Wednesday, November 8, 2017

Simulizi SITAMSAHAU FRANC EPISODE 15

Story::::           SITAMSAHAU FRANC
Mwandishi ::   FRANCO SAMUEL
Whatsapp ::    0768800687
Episode ya 15.....

 Ilipoishiae Episode iliyopita...

Taarifa zilipelekwa kwenye ubongo wa nyuma kisha mbele na kumbukumba za ubongo zikanambia hao ni Rama na Kriss wale wa kule porini. Lau aliniangalia na kunipa ishara fulani kama wanenavyo wahenga kuwa waswahili wa pemba hujuana kwa vilemba. Bila kuchelewa nikamuona kondakta akitoka kwa hasira na kumkwida Kriss ambaye alimuangalia tu kondakta bila kumfanya lolote. Kondakta kuona vile kwa hasira alimpiga Kriss Ngumi ya uso, Kriss wala hakutikisika badala yake alimtandika kondakta kofi moja lilompeleka chini kama gunia la viazi na kumfanya apige ukelele wa maumivu makali mno.

Walimuacha  kondakta akiugulia maumivu na kimadaha Kriss na Rama wakaanza kuja kwenye basi. Sijui nani aliwaonesha kuwa tuko kwenye hili gari, nilijikuta nikiwaza bila jibu. Nilijua tu ni mimi na Lau ndio mawindo yao. Na kweli wametupata. Hakuna pa kukimbilia. Abiria walianza kupiga mayowe ya hasira huku wakiwa hawajui nini kinaendelea.  Mimi,  Lau,  Rama na Chriss ndio tulikuwa tunaujua mtanange mzima.

Songa nayo hapaa


Rama alionekana mwenye hasira nikakumbuka maneno ya Lau kuwa huwa hana utani hasa awapo kazini.  Ulikuwa mtihani mwingine wa kuukabili mimi na Lau, kwa misuli waliyokuwa nayo akina Rama na Chriss sikuzani kama tutaweza na niliona mwisho umefika wa maisha yetu.
"Lau tukubali tu yaishe acha tu watukamate. Maana sioni tumaini  la kuokoka hapa kabisa" nilimwambia Lau kwa sauti ya kukata tamaa. Lau aliniangalia bila kisema chochote kile,  Wakati huo walikuwa wanaingia kwenye basi. Kwa muonekano wa macho yao mekundu nilibaini wamevuta kitu cha Arusha au kama sio hivyo basi wana hasira kali mno.

"We msaliti toka nje faster na tusipotezeane muda" alifoka Rama huku akimkazia Lau macho yake mekundu.  Sasa watu wakawa wakiangalia picha lililoibuka bila hata director wakiwa hawajui mwanzo wake. Lau alikausha kama hajasikia,  Rama kuona vile akatifuta pale kwenye siti. Kriss muda wote alikaa mlangoni.  Nilichungulia nje akili ikanituma kuruka kupitia dirisha. Wakati nikijianda kuruka Rama alimkamata Lau na kuanza kumtoa nje kwa nguvu,  kabla hajafika mlangoni kondakta alikuwa kaamka na kuanza kumshambulia Kriss aliyekuwa mlangoni. Mapigano yale hayakumuacha kando dereva kwani nae aliachia usukuni kwankulizima gari na kuanza kumshambulia Kriss akiwa na lengo la kumuokoa kondakta wake aliyeonekana kuzidiwa na makonde yenye ujazo aliyotupiwa na jitu lenye mwili wa mazoezi Kriss.

Rama akiendelea kumlazimisha Lau ashuke huku akimshikilia alipokea teke la tumbo lilimpeleka chini na kumfanya aisalimu lami. Teke hilo lilirusha na Lau kwa ustadi kabisa na Rama hakutarajia kama angepokea teke la tumbo toka kwa adui yake Lau. Kudondoka tu gari lilipita nusura limgonge ila akalikwepa kwa ustadi na haraka. Watu kwenye basi walibaki wakishangaa,  huku akina mama wakifumba macho wasione kinachoendelea. Baadhi ya abiria kama kawaida wakachua simu na kuanza kupiga picha huku wengine wakirekodi video ya filamu iliyoanza bila hata muongozaji.

