi namna unavyoweza kuepukana na matatizo yao.
Tazama upande wa pili: Unapokumbana na vikwazo vikubwa, chukulia kuwa ni nafasi ya kujifunza na kukomaa. Kama ni maamuzi yako mwenyewe ndiyo yaliyokusababishia matatizo, chukua nafasi hiyo kutafakari na kujifunza kwa maamuzi yako ya baadaye.
Jifunze kusamehe: Lazima ukubali kuwa tunaishi katika ulimwengu wenye mapungufu mengi na kwamba binadamu kufanya makosa ni kawaida. Usiwe na hasira na chuki, jifunze kusamehe na kuendelea na mambo mengine.
5. Pumzisha Na Burudisha Mwili Wako Mwili wako utapata uwezo mkubwa zaidi wa kukabiliana na msongo wa mawazo endapo utaulea kwa kupata muda wa kuupumzisha na kuuburudisha. Katika kuulea mwili wako unaweza kufanya yafuatayo:
• Fanya matembezi, Pumzika kwenye bustani au sehemu zenye mazingira ya asili
• Mkaribishe rafik nyumbani na kupiga stori za kwaida zisiwe za jambo linalookupa msongo wa mawazo
• Soma kitabu kizuri, Sikiliza muziki, Angalia vichekesho.
• Jichanganye na marafiki wenye mawazo mazuri, hao watakusaidia kuondokana na madhara yanayotokana na kuwa na msongo wa mawazo. Jaribu kuwa ni mtu wa kufurahisha na kufurahia mambo kwani kicheko ni dawa ya kuondoa msongo wa mawazo kwa njia nyingi.
• Mazoezi Na Chakula Kizuri Unaweza kuongeza uwezo wako wa kukabiliana na msongo wa mawazo kwa kujenga afya ya mwili wako.
• Punguza matumizi ya kahawa na sukari.
• Acha sigara, pombe na kushiriki Ngono kama sehemu ya kuondoa msongo wa mawazooo
*******************Njia mbaya za kuondoa msongo wa mawazo**************
Hebu tazama njia ambazo baadhi ya watu hutumia, njia ambazo hupunguza tatizo kwa muda mfupi na kulifanya tatizo kuwa kubwa zaidi baadaye:
Kuvuta sigara, Kunywa pombe sana
Kula sana au kula kidogo
Kukaa kwenye TV au kompyuta, saa nyingi sana
Kujitenga na marafiki, familia na shughuli.
Kutumia vidonge
Kulala sana
Kuahirisha mambo
Kujishughulisha saa zote kuepuka matatizo
Kuwatulia wengine msongo wao (kubwatuka, kufoka, kupigana)
Yafanyie kazi haya yatakusaidiaaa…
Franco Samuel
No comments:
Post a Comment