Tuesday, October 10, 2017

Diamond Platinum Apeta Ughaibuni

 Diamond Platinum azidi kupeta majuu zaidi...

 

  Hallelujah ya Diamond ft Morgan Heritage imechukua headlines Uingereza   na nchi nyinge za  ugaibuni.

        Baada ya Diamond platnumz kuachia ngoma yake ya Hallelujah aliowashirikisha kundi la Morgan Heritage kutokea Jamaica kufanya vizuri na kuvunja rekodi ndani ya saa 15 kupata views millioni 1.  Wimbo huo umeonekana kufanya vizuri katika kituo cha BBC Radio 1Xtra  nchini Uingereza baada ya kushika namba moja katika  top 5 katika  kipindi cha Afro Boss cha radio hiyo kwa kuzishinda ngoma nyingine kama ‘Inde’ ya Heavy K, ‘Maradona’ ya Niniola, ‘My Baby’ ya Magnom na ‘Nhema’ ya EXQ.  

 

 

  Diamond platnumz azidi kuivusha mipaka ya bongo fleva na kuipeleka mbali zaidi kwa mashabiki wa nje ya Afrika kuzidi kuupenda wimbo huo kwa kusikilizwa na watu wengi  na kupigwa zaidi kwenye vyombo vya habari.

No comments:

Audio