SIKUMPENDA, NILIMTAMANI TU ILA ALIKUFA KWAAJILI YANGU!
Mwanzoni sikumpenda kutoka moyoni, nilimpenda kwa kuwa tu alikuwa mrembo haswa..kwa kifupi nilimtamani tu...yaani nilitegemea akinivulia nguo zake tukashiriki tendo hamu yangu itaisha na nitaachana naye! 👇
Image
KUKUTA NAE KAMA UTANI
Back then katika mihangaiko ya maisha, nikiwa nasota na nimepigika kweli. Si unajua ile umehitimu chuo kupata kazi ilivyo kazi? Sikuwa hata na uelekeo wa maisha! Nikapita kwenye kampuni fulani ambayo nilikuwa nimetuma maombi ya kazi ili nijishikishe hapo..
Kiufupi ni kuwa maisha baada ya chuo kama hujajipanga basi yenyewe yatakupanga! Vyuma hukaza hata upake wese havilegei!
Nilifika na kuzama ndani ya ofisi, sehemu ya mapokezi alikaa mdada fulani mzuri mzuri sana! Lips amazing, jicho la kulegea na sura fulani yake ya kiblack 👇
Image
beauty yenye kupendeza! Nikampa heshima zangu kwa salamu na akaitikia kwa kupoa sana. Si nikamuuliza dada wenywe wapo! Maana alikaa kwenye kiti cha wageni! Jibu lilikuwa rahisi tu “wameniambia niwasubiri sio muda mkurugenzi anakuja. Vipi kwan wewe unashida na nani kaka!?”
Aliongea sauti ile tamu, yenye upole na kubembeleza! Kiasi nikajikuta nahama kimawazo! Yaan mm nina matatizo kweli, sasa nawaza nini badala ya kufikiri kilichonituma pale
“We kaka unawaza nini!?”
Nikagutuka toka mawazoni. Aibu kiasi ikanipata “ahaa mimi nina shida na Mkurugenzi”
Image
“Ohh shida yako km yangu! Umekuja kuomba kazi kama mimi ehe?” akachombeza kwa upole na sauti ya chini zaidi.
“Ndio. Sijui wewe mwenzagu” nikamjibu kwa swali
“Ndio nimekuja kuomba kazi na leo ndio usaili una......” akakatisha kuongea baada ya kuona mdada wa mapokezi anakuja!👇
Tukabaki kimya huku moyo wangu ukidunda. Yule dada wa mapokezi akasema na sisi “jamani karibuni sana, tutafanya usaili na mkurugenzi na team yake wapo tayari hivyo nimetumwa niwaite lakini tutaanza na wakwanza dada hapo then kaka utafuata huyu akitoka!”
Akamaliza na yule dada
akasimama kuchukua uelekeo kuingia sasa rasimi kwenye usaili!
Uoga wa interview ukaanza kunipanda! Nikawa muoga mno! Mbona tuko wawili tu? Ina maana nafasi ni moja tu? Vipi kama huyu dada akipita mm nisipite? Lazima nishinde! Yes! I must win! Kichwa changu kiliwaza sana.
Soon nikajikuta nina hisi kama haja ndogo inabisha hodi! Uoga wa interview huo, nikaomba kuoneshwa washroom na bila kusita yule dada wa mapokezi akanionesha nikafanya yangu na kurudi nikatulia kwenye kiti.
Sijakaa sawa yule dada akatoka! Akatembea pole pole na kuaga kwa dada wa
mapokezi kuashiria mimi natakiwa kuingia! Akafika kwangu na kunipa mkono! Haukuwa mkono tupu, kuna kitu akaniachia! Kilikuwa nini sikuwa na muda wa kuangalia nikaweka mfukoni! Akaniambia tu
“Nakutakia mafanikio, Tutaonana!”
Nikatabasamu tu na kuongoza njia kuingia sasa kwenye
Image
Interview huku kijasho chembamba kikitiririka kwapani bila kupenda! Interview sio mchezo wapwa! Basi nikawakuta panellist wamekula zao suti! Maswali yakaulizwa, mengine simple mengine magumu na mengine mepesi ila huoni majibu yake! Interview ikaisha huku wakiniambia baada ya
kujumlishwa marks nitaitwa na nikatakiwa kuacha namba za simu.
Nitaitwa siku gani hilo swali huwa hatuwaulizi panellist. Basi nikainuka huku nikiona dalili za kuwa nimevurunda kabisa.
Mdogo mdogo nikasonga na kutoka njee ya ofisi huku nikiomba kwa Mungu anijalie nipate ile kazi.
Nikazidi kuuchapa mwendo, nikakumbuka kitu nilichopewa na yule dada. Mkono chap ukazama mfukoni na kutoka na kikaratasi! Kiliandikwa mwandiko mzuri unaosomeka vema
“Naitwa Irene, nimefurahi kukuona! Ukitoka nitafute na 07688006...”