Rama alijitahidi kuamka ila Lau akamshindilia kwa ngumi ya uso na kumfanya aendelee kulala pale chini. Wakati huo Kriss alionekana mtata kwa kuwasambazia kipigo Kondakta na dereva. Masikini kondakta uso wake ulivimba pima kama mtu aliyeng'atwa na nyigu.  Niliwashangaa baadhi ya wanaume wakiwa kimya ndaninya basi bila kwenda kuamlia ugomvi. Akili ikanituma kushuka nikainuka na kushuka haraka ila nilipofika mlangoni nilipigwa kikumbo cha tumbo na Kriss aliyeoneka bado ana utawala mpambano ule.

Tumbo lilizizima kwa maumivu ya kikumbo kisichotarajiwa toka kwa Kriss. Lau akanipa ishara ya kuondoka pale.  Sikujua hata kwa kwenda,  tayari watu wengine walishuka na kuafanya wapita njia  kukusanyika. Rama aliinuka na kuanza kumshambulia Lau kwa makonde ya ngumi za uso,  tumboni na kifuani. Kweli ilikuwa kutesa kwa zamu. Lau  alipigwa ngumi nyingi mfululizo nikashuhudia akidondoka chini. "sasa nimekwisha leo siponi kabisa" nilijisemea na jasho likanitoka licha ya kuwa ile ilikuwa ni   asubuhi kabisa.
Dereva bado alipambana na Kriss akafanikiwa kumkata ngebe kwa ngumi ya uso. Rama alimsogelea Lau pale chini na kuanza kuinama ili amsulubu vema adui wake lakini wakati akiinama alikutana na teke la uso kutoka kwa Lau. Teke lilimfanya akadondokee mgongo na kisogo na kuugulia maumivu.

Niliona kama Lau amefufuka vile, aliinuka na kunishika mkono tukaanza kukimbia. Mbele kidogo kulikuwa na  magari mengi. Watu wakawa wanatushangaa tu. Niligeuka nyuma nikamuona Kriss akija kwa kasi ya ajabu, spidi ya Lau ilikuwa ndogo nikaanza kumvuta. Mbele kidogo tukaikuta taxi,  bila maneno Lau alifungua mlango na kuzama ndani bahati nzuri dereva alikuwa ndani na gari likuwa limewashwa.

"Ondosha gari haraka kijana Kuna hatari" alisema Lau huku akihema. Kuona vile dereva hakuwa na ubishi aliondosha gari kwa sipidi kali sana. Nilichugulia kupitia tinted na kumuona Kriss akilikaribia gari,  aliiruka gari na kutua nyuma huku akijaribu kujishikiza vizuri.
"Lau Kriss huyo nyuma ya gari kashikilia kweli" nilimstua Lau akiwa anahema huku damu ikimtoka puani.
"Oya dereva piga break fasta na ondosha gari" dereva alipiga break,  hali ile ilifanya Kriss kukosa balance akagonga kioo na kudondoka kisha gari likaendlea. Tabasamu likachanua usoni. Nikamuona Lau bonge la shujaa. Nikamuangilila,  usoni amevimba huku akitoka damu puani. Niliumia sana, kweli mapenzi kitu kingine, mateso yote haya kisa penzi la Franc..

"Lau pole sana,  nitakupa kitu kizuri tukipona katika hii hatari" niliongea kwa unyonge ila Lau akaonekana kukoroma tu na ni kama alikuwa hasikii ninachoongea!  Nikawaza hivi akiuliza hicho kitu kizuri nitajibu nini,  sikupata jibu.Nilimfuta damu, kwa kutumia tisheti,  wakati huo dreva akiwa kimya akiendesha gari kuitafuta Dar Es Salaam katikati ya mji. Alipoona natumia tisheti,  alipunguza mwendo na kutupatia kiboksi cha first aid.  Nilichukua na kufungua nikatoa pamba na iodine tincture na kunza kufuta ili damu ingande isiendelee kuvuja. Lau alilalamika kwa maumivu kisha akatulia kidogo.
"Nawapeleka wapi maana hata sijui tunakoenda" aliuliza dereva.  Sikuweza kujibu,  kwani sikujua anapokaa Lau japo kwetu ni Osterbay meeneo ya Masaki. Nilimstua Lau na kumuuliza wapi dereva atupeleke akamwambia dereva atupeleke Ubungo External. Dereva aliendesha gari na kujitahidi kuzikabili foleni kwa kupita njia za mkato zaidi. Haikuchukua muda, tulifika maeneo ya Ubungo External huku Lau akiomba dereva aingize gari ndani zaidi ili tusionwe na watu.

