Wednesday, October 11, 2017

Ujauzito Jukumu la Wote

 Ujauzito jukumu La Wote

Hujambo mfuatiliaji wa blog yetu.. 
Leo tutajifunza umuhimu wa ushirikiano kipindi cha ujauzito baina ya wazazi wawili. Kwa utamaduni wa Kiafrika  watu wengi hasa wanaume huchukulia kama ujauzito ni jukumu la mwanamke tu. Wengi hifurahia kuitwa baba au baba kijacho bila kukumbuka kuwa kulea ujauzito ni jukumu la kushrikiana kwani kwa kufanya hivyo hufanya mtoto akue vema kisaikojia. 

Bahati mbaya kuna wanawake wengine  hupata  ujauzito na wakawa mbali na waume zao au pengine kutokuwa na maelewano mazuri na mwanaume anayehusika na ujauzito huo. Hawa hukosa  kitu kikubwa sana. 
Faida za kuwa karibu  kipindi cha ujauzito ni pamoja na  kujenga dhana bora ya kisaikolojia kwa mtoto atakaye zaliwa.  Inaaminika kuwa mtoto huwa na furaha pindi wazazi wakifurahi pamoja. 

Faida nyingine ni kusaidiana ikitokea tatizo. Mfano  mwanamkea anaweza  kuumwa ghafla   hivyo uwepo wa mwanaume utasaidia kutoa msaada na kuepusha madhara  ya mimba kuharibika nk. 

Pia inasaidia kufanya maandalizi kwaajili ya mtoto ajae,  maandalizi ya pesa,  nguo na kadharika yakifanywa mapema na wazazi wote wawili huwa mazuri zaidi na huzuia kupunguza gharama na mzigo kumwelemea mtu mmoja ambapo mara nyingi huwa ni  mwanamke. 

Pia kukumbusha tarehe muhimu za kliniki na  kupata chanjo.  Hii husaidia kumkinga mtoro dhidi ya magonjwa na kumpa kinga itakayo mfanya awe na uwezo wa kustahimili magonjwa na hivyo kuepusha bifo vya watoto chini ya mwaka 0 hadi 5

Ni wajibu wa kila mzazi kujua jukumu lake na kufanya kwa usahihi kabisaa


No comments:

Audio