Moyo ukafurahi! Nikarudia kukisoma mara kadhaa.
Nikazama mfukoni chapu na kutoa kiswaswadu chagu, kimefungwa manati utafikiri mfungwa wa Guantanamo.
Nikaandika namba kwa umakini kabisa nikasave na kisha kupiga na kuweka sikioni..
“Hauna salio la kutosha tafa....” What the f***! Nikakata na kucheki mfukoni nina buku mbili tu
Tumbo nalo likaunguruma kunikumbusha kuwa sijalipa haki yake. Magetoni ninakoenda ni mbali. Natakiwa kupanda gari. Vocha sina na natakiwa kumtafuta Irene!
Ewaaa! Niamue kipi, Ninunue vocha nikae njaa na kukanyaga kwa miguu? Au nipate chai nisinunue vocha na nikanyage ya mguu?
Baada ya fikira za kubishana ubongoni nikajisemea mbona mimi nilienda JKT najua kila aina ya mwendo acha ninywe chai then nikatishe chochoro nifike home!
Sasa buku 2 inatosha nini? Potelea pote nikatimba kwa mama Ntilie wale wa barabarani nikanunua chips dume a.k.a mihogo!
na kutia pilipili kwa wingi! Nikapiga mpaka macho yakatoa machozi Tumbo likanishukuru nikaomba na maji nikanywa. Basi nikawa fiti sasa naweza kukanyaga ndefu ndefu mpaka geto! Nilishazoea chochoro so nikazama vichorochoroni huku nikiwaza napataje pesa niweke vocha! Maana kichwa
kinamuwaza tu Irene! Sina hili wala lile kucheki mbele kuna njemba mbili zimeshiba mazoezi geuka nyuma kunazo mtu tatu! Katikati ya ukuta huku na huku! Sijakaa sawa njemba moja ikaongea “oyaa dogo hatutaki mazoea na wewe! Tugei chetu chap kabla hujala spana “ kilafudhi fulani cha
Image
machari ya R, Chuga huko! Nikajisemea mimi mhuni wa Ungalimited watanifanya nini! Nikapiga plan za kuhepa kwa spidi ila kabla hata sijachapa hatua, wahuni wakanitia kati! Nikapigwa rungu, mateke na kifinyo cha maana! Nikajaribu mbinu zote za JKT ila hazikuzaa matundaaa kabisa.
Nikachezea kichapo huku wakitaka nitoe nilivyo navyo! Wakachomoa kiswaswadu na kunikuta sina kingine! “Oya anazingua huyu! Vueni hiyo kiatu chake na suruali na shati viko byeee tutauza tupate ya unga leo” mmoja akaamrisha bila huruma wakisaula viwalo! Nikabaki na soks, singlendi
na boxer! Mchozi wa uchungu ukanitoka! “Kaka jambazi naomba nichukue namba ya muhimu iko kwenye karatasi ndani ya hiyo suruali “ nikaomba kwa uchungu! Muhuni akajawa huruma na kunipa kikaratasi kisha wakahepa! Nikabaki pekee. Ikabidi nitembee tu km chizi huku nikilia kwa uchungu!
Niliwalaani mno wale wahuni. Nikalaani kupita njia ile! Nikaona wamenikosea mnoo.
Nilibaki na tumaini moja tu
namba ya Irene! Ona nilivyo mjinga sikukumbuka kuomba wanipe line ila tu namba ya Irene! Kweli mi ni mjinga, nikajisemea na kukimbia kama chizi huku nikiwa na hasira.
Nikatimba geto, watu wakashangaa kidogo kulikoni niko hivyo! Chap chap nikaoga na kujitibu majeraha kidogo kwa chumvi!
Nikaomba simu kwa majirani na kupiga simu kwa baba na mama kuwaeleza yaliyonikuta! Wazazi walinihurumia sana! Upendo wa baba acha tu, alituma pesa nika
wahi kwenda kununua kiswaswadu na kurenew line! Mambo yakakaa sawa na sikuchelewa nikaandika namba ya Irene na kupiga bila kuchelewa nikaweka simu sikioni..
“Namba unayopiga haipatikani kwa sasa. Tafadhali jaribu..”
Nikajikuta nakasirika, mbona hapatikani tena? Kuna nini?
Hakuna ambaye angejibu maswali yangu! Ikabidi niwe mpole!
Nikatafakari maisha kiukweli nilikata tamaa, sikuwa na mwelekeo! Geto kulikuwa kubaya!
Nikachukua simu na kumpigia tena Irene, simu yake ikaita. Ewaah
“Tiii tiii"
Usisahau tena part two 2 coming soon
No comments:
Post a Comment