Showing posts with label Habari Mchanganyiko. Show all posts
Showing posts with label Habari Mchanganyiko. Show all posts

Friday, November 17, 2017

NDEGE YA BRITISH AIRWAYS YAVAMIWA HEWANI

11/17/2017 09:06:00 AM 0
British airways yavamiwa ikiwa hewani


Ndege ya British Airways ikiwa imevamiwa na kundi la ndge hewani muda mfupi baada ya kupaa


Kundi la ndege walao nyama limevamia ndege yakutoka Uingereza kampuni ya British Airways na kuleta tafrani kwa marubani, wasimamizi wa ndege na abiria. Kundi hilo la  ndege  limeishangaza dunia kwani kwa kipindi kirefu haijawahi tokea kama hivyo. 

Moja ya ndege akiwa amenasa kwenye ndege baada ya kutua

Bawa la ndege likiwa limeharibiwa vibaya na ndege

Hata hivyo wataalum wanatabahi kuwa huenda kutokana na ukosefu wa chakula ndiyo inaweza kuwa sababu kubwa ya ndege hiyo kuvamiwa na kundi hilo la ndege walao nyama. 
Hata hivyo rubani alititumia akili ya ziada na kuweza kufanikiwa  kutua kwa ndege hiyo bila kuleta madhara kwa abirua wala ndege hiyo.. 
Picha zaidi ziko hapa





Ndege ikiwa imeshatua salama

Monday, November 13, 2017

Hukumu ya Lulu yatolewa

11/13/2017 11:56:00 AM 0
Dar Es Salaam

Mahakama leo imemhukumu mwigizaji Elizabeth Michael maarufu kama Lulu kifungo cha miaka miwili jela baada ya kupatikana na hatia ya kuua bila kukusudia msaani mwenzake Steven Charles Kanumba
Hukumu hiyo imetolewa mapema leo asubuhi na jaji aliyekuwa akisikilza kesi hiyo Rumanyika. Lulu atatumikia kifungo cha miaka miwili jela kama adhabu ya kupatikana na hatia ya kuhusika na kifo cha msanii mwenzake miaka iliyopita

kulinganana na maelezo na ushahidi iliotolewa na pande zore mbili ikiwemo mashawakili wa utetezi Lulu alibainika kusababisha kifo cha msani mwenzake bila kukusudia hivyo kuamriwa kufungwa miaka miwili jela ..

Tuesday, October 10, 2017

Moto mkubwa Waikumba Marekani

10/10/2017 11:55:00 AM 0
Moto mkubwa waikumba Marekani katika mji Mmoja wa California 
Moto mkubwa wasababisha maafa California, Marekani 10 Oktoba 2017.

Nyumba zaidi ya1,500 zimeharibiwa na moto huo Maeneo ya jimbo la California ambayo hukuza mizabibu yameathiriwa na moto mkubwa ambao unaenea kwa kasi sana na kusababisha vifo vya watu 10.


Mamia ya watu wamehamishwa makwao na inakadiriwa kwamba zaidi ya nyumba 1,500 zimeharibiwa na moto huo. Watu saba waliuawa katika wilaya ya Sonoma, maafisa wamesema. Watu zaidi ya 20,000 wamekimbia wilaya za Napa, Sonoma na Yuba baada ya moto mbaya zaidi wa nyika kuzuka maeneo hayo. Gavana wa jimbo la California ametangaza hali ya dharura.


 Moto unawaka katika maeneo 14 katika wilaya nane za kaskazini mwa California "Moto huu umeharibu sana nyumba na miundo mbinu mingine na unaendelea kutishia maelfu ya nyumba, jambo ambalo limesababisha haja ya kuwahamisha maelfu ya watu," taarifa ya gavana imesema. Kando na watu waliofariki Sonoma, wengine wawili wamefariki Napa na mwingine mmoja Mendocino.

Inaarifiwa kwamba kuna majeruhi wengine zaidi na wapo pia watu ambao bado hawajulikani waliko. Marian Williams mkazi wa Kenwood, Sonoma amesema yeye na majirani zake waliutoroka moto huo kwa msafara wa magari. "Ni moto mkubwa ajabu, hatujawahi kuona moto kama huo," ameambia shirika la utangazaji la NBC. Mkuu wa idara ya misitu na kinga dhidi ya moto California Kim Pimlott, amesema nyumba 1,500 kufikia sasa zimeharibiwa.


Chanzo cha moto huo uliozuka Jumapili usiku bado hakijabainika. Mkuu wa kukabiliana na moto wilaya ya Napa amesema hali ya kiangazi katika eneo hilo inaathiri juhudi za kuukabili moto huo na kwamba wameomba usaidizi kutoka wilaya nyingine jirani. Wafanyakazi wengi wa mashamba hayo ya mizabibu wamehamishiwa maeneo salama kwa ndege. Moto huo unaenea kwa kasi sana kutokana na upepo mkali, ukavu na joto kali. Idara ya Utabiri wa Hali ya Hewa imetoa tahadhari eneo lote la San Francisco na kusema "moto ukizuka basi kuna uwezekano utaenea kwa kasi sana".
Kwa Picha:
 Moto mkubwa California Mmiliki mmoja wa mizabibu aliambia gazeti la LA Times kwamba anaamini shamba lake limeharibiwa baada yake na familia yake kukimbilia usalama Jumapili. "Upepo ulikuwa unazuka na kufifia. Ndimi za moto zilituzingira," amesema Ken Moholt-Siebert. Maafisa wa kuzima moto California wanakadiria kwamba eka 70,000 zimeteketezwa na moto huo.

Jimbo la California limekuwa likiathiriwa na moto miezi ya karibuni. Septemba moto mkubwa uliathiri jiji la Los Angeles.

Monday, October 9, 2017

Breaking News: Prof Mkumbo ajivua Uanachama

10/09/2017 08:21:00 PM 0

MKUMBO AJIVUA UANACHAMA

 PIGO KWA ACT.... 


Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Prof Kitila Mkumbo ameandika barua ya kujivua uanachama wa ACT-Wazalendo kuanzia leo.

  - Prof. Mkumbo alikuwa mshauri wa chama hicho na baadae kujiuzulu alipoteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji....

4

Audio