Mbele kidogo tulishuka na tukatembea nikimfuata Lau. Hatua kadhaa mbele yetu kulikuwa ilikuwa nyumba  chakavu na kuukuu ya muundo wa zamani. Alitoa ufunguo na kuanza kufungua kitasa kilicholeta mgomo kwa muda kutoka na kutu. Afadhali kwani watu walikuwa wachache na niliona tulikuwa sehemu salama kabisa..Alifanikiwa kufungua kitasa na kunikaribisha ndani nikaingia, aliongoza moja kwa moja chumbani na bada ya muda alitoka na noti za hela na kwenda kumkabidhi dereva.
Akarudi na kuja kukaa kwenye sofa,  nilijkutaa nikimkumbatia kwa nguvu na kumbusu Lau kwenye paji la uso. Sikujali majeraha na michubuko aliyonayo..
*****
Askari aliyekuwa akifanya uchunguzi TCRA aliridhika na taarifa na kugundua kuwa mara ya mwisho simu ya Irene ilitumika huko Iringa mjini na sasa simu hiyo ilikuwa ikitumika na mtu mwingine aliyeko Mufindi. Japo laini ya Irene ilikuwa haijatumika muda mrefu. Aliridhika na taarifa akamua kurudi kituoni Osterbay majira ya saa tano na nusu asubuhi.
Askari aliyekuwa chuoni,  hostel ya Mabibo Hall 5 Chumba A6 alikuwa akipiga stori na wadada waliokuwa hapo chumbani. Stori za hapa na pale ziliwavuta wadada hao na kufanya wajikute wakitoa ubuyu bila kujua.

"Eti hivi humu mnakaa watatu tu?" alihoji asakari akiwa kavalia nguo za nyumbani.
"Hapana bwana tupo na mwenzetu ila kwa sasa hayupo hapa chuoni" alijibu moja ya wananafunzi hao

"Yuko wapi na saaizi ni muda wa masomo"

"Kutoka tufunge aliondoka bila kuaga. Baaada ya chuo kufungua akawa hajaja. Muda ukaenda kimya bila simu,  tulipiga simu yake haipatikani. Na bahati mbaya hatukuwa na namba za Wazazi. Pita pita katika notsi board ndio tukaona  jina lake likiwa ilimebandikwa kama moja na wanafunzi waliochelewa kusajiliwa hivyo,  asingeendelea na masomo.  Juzi juzi tumepata taarifa kuwa mwenzetu kapotea na haonekani" alijieleza mwanadada.

"Kibaya zaidi,  Irene hakuwa mtu wa kujichanganya na watu sana.  Pia wakati mwingi alipenda kukaa pekee na sio mtu wa kuongea sana. Hatujui yuko wapi, nini kimempata na kwao hatukujui" aliongezea dada mwingine..

"Okay sawa,  kwanini hamkutoa taarifa mapema?" alihoji askari

"Isingekuwa rahisi kwa kuwa hatukujua yuko wapi. Ujue wakati mwingine mtu anaweza chelewa maybe kakosa ada na some other reasons so haikuwa rahisi kwa sisi kujua hilo" alijubu mwanafunzi mwingine.

"Mie niwaambie ukweli, nipo nafanya upelelezi. Tumepewa taarifa na mama Irene kuwa mwanaye hapatikani.  Mbaya zaidi mumewe yaani baba Irene amefariki kifo cha kutatanisha mno. Kwahiyo nashukuru kwa taarifa zenu. Naondoka!"  Masikitiko na majonzi zikawajaa wadada waliokuwa wakikaa na Irene,  nyuso zikajikunja ila askari akawapa moyo kuwa Irene yu mzima. Aliwatuliza  na kuondoka zake tayari kurudi kituoni kitoa taarifa.

