Friday, October 6, 2017

Mungu ni Mkuu



Mama mmoja alitoka shamabani akiwa amechoka sana kwani alikuwa na ujauzito huku mumewe akimuacha na kutangulia pekee nyumbani.  Jua lilikuwa kali sana na alipata taabu kweli. Alifika mahali na kukaa chini ya kivuli cha mti mkubwa ambao pia ndege wengi walikuwa wakiimba  na kuruka ruka kwenye matawi yake wakifurahia uzuri wa maua ya mti.    

Akiwa pale chini ya kivuli,  kizuri chenye upepo mwanana alihisi mtoto wake akicheza tumboni.  Alihisi faraja sana mtoto wake kucheza tumboni. Bado kiu ilikuwa kali mno,  alitamani maji ila hakukuwa na maji.   Akiwa pale chini ya kivuli mara matone ya maji yalianza kudondoka.  Ilikuwa ni furaha, haraka mama yule alichukua kikombe kilichokuwa kwenywe mkoba na kuanza kukinga maji yale tone kwa tone. Wakati kikombe kikikaribia kujaa kabisa mara ndege mmoja alitokea kushuka chini kwa kasi na kwa kumstua ndege alipiga kikombe na maji yakamwagika. Mama yule mwenye kiu kuu ya maji aliuumia mno....na kulaani uzao wa yule ndege. 

  Hakukata tamaa akaokota kikombe na kuendelea kukinga tone baada ya tone. Safari hii mama alijipanga ili ndege akitokea ampige. Lakini wakati akifurahia maji kukaribia kujaa ndege akatokea tena na kupiga kikombe maji yakamwagika. Mama alichukia mno. Aliwaka hasira kali moyoni. Akachukua jiwe na kupiga yule ndege na kumuua.   Alikinga tena maji na yakajaa vema. Safari hii ndege  hakutokea tena. Alitabasamu na kuinua kikombe cha maji juu akimshukuru  Mungu Kwa kikombe kile cha maji. Akiwa katika kuomba mara joka kubwa lilindoka toka juu ya mti na kumfanya astuke na kumwaga tena maji. Alipochunguza aligundua kuwa kumbe yale hayakuwa maji bali ilikuwa ni sumu ikidondoka kutoka kinywani mwa joka lile kubwa na la kutisha.

   Aliumia sana kwa kumuua ndege aliyesababisha kumwaga maji yake. Alijiona mwenye hatia kumuua ndgege aliyetumwa na Mungu kumuokoa. Alirudi nyumbani akishukuru ukuu wa Mungu..

   Funzo. 
 Kuna  vitu ulijua ni vymea kumbe ni sumu ulijua maji kumbe ni  shubiri kali.  Mungu mwema akuondolee maumivu unayopitia.   

  Usiwe mwepesi wa maamuzi,  kuna vitu vingine vimetumwa kuja kukuokoa. Jambo likikutokea angalia upande wa roho pia,  usiwe kimwili tu.  
    Amini Mungu anaweza kukuoka wakati wowote ule na kwa  njia yeyote ile.    Ukiweka Imani kwa Mungu hakuna linaloshindikana....   
   Kabla ya kufanya chochote Muombe Mungu kwanza..
   Tumia sekunde 3 Umshukuru Mungu kwa meme yote na mabaya aliyokuepusha kwa  kuandika  "ASANTE MUNGU MWEMA" AMINA  

 Na mwisho usiwe mchoyo share na wengine ili wajifunze,  comment yako pia muhimu...  Like share,

No comments:

Audio