Askari aliyekuwa akimpeleleza mama Irene alimuuliza kuhusu uhusiano wake na ndugu wengine. Mama Irene aliona swali lile kama gumu sana. Alafikiri na kumweleza askari kuwa amekuwa akiishinna watu. Japo mumewe alikufa kifo cha kutatanisha baada ya kupotea kwa siku tatu na kisha mwili wake ukaja kupatikana ukiwa umeharibika kabisa hali iliyolazimu kuzikwa kwa haraka. Alieleza siku zote tokea mumewe apotee hakumtaarifu binti kwani aliogopa kumchanganya na masomo.  Baada ya kupatikana kwa mwili ndio nikampigi simu na iikiwa likizo hakupatikana, nikajua labda ubize na chuo. Ikanilazimu kuja na chuo pia wakasema hayupo. Hata waliokaa nae chumba kimoja wakadai kutojua alipo. Maelezo ya mama Irene yalijitosheleza na kumwacha askari pasi na walakini.

"Pole sana kwa matatizo,  mwanao atapatikana akiwa mzima wa afya kabisa. Sisi tutajitahidi. Nakuomba uende nyumbani ila acha simu namba ya simu tutakupigia" alisema askari na kumkabidhi mama Irene kijitabu kidogo akaandika namba na kuondoka huku chozi likimtoka

"Mume wangu kafariki kwa kifo cha kutatanisha na mwanangu huonekani, mwaniacha na nani huku ugenini?" alijisemea mama Irene huku chozi likizidi kutiririka.

*******    ******* **********
Niliendelea kumbusu Lau na kumkubatia kwa muda. Uso wake bado ulivimba baada ya muda tulisitisha zoezi la kukumbatiana huku Lau akinambia tupike. Alinionyesha jiko lilipo katika nyumba yake hiyo chakavu kwa nje ila kwa ndani ikiwa ni nzuri. Kama mtu angepita tu kwa nje hata asingejua kama ndani kuna vitu vya thamani kiasi kile. Kulikuwa na masofa mazuri,  kabati,  flat Screen TV kubwa ya maana na pia vyombo vya thamani sana. Ijapo vumbi lilivamia kwa kuwa muda ulipita bila mtu kukaa mle kwenye nyumba. Kweli Lau alikuwa vizuri. Niliwasha jiko la gesi na kupasha maji. Niliingia Karibu kila chumba isipo kuwa alichokuwa Lau, vyumba vyote vilikuwa ni self contained. Baada ya maji kupata uvugu vugu nilimwita Lau na kumkanda kanda. Kidogo uso wake ukapungua uvimbe uliokuwapo na akawa amebakia ni michubuko na majeraha madogo.

Nikaweka maji na kumuomba akaoge. Allikubali kufanya hivyo na wakati huo nikafanya fanya usafi wa nyumba. Nilipukuta vumbi illotanda kila mahali ikifuatiwa na deki. Lau baada ya kutoka kuoga alipiga simu na kuongea na mtu. Sio muda gari ilikuja na kushusha baadhi ya vitu vya kula. Nilipika chai ya maziwa nikamwita mezani tukala. Njaa ilikuwa kali sana. Niljikuta nikila chapati kama sio mtoto wa kike hadi Lau akanishanga. Baada ya kula nikamwomba niende kuoga. Sikujua hata nikioga nitavaa nguo gani.

Niliingia bafuni moja ya vyumba vya mle ndani nikawa naoga. Nilisikia mtu akigonga mlango. Nilijihisi vibaya sana maana niijua ni Lau tu. Aligonga kisha akasema baada ya kuona niko kimya.

"Nimekuletea taulo Sorry nilisahau kukupa muda unaenda kuoga." alisema na kisha nikasikia hatua za miguu zikitembea kuashiria alikuwa kaondoka. Bila kuchelewa nilifungua mlango nusu na kulichukua taulo. Nilioga haraka baada ya kupata wazo la kumpigia mama.
Nilitoka bafuni na kuelekea chumba alichonionesha Lau. Nilifurahi sana baada ya kukuta nguo mpya,  gauni,  kibrazia kidogo kama vile alinipima mimi na chupi. Pia kulikuwa na mafuta ya kupakaa pale. Nilimshukuru Mungu ila nikawa naona aibu. Nikajiuliza Lau kajuaje size ya nguo zangu. Nilienda mbali zaidi na kufikiri huenda nguo hizi alimnunulia mpenzi wake. Wivu ukanikaba nikiwaza akija huyo mtu wake itakuwaje. Lakini tena zilikuwa mpya kabisa  zikinukia dawa za dukani,  liwalo na liwe nilisema. Kisha nikaanza kujipaka mafuta. Nilidondosha taulo na kujiangalia kwa kioo kilichokuwa mbele yangu. Nilikuwa nimepungua sana na kupauka.

"Mungu asante Leo naenda kuonana na mama yangu kipenzi."  Nilijisemea na kuchukua chupi ili nivae. Sijamaliza kuvaa mlango ukagongwa na kufunguliwa kwani nilikuwa nimeegesha tu. Nikazubaa tu kama kuku mwenye kideri na kukodoa macho mlangoni kucheki nani alikuwa akiingia. Ni Lau ndio alikuwa akiingia. Alistuka baada ya kuniona nikiwa karibu uchi kwani nilikuwa nimevaa chupi tu. Nikaanza kujificha kwa kuokota taulo haraka huku mkono mmoja nikijitahdi kificha manyonyo yangu madogo Lau asiyaone.

"Lau sijavaa bwana naomba usibiri please" nilisema baada ya kuhakikisha taulo imenikaa vyema. Bado alisimama mlangoni bila kusema kitu. Ubongo kitu kingine kabisa, nikahisi pengine anataka penzi.  Nikamuona mjinga, anawaza penzi wakati mimi hata wazazi sijui wanaendeleaje..nikiwa katika kuwaza Lau akasema..

"Sorry sana ila nilikuwa nataka.. nataka nikwambie kitu kimoja hivi" aliongea kwa kukata kata sauti yake sikujua sababu yake ni nini. Kwa sauti yake ya uoga nikahisi kabisa kuwa fikra zangu za kumuhisi akinitaka kimapenzi zilikuwa sahihi.  Sikujibu chochote nikabaki kimya tu. Nadhani alipoteza point baada ya kuniona nikiwa vile bila nguo.. "ila nahangaika nini,  mbona alishaniona toka kule porini,  pale mgahawani alinishika shika shida ninil? " niliona yuko sahihi kutaka penzi langu ila muda haukuwa sahihi kwani mimi fikra zangu zote zilikuwa kwa wazazi na kufika nyumbani.

"Ukimaliza kuvaa njoo chumbani kwangu tafadhali" alinistua Lau na kunitoa kwenye mawazo yangu ya kijinga. Alifunga mlango na kuondoka kuelekea chumbani kwake. Nikavaa huku nikiwaza huko chumbani kuna nini? Kama kuna cha kuongea si tukutane tu sebuleni? Mawazo mengi yaliniandama hadi nikahisi kichwa kuuma.  Nikatoka baada ya kuvaa na kwa hatua za uoga nikaanza kutembea kuelekea chumbani kwa Lau. Nilifika mlangoni na kuchungulia nione anafanya nini. Alikuwa akibonyeza kicharazio cha kompyuta mpakato yake. Nikawaza anataka nini kwangu? Liwalo na liwe niliamua baada ya kufikiri kwa dakika kadhaa kisha nikagonga mlango kwa woga
"ngo ngo ngoo"
"Ingia tafadhali" alisema Lau akiwa ndani ya chumba chake kunikaribisha.. Nikashika kitasa tayari kuufingua mlango wa chumba cha Lau.

Itaendelea..
Je Lau anataka nini kwa Irene?
Tuseme ndio anataka malipo ya msaada aliompa Irene?
Wanaume Mungu anawaona...
Bado kuna mengi utayajua.
Usikose  iko hapa 1 6...http://francosamuel.blogspot.com

No comments:

Post a Comment

